Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Dr. Kitila CDM nilijiunga kutokana na katiba yake sasa umefukuzwa uanachama kwa makosa yako unataka tukutetee, haitawezekana jitahidi kufahamu unachokifuata kabla haujakiamini. chama chako kipya utakuwa katibu mkuu.
 
- pole sana dr. Kitila ila maandishi yako kwangu ninayejua siasa yanaonyesha kwamba wewe sio mwanasiasa, ungekuwa basi usingeandika maneno ya kukata tamaa mapema hivi ulitakuwa kuwa kama zitto kupigana mpaka damu ya mwisho wewe hujapigana, umekalia maneno maneno tu ya kulia lia kama haya yatakusaidia nini? Nani anayasikiliza haya now, watu wanasonga mbele kaka umeshirikana na hawa wahuni huko chadema sasa wamekutema unaleta hizi? Wote huko mlikuwa wammoja ni zitto tu peke yake ndiye hakuwa na nyinyi siku zote na ndio maana mpaka leo anasimama nao na kinaeleweka,

- kitila wewe ndugu yangu sana naomba kukwambia bila kuchanganya maneno wewe sio mwanasiasa ni mbabaishaji, sasa wachana na hii field ya siasa endelea na kufundisha kaka, zitto ni politician sio wewe kaka badilisha field now ulikimbia ccm sasa umekimbizwa chadema, ni wakati wa kuwacha siasa tu ninakwambia hvii kwa sababu ninakuheshimu sana wacha siasa huziwezi kaka!!

Le mutuz

kama ndio hivyo hawezi kumuondoa mwigulu miaka 8000 labda mwigulu mwenyewe apende.
 
..Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM...
....Wewe ulivyofukuzwa umetimka na washabiki wangapi?.
 
Dr .kitila sio mshabiki wa zito ni mshabiki wa ccm.

Hivi kwa nini tusijiulize pale udsm bado yupo licha ya kujipambanua kuwa ni mwanagwanda?????

Hivi pro baregu ilikuaje pale ud??

Naaamini mwigulu na dr .kitila ni marafiki wakubwa tu.

Maneno makali ya kitila ni siasa tu.
 
Namuonea huruma Kitila na wenzake, wanatia aibu hata elimu yao pia wameitia aibu kuu. Wameshindwa kujua malengo ya chama chao na hata sababu ya kuwa Upinzani. Kitu ambacho hata mtoto wangu wa Darasa la kwanza analielezea vizuri. Huruma yangu ipo katika kona waliyonaswa tena vijana, alafu wasomi, ushauri kwao ni kukaa kimia Jamii iwasahau na wasirudi tena kwenye siasa. Waliingia kwenye mtego bila kujua wakijua ni Misaada ya kawaida ya kibinadamu mbaya zaidi walinashwa hata kabla hawajua kuwa watalazimishwa kufanya wasiyoyapenda na hawata kuwa na jinsi maana tayari wameneswa tunduni, wale Jamaa ni hatari ndio fani yao wapo makini na wanatumia akili nyingi sana, kama una akili za kalatasi huwezi kujua unapoperekwa maana mngelijua msingekubali kwa namna ninavyowajua Mwl. Kitila na mm.

Hakuna msomi aliye elimika ambaye hasingejua kuwa kwasasa priority nikuondoa CCM kwanza hata kama inafanyika bila chama kuwa na Mwenyekiti au hata kama Mwenyekiti aliopo anamapungufu ya aina yoyote achilia mbali upuuzi wanaoeleza sasa. Maneno ya Kitila na utetezi anaotoa ukilinganisha na umuhimu wa jambo lenyewe unaletashaka kama kweli ni Dr. Huwezi kuongelea kubadili Mkuu wa majeshi wakati mpo mstari wa Mbele vitani tena wakati ambapo umoja unahitajika ili kushinda vita husika, huo ni usaliti tosha inashangaza sana Dr mzima haoni hili. Watu wanaojua historia ya vita vya Rwanda vilivyomuingiza Kagame madaraka wanaojua fika nini kilifanyika kuweka askali katika morali ya ushindi baada ya Mkuu wa operation hiyo kufariki mwishoni kabisa wakati bado kidogo wapate ushindi. Kitila ni msomi anajua kwanini Mwl. Nyerere aliongoza TANU wakati wa mapambano ya Uhuru na hata baada ya Uhuru, sio kuwa hakuwepo mwenye kumshinda kiakili na ki mawazo.

Hakuna mjinga atakaye waelewa bora mnyamaze mnaweza kurudisha heshima yenu kwa ukimia.
 
Dr. Mkumbo ungejiuzulu uanachama na kusema haya basi kusingekuwa na shaka yoyote ya kwamba una syndrome ya "sizitaki mbichi hizi", lakini kwa sasa siwezi kusema kwamba huna syndrome hii.

Kwa nini uling'ang'ania chama kibovu hiki mpaka ukafukuzwa?
 
.kwani ni kosa zitto kutaka kuwa kiongozi Wa chademA au kwa vile anatoka kigoma name cha in cha familia yw kaskazini? A cha kuwalaz akili watanzani kwa mapenzi yako kwa viongozi Wa cha.dema
 
Dr Kitila,

Kwanza salaam mkuu wangu na hakika nimekusoma vizuri na kukuelewa tofauti na wengine waloyasoma maelezo yako na kuyatafsiri kama Biblia. Na wala jambo hili lisikuponze maana asili yetu sisi wote humu ni WADANGANYIKA wale tunaofikiri tunajua kumbe maamuma tu.

Mimi nimeshasema maadam vyama vyetu vya kisiasa ukiacha CCM tu, vimeanzishwa na mtu mmoja, akawakusanya kundi la watu na kuwaomba washirikiane naye kuunda chama basi bila shaka vyama hivi vyote ni mali ya mtu sii vyama vya kisiasa. Na ndio maana hata wadanganyika wenyewe ukiwauliza - Hivi ukimwondoa Mrema huko TLP bado kutakuwa na TLP? - sidhani kama wanalo jawabu. Na hofu hii ndio inayowatisha wengi japo hawasemi - Ukweli ni kwamba Chadema ya leo pasipo Dr.Slaa hakuna chama! ni mfumo hodhi wa kiimla sio kihafidhina kama anavyodai Zitto.

Na kibaya zaidi wengi wamefikia hata kuipima ELIMU yako kutokana na bandiko hili pasipo kujua kwamba ELIMU ya mtu sii utabiri bali ina deal na hali halisi, na wala elimu haiondoi subra bali mwenye subra ndiye hutumia elimu yake kutafuta ufumbuzi wa swala lilipo mezani. Mila na desturi yetu wadanganyika siku zote ni kwamba kila tatizo lazima kuna mkono wa mtu na Mungu akipenda hata liwe la kishetani. Na kwa mwenye kufanya mabaya, shahidi yeyote wa mabaya hayo huitwa mwongo na hasidi wakidai mwenye ushahidi awe wa kwanz akurusha jiwe!

Mkuu wangu wakati wa Yesu wale watu waloshndwa kumpiga mawe Magdalena walijua kwamba yeyote atakaye yupa jiwe la kwnaza lazima iwe yeye kisha tembea naye maana huo Umalaya wake ameujua vipi?. Na ndio yanayotukuta hapa. Tumeibiwa toka Richmond na walosema wizi huo (wa kwanza kurusha jiwe)wameonekana wafikitini. Jirani yako akiwa muuza unga, ukiita Polisi wewe ndio mwongo na hasidi hivyo utachukiwa mtaa mzima maana fisadi hilo hupeleka kilo ya nyama kwa majirani. Ukimshutumu mtu anaiba TRA ama benki kuu basi wewe una hiyana na wivu. Tumeyaona toka enzi za Rodi Rajpa, kina Yona, Mramba, Mkapa na hata Dr.Slaa na list of shame ambao hadi leo hii wako mtaani wanatesa. Wale walokuwa na kihelehele cha kuitafuta haki na sheria ndio wachawi wenyewe.

Kwa hiyo usishangae wala kusema kwa nini watu hawanielewi maana kuna ukweli mkubwa kwamba wapo watu walifumbwa macho hawaoni japo wanaona, hawasikii japo wana masikio hata kama ukweli upo mbele yao. Hivyo, basi maadam tumeisha amini kwamba kuna father Christmas anayepaa na swala kuleta zawadi, basi acha waendelee kusuburi usiwakatishe tumaini wale walojengewa imani hiyo!
 
Comrade Mkandala salaam,

Tunachokitafuta Tanzania ni check and balance, hii ndio itazalisha utawala bora, kwangu mimi ni ukweli usiopingika binadamu bila sheria atakuwa mbaya tu, binadamu bina mipaka ni kichaa.

Tunachohitaji kwa sasa ni kujenga chama ambacho kitatoa ushindani wa kweli na CCM ili kubanana katika utendaji bila kuogopana, na ili kufikia hapo lazima vyama vibadilishane madaraka ili kutoa hii hali ya umangimeza. katika safari kunahitajika uvumilivu na umakini wa hali ya juu. Bado Tanzani hakuna demokrasia pana kama watu wanavyosema, ila inakua na tutafika.

Mkuu wangu hata TAA, ilianzishwa na mtu na kuomba wengine waunge mkono then TANU, CCM. Ni swala la muda tu CDM ilianzishwa na waasisi zaidi ya 20 ila leo wapo 5 tu hai, iko siku vyama vyote waasisi wake ama hawatakuwepo madarakani ama watakuwa wamezeeka na kufa. Je mnataka hizi nguvu tuziuewe kwasababu lilikuwa wazo la mtu mmoja na wengi sasa wanashiriki nakumiliki hiki chama.?

CDM inakua na kujitanua kila mwaka, sasa ipo kwenye madaraka kwenye majimbo, ina wabunge zaidi ya 20 wakuchaguliwa na madiwani wengi tu. Hawa wote wamechaguliwa na watanzania wanaoamini chama na wagombea wao. Taasisi kubwa kama CDM lazima ipitie vipindi. Nakumbuka ANC ilipitia vipindi vigumu sana na ilianzishwa na wazo la mtu mmoja.

Demokrasia ni kujifunza na demokrasia ni kukubaliana na wengi, na kwa hili ndipo kasheshe inapozuka wengi wanaweza kuwa hawapo sahihi au sahihi ni kama kuchagua chakula kwa kura.

Ninaamini kabisa CDM wanademokrasia pana kuliko vyama vingi vya siasa TZ na CCM combine. Changamoto zipo na zitaendelea kuwepo. Kuwajibishana ni kutengeneza std ili asije kuogopwa mtu siku za usoni.

Kuendela kulia na waasisi ni sawa na baadhi ya watu mpaka leo wanamlaumu Nyerere kwa maisha yao kuwa magumu he is gone 20 years ago and dead 13 years ago.

Tutafika, naowaomba waliadhirika na vurugu hizi wakubali matokeo lazima chama kisonge mbele.
 
kama mlitengeneza mkakati wa kuhakikisha mtu mmoja tu ndie anaekuwa kiongozi, demokrasia mnayopigia kelele inasimamia wapi!?

kama kweli wewe ni Dr na una intelectual mind na si mnafiki tuambie faida na hasara za mtu mmoja kuwa na network binafsi sambamba na ya chama kuanzia tawi hadi taifa!? kwako hii ndio demokrasia na kujenga chama!?
 
.kwani ni kosa zitto kutaka kuwa kiongozi Wa chademA au kwa vile anatoka kigoma name cha in cha familia yw kaskazini? A cha kuwalaz akili watanzani kwa mapenzi yako kwa viongozi Wa cha.dema

uenyekiti wa hila ni mapunguani tu ndio watakaotoa hiyo fursa ukiacha mapungufu lukuki ya uaminifu aliyonayo

Dr Kitila aliandika mkakati na wenzake na kuibua tuhuma za uongo ili kudhohofisha uongozi uliopo... alipoitwa CC alipewa ushahidi akaishia kutoa macho tu..

atuambie kwanini walipotosha watu kuhusu katiba kunyofolewa na mengine kibao! lengo likikuwa nini!?
 
Huyu kitila naona anajichanganya tu,msomi unapokubali kua msaliti kwa maslahi yako binafsi unakua useless na haufai hata kidogo, ni wajinga tu ndio watakao kuelewa dr kitila,umesha poteza vision kitila.....GO TO HeLL
 
Hongera sana Kitila, na wewe ni shujaa ,tusubirie madhala ya kuwanyanyaseni na ndipo watakapotambua nia mbaya ya MBOWE juu ya chama
 
Kwa upande wa CDM nimegundua mashabiki binafsi ni wengi kuliko wanachama wenye kadi waliotayari kukiona chama chao kinasonga mbele, kosa hasa la kina Dr Kitila ni nini? Kuweka mikakati ya kukabiliana na matarajio ya ndoto yako ni kosa?.nini maana ya democrasia?.tuachane na uongozi kandamizi kwa faida binafsi.
 
Dr alipoingia CHADEMA aliapa kuwa ataifuata,kuitetea na kuilinda katiba ya chama hicho. Hayo aliyoyafanya yeye na wenzake yametafsiriwa kama makosa ndani ya katiba na adhabu yake ya juu ni kufukuzwa uanachama. Mi naona kama anatapatapa tu. Kama mmeshaunda chama cha siasa,leteni sera zenu watakaovutiwa watajiunga kwa hiari yao. Sio kujaribu kuwaaminisha watu uongo.
 
Back
Top Bottom