Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Namuonea huruma Kitila na wenzake, wanatia aibu hata elimu yao pia wameitia aibu kuu. Wameshindwa kujua malengo ya chama chao na hata sababu ya kuwa Upinzani. Kitu ambacho hata mtoto wangu wa Darasa la kwanza analielezea vizuri. Huruma yangu ipo katika kona waliyonaswa tena vijana, alafu wasomi, ushauri kwao ni kukaa kimia Jamii iwasahau na wasirudi tena kwenye siasa. Waliingia kwenye mtego bila kujua wakijua ni Misaada ya kawaida ya kibinadamu mbaya zaidi walinashwa hata kabla hawajua kuwa watalazimishwa kufanya wasiyoyapenda na hawata kuwa na jinsi maana tayari wameneswa tunduni, wale Jamaa ni hatari ndio fani yao wapo makini na wanatumia akili nyingi sana, kama una akili za kalatasi huwezi kujua unapoperekwa maana mngelijua msingekubali kwa namna ninavyowajua Mwl. Kitila na mm.

Hakuna msomi aliye elimika ambaye hasingejua kuwa kwasasa priority nikuondoa CCM kwanza hata kama inafanyika bila chama kuwa na Mwenyekiti au hata kama Mwenyekiti aliopo anamapungufu ya aina yoyote achilia mbali upuuzi wanaoeleza sasa. Maneno ya Kitila na utetezi anaotoa ukilinganisha na umuhimu wa jambo lenyewe unaletashaka kama kweli ni Dr. Huwezi kuongelea kubadili Mkuu wa majeshi wakati mpo mstari wa Mbele vitani tena wakati ambapo umoja unahitajika ili kushinda vita husika, huo ni usaliti tosha inashangaza sana Dr mzima haoni hili. Watu wanaojua historia ya vita vya Rwanda vilivyomuingiza Kagame madaraka wanaojua fika nini kilifanyika kuweka askali katika morali ya ushindi baada ya Mkuu wa operation hiyo kufariki mwishoni kabisa wakati bado kidogo wapate ushindi. Kitila ni msomi anajua kwanini Mwl. Nyerere aliongoza TANU wakati wa mapambano ya Uhuru na hata baada ya Uhuru, sio kuwa hakuwepo mwenye kumshinda kiakili na ki mawazo.

Hakuna mjinga atakaye waelewa bora mnyamaze mnaweza kurudisha heshima yenu kwa ukimia.

Well said!!!
 
Mr Mkumbo ww ni msomi wa hali ya juu kabisa, unatakiwa kutoa mchango nn kifanyike na c kukiponda chama kiani, Chama ni taasisi na c mtu. Mlichokifanya hakikuzingatia katiba! Alafu ww ni mdau kwenye tatizo husika, kama yaliyowakuta CUF na NCCR yaani Kafulila na Ahamed Rashid, mbona huwasemi hawa? Hivyo basi ungeandika "tutafute mbadala wa ccm,cdm.cuf na nccr! Kuwa mkweli usiwe bias. Toa mchango wako wajumla nn kifanyike kukuza upinzani na kuepuka migogoro. Ulafi wa madaraka uliwaponza. Hakuna cha mgawanyiko cdm.
 
Hata mkiunda chama kipya kama nyie ni wasaliti mtaendelea kusalitiana tu.
 
Niseme tuu kuwa sikushangazwa na DR.Kitila kuandaa na kuhariri huo waraka anautetea leo bado maana nilikuwa najiuliza,
1.Hivi huyu jamaa mbona ni mtumishi wa umma lakini ni kiongozi wa kisiasa tena waziwazi,
2.Kiongozi wa kisiasa tena wa upinzani anapandishwa cheo na kuwa Dean of faculty of Education,how is it possible?
3.Kuna tetesi kuwa undergraduate GPA ni 2nd lower class,kama ndivyo inakuaje aruhusiwe kufundisha chuo kikuu?
NB.1.Kwa kosa moja tuu la kuwahujumu na kukihujumu chama Singida mjini na Musoma Vijijini Zitto alistahili adhabu kali sana hata kufukuzwa uanachama
NB 2.Dr Kitila sio mtu makini kama anavyotaka tumuone,alisema watu makini hawajiungi na siasa ilhali yy tayari alikuwa kiongozi
NB3.DR.Kitila amekuwa mfuasi wa Zitto siku nyingi na aache kutunyoshea kidole ati tunafuata uongozi na si chama
 
Mbona Dr mwenyewe ni mshabiki wa zito.. Kutufundisha kutokuwa washabiki wa viongozi hali wewe umeonyesha kwa uwazi mkubwa kuwa ni mshabiki wa kiongozi fulani tutaelewa kweli hilo somo.. Ubiri unachoishi

Umeniwahi,

Dr Kitila nafikiri hajielewi. Mwenyewe anashabiki mtu. Vikao wanafanya usiku mtu wao apite kama sio unafiki nini ?
 
Mkumbo, umedokeza mambo muhimu(nyeti) sana, lakini pamoja na huja zako za kutaka kuwazindua Watanzani hasa sie wafuasi na mashabiki wa Chadema, lakini aliyeturoga hafahamiki kama ni nani na yu hai au kesha kufa?!

Nilivyo kuelewa ni kwamba mangi machafu yapo vifuani mwa watu na hata weye mwenyewe pana baadhi unayo, lakini kwa sababu issue inakuhusu waogopa/wachelea mashabiki tulivyokaririshwa tutakupinga bila hata kusoma au kutafakari kwa undani uloyaeka wazi na si kukutizama weye kama Mkumbo!

Tusubiri mziki huu naami.i mwisho utapatikana tuu!, na hapo ndo tutajua wenye kushikiwa akili na wenye kuchambua mambo.
 
"Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA"-Dr. Kitila.

Hii ni statement fupi lakini imebeba ujumbe mpana na mzito sana katika mtazamo wa siasa za Tanzania.

Sijashangazwa na hii sentensi yake bali nimeshangazwa na ujumbe uliopo kwenye article yake kuhusu uendeshaji wa CHADEMA. Ninawaza na kujiuliza. Kama mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kwa muda mrefu hawezi kufahamu mzizi au kiini cha uendeshaji wa chama mpaka pale alipojaribu kuutingisha mwenyewe, itakuwaje hawa watu wengine wengi wanaojiita wapenzi na wanachama lakini hawafahamu hata ofisi za chama zilipo achilia mbali katiba na vikao vya chama.

Kwa andiko lake hili, inanipelekea kutambua kuwa kuna uwezekano mkubwa kabisa kuna watu ndani ya CHADEMA wanaodai ni wapigania ukombozi lakini kiuhalisia siyo wakombozi na wako ndani ya CHADEMA kwa sababu tu ya maslahi yao binafsi na maslahi hayo yanawafunga midomo katika kutingisha utendeshaji wa chama. Hawa ni wanafiki wa kupindukia.

Kuna wanazi wa CHADEMA walikuwa wanampa sifa Dr. Kitila huku wakidai kuwa ameamua kukaa kimya kwa sababu ana hekima na busara. Hawakufahamu kile wajuvi wa mambo wanasema, "If you see a lion that's been soaked in rain, do not mistake it for a cat".

Well, ameanza kufunguka na anafunguka na hoja ambazo hazitaki majibu ya mlengo wa kitoto.

Ni kweli usemalo, wapo wengi ndani ya CDM. Wengine wapo kwa kazi maalum ya kuiua Cdm. ..cladded in sheep skin, but deadly foxes
 
Umeniwahi,

Dr Kitila nafikiri hajielewi. Mwenyewe anashabiki mtu. Vikao wanafanya usiku mtu wao apite kama sio unafiki nini ?

Keshasema yeye ni mjinga na kweli ni mjinga mwaacheni apumzike na kuangalia chama chao mbadala, namwonea huruma anaposema eti wanachama watamfuata ZZK...Never on earth Mr Kitila bali ni sahihi kama ungesema nyie mliokuwa mnarambishwa vijisenti vya CCM bila aibu kupitia ZZK hao ndio mtakaomfuata huko atakakoishia Zitto wenu na twawatakia safari njema huku mtuachie CDM imara
 
Sitegemei mke alieachika kumsifu mme wake aliemuacha. Pia siasa za tz zinatakiwa kuepuka waoga wanaojipa majina ya m1,m2 na m3
 
Huyu Ndg. Kitila Mkumbo; anatafuta huruma ya wa Tanzania, kwanza ameidhalilisha sana hicho kinachoitwa (u Dr) sikutegemea yeye na kisomo chote hicho angeshiriki mkakati haramu ndani ya chama bila kufuata taratibu,kanuni na misingi ya chama. Hapa anataka tuamini kuwa njama na mkakati wao ulikua sahihi? Kukifananisha nccr ya enzi hizo na CDM ya sasa; kuwa akifukuzwa Zito, CDM itakufa....! Atasubiri milele. Hivi hawa wanaojiita wasomi wameisaiaje Taifa letu?
 
Hata mkiunda chama kipya kama nyie ni wasaliti mtaendelea kusalitiana tu.

kamanda acha kukaririshwa vibaya, hakuna cha usaliti wala nn ni woga wa demokrasa wa mzinzi mbowe na vibaraka wake tuuu!!!!!!
 
Mkumbo, umedokeza mambo muhimu(nyeti) sana, lakini pamoja na huja zako za kutaka kuwazindua Watanzani hasa sie wafuasi na mashabiki wa Chadema, lakini aliyeturoga hafahamiki kama ni nani na yu hai au kesha kufa?!

Nilivyo kuelewa ni kwamba mangi machafu yapo vifuani mwa watu na hata weye mwenyewe pana baadhi unayo, lakini kwa sababu issue inakuhusu waogopa/wachelea mashabiki tulivyokaririshwa tutakupinga bila hata kusoma au kutafakari kwa undani uloyaeka wazi na si kukutizama weye kama Mkumbo!

Tusubiri mziki huu naami.i mwisho utapatikana tuu!, na hapo ndo tutajua wenye kushikiwa akili na wenye kuchambua mambo.
Mkuu wabara

Bahati mbaya sana wafuasi wa Chadema wengi hawajitambui kabisa sijui kwa nini watu wamekuwa na tabia za nyumbu.
 
Last edited by a moderator:
Hadi sasa zitto ni kama keshatimuliwa,mbona mashabiki wake hawaondoki kama wapo? Au ndo yaleyale ya shuleni ambapo mwanafunzi akishatimuliwa wafuasi wake wanaskitika siku 2 na kumsahau? Zitto na nyie mamluki wake mmeshasahaulika cdm na makamanda tunaendelea na CDM NI MSINGI kama kawa.Alikuwa wapi kuyasema hayo ndani ya vikao? Au hakujua wajibu wake kama mjumbe wa kamati kuu? Na ingependeza kama angetujuza zile laki 2 alizokuwa akilipwa na MM zilikuwa zinatoka wapi na kwa malengo yapi? hata hivyo kauli zake hizi tulizitarajia kwani kila mfa maji lazima atapetape!
 
Niseme tuu kuwa sikushangazwa na DR.Kitila kuandaa na kuhariri huo waraka anautetea leo bado maana nilikuwa najiuliza,
1.Hivi huyu jamaa mbona ni mtumishi wa umma lakini ni kiongozi wa kisiasa tena waziwazi,
2.Kiongozi wa kisiasa tena wa upinzani anapandishwa cheo na kuwa Dean of faculty of Education,how is it possible?
3.Kuna tetesi kuwa undergraduate GPA ni 2nd lower class,kama ndivyo inakuaje aruhusiwe kufundisha chuo kikuu?
NB.1.Kwa kosa moja tuu la kuwahujumu na kukihujumu chama Singida mjini na Musoma Vijijini Zitto alistahili adhabu kali sana hata kufukuzwa uanachama
NB 2.Dr Kitila sio mtu makini kama anavyotaka tumuone,alisema watu makini hawajiungi na siasa ilhali yy tayari alikuwa kiongozi
NB3.DR.Kitila amekuwa mfuasi wa Zitto siku nyingi na aache kutunyoshea kidole ati tunafuata uongozi na si chama

kama ni kuhujumu chama mbowe naye ameajwa, mbona chama kipo kimya kuhusu tuhuma zake - tena alikaririwa akikiri kwamba kosa si kuchukua pesa kwa ccm, hoja ni umezitumia kwa shughuli gani!!
 
kamanda acha kukaririshwa vibaya, hakuna cha usaliti wala nn ni woga wa demokrasa wa mzinzi mbowe na vibaraka wake tuuu!!!!!!

Lazima tujiulize,chanzo cha pesa za kujenga mtandao wao wa ushindi kuanzia mawilayani kwa mujibu wa waraka kilikuwa ni kipi? ni CCM au TISS?
 
Nchi hini kwa kizazi hiki hapa Tanzania hadi itutukue miaka 50 tena ndipo tutajitambua.

Yaani pamoja na jitihada zote hizo za kubainishiwa kuwa pana kitu ndani ya chama lakini bado tu tumeshikilia misimamo isokuwa na tafiti?

Naona yanipasa kuamini akili zetu sawa na vichaa kushikilia kaa la moto.

Kikwete ana kazi sana kuongoza watu wa namna hini, astahiki pongezi kama kaifikisha nchi ya wapokwa na fikra kama niwaonavyo humu jukwaani.
 
Hadi sasa zitto ni kama keshatimuliwa,mbona mashabiki wake hawaondoki kama wapo? Au ndo yaleyale ya shuleni ambapo mwanafunzi akishatimuliwa wafuasi wake wanaskitika siku 2 na kumsahau? Zitto na nyie mamluki wake mmeshasahaulika cdm na makamanda tunaendelea na CDM NI MSINGI kama kawa.Alikuwa wapi kuyasema hayo ndani ya vikao? Au hakujua wajibu wake kama mjumbe wa kamati kuu? Na ingependeza kama angetujuza zile laki 2 alizokuwa akilipwa na MM zilikuwa zinatoka wapi na kwa malengo yapi? hata hivyo kauli zake hizi tulizitarajia kwani kila mfa maji lazima atapetape!

mie ni m1 wa team zito, sitoki chadema ila nabaki huko huko kuharibu tuuu, kwa sababu ya fitna zenu wahafidhina dhidi ya zito tutahakikisha tunamwaga mbona - bora maccm yaendelee kushika hatamu kuliko kuleta demokrasia ya kise.ge!!!
mlishindwa nn kuitisha uchaguzi mkuu ndaniya chama hatimaye kummwaga kwenye kura so long hakubaliki?!
 
Kitila nenda mwana kwendraa bwana acha kugeuka nyuma utageuka jiwe la chumvi bure. Umeona vyama ni CCM na chadema tu? Anza kuongelea CHAUMA
 
Back
Top Bottom