Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

kamanda umeandika ukweli hadi nimetetemeka !
Mkuu, huyu jamaa anasema bayana kuwa wanahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA, halafu akiambiwa kuwa lengo lake na Zitto lilikuwa ni kuua CHADEMA anajidai kubisha, hivi huyu jamaa ana PHD kweli!!!??, let me reserve my next word, nitapigwa Ban.
 
Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

ITACHUKUA muda kuelewa nini hasa kilichokikumba Chama Kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA) hadi kikashindwa kutatua mgogoro wa uongozi na hatimaye kuingiza nchi katika kizungumkuti cha kisiasa tunachokishuhudia leo. Binafsi, kama mmoja ya wahusika wakubwa katika mgogoro huu nimepokea pole, lawama, na kwa kiasi fulani hongera kwa kumudu kuhimili mikikimikiki iliyonikumba. Nimepokea pole kutokana na misukosuko niliyokumbana nayo katika sakata hili hadi kufikia kufukuzwa uanachama.

Hili si jambo dogo katika maisha ya binadamu. Kufukuzwa katika ushirika wowote ni jambo linalosababisha mfadhaiko na ninazipokea pole nilizopewa kwa unyenyekevu. Ninashukuru pia kwa wale walionitia moyo kwamba hii ni ajali katika safari na nisikate tamaa katika kutoa mchango wangu katika harakati za mabadiliko ya kisiasa nchini. Nami nawaahidi kwamba bado nipo imara na nitaendelea kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa hapa nchini, ndani na nje ya vyama vya siasa.

Walionipa lawama ni wale waliokubaliana mia kwa mia na viongozi wa CHADEMA waliotujengea taswira ya usaliti na uhaini kwa chama kwa uamuzi wetu wa kuandaa mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya CHADEMA; mkakati ambao ulikuja kutafsiriwa kama mkakati wa mapinduzi ya uongozi halali ndani ya chama. Na kwa kuwa viongozi waliongea sana na kulirudia jambo hili mara kwa mara, na kwa kuwa jamii yetu imejengwa katika kuamini uongozi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, wapo watu wengi ambao wameafikiana na tafsiri ya uongozi kwamba waraka ule ulikuwa ni mkakati wa mapinduzi na haukuwa na nia njema.

Wapo pia wananchi walionilaumu kama sehemu ya uongozi wa chama kwa kushindwa kuyamaliza mambo yetu ndani ya chama. Na wengine wamenilaumu kwa kutokuwa na moyo wa kubali yaishe, kwamba ningekubali kosa, hata kama siamini kwamba ni kosa, ili niombe msamaha yaishe, tusonge mbele. Natamani ingekuwa rahisi hivi na kwamba kungekuwa na nia njema kwa pande zote mbili, pengine neno samahani lingetosha kumaliza mgogoro huu.

Kwa sababu hii nazipokea lawama zote kwa unyenyekevu pia na ninakubali kwamba nimeshiriki, bila kutarajia, kusababisha usumbufu na kutatiza tamanio na tumaini la mamilioni ya Watanzania katika kuitoa CCM madarakani. Hata hivyo, taswira ya mgogoro huu ni pana kuliko inavyoonekana na pengine tutapata nafasi nzuri zaidi mbele kueleza vizuri kilichotokea katika maandishi ili watu waelewe na waielewe CHADEMA na viongozi wake vizuri, na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Sitarajii katika makala haya kukidhi kiu ya watu wengi wanaotamani kujua ukweli wa mgogoro ndani ya CHADEMA na pengine mimi siye mtu sahihi kueleza jambo hili kwa kuwa nina maslahi ya moja kwa moja. Ninatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa kulifanyia utafiti jambo hili na kuliweka bayana, ili watu wapate kujifunza na kulijua vizuri.

Nieleze tu kwamba mgogoro huu unatukumbusha kuwa, pamoja na kwamba tupo katika mfumo wa vyama vingi, bado tumeendelea kuukumbatia utamaduni wa chama kimoja. Kwa hiyo tuna vyama vingi vya siasa, lakini vyama hivi bado vinakumbatia utamaduni wa chama kimoja. Utamaduni wa chama kimoja ni utamaduni hodhi na wa kiimla. Uongozi katika utamaduni wa chama kimoja unapatikana kwa njia za uteule, ukiwahusisha watu wachache wateule. Utamaduni wa chama kimoja unakataa ushindani wa wazi. Katika utamaduni wa chama kimoja kutamani cheo fulani ndani ya chama na katika serikali ni ulafi na uroho wa madaraka. Ndio maana vyama vyetu vyote vikubwa hapa nchini vinakataza na kukemea wanachama wao kutamani na kutangaza nia ya kuwania madaraka makubwa kama vile urais au uenyeviti wa vyama.

Kutamani madaraka peke yake kunakatazwa, achilia mbali kuandaa mkakati wa kushinda nafasi unayoitamani. Na hili ndilo kosa tulilolifanya. Tulikuwa wajinga sana kudhani kwamba tupo katika mfumo na utamaduni wa vyama vingi ambapo mtu yupo huru kutamani cheo chochote katika chama chake cha siasa, na kutengeneza mikakati ya kushinda cheo hicho katika uchaguzi huru ndani ya chama. Tulikuwa wajinga kwa kujaribu kuachana na utamaduni wa kuvizia cheo na kujifanya hutaki wakati unataka.

‘Msaliti’ mwenzetu Zitto Kabwe alianza siku nyingi mwaka 2009 kwa uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama bila kupata ridhaa ya wazee wa chama. Alikuwa mjinga kudhani kwamba uongozi katika mfumo wa chama kimoja unapatikana kwa kujaza fomu na kuomba kura. Nami nilikuwa mjinga nisiyeelewa kwa kumuunga mkono na kumtaka asonge mbele katika nia yake hiyo. Hakuishia hapo, Zitto Kabwe akafanya ujinga mwingine kwa kutamani na hatimaye kutangaza kugombea urais kupitia chama chake. Huu nao ulikuwa ni usaliti kwa utamaduni wetu wa chama kimoja, kwa sababu katika utamaduni huu nafasi kama hii ni ya kiteule na wateule na wateuaji wapo.

Ninapokubali kupokea lawama katika kushiriki kusababisha mgogoro unaoendelea ndani ya CHADEMA, naomba nami niwarushie lawama tele wanachama na mashabiki wa chama hiki, na wapenda mabadiliko kwa ujumla. Nawarushia lawama wanachama na washabiki wa CHADEMA kwa kuwashabikia viongozi wa chama chao katika kukinyonga chama. Viongozi wa chama hiki wamefanya makosa mengi na makubwa hadi kusababisha mgogoro ufike ulipofika, lakini wanachama na mashabiki wa chama wamekuwa wakishwashangilia katika kila hatua walioifanya. Kwa hiyo lawama ya kwanza kwa wanachama na mashabiki ni pale walipokubali kugeuzwa kuwa mashabiki wa viongozi ndani ya chama badala ya kuwa mashabiki wa chama. Na kwa kuwa ushabiki hupofusha macho na akili, mashabiki wa viongozi hawatofautishi kati ya uongozi na chama. Ni kama vile wamedanganywa na viongozi waliopo na wakakubali kudanganyika, kwamba uongozi wa chama ndio chama, na chama ndio uongozi!

Ni kwa sababu ya ushabiki kwa viongozi, ndio maana ilifika mahala wanachama na mashabiki wa CHADEMA wakagawanyika katika makundi ya washabikia viongozi, na chama kikakosa watu wa kukishabikia na hapo kikajikuta hakina mlinzi.

Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama.

Mrema alipotimka, akatimka na mashabiki wake. Hicho ndicho kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Kuna watu wenye mtazamo finyu wanaamini kwamba chama hiki ni imara sana kwa sasa kiasi kwamba hata wakimfukuza Zitto kitaendelea kubaki imara. Wamesahau kwamba wamejenga ufuasi kwa viongozi, na hivyo watakapomfukuza Zitto atatimka na wafuasi wake na chama kitayumba. Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza, viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila. Lakini kwa sababu ya upofu unaoendelea unaotokana na kugubikwa na ulevi wa utamaduni wa chama kimoja kwa upande mmoja, na ulevi wa umaarufu kwa upande mwingine, hawatakubali yaishe nje ya Mahakama, na hatimaye watamfukuza Zitto. Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA.

Source:
Raia Mwema

umebakia kidampa
 
Mimi kiukweli hata kusoma sijasoma maelezo ya kitila,mimi namuona msaliti tu,pamoja na mh.zzk wote wasaliti
hata kama kulikuwepo matatizo ndani ya chama hawa watu na washirika wao walitakiwa kujua majira na nyakati.
Huu haukuwa muda wa kurumbana,ulikuwa muda wa kuimarisha chama kwanza kivuke afu ndo mambo mengine yafuate.
Chukulia unaendesha gari afu lipate slow puncture mbele ya kundi la simba,je utasimama ili uzibe pancha au utaendelea ili uvuke maadui hao kisha ndo uzibe pancha?
Kama kweli hawa watu hawakuwa na nia mbaya mbona walikataa kumtaja mwenzao m4? Hata majambazi huwa wako tayari kufa ili wasiwataje wenzao,
Binafsi nimekerwa na raia hawa na sioni tena sababu ya mtu kuwa msomi aliyetumia fedha ya walipakodi afu ndo anachanganya watanzania.
Mimi sina jina nchi hii ila mimi ni mmojawapo wa waliowapuuza mkumbo,zzk na wenzao akiwemo yule aliyejichubua akalazwa hospitali akadai ametekwa.
 
Kweli Kabisa Kitila na busara Zako, nakuheshimu sana mwalimu wangu, ila you are messing with people's minds. You could have used a little bit of your psychology. You are right, but where were you Mkumbo? This is a shame. Zitto ana tuhuma za mda mrefu ambazo hajakanusha tangu enzi za -----------, leo unaandae naye mkakati? People won't beleave you even if you are right. May be you had a big picture. God bless you.

true indeed....mkuu upo vizuri bravo!
 
Lawama zingine Dr. Kitila hujazitaja ni mmetumia muda mwingi kutengeneza mashabiki wa viongozi na mkaharibu mpaka JF na kulundika mamluki wa kuunga mkono hoja zenu humu ndani na sasa inakula kwenu.

Mmetumia muda mwingi kurusha mawe iCCM na utaratibu huo huo unakula kwenu Nyerere aliionya mkapuuzia dhambi za ubaguzi, mmebagua wapinzani wenzenu, mkabagua CCM, na sasa mnabaguana.

Mengine umeongea vizuri wahafidhina hawanaga ushauri bora wakaushieni wakati utawachukulia hatua.
 
Kwenye andiko hili la Mh Dr. Kitila nimeona kuna sehemu mbili au tatu kama kajichanganya

1.Anaposema uteuzi ni kwa wateule tu

na sio kama utaratibu ulivyo wa kujaza fomu na kurudisha

Swali katika waraka huo ambao waliuandaa je walipiga kura wenyewe wa nne kwa maana dr kitila,zitto,mwigamba na huyo mm2 na zito akashinda?au waliamua tu kumteua au alijiteua zito mwenyewe?

2.Chama hakijengi mfumo wa kushabikiwa ila viongozi wametengenexa mfumo wa kushabikiwa wao,viongozi

Je hapo haoni kama zitto nae amehusika kutengeneza mfumo huo mbona na yeye alikuwa na watu wanaomuunga mkono yeye kama yeye?

3.Hivi dr katiba yetu ya leo na hii rasimu ikipita umri wa MGOMEA URAIS UTAKUA NA NIKUANZIA MIAKA MINGAPI

JE zitto mungu akitujalia uhai atakua amefikisha umri halisi wa kupigiwa kura kama rais????

4.Hivi NCCR MAGEUZI NA CHADEMA mwaka 2010 waliopeperusha bendera ya kugombea urais walikuwa wenyeviti wa VYAMA VYAO????????

SHUKRANI MLETA UZI NA DR KITILA.

Kosa lingine ambalo mtaalam wetu huyu anapokosea ni pale anaposema: tabia ya chama kimoja ya kutokubali ushindani wa uwazi! Sasa kwenye sentensi hiyo hapo tu unaona ni kujichanganya kwa wazi kabisa. Je ni kweli ule waraka ulikuwa wa wazi? Kwa watu wasio wanasiasa kama sie, lakini tunatafakari,hapo katudanganya,kwa kuwa waraka wake Dr wetu huu haukuwa USHINDANI WA UWAZI, kwa kuwa haukuweka wazi kwa wanachama wenzao wote wa chama chao. Kwa hapo tu Dr umetuacha tujiulize ukweli wa makala yako hii!
 
Hii inatia shaka kwa manaoitwa wasomi wetu wa 'udaktari wa falsafa' huyu Km anaumizwa tu na Mgao aliopewa na ZZK hakumjua vizuri kwamba anatumika na yeye anatumiwa!
 
Kweli Kabisa Kitila na busara Zako, nakuheshimu sana mwalimu wangu, ila you are messing with people's minds. You could have used a little bit of your psychology. You are right, but where were you Mkumbo? This is a shame. Zitto ana tuhuma za mda mrefu ambazo hajakanusha tangu enzi za -----------, leo unaandae naye mkakati? People won't beleave you even if you are right. May be you had a big picture. God bless you.

Watanzania kama wewe ambao hudhani wna akili ndio ambazo mpaka leo mmelifikisha hili taifa hapa.

unasema Zito ana tuhuma za muda mrefu kuanzia lini? umeaminishwa uongo na umeuamini na kuumeza. huwezi kubadilika kusikia tofauti

umekuwa kama mwislamu au mkristoa ambaye ana amini dini za wazazi wake bila kuuliza

nina hakika, na wewe ni shahidi, katika tuhuma zote za zitto, sijawahi kuona ushahidi wowote wa madai yako
 
Mwigamba aliongea ukweli sana ! kwamba lengo lao lilikuwa kuupindua uongozi na kwamba kama wangeshindwa na ikajulikana basi Wangefukuzwa wao , na wala hakuwa shocked na kutimuliwa kwao maana anaamini walistahili ! Sasa hizi ngonjera za kitila hazina mashiko maana walikuwa pamoja na mwigamba .

Mkuu apo ndio pana nipa Shida sana, Dr mkumbo kafwata mkumbo, anazani watz ni wale wa miaka ya 95
 
Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

ITACHUKUA muda kuelewa nini hasa kilichokikumba Chama Kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA) hadi kikashindwa kutatua mgogoro wa uongozi na hatimaye kuingiza nchi katika kizungumkuti cha kisiasa tunachokishuhudia leo. Binafsi, kama mmoja ya wahusika wakubwa katika mgogoro huu nimepokea pole, lawama, na kwa kiasi fulani hongera kwa kumudu kuhimili mikikimikiki iliyonikumba. Nimepokea pole kutokana na misukosuko niliyokumbana nayo katika sakata hili hadi kufikia kufukuzwa uanachama.

Hili si jambo dogo katika maisha ya binadamu. Kufukuzwa katika ushirika wowote ni jambo linalosababisha mfadhaiko na ninazipokea pole nilizopewa kwa unyenyekevu. Ninashukuru pia kwa wale walionitia moyo kwamba hii ni ajali katika safari na nisikate tamaa katika kutoa mchango wangu katika harakati za mabadiliko ya kisiasa nchini. Nami nawaahidi kwamba bado nipo imara na nitaendelea kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa hapa nchini, ndani na nje ya vyama vya siasa.

Walionipa lawama ni wale waliokubaliana mia kwa mia na viongozi wa CHADEMA waliotujengea taswira ya usaliti na uhaini kwa chama kwa uamuzi wetu wa kuandaa mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya CHADEMA; mkakati ambao ulikuja kutafsiriwa kama mkakati wa mapinduzi ya uongozi halali ndani ya chama. Na kwa kuwa viongozi waliongea sana na kulirudia jambo hili mara kwa mara, na kwa kuwa jamii yetu imejengwa katika kuamini uongozi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, wapo watu wengi ambao wameafikiana na tafsiri ya uongozi kwamba waraka ule ulikuwa ni mkakati wa mapinduzi na haukuwa na nia njema.

Wapo pia wananchi walionilaumu kama sehemu ya uongozi wa chama kwa kushindwa kuyamaliza mambo yetu ndani ya chama. Na wengine wamenilaumu kwa kutokuwa na moyo wa kubali yaishe, kwamba ningekubali kosa, hata kama siamini kwamba ni kosa, ili niombe msamaha yaishe, tusonge mbele. Natamani ingekuwa rahisi hivi na kwamba kungekuwa na nia njema kwa pande zote mbili, pengine neno samahani lingetosha kumaliza mgogoro huu.

Kwa sababu hii nazipokea lawama zote kwa unyenyekevu pia na ninakubali kwamba nimeshiriki, bila kutarajia, kusababisha usumbufu na kutatiza tamanio na tumaini la mamilioni ya Watanzania katika kuitoa CCM madarakani. Hata hivyo, taswira ya mgogoro huu ni pana kuliko inavyoonekana na pengine tutapata nafasi nzuri zaidi mbele kueleza vizuri kilichotokea katika maandishi ili watu waelewe na waielewe CHADEMA na viongozi wake vizuri, na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Sitarajii katika makala haya kukidhi kiu ya watu wengi wanaotamani kujua ukweli wa mgogoro ndani ya CHADEMA na pengine mimi siye mtu sahihi kueleza jambo hili kwa kuwa nina maslahi ya moja kwa moja. Ninatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa kulifanyia utafiti jambo hili na kuliweka bayana, ili watu wapate kujifunza na kulijua vizuri.

Nieleze tu kwamba mgogoro huu unatukumbusha kuwa, pamoja na kwamba tupo katika mfumo wa vyama vingi, bado tumeendelea kuukumbatia utamaduni wa chama kimoja. Kwa hiyo tuna vyama vingi vya siasa, lakini vyama hivi bado vinakumbatia utamaduni wa chama kimoja. Utamaduni wa chama kimoja ni utamaduni hodhi na wa kiimla. Uongozi katika utamaduni wa chama kimoja unapatikana kwa njia za uteule, ukiwahusisha watu wachache wateule. Utamaduni wa chama kimoja unakataa ushindani wa wazi. Katika utamaduni wa chama kimoja kutamani cheo fulani ndani ya chama na katika serikali ni ulafi na uroho wa madaraka. Ndio maana vyama vyetu vyote vikubwa hapa nchini vinakataza na kukemea wanachama wao kutamani na kutangaza nia ya kuwania madaraka makubwa kama vile urais au uenyeviti wa vyama.

Kutamani madaraka peke yake kunakatazwa, achilia mbali kuandaa mkakati wa kushinda nafasi unayoitamani. Na hili ndilo kosa tulilolifanya. Tulikuwa wajinga sana kudhani kwamba tupo katika mfumo na utamaduni wa vyama vingi ambapo mtu yupo huru kutamani cheo chochote katika chama chake cha siasa, na kutengeneza mikakati ya kushinda cheo hicho katika uchaguzi huru ndani ya chama. Tulikuwa wajinga kwa kujaribu kuachana na utamaduni wa kuvizia cheo na kujifanya hutaki wakati unataka.

‘Msaliti' mwenzetu Zitto Kabwe alianza siku nyingi mwaka 2009 kwa uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama bila kupata ridhaa ya wazee wa chama. Alikuwa mjinga kudhani kwamba uongozi katika mfumo wa chama kimoja unapatikana kwa kujaza fomu na kuomba kura. Nami nilikuwa mjinga nisiyeelewa kwa kumuunga mkono na kumtaka asonge mbele katika nia yake hiyo. Hakuishia hapo, Zitto Kabwe akafanya ujinga mwingine kwa kutamani na hatimaye kutangaza kugombea urais kupitia chama chake. Huu nao ulikuwa ni usaliti kwa utamaduni wetu wa chama kimoja, kwa sababu katika utamaduni huu nafasi kama hii ni ya kiteule na wateule na wateuaji wapo.

Ninapokubali kupokea lawama katika kushiriki kusababisha mgogoro unaoendelea ndani ya CHADEMA, naomba nami niwarushie lawama tele wanachama na mashabiki wa chama hiki, na wapenda mabadiliko kwa ujumla. Nawarushia lawama wanachama na washabiki wa CHADEMA kwa kuwashabikia viongozi wa chama chao katika kukinyonga chama. Viongozi wa chama hiki wamefanya makosa mengi na makubwa hadi kusababisha mgogoro ufike ulipofika, lakini wanachama na mashabiki wa chama wamekuwa wakishwashangilia katika kila hatua walioifanya. Kwa hiyo lawama ya kwanza kwa wanachama na mashabiki ni pale walipokubali kugeuzwa kuwa mashabiki wa viongozi ndani ya chama badala ya kuwa mashabiki wa chama. Na kwa kuwa ushabiki hupofusha macho na akili, mashabiki wa viongozi hawatofautishi kati ya uongozi na chama. Ni kama vile wamedanganywa na viongozi waliopo na wakakubali kudanganyika, kwamba uongozi wa chama ndio chama, na chama ndio uongozi!

Ni kwa sababu ya ushabiki kwa viongozi, ndio maana ilifika mahala wanachama na mashabiki wa CHADEMA wakagawanyika katika makundi ya washabikia viongozi, na chama kikakosa watu wa kukishabikia na hapo kikajikuta hakina mlinzi.

Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama.

Mrema alipotimka, akatimka na mashabiki wake. Hicho ndicho kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Kuna watu wenye mtazamo finyu wanaamini kwamba chama hiki ni imara sana kwa sasa kiasi kwamba hata wakimfukuza Zitto kitaendelea kubaki imara. Wamesahau kwamba wamejenga ufuasi kwa viongozi, na hivyo watakapomfukuza Zitto atatimka na wafuasi wake na chama kitayumba. Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza, viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila. Lakini kwa sababu ya upofu unaoendelea unaotokana na kugubikwa na ulevi wa utamaduni wa chama kimoja kwa upande mmoja, na ulevi wa umaarufu kwa upande mwingine, hawatakubali yaishe nje ya Mahakama, na hatimaye watamfukuza Zitto. Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA.

Source:
Raia Mwema

Hii ni sawa na hadithi ya Sungura ya sizitaki hizi mbichi.Mtani wangu KM kajipange vizuri,but you've lost a golden chance,no second chance at all,what remain is "i ought have known'!.
 
ungekuwa na maana kama ungetueleza peza ulizokuwa unapewa na zito kila mara kupitia kwenye kwenye simu yako zilikuwa kwa kazi gani? na alikuwa anazipata wapi? hizo mishara mulikuwa mnapewa na zitto hiyo tu ndiyo watanzania wanataka kujua juu yako ili waamini maelezo yako hayo
 
Mshauri ajikite na kufundisha wanafunzi siasa hawezi huyu mchumia tumbo! Msomi wa PHD unafanya vitu ambavyo hata kijana aliyemaliza std 7 hawezi kuvifanya hafu sasa anajipangusa mdomo eti wanatafuta mbadala yaani watanzania kila siku wawe wanazungushwa na wanasiasa eti tunakuja na cham mbadala! Watu wanataka mabadiliko lakini siyo hayo wanayo wafikiria akina Mkumbo &Co

Kitila Mkumbo My all time favourite Lecturer.........
 
Kitila anaburuzwa na ZItto tu, namjua vizuri ni kilaza flani hivi. Kana uroho wa madaraka ile mbaya. Kana maneno mengi ndo maana kanaonekana kanajua kitu...kalisoma PCB pale Pugu kakapata ufaulu hafifu kakapita njia za panya kwenda chuo kusoma ungwini...ati nako kana PhD!
Zitto ni kama mlima kwa haka kajamaa..ndo maana anakadrg kwenye matope na ki PhD chake!
However, ni ka home boy kangu na nilikuwa mbele yake pale Pugu A-level.

Upuuzi,respond kwenye hoja..Albert Einstein alifail shule pia,Bill gates, na wengine wengi wakafanya mambo makubwa.And kama ni kahome boy kako si tufanyeje,mi jirani yangu...so what?attach hoja zake za kiubinafsi za kutokuitakia mema chadema, kujidai wanajua kuliko watanzania wengine,kuandaa agenda ya mabadiliko cha kuchafua viongozi wengine na hivyo kukipasua chama,
 
Kumbe ndio maana Yule mgonjwa wa akili anayeitwa Mwigulu Mchemba kasema U Dr wa Kitila Mkumbo ni wa kimagumushi leo naamini hajakosea japokuwa simfagilii Mwigulu sasa kalikologa na limemshinda kulizoa na sasa anatokwa na povu ati Chadema wayamalize kimya kimya na Zitto Kabwe ili chama kisijekuwa kama NCCR-Mageuzi teh teh teh hana lolote huyu njaa tu ndio inamsumbua ama kweli wasomi wa Bongo uchwara tu yaani hizi Dr na Proffesor wanaziokota wapi.Mtu umesababisha mwenyewe na sasa unatapatapa ati CHADEMA kimsamehe ZITTO what F****'22""##¤%¤&%&%& ck are you talking about you A''''''***S*****SSSSS Ho''''''****#%¤%&%/le so called Kitila Mkumbo
 
Watanzania kama wewe ambao hudhani wna akili ndio ambazo mpaka leo mmelifikisha hili taifa hapa.

unasema Zito ana tuhuma za muda mrefu kuanzia lini? umeaminishwa uongo na umeuamini na kuumeza. huwezi kubadilika kusikia tofauti

umekuwa kama mwislamu au mkristoa ambaye ana amini dini za wazazi wake bila kuuliza

nina hakika, na wewe ni shahidi, katika tuhuma zote za zitto, sijawahi kuona ushahidi wowote wa madai yako

hata mwenendo wake na kauli zake yinathibitisha kutumika kuhujumu cdm! tuhuma za kusambaza pesa kwa wale masalia hajawahi kuzikanusha na nadhani kwa kuhofia kuumbuliwa na akina ben saanane na wenzake! kumbuka andiko la mtela mwampamba hapa jf kutishia kumwaga ukweli wote kumhusu zitto kama ataendelea kujifanya hawatambui! unaweza kutuambia ilikuwaje mkutano wake na waandishi wa habari pale serena ukaratibiwa na lumumba fc? wasaliti ni wasaliti tu na lazima wote wafukuzwe wakapigie kelele zao za mfa mji magazetini!
 
"Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama".
Mrema wa mwaka 1995 usingeweza kumlinganisha na zzk wa sasa hata na wa miaka iliyopita kwani mrema alikuwa waziri aliyefanya kazi jina lake likavuma mpaka akapewa cheo cha waziri mkuu msaidizi ambacho hakuna aliyewahi kupewa baada ya mrema,naweza thubutu kusema mrema alikuwa maarufu kuliko NCCR miaka hiyo,sasa hapa umaarufu wa zzk dhidi ya CDM uko wapi? Je zzk aliifanya CDM ijulikana au CDM imemfanya zzk ajulikane?
Na kitendo cha kuandaa waraka wa siri kinaonyesha zzk akishika nchi atafanya kazi kwa majungu na woga wa kukosoa na kukemea hadharani,tatizo ambalo ndo linaikumba ccm,CDM kwa kuwafukuza hawa vinara hadharani wameonyesha uthubutu wao wa kuwagusa wenye makosa bila kujali vyeo vyao.
 
Back
Top Bottom