Dr.Kitila Mkumbo: Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

Kwa maoni yangu akina Kitila wanaweza wakawa ni matatizo yao lakini naamini kabisa uongozi wa chama ambacho mpaka majuzi tu nilidhani ni imara na umeiva kuchukua madaraka ya dola nilikosea sana!

Uongozi ambao umeshindwa kumaliza tatizo hili ktk hali ambayo wenye akili tutakubaliana na hatua zinachokuliwa hauna uwezo wa kupewa madaraka ya dola. Na kama hatutaki kuubadili uongozi wa aina hii basi December,2015 itakua kilio na visingizio vya kuibiwa kura!
 
PHD bongo ?kuna watu wanaiba mitihani kuanzia la Saba,form four,form six,hadi chuo kikuu na wanakuwa na vyeti na Madgee feki kichwani kwa Elimu hii hii unadhani kuna PHD ngapi Feki? Pia wapo wenye mbinu ya kukariri tu mpaka wanafaulu na kupata vyeti kwa ajili ya kuwafurahisha wazazi wao huku wakijua kichwani hamna kitu Hakuna Taaluma yeyote ile hapa Tz isiyokuwa na Magumashi na Rushwa ya ngono tuna wasomi feki chungu mzima Ndio Maana soko la Ajila limetawaliwa na wageni. Huu ushabiki wa huyu DR juu ya mbowe ni ushabiki wa inzi juu ya kidonda hatari na aina ya ushabiki huu unahatarisha Taaluma ya mtu Kwani pale Chadema Kuwa watu wanakerwa na vioja vya Mbowe lakini kwa Kuwa wanamwogopa sana imebaki Akili ya Kawaida kuwaongoza wanaojiita Wasomi na wanasheria
 
Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

ITACHUKUA muda kuelewa nini hasa kilichokikumba Chama Kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA) hadi kikashindwa kutatua mgogoro wa uongozi na hatimaye kuingiza nchi katika kizungumkuti cha kisiasa tunachokishuhudia leo. Binafsi, kama mmoja ya wahusika wakubwa katika mgogoro huu nimepokea pole, lawama, na kwa kiasi fulani hongera kwa kumudu kuhimili mikikimikiki iliyonikumba. Nimepokea pole kutokana na misukosuko niliyokumbana nayo katika sakata hili hadi kufikia kufukuzwa uanachama.

Hili si jambo dogo katika maisha ya binadamu. Kufukuzwa katika ushirika wowote ni jambo linalosababisha mfadhaiko na ninazipokea pole nilizopewa kwa unyenyekevu. Ninashukuru pia kwa wale walionitia moyo kwamba hii ni ajali katika safari na nisikate tamaa katika kutoa mchango wangu katika harakati za mabadiliko ya kisiasa nchini. Nami nawaahidi kwamba bado nipo imara na nitaendelea kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa hapa nchini, ndani na nje ya vyama vya siasa.

Walionipa lawama ni wale waliokubaliana mia kwa mia na viongozi wa CHADEMA waliotujengea taswira ya usaliti na uhaini kwa chama kwa uamuzi wetu wa kuandaa mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya CHADEMA; mkakati ambao ulikuja kutafsiriwa kama mkakati wa mapinduzi ya uongozi halali ndani ya chama. Na kwa kuwa viongozi waliongea sana na kulirudia jambo hili mara kwa mara, na kwa kuwa jamii yetu imejengwa katika kuamini uongozi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, wapo watu wengi ambao wameafikiana na tafsiri ya uongozi kwamba waraka ule ulikuwa ni mkakati wa mapinduzi na haukuwa na nia njema.

Wapo pia wananchi walionilaumu kama sehemu ya uongozi wa chama kwa kushindwa kuyamaliza mambo yetu ndani ya chama. Na wengine wamenilaumu kwa kutokuwa na moyo wa kubali yaishe, kwamba ningekubali kosa, hata kama siamini kwamba ni kosa, ili niombe msamaha yaishe, tusonge mbele. Natamani ingekuwa rahisi hivi na kwamba kungekuwa na nia njema kwa pande zote mbili, pengine neno samahani lingetosha kumaliza mgogoro huu.

Kwa sababu hii nazipokea lawama zote kwa unyenyekevu pia na ninakubali kwamba nimeshiriki, bila kutarajia, kusababisha usumbufu na kutatiza tamanio na tumaini la mamilioni ya Watanzania katika kuitoa CCM madarakani. Hata hivyo, taswira ya mgogoro huu ni pana kuliko inavyoonekana na pengine tutapata nafasi nzuri zaidi mbele kueleza vizuri kilichotokea katika maandishi ili watu waelewe na waielewe CHADEMA na viongozi wake vizuri, na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Sitarajii katika makala haya kukidhi kiu ya watu wengi wanaotamani kujua ukweli wa mgogoro ndani ya CHADEMA na pengine mimi siye mtu sahihi kueleza jambo hili kwa kuwa nina maslahi ya moja kwa moja. Ninatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa kulifanyia utafiti jambo hili na kuliweka bayana, ili watu wapate kujifunza na kulijua vizuri.

Nieleze tu kwamba mgogoro huu unatukumbusha kuwa, pamoja na kwamba tupo katika mfumo wa vyama vingi, bado tumeendelea kuukumbatia utamaduni wa chama kimoja. Kwa hiyo tuna vyama vingi vya siasa, lakini vyama hivi bado vinakumbatia utamaduni wa chama kimoja. Utamaduni wa chama kimoja ni utamaduni hodhi na wa kiimla. Uongozi katika utamaduni wa chama kimoja unapatikana kwa njia za uteule, ukiwahusisha watu wachache wateule. Utamaduni wa chama kimoja unakataa ushindani wa wazi. Katika utamaduni wa chama kimoja kutamani cheo fulani ndani ya chama na katika serikali ni ulafi na uroho wa madaraka. Ndio maana vyama vyetu vyote vikubwa hapa nchini vinakataza na kukemea wanachama wao kutamani na kutangaza nia ya kuwania madaraka makubwa kama vile urais au uenyeviti wa vyama.

Kutamani madaraka peke yake kunakatazwa, achilia mbali kuandaa mkakati wa kushinda nafasi unayoitamani. Na hili ndilo kosa tulilolifanya. Tulikuwa wajinga sana kudhani kwamba tupo katika mfumo na utamaduni wa vyama vingi ambapo mtu yupo huru kutamani cheo chochote katika chama chake cha siasa, na kutengeneza mikakati ya kushinda cheo hicho katika uchaguzi huru ndani ya chama. Tulikuwa wajinga kwa kujaribu kuachana na utamaduni wa kuvizia cheo na kujifanya hutaki wakati unataka.

‘Msaliti' mwenzetu Zitto Kabwe alianza siku nyingi mwaka 2009 kwa uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama bila kupata ridhaa ya wazee wa chama. Alikuwa mjinga kudhani kwamba uongozi katika mfumo wa chama kimoja unapatikana kwa kujaza fomu na kuomba kura. Nami nilikuwa mjinga nisiyeelewa kwa kumuunga mkono na kumtaka asonge mbele katika nia yake hiyo. Hakuishia hapo, Zitto Kabwe akafanya ujinga mwingine kwa kutamani na hatimaye kutangaza kugombea urais kupitia chama chake. Huu nao ulikuwa ni usaliti kwa utamaduni wetu wa chama kimoja, kwa sababu katika utamaduni huu nafasi kama hii ni ya kiteule na wateule na wateuaji wapo.

Ninapokubali kupokea lawama katika kushiriki kusababisha mgogoro unaoendelea ndani ya CHADEMA, naomba nami niwarushie lawama tele wanachama na mashabiki wa chama hiki, na wapenda mabadiliko kwa ujumla. Nawarushia lawama wanachama na washabiki wa CHADEMA kwa kuwashabikia viongozi wa chama chao katika kukinyonga chama. Viongozi wa chama hiki wamefanya makosa mengi na makubwa hadi kusababisha mgogoro ufike ulipofika, lakini wanachama na mashabiki wa chama wamekuwa wakishwashangilia katika kila hatua walioifanya. Kwa hiyo lawama ya kwanza kwa wanachama na mashabiki ni pale walipokubali kugeuzwa kuwa mashabiki wa viongozi ndani ya chama badala ya kuwa mashabiki wa chama. Na kwa kuwa ushabiki hupofusha macho na akili, mashabiki wa viongozi hawatofautishi kati ya uongozi na chama. Ni kama vile wamedanganywa na viongozi waliopo na wakakubali kudanganyika, kwamba uongozi wa chama ndio chama, na chama ndio uongozi!

Ni kwa sababu ya ushabiki kwa viongozi, ndio maana ilifika mahala wanachama na mashabiki wa CHADEMA wakagawanyika katika makundi ya washabikia viongozi, na chama kikakosa watu wa kukishabikia na hapo kikajikuta hakina mlinzi.

Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama.

Mrema alipotimka, akatimka na mashabiki wake. Hicho ndicho kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Kuna watu wenye mtazamo finyu wanaamini kwamba chama hiki ni imara sana kwa sasa kiasi kwamba hata wakimfukuza Zitto kitaendelea kubaki imara. Wamesahau kwamba wamejenga ufuasi kwa viongozi, na hivyo watakapomfukuza Zitto atatimka na wafuasi wake na chama kitayumba. Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza, viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila. Lakini kwa sababu ya upofu unaoendelea unaotokana na kugubikwa na ulevi wa utamaduni wa chama kimoja kwa upande mmoja, na ulevi wa umaarufu kwa upande mwingine, hawatakubali yaishe nje ya Mahakama, na hatimaye watamfukuza Zitto. Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA.

Source:
Raia Mwema

Hili ni changa la macho na blah blah tu. Wanasiasa wote mnatafuta ulaji tu na manufaa binafsi. Hamna lolote! When you see grown, seemingly "educated" men bickering like spiteful bitches then it gotta be all about cheddar and power.
 
ungekuwa na maana kama ungetueleza peza ulizokuwa unapewa na zito kila mara kupitia kwenye kwenye simu yako zilikuwa kwa kazi gani? na alikuwa anazipata wapi? hizo mishara mulikuwa mnapewa na zitto hiyo tu ndiyo watanzania wanataka kujua juu yako ili waamini maelezo yako hayo

Umesema kitu cha msingi sana kamanda,angetueleza zile laki 2 alizokuwa anapewa na zitto zilikuwa zinatoka wapi na kwa malengo yapi?
 
Asante saana dr. Itafamika tuuu!historia inatuanyesha kwa hiyo ni dhahiri yatatokea yaliyotokea kabla....
 
Nilifikiri kwamba kwakua wewe ni mkufunzi basi utakua na akili kubwa sana. Kumbe kuitwa Dr sio lazima kuwa na akili. My take sio kukudhalilisha ila nimekusikitikia sana.

Zaid hata mzee Ulimwengu naona wazi rais wetu mstaafu wa awam ya tatu hakua anakuonea kipindi cha nyuma ila utakua una shida kidogo. Kwa namna nilivyokuwa nakupa credit nimeshindwa kukuelewa haswa kuwa na upande ambao unaona wazi walivunja katiba. Si bure hata wewe unaweza kupindua nchi kwa ushabiki wa kijinga.

Tutasoma gazeti la ----- lenye makala za kuelimisha. Kitila wewe kuwa makin mwenzio ni mwanasiasa wewe ni mkufunzi wanafunzi watakudharau na mwishowe utaanza kuvaa mapama na sun glases kwakuficha sura. Uongozi haulazimishwi bali unakujaga wenyewe automatically.
 
mkumbo amefuwata mkumbo na kuwa kitoroli wa zitto ni aibu na fedhea wa wasomi na pia kwa elimu yako.
 
Kwa maoni yangu akina Kitila wanaweza wakawa ni matatizo yao lakini naamini kabisa uongozi wa chama ambacho mpaka majuzi tu nilidhani ni imara na umeiva kuchukua madaraka ya dola nilikosea sana!

Uongozi ambao umeshindwa kumaliza tatizo hili ktk hali ambayo wenye akili tutakubaliana na hatua zinachokuliwa hauna uwezo wa kupewa madaraka ya dola. Na kama hatutaki kuubadili uongozi wa aina hii basi December,2015 itakua kilio na visingizio vya kuibiwa kura!

Umejaa ushabiki wa kipuuzi,ulitaka msaliti aachwe ndipo uiamini cdm? dawa ya wasaliti ni kuwatimua tu! toka apigwe chini MM vibaraka vyake na magamba hawalali,wanaweweseka ile mbaya!!!
 
PHD bongo ?kuna watu wanaiba mitihani kuanzia la Saba,form four,form six,hadi chuo kikuu na wanakuwa na vyeti na Madgee feki kichwani kwa Elimu hii hii unadhani kuna PHD ngapi Feki? Pia wapo wenye mbinu ya kukariri tu mpaka wanafaulu na kupata vyeti kwa ajili ya kuwafurahisha wazazi wao huku wakijua kichwani hamna kitu Hakuna Taaluma yeyote ile hapa Tz isiyokuwa na Magumashi na Rushwa ya ngono tuna wasomi feki chungu mzima Ndio Maana soko la Ajila limetawaliwa na wageni. Huu ushabiki wa huyu DR juu ya mbowe ni ushabiki wa inzi juu ya kidonda hatari na aina ya ushabiki huu unahatarisha Taaluma ya mtu Kwani pale Chadema Kuwa watu wanakerwa na vioja vya Mbowe lakini kwa Kuwa wanamwogopa sana imebaki Akili ya Kawaida kuwaongoza wanaojiita Wasomi na wanasheria

wezi wa mitihan, mfano mzuri ni J Makamba pale Galanos
 
Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA

ITACHUKUA muda kuelewa nini hasa kilichokikumba Chama Kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA) hadi kikashindwa kutatua mgogoro wa uongozi na hatimaye kuingiza nchi katika kizungumkuti cha kisiasa tunachokishuhudia leo. Binafsi, kama mmoja ya wahusika wakubwa katika mgogoro huu nimepokea pole, lawama, na kwa kiasi fulani hongera kwa kumudu kuhimili mikikimikiki iliyonikumba. Nimepokea pole kutokana na misukosuko niliyokumbana nayo katika sakata hili hadi kufikia kufukuzwa uanachama.

Hili si jambo dogo katika maisha ya binadamu. Kufukuzwa katika ushirika wowote ni jambo linalosababisha mfadhaiko na ninazipokea pole nilizopewa kwa unyenyekevu. Ninashukuru pia kwa wale walionitia moyo kwamba hii ni ajali katika safari na nisikate tamaa katika kutoa mchango wangu katika harakati za mabadiliko ya kisiasa nchini. Nami nawaahidi kwamba bado nipo imara na nitaendelea kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa hapa nchini, ndani na nje ya vyama vya siasa.

Walionipa lawama ni wale waliokubaliana mia kwa mia na viongozi wa CHADEMA waliotujengea taswira ya usaliti na uhaini kwa chama kwa uamuzi wetu wa kuandaa mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya CHADEMA; mkakati ambao ulikuja kutafsiriwa kama mkakati wa mapinduzi ya uongozi halali ndani ya chama. Na kwa kuwa viongozi waliongea sana na kulirudia jambo hili mara kwa mara, na kwa kuwa jamii yetu imejengwa katika kuamini uongozi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, wapo watu wengi ambao wameafikiana na tafsiri ya uongozi kwamba waraka ule ulikuwa ni mkakati wa mapinduzi na haukuwa na nia njema.

Wapo pia wananchi walionilaumu kama sehemu ya uongozi wa chama kwa kushindwa kuyamaliza mambo yetu ndani ya chama. Na wengine wamenilaumu kwa kutokuwa na moyo wa kubali yaishe, kwamba ningekubali kosa, hata kama siamini kwamba ni kosa, ili niombe msamaha yaishe, tusonge mbele. Natamani ingekuwa rahisi hivi na kwamba kungekuwa na nia njema kwa pande zote mbili, pengine neno samahani lingetosha kumaliza mgogoro huu.

Kwa sababu hii nazipokea lawama zote kwa unyenyekevu pia na ninakubali kwamba nimeshiriki, bila kutarajia, kusababisha usumbufu na kutatiza tamanio na tumaini la mamilioni ya Watanzania katika kuitoa CCM madarakani. Hata hivyo, taswira ya mgogoro huu ni pana kuliko inavyoonekana na pengine tutapata nafasi nzuri zaidi mbele kueleza vizuri kilichotokea katika maandishi ili watu waelewe na waielewe CHADEMA na viongozi wake vizuri, na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Sitarajii katika makala haya kukidhi kiu ya watu wengi wanaotamani kujua ukweli wa mgogoro ndani ya CHADEMA na pengine mimi siye mtu sahihi kueleza jambo hili kwa kuwa nina maslahi ya moja kwa moja. Ninatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa kulifanyia utafiti jambo hili na kuliweka bayana, ili watu wapate kujifunza na kulijua vizuri.

Nieleze tu kwamba mgogoro huu unatukumbusha kuwa, pamoja na kwamba tupo katika mfumo wa vyama vingi, bado tumeendelea kuukumbatia utamaduni wa chama kimoja. Kwa hiyo tuna vyama vingi vya siasa, lakini vyama hivi bado vinakumbatia utamaduni wa chama kimoja. Utamaduni wa chama kimoja ni utamaduni hodhi na wa kiimla. Uongozi katika utamaduni wa chama kimoja unapatikana kwa njia za uteule, ukiwahusisha watu wachache wateule. Utamaduni wa chama kimoja unakataa ushindani wa wazi. Katika utamaduni wa chama kimoja kutamani cheo fulani ndani ya chama na katika serikali ni ulafi na uroho wa madaraka. Ndio maana vyama vyetu vyote vikubwa hapa nchini vinakataza na kukemea wanachama wao kutamani na kutangaza nia ya kuwania madaraka makubwa kama vile urais au uenyeviti wa vyama.

Kutamani madaraka peke yake kunakatazwa, achilia mbali kuandaa mkakati wa kushinda nafasi unayoitamani. Na hili ndilo kosa tulilolifanya. Tulikuwa wajinga sana kudhani kwamba tupo katika mfumo na utamaduni wa vyama vingi ambapo mtu yupo huru kutamani cheo chochote katika chama chake cha siasa, na kutengeneza mikakati ya kushinda cheo hicho katika uchaguzi huru ndani ya chama. Tulikuwa wajinga kwa kujaribu kuachana na utamaduni wa kuvizia cheo na kujifanya hutaki wakati unataka.

‘Msaliti’ mwenzetu Zitto Kabwe alianza siku nyingi mwaka 2009 kwa uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama bila kupata ridhaa ya wazee wa chama. Alikuwa mjinga kudhani kwamba uongozi katika mfumo wa chama kimoja unapatikana kwa kujaza fomu na kuomba kura. Nami nilikuwa mjinga nisiyeelewa kwa kumuunga mkono na kumtaka asonge mbele katika nia yake hiyo. Hakuishia hapo, Zitto Kabwe akafanya ujinga mwingine kwa kutamani na hatimaye kutangaza kugombea urais kupitia chama chake. Huu nao ulikuwa ni usaliti kwa utamaduni wetu wa chama kimoja, kwa sababu katika utamaduni huu nafasi kama hii ni ya kiteule na wateule na wateuaji wapo.

Ninapokubali kupokea lawama katika kushiriki kusababisha mgogoro unaoendelea ndani ya CHADEMA, naomba nami niwarushie lawama tele wanachama na mashabiki wa chama hiki, na wapenda mabadiliko kwa ujumla. Nawarushia lawama wanachama na washabiki wa CHADEMA kwa kuwashabikia viongozi wa chama chao katika kukinyonga chama. Viongozi wa chama hiki wamefanya makosa mengi na makubwa hadi kusababisha mgogoro ufike ulipofika, lakini wanachama na mashabiki wa chama wamekuwa wakishwashangilia katika kila hatua walioifanya. Kwa hiyo lawama ya kwanza kwa wanachama na mashabiki ni pale walipokubali kugeuzwa kuwa mashabiki wa viongozi ndani ya chama badala ya kuwa mashabiki wa chama. Na kwa kuwa ushabiki hupofusha macho na akili, mashabiki wa viongozi hawatofautishi kati ya uongozi na chama. Ni kama vile wamedanganywa na viongozi waliopo na wakakubali kudanganyika, kwamba uongozi wa chama ndio chama, na chama ndio uongozi!

Ni kwa sababu ya ushabiki kwa viongozi, ndio maana ilifika mahala wanachama na mashabiki wa CHADEMA wakagawanyika katika makundi ya washabikia viongozi, na chama kikakosa watu wa kukishabikia na hapo kikajikuta hakina mlinzi.

Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama.

Mrema alipotimka, akatimka na mashabiki wake. Hicho ndicho kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Kuna watu wenye mtazamo finyu wanaamini kwamba chama hiki ni imara sana kwa sasa kiasi kwamba hata wakimfukuza Zitto kitaendelea kubaki imara. Wamesahau kwamba wamejenga ufuasi kwa viongozi, na hivyo watakapomfukuza Zitto atatimka na wafuasi wake na chama kitayumba. Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza, viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila. Lakini kwa sababu ya upofu unaoendelea unaotokana na kugubikwa na ulevi wa utamaduni wa chama kimoja kwa upande mmoja, na ulevi wa umaarufu kwa upande mwingine, hawatakubali yaishe nje ya Mahakama, na hatimaye watamfukuza Zitto. Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA.

Source:
Raia Mwema

Dr kitila nina muheshimu sana kwa Elimu na ufahamu wake mpana kwenye jamii,lakini kwa kauli yako hii uliyotoa nakuona kama mwanafunzi wa darasa la saba katika siasa,nimeamini kua hata malengo ya zito ww huyajui,zito amekuburuza tu,chadema siyo mtu(kiongozi) mmoja,chadema bado inaweza kusimama hata bila slaa wala mbowe kuwepo,kama nia yenu ilikua njema ya kukijenga chama,kwanini msifuate taratibu sahihi za kikatiba ndani ya chama? kwanini mfanye kwa siri? kwanini iwe sasa(wakati uchaguzi mkuu umekaribia) na si wakati mwingine?
Sema usemavyo andika uwezavyo lalama kadri uwezavyo, lakini ukweli ninyi niwasaliti kwa pesa za ccm,na ipo siku uhalifu wenu huu utakuja kuwarudia,ipo siku mtagharamika kwa haya makosa mliyofanya hata kama itakua ndani ya nafsi zetu kwakua dhamiri huchoma kuliko moto.
 
Mbadala wa CCM ni CHADEMA, na CHADEMA haijawa na mbadala bado na ili awepo inabidi kusota kwanza nje, Kitila anza kuchakalika, ila siku zote katika harakati zako fahamu chama cha kufukuzana ni kizuri kuliko chama cha kulindana.

Nyie jifarijini kwa kutumia study za Yeriko.
 
"Tunahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA"-Dr. Kitila.

Hii ni statement fupi lakini imebeba ujumbe mpana na mzito sana katika mtazamo wa siasa za Tanzania.

Sijashangazwa na hii sentensi yake bali nimeshangazwa na ujumbe uliopo kwenye article yake kuhusu uendeshaji wa CHADEMA. Ninawaza na kujiuliza. Kama mjumbe wa Kamati Kuu ya chama kwa muda mrefu hawezi kufahamu mzizi au kiini cha uendeshaji wa chama mpaka pale alipojaribu kuutingisha mwenyewe, itakuwaje hawa watu wengine wengi wanaojiita wapenzi na wanachama lakini hawafahamu hata ofisi za chama zilipo achilia mbali katiba na vikao vya chama.

Kwa andiko lake hili, inanipelekea kutambua kuwa kuna uwezekano mkubwa kabisa kuna watu ndani ya CHADEMA wanaodai ni wapigania ukombozi lakini kiuhalisia siyo wakombozi na wako ndani ya CHADEMA kwa sababu tu ya maslahi yao binafsi na maslahi hayo yanawafunga midomo katika kutingisha utendeshaji wa chama. Hawa ni wanafiki wa kupindukia.

Kuna wanazi wa CHADEMA walikuwa wanampa sifa Dr. Kitila huku wakidai kuwa ameamua kukaa kimya kwa sababu ana hekima na busara. Hawakufahamu kile wajuvi wa mambo wanasema, "If you see a lion that's been soaked in rain, do not mistake it for a cat".

Well, ameanza kufunguka na anafunguka na hoja ambazo hazitaki majibu ya mlengo wa kitoto.
 
Laiti kama Dr Mkumbo angemjua ZZK ni mtu wa namna gani asingejaribu kufanya haya yaliyozimisha nyota yake kisiasa!
 
Dear Kitillya Mkumbo,

CHADEMA inakwambia 'Good Riddance'. It wish you all the best on your new endeavours. It has no regret for its decision whatsoever and it doesn't hold any hard feelings for you as well.

You were offered an 'olive branch' a rarely opportunity to reconciled with the party, because initial your character convinced many within the party that you are a gentleman and that you do deserved a second chance. Surprisingly, you stood to be a trouble maker rather than a piece maker. You didn't wish to choose for a peacefully ending. Your arrogance and selfishness ended up disappointing even those who have begged for mercy on your behalf (those who initial gave you a benefit of doubt).

So, it's about the high time now for you to leave CHADEMA alone. Deeply inside of your heart you know and We are all knowing that you were just simply caught up in a trap of making choices of serving two masters. With CHADEMA means the game is over. So, you better accept it and you gotta move up to the next mission bro!.
 
Sikuwahi kufikiria Nd. Kitila Mkumbo anaweza kuja na urojo kama huu akiuita ni uchambuzi wa makini kuhusu sakata lao la kuwafukuza uanachama kwa makosa yaliyowafukuza. Kwanza, naomba ndugu zangu wana JF mnielewe; nimemtaja Nd. badala ya Dr. Kitila kwa sababu, kuanzia sasa nimeanza kukubaliana na Dr. wangu mmoja wa hapo UD aliyeniambia siku moja katika mazungumzo ya kawaida kwamba mojawapo ya walimu walioajiriwa kimakosa UD ni Nd. Kitila Mkumbo ambaye aliajiriwa akiwa na GPA 3.4 wakati by then, the minimum qualification ilikuwa upper second yaani 3.5.

Nd. Kitila, hebu fafanua vizuri unamaana gani kusema kwamba eti "Tulikuwa wajinga sana kudhani kwamba tupo katika mfumo na utamaduni wa vyama vingi ambapo mtu yupo huru kutamani cheo chochote katika chama chake cha siasa, na kutengeneza mikakati ya kushinda cheo." Yaani mtengeneze mikakati ya siri mkiwa ndani ya chama hichohicho na chama kifurahie uhaini wenu huo. Unatuambia nini sisi wananchi bw. Kitila?

Binafsi, japokua siyo mchambuzi wa masuala ya siasa lakini ninaufahamu mdogo tu kuwa maana ya chama ni mkusanyiko wa watu wenye nia na malengo yanayofanana na viongozi wake hupatikana Kwa utaratibu flani ambao chama kitakuwa kimejiwekeaa (katiba), je wewe ndugu kitila, unamaana gani kusimama kuzungumza hadharani kwamba mlikuwa na mkakati wa kupindua uongozi wa juu pasipo kufuata taratibu za kikatiba? Ni chama gani hapa duniani ambacho kinajiita cha kidemocrasia kisichokuwa na utaratibu wa kufuata katika kuendesha mabo yake. Au kwa kuwa wewe ni daktari maana ya democrasia kwako ni zaidi ya sisi tunavyodhani?

Ndugu Kitila utabiri wako wa sasa unaoufanya kwamba CDM itakufa, ni utabiri unaofanana na wa babu yangu mbishi MZEE WASIRA ambao ni utabiri wa waganga njaa. WEWE (Kitila) pamoja na mzee Wasira mawazo yenu ni yaleyale, yanayofanana na yasiyo na chembe za kitafiti hata kidogo. UTABIRI WA WAGANGA WA KIENYEJI. Ninasema hivyo kwa sababu zifuatazo;-

1. NCCR- ya enzi hizo si CDM ya sasa, mazingira, muda na falsafa ni tofauti
2. Watu wa sasa (wananchi) sio watu wa miaka ya tisini- wamebadilika.
3. Technolojia na wigo wa vyombo vya habari (i/u)mekua si kama ya enzi za NCCR.
4. Wabunge wa sasa si wabunge wa enzi za miaka ya tisini waliokuwa watiifu 80% "zidumu fikra sahihi."
n.k

Ushauri, ndugu Kitila ni bora unyamaze, watu wakuonee huruma kuliko kuropoka yale unayoropoka sasa. Kikubwa zaidi unamsemea mpaka zzk bosi wako mtarajiwa wa chama mta(mli)kachokianzisha. Kuna mengi ya kuchambua kwenye hako kaandiko kako ulikokaita uchambuzi makini wa siasa za tanzania; na unapenda uweke kumbukumbu sahihi kwa vizazi vijavyo~dear me!!! rubish.
 
Nakushauri nawe uwapime viongozi wako wapo salama?

Viongozi wangu wapo salama ndio maana unaona wanawajibishana kwa kufuata taratibu tulizojiwekea, haogopwi mtu kwa ukubwa wa cheo.
 
Mkuu bandiko la Dr Kitila limekuzidi uzito zaidi ya upeo wako wa kufikiri
Ni watu wachache sana wenye weledi wa mambo ndio wanaweza kumuelewa Dr Kitila anasema nini
 
Kamwe hainiingii akilini kabisa unapojaribu kutuaminisha ya kuwa eti Chadema wakimfukuza ZZK basi chama kitapasuka vipande vipande. Wananchi wa sasa si wale wa miaka ya 90 enzi za NCCR. Wananchi wa sasa wanajua kutofautisha kati ya mimba na kitambi. Hao wafuasi unaowazungumzia wa ZZK ni wapi hao?? Mbona hatukuwaona kumuunga mkono ZZK pale mahakamani siku ya kwanza?? Au ni wale madereva wa bodaboda wanaopewa elfu ishirini ishirini na Magamba ili kutuaminisha kuwa Msaliti bado ana wafuasi ndani ya chama??? Msingi mkuu wa hii makala yako ni kujaribu kumwombea MSAMAHA MSALITI ili abaki ndani ya chama. Hii misingi ya kuamini kuwa mtu ana nguvu zaidi ya chama ndio inawagharimu CCM sasa. Wanashindwa kuwawajibisha wenye tuhuma ndani ya chama kwa kuhofia chama kugawanyika na pengine kuvunjika kabisa. Sifa moja wapo ya kiongozi ni kusimamia misingi ya chama hata kama utawaudhi baadhi ya watu. Kosa kubwa kama viongozi wa Chadema watamwacha ZZK ndani ya chama eti kwa kuhofia chama kuvunjika. BORA PENGO KULIKO JINO BOVU. Magamba wanajaribu kutumia kila mbinu ili Msaliti aendelee kubaki ndani. Hata Dr. Kitila mwandishi wa hii makala haamini kama huyo Msaliti akifukuzwa ataondoka na wafuasi wengi wa kukiacha Chama taabani. HAKUNA MWALIMU MZURI KAMA MUDA (NYAKATI) Dr. Kitila acha Nyakati ziamue. ZZK ataondoka na Chadema itabaki pale pale. Chadema ni mpango wa MUNGU kuwakomboa toka mikononi mwa Majangili Magamba. RIP ZZK, RIP WASALITI.
 
Back
Top Bottom