Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,303
Katika swali langu sikuzumzungumzia chochote kufariki kwa mtoto wa Mbeki kwa sababu wala sijui hilo jambo. Swali langu lililenga kupata ufafanuzi juu ya madai ya Thabo Mbeki alipokuwa Rais kwamba UKIMWI hausababishwi na virusi vya UKIMWI bali unasababishwa na kuharibiwa kwa mfumo wa kinga mwili kwa sababu ya umaskini na lishe duni. Msimamo wake ulisababisha Afrika Kusini kukataa kupokea msaada wa ARVs na maelfu ya watu kufa bila sababu.
Ahsante kwa ufafanuzi wa swali lako. Ila wanasiasa inabidi mjitokeze haraka kufafanua mambo kwa sababu hapa sio tu kuwa kumesambaa habari ambazo si za kweli kuhusu wewe, bali hata kumhusu Mbeki na familia yake
Nikija kwenye swali lenyewe nina haya machache
In the 1990s, supported by scientists described as minority, dissident and maverick, you boldly and courageously claimed that AIDS is not caused by HIV, but by a collapse of the immune system due to poverty and poor nutrition. As a result of your stance, your Government refused to receive the ARV assistance from international pharmaceutical industries. Your stance also almost caused a moratorium in HIV prevention efforts not just in south africa, but in the whole continent..
i) Reflecting and looking back to your presidency, and given the pace at which South Africa has reduced the HIV infection rates and HIV related deaths, do you still maintain the same position regarding the cause of HIV?
ii) Do you have any regrets over your position?
Swali lilikuwa zuri na lingejibika vyema iwapo mtazamo na msimamo wa Mbeki juu ya swali hilo unaonekana kubadilika. Ukifuatilia kwenye vyombo vya habari, ni wazi kuwa msimamo wa Mbeki haujabadilika. Na ili aweze kutolea ufafanuzi msimamo wake huo ambao hauendani na mtazamo wa wengi na unatizamwa kwa jicho hasi, angehitaji muda mrefu zaidi ya ule unaopatikana kwenye kongamano hilo dogo.
Swali lingekuwa general zaidi kwamba anazinaonaje sera za UKIMWI zinazochukuliwa na serikali za Afrika ukilinganisha na zile alizochukua yeye, ninadhani labda tungeweza kupata undani wake juu ya swali hilo indirecty.
Recently, Harvard scientists published a study report showing that about 300,000 died in South Africa because of your policy stance. The findings of this study have been validated by my scientists, including those in South Africa
Licha ya kuwa hizi data inaweza kuonekana kwamba zimeongezea nguvu swali lako, ukizitazama kwa upande wa Mbeki (na kwa upande wa mantiki) zimedhoofisha mno hoja yako.
Mbeki yeye msimamo wake unapingana na wanasayansi hao wa silka ya Harvard halafu wewe unamnukulia data kutoka kwa hao hao wanasayansi anaopingana nao kuonyesha kuwa anakosea kuwapinga hao wanasayansi?!
Ni sawa na kumuuliza Kikwete kuhusu ongezeko la haraka la umaskini Tanzania kwa ku-back up hoja yako kwa nukuu iliyotolewa na utafiti wa Chadema Arusha.
Atakujibu "tumeshasema hao wana kiwanda cha uongo huko Arusha", na atakuwa amefifilisha kabisa hoja kuu ya ongezeko la umaskini Tanzania. Na hicho hasa ndicho alichofanya Mbeki. Kafifilisha hoja kuu kwa sababu ya data zako.