Dr. Kafumu (CCM) avuliwa ubunge Igunga!

Dr. Kafumu (CCM) avuliwa ubunge Igunga!

Amegundua hata kama wakirudia na sasa cuf nayo imekufa huyu jamaa wa cdm atachukua ndio maana kakimbia game. Kwanza hii kesi ilikuwa nyepesi sana aache kusema jaji hakuwa na imani naye (bastola ya rage, kutukmika kwa mawaziri kama serikali na kumpigia kampeni) sasa hata mimi ningekuwa ni jaji ambaye sina elimu ni hukumu hivi hivi na bakora juu.
 
masikini kumbe hakuwa na imani na jaji hivi majaji huteuliwa na mwenyekiti wa chama gani? nayeye ni chama gani? bora angenyamaza kama aishe

mkuu, huyu aliwekwa a CCM, hawezi kusema lolote, hapo anatuzuga tu. CCM itakata rufaa. . . Thats how it gonna work bro.
 
Another bilion 20 zinaenda kuteketea tena Igunga. nadhani tubadili katiba sasa mtu akivuliwa ubunge basi anayemfuatia kwa kura nyingi ndo achukue ubunge

Hizi ndizo gharama za demokrasia. Hapa kulikuwa na uzembe wa watu fulani kufanya upendeleo wa wazi na wizi wa kura juu. Nafikiri sheria inayotakiwa kutungwa au kurekebishwa na ile ya wasimamizi wa uchaguzi. Ukionekana au kugundulika kuwa umecheza faulo basi unyongwe. Hii itarudisha ethics kwenye shughuli na haki za wananchi.

Kupoteza hizo hela zote maana yake kuna uzembe wa mtu na anatakiwa kuwajibika na kwenda kuishi Segerea vilevile.
 
Kuna kitu bado sijaelewa hapa wakuu .....
Kwa Dr. Kafumu kushindwa kesi je, tunarudia uchaguzi tena Igunga, ama ni by default Mwl. Kashindye anachukua Ubunge wa Igunga??
hata mm naungana nawe kuhusu hilo,ila umenkera kumwita dr huyo kmeo
 
Safari moja huanzisha nyingine..............huu mwendo hadi magogoni mwaka 2015.
 
Peoples......................................!
Power..........................................!

Tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu.
 
Hata hivo si alilazimishw agombee na akinaMwig.... yeye mwenyewe alijua wananchi wake hawammaind. Kwa hiyo hii ni afadhali kwake na maumivu kwa akina yakhe, wapiga debe maarufu.
 
Mbona inaonekana amekata tamaa na hana mpango wa kukata rufani? Nadhani amegundua wananchi hawako tena na CCM, na kuwa CCM ipo kwa kuwa inaungwa mkono na dola.
Alikuwa na kila sababu za kukata tamaa na kwa kweli anajihisi kupata nafuu kwa sababu wananchi wa Igunga walimnyanyapaa kutokana na mizengwe iliyompatia ushindi haramu uliobatilishwa leo. Hakuwa na amani hata kidogo na alipoitisha mkutano wananchi waliubeza na wachache waliohudhuria walimzomea na kuishia kuaibika. Ni katika mazingira haya anajisikia kupata nafuu.
 
kweli sasa CCM inabanwa kila sehemu kama hii hapa Kiongozi wa CCM alia na POLISI kutoisadia :



video kwa hisani ya ITV TANZANIA ya youtube
 
Last edited by a moderator:
Pole ndugu yangu hayo ndiyo maisha. Katika hili unatakiwa ujue kuwa aliyekutafuna si mwingine bali ni wana ccm wenzio, mafisadi waliwatumia wapiga kampeini wako kukutengenezea mazingira ya kuondolewa.
 
Asubiri uteuzi wa ubalozi kama ilivyokuwa kwa akina Batilda Burhani, Dr Kamala, Phillipo Marmo etc au asubiri uteuzi wa wakuu wa mikoa mipya anaweza kukumbukwa kama akina Mwatumu Mahiza, Joel Bendera etc.
Mkoa mpya upi tena, au wanataka kuunda mkoa mpya wa Igunga!!!!
 
Dr kafumu na CCM,poleni sana kwa yote yaliyowakuta huko mahakamani,hizo ndiyo mahakama zetu zilizokuwa zinawapendelea sana,nazo zimegeuka,Nafikiria sana siku mwenyekiti wa CCM atakapokuwa wa upinzani naye akapigwa mabomu na FFU
 
Hapo mahakama imetenda haki. Mkishindwa huwa haikutenda haki!!! Mnachekesha!!!!!!

na bado utachekeshwa sana, hata alipotangazwa mshindi tulilalamika mkasema sisi wazushì. sipati picha kashindye angeshindwa mngeropokaje but now mmekuwa wadogo kuliko piriton
 
na bado utachekeshwa sana, hata alipotangazwa mshindi tulilalamika mkasema sisi wazushì. sipati picha kashindye angeshindwa mngeropokaje but now mmekuwa wadogo kuliko piriton
Subiri uchaguzi mdogo, msije mkasema tena kuwa kuna rushwa, mara hongo, mara serikali, mara polisi, maana ndiyo zenu.
 
Back
Top Bottom