Dr. Kafumu (CCM) avuliwa ubunge Igunga!

Dr. Kafumu (CCM) avuliwa ubunge Igunga!

aliyekuwa mbunge wa jingo la igunga amefunguka na kusema kuwa hakuwa na imani na jaji kwa kuwa aliegemea upande wa chadema na matokeo yake ameipa chadema ushindi, pia Dk. kafumu ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa yeye siyo mbunge tena na ataendelea na kazi yake ya utafiti wa madini.

source EAT

Wana JF niliwaambia mapema Magufuli haendi Igunga kwakuwa anajua Dalai Lama wa Igunga asingepona ng'o hata kwa mbinde, Namshukuru Kafumu kwa kutambua hata akikata rufaa hashindi na sasa apumzike kwa amani katika Politiki za Magamba hiyo inaitwa KATA UJUTE, MABILIONI YALIYOTUMIKA IGUNGA KWENYE KAMPENI YANGEIBADILI IGUNGA NA KUWA MANISPAA, Na hapo bora Apishwe Kashindye tu na siyo tena tuingie hasara kutafuta Mbunge wakati Mbunge anajulikana ni kutoka peoples poweeeeeeeer
 
Hawalaumu w.a.j.i.n.g.a waliojaa C.c.m kama kina Rage,Lusinde,Malock etc,ndio waliomponza,wala asimlaumu jaji,maana jaji amesimama kwenye taaluma yake sawa sawa bila kupindisha kitu
 
Masikini Dalali Kafumu mbona katumikia muda mfupi sana??

Si tu muda mfupi bali pia kwa gharama kubwa. Majuzi alitoa msaada wa shilingi milioni 400 kwa waliokuwa wapiga kura wake. Swali la kujiuliza hapa ni kama fedha hiyo ni halali na kaipataje? Na kama ni ya mkopo vipi atairudisha ikiwa ubunge wenyewe ndo umeota mbawa!
 
Mimi ninakubaliana na Ritz kuwa mahakama imetenda/hutenda haki, tatizo ni kuwa pale inapoamua kwa upande wetu tunasifu mahakama lakini inapoamua in favour ya upande mwengine tunaanza kulalamika.

Hata hivyo ningemshauri Dk. Kafumu kukata rufaa kwani ni haki yake na haki ya mtu haipotei.

akate nini? Eti rufaaaaa mkubwa unachekesha jamaa hana chake tena kwani aliamini angepewa uwaziri lakini kapotea njia hakuna cha uwaziri wala ubunge sasa na jimboooooo hiloooooooo kwa chadema mnune tuuu mwaka huu kwani kwa mwendo huu chichiem imejifia
 
Last edited by a moderator:
Aiseee baba yangu wamemnganga lile vx te te te te et
aende kongo akachimbe madini
 
Hivi huyu mzee si bora angebaki tu na kazi yake pale nishati na madini..huku sijui alidanganywa na nani kuwa kunafaa..
 
Ni bora kagundua mapema kuwa yeye sio mbunge alipotea njia.
 
Hapo mahakama imetenda haki. Mkishindwa huwa haikutenda haki!!! Mnachekesha!!!!!!
 
Haya tamaa zake zimemponza alikuwa kwenye position nzuri akataka aongeze nyingine, badala yake amezikosa zote
aje uku nimbuluze atabeba mabegi ya vifaa mpaka apinde mgongo uku tunakwenda pori kwa pori

Mkuu avatar yako inatisha eeh. Utafikiri Stephen Waira
 
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Igunga amefunguka na kusema kuwa hakuwa na imani na jaji kwa kuwa aliegemea upande wa CHADEMA na matokeo yake ameipa CHADEMA ushindi.

Dk. Kafumu ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa yeye siyo mbunge tena na ataendelea na kazi yake ya utafiti wa madini.


source EAT

Hongera Docror, umedhihirisha usomi wako. unatambua kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani.
Kila la heri huko uendako. Waachie Chadema wajenge nchi.
 
Magufuli amezid kupenda sifa nakuongea bila nidhamu,. Yani hata material ya kumpa uongozi nyeti,. Magufuli ukome kulopoka
 
Hadithi inayokuja,Ni ya Sungura sikia,...Hadithi uliyongoja,Leo ninakuletea.... Alitoka siku moja,njaa aliposikia,..Siku ile akaenda,porini kutembelea...Akayaona matunda mtini yameenea....Sungura akayapenda mtini akasogea,...Karuka tena karuka,Matunda hakufikia,mkononi hakutia Sungura nakuambia..SIZITAKI MBICHI HIZI sungura nakuambia,NAONA NAFANYA KAZI BILA FAIDA KUJUA.
 
Kuna kitu bado sijaelewa hapa wakuu .....
Kwa Dr. Kafumu kushindwa kesi je, tunarudia uchaguzi tena Igunga, ama ni by default Mwl. Kashindye anachukua Ubunge wa Igunga??
 
Kumbe aliombewa kura na huyu nyani Wasira! Kwani alikosa watu. Hivi Jaji hakuongelea kupiga marufuku kuleta wanyama kwenye mikutano inayohudhuriwa na binadamu?
Huogopi kifungo?bora mimi sijasema.
 
Hili ni fundisho kwa wale wote wanaoacha taaluma zao na kuona kwenye siasa ndio pakuja kutajilika kirahisi rahisi tu.
 
Back
Top Bottom