tizama wheel cover ilivyo vunjikavunjika, kumbuka hiyo ni sports rim hivyo hakuna ubishi kuna kitu kiligonga nyuma, ila ukitizama ubavuni kuna kitu kiliparuza gari kutokea mlango wa nyuma hadi mbele kidogo ya mlango wa mbele ndio maana bati limefumuka kuelekea mbele, ingejiburuza lisingebanduka kuelekea mbele. Tizama picha ya pili na tatu inaonekana limegongwa kulia na kushoto kwa maana nyingine yalihusika magari matatu au zaidi, lile lililogonga nyuma, kulia na kushoto.
Tatizo jingine hiyo tairi ya nyuma kushoto inapancha liligongwaje hadi tairi likapasuko nao ni mtihani.