Tetty
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 26,355
- 21,422
- Hata mambo madogo tu wameyafanya yamekuwa magumu ili tu wawakomeshe vijana wa taifa hili. Vijana wa taifa hili ni kama wako JEHANNAM
Leo hii unamwambia Kijana akalime hebu tuangalie kijana huyu aliyemaliza Chuo kikuu yukoje:
1.Kwanza kasoma kwa mkopo hivyo kijana huyu hana pesa ya kutosha hata ya kujikimu mwenyewe anamtegemea mzazi.
2.Kumiliki shamba hata la robo eka lazima awe na si chini ya laki mbili au tatu atategemea baba au mama amnunulie.
3.Kijana huyu alitoka kwenye familia masikini wazazi wameuza ng'ombe na mashamba ili kijana wao afike elimu ya juu.
4.Kijana huyu atahitaji Pembejeo ili aweze kupata pembejeo lazima atahitaji fedha.
5.Kijana huyu atahitaji kujikimu awapa kwenye shamba hilo hana hata kibanda anajikimu vipi.
Leo unamwambia kijana nenda kachukue mkopo hana hata asset ya kuweka collateral labda vyeti vyake,baada ya miaka mitatu unamnyang'anya ardhi unasema ameingia kwenye mali asili/msitu wa taifa unachoma nyumba yake na mali yake yote.
Kesho asubuhi unaadvertise vijana mjiajiri.Kuna wakati natamani Mungu awachukue watawala wote waliotufikisha hapa na akawatupe kwenye moto wa milele.Trully I hate them