August 30 2017 saa 12:57pm ni siku ambayo DR.Hamisi Andrea Kigwangalla, alituma picture kwenye page yake ya Facebook ilionyesha idadi ya vijana wengi waliokuwa wanafanya usaili na kuweka maneno yafuatayo.
1. Ni kwamba kuna nafasi chache sana za ajira nchini ama watu wetu wanachagua sana kazi za kufanya?
2. Je, hakuna utaratibu bora zaidi, wenye staha na heshima, unaoweza kutenda haki kirahisi zaidi kuliko huu?
[HASHTAG]#NjeYaBox[/HASHTAG] #HK
Wakati Dr. Hamisi Andrea Kigwangalla akishangaa utaratibu wa usaili na muundo wake na mimi nilikuwa namshangaa Hamisi Andrea Kigwangalla, kuwa inakuwaje waziri mwenye dhamana kubwa kwa taifa ashindwe kutambua tatizo la ajira na muundo wake?
Kwa mujibu wa mtandao wa
www.worldometers.info/world-population/tanzania-population/ Kwa sasa Tanzania ina idadi ya watu 55.57 million.Tanzania kwa sasa ina vyuo vikuu vya serikali 30 na ina vyuo vya vikuu binafsi 29 na kufanya idadi ya kuwa na jumla ya vyuo vikuu 59.
Je DR.Hamisi Andrea Kigwangalla, anajua ni graduates wangapi wanamaliza kwa mwaka? je anajua ni graduates wangapi hawana ajira ?
Tatizo la ajira kwa sasa ni tatizo kubwa sana ambalo bado halijafanyiwa uvumbuzi wa kulitatua.Kauli ya Dr.Hamisi Andrea Kigwangalla imenikumbusha msemo wa “Tanuru hupima kazi ya mfinyazi ndivyo pia mazungumzo yanavyompima mtu” kauli yake inaonyesha serikali ya Tanzania haijui mfumo wa usaili wa ajira na muundo wake ulivyo.
Kama waziri anashangaa tatizo la ajira na muundo wake itakuwaje kwa Diwani ? “Je, hakuna utaratibu bora zaidi, wenye staha na heshima, unaoweza kutenda haki kirahisi zaidi kuliko huu?” kwa hiyo CCM ingempitisha kama mgombea wa chama cha CCM leo ndio angekuwa raisi wa Tanzania asiyejua tatizo la ajira kwa vijana.
Tanzania tumekosa viongozi wenye karama ya uongozi na ndio maana ,serikali imeshindwa kutatua kero na matatizo ya wananchi sababu uongozi ni karama ambayo ndani yake imebeba: hofu ya Mungu,maono,upendo ,haki lakini kwa sasa wanasiasa wanachaguana kwa kuangalia vyeti na sio karama wala utashi wa kiongozi.
Unaweza kuwa msomi mwenye PHD na usiwe kiongozi mzuri. Kuna idadi kubwa sana ya vijana waliomaliza vyuo vikuu na hawana ajira ila viongozi wetu wasomi wametoa orodha ya graduate wote waliosoma kwa njia nya mkopo na hawajalipa pesa za serikali.
Serikali yetu ina idadi ya wasomi wadaiwa sugu ila haina idadi ya graduate ambao hawana ajira.Graduate atalipaje deni akiwa hana ajira wala biashara ? Put the politicians on minimum wage. Watch how fast things change.
Nitaendelea kesho……[emoji310][emoji310][emoji310][HASHTAG]#UongoziNiKarama[/HASHTAG]
Sent using
Jamii Forums mobile app