Dr. Francis wa CCM: Tutajenga reli kwa kiwango cha lami

Dr. Francis wa CCM: Tutajenga reli kwa kiwango cha lami

CCM walifanya uchaguzi sahihi wa kumpeleka Dr. Francis pale...maana alikuwa akifafanua kwa data hadi unafurahi..sio blablah za Mnyika alizokuwa akipiga anazunguka weee kuelezea katiba ya chadema wakati walikuwa wakijadili ilani za vyama.

1442063882863.jpg
 
huyu ni kada wa ccm na alikuwa mwalimu wangu pale udbs chuo kikuu udsm. Jana alikiwakilisha chama chake cha ccm kwenye kipimajoto itv.

Akadai wao kama ccm wamepanga kujenga reli zote kwa kiwango cha lami. Hata alipoulizwa na mzee masako alirudia tena. Sasa jamani hawa watu wapo serious kweli?

Dr francis mwezi uliopita aligombea ubunge jimbo la kigoma mjini kwa tiketi ya ccm lakini aliangushwa kura za maoni na dr. Waridi kaburu

si hadaa za mchana kweupe?
dk wangu msaniisana jaman nimecheka hiyo mtoto kaniacha hoi alipoulizwa swala labmaendeleo vyaviwanda akaanza kutaja kiwanda cha bakheresa moia ya mafanikio ya ccm nkapga simu ikawa busy niulize na zile meli ccm mnashare nn
 
matatizo tuliokuwa nao watanzania tunadhani professors wote ni waelewa bila kutizama amespecialize kwenye nini, inaelekea hata hajui technology mpya za treni hadi anafananisha na lami,makosa ni yetu vijana tunakazana kuwapigia debe wazee wenye mawazo ya karne ya 20 ndani ya karne ya 21,hii ni aibu kwa mtu msomi kushindwa kujua magnetic-levitation-trains ambayo ndiyo technology ya sasa na kutoa hoja bila utafiti.

Genius langu..
 
Unajua Nilimsikia Prof. mmoja anasema kwa jinsi elimu hapa nchini ilivyoshuka hata level za Madaktari basi yeye angerudisha PhD yake kama kungekuwa na utaratibu huo. Anasema anajisikia kudhalilika kwa namna hao Madaktari wa filosofia wanavyotia aibu. Sasa nimemuelewa Prof.
 
Haaaaaa... Daaah... Ma Dr. wa CCM viazi tupu.. !!
 
Dr Francis ni jembe. Alimsambaratisha Mnyika hadi akaanza kutoa povu. Dr yule yuko vizuri.
 
ILANI YA CCM NA UJENZI WA RELI, HAIAKISI UWEZO WA KIFEDHA, KUITEKELEZA

Na; Mr Florian Mgeni, Mtaalam na Mchambuzi wa Fedha(+255 754 673 726)

Kwa watu waliosoma Finance na kwa wale waliosoma Economics kuna concept inaitwa "Financial Feasibility", pamoja na mambo mengine, unapotokea mradi unaoitaji uwekezaji mkubwa wa pesa lazima uchambue na ufanye upembuzi yakinifu juu ya uwezekano wa upatikanaji wa fedha zitazowezesha utekelezaji wa mradi huo

Nna mashaka watunga ilani wa CCM akiwamo mzee wangu Steve Wassira aka Tyson, kama kawaida yao waliongozwa na siasa za kuwadanganya wananchi na sio utaalam ktk kuweka miradi ya ujenz wa reli ktk ilan iyo

Ilani ya CCM 2015-2020 ukurasa wa 56-57 imetaja reli kadhaa ambazo serikali yake itazjenga KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA endapo wakifankiwa kuingia Ikulu, ambazo ni:-

I) Dar-Tbr-Kgm/Mwnz(1294 km)

II)Mtwara-Songea-Mbambabay-Mchuchuma/Liganga(819 km)

III) Uvinza-Msongati(Burundi) na Isaka-Kigali (Rwanda) 563 km

IV) Tanga-Arusha-Musoma (905 km)

JUMLA ya urefu wa reli zote ni km 4076

Ilani hiyo haijasema fedha za ujenz huo ni shingapi na itazipata wapi, ambazo kwa makadirio zinaweza fika kati ya TZS TRILIONI 46 had 50!!!

Nchi za Ethiopia na Djibouti zilianza ujenz wa reli ya aina hiyo yenye urefu wa km 752 ilotarajiwa kuchukua miezi 60(5 years) kukamilika, na imewagharim US DOLLAR 4 Billions sawa na ela zetu TZS 8.5 trilion!! Reli iyo itakamilika mwakan

Ukijaribu "kucross multiply", km 752 zimegarim USD 4 biilions, je km 4076 wanazosema CCM watazjenga Tz zitagarim shingap?
JIBU utapata serikali ya CCM itaingia garama ya USD 22 billions kumaliza ujenzi huu!!! Ambazo ni sawa na trillion za kitanzania 46.3 shillings.

Samuel Sitta waziri wa uchukuz amekaririwa wiki ilopita akidai reli ya kati tu (km 1294) itatumia trillion 16, Hii inamaana kwamba kwa km zote 4076 itatugarim trillion 50.4 shs (ukicross multiply)

SWALI LINALOBAKI, je serikali ya CCM hela hii (kat ya trillion 46-50) ya ujenz wa reli hizi wanayo???

Kama Ethiopia inayotajwa dunian kama moja ya the fastest-economically-growing country imesumbuka na ku-finance trillion 8 za ujenz wa reli yake ya km 752 ktk bajeti za miaka 5, inamaana Tz ingeweza kutumia miaka 27(awamu 5 na nusu) kumaliza reli zote izo(ukiassume kasi ya kutenga pesa zetu za ujenz inaenda sawa na ya waethiopia maarufu kama wajukuu wa mfalme Suleiman)

UKWELI NI KWAMBA serikali ya CCM haina ela za kujenga reli hizo kama inavyojinadi ktk ilani yake ya 2015-2020

TUJADILI

Kwanza, pesa iyo trillion 50 (itayoweza kutengwa trillion 10 kila bajeti kwa miaka 5) serikali ya CCM haina dalili inaweza kuzipata kwajili ya ujenz wa reli ikizingatiwa had sasa serikali hiihii ya CCM uwezo wake ni kukusanya trillion 13 tu bhaaaaaaas haiwez kuthubutu kuzitenga tril 10 kila mwaka kati ya hizo 13 kujengea reli tu, na wakat matumiz ya serikali kwaajili ya matumiz ya ofisin tu na utawala yanafika trillion 16.6 na hii ni bila kuweka garama za maendeleo (ununuz na ujenz wa bidhaa za muda mrefu EG ununuz Magari, ujenz roads)

Hii inamaanisha serikali ya Tz chin ya CCM haiwez kukusanya mapato yake yatayoweza kulipia ata mishahara, kulipia manunuz ya rim, peni ofisin had ikope tena trillion 3.5!!!
Ndo serikali iyo inathubutu kuwadanganya wananchi itajenga km 4076 za reli akat haiwez kuwalipa wafanyakazi wake mishahara had ikope, ikawapgie magoti nchi wahisan na taasis za fedha!!!
Ni serikali isiyoweza kulipa ata bili za sim na umeme had ikope

Hivyo BA's serikali hii haiwez kutenga trilion 10 kat ya 13 na kubakiwa na trilion 3 kwa matumiz mengine tu akat garama za mishahara inafkia trilion zaid ya 6!! Nan atakubali kwenda kazin bila mshahara?

Pili, serikali ya CCM inaweza jidai kukimbilia kukopa, kwa trend hii ya ukuaji wa deni LA serikali lililofkia zaid ya trilion 35, kama wasipopunguza kasi ya kukopa kuna hatari ya nchi kuingia ktk list ya "NCHI ISIYOAMINIKA KUKOPESHEKA"
Kama Rais Mwinyi alivowai kuipeleka Tz kuwa moja ya nchi isiyokopesheka (Highly-Indebted Poor Country HIPC) kutokana na kushuka kwa "Credit rating" na "credit wortness" yake ivo nchi wahisan, mabenk, masoko ya fedha nk kukataa kuikopesha Tz kwakuwa haikuwa na uwezo na haiaminik kurudisha mikopo.
Na ndo hali nnayoiona inaenda kutokea Tz kama tukiipa CCM hatam nyingine inamaana hadi 2020, den LA taifa linaweza fika had Tsh trilion 130 (tril 35 za saiz+50 ukopaji reli+45 ukopaji usio wa reli)
Kasi ya ukopaji wa serikali ya CCM imesababsha mabenk kupandisha garama za riba kwakuwa uhitaji/demand wa mikopo umekuwa mkubwa mno, ivyo kuwatesa wananchi kwakuwa wanashindana na serikali yao kukopa

HITIMISHO:

Watanzania wengi mnadanganywa sana na CCM kwakuwa wanajua hamjui "kureason" afu hamtunz kumbukumbu.
Mwaka 2010 tuliaidiwa meli ziwa Viktoria na Nyasa, tukawashangilia sana, hazjaletwa, hatujawauliza kwann hazjaletwa, tumeshasahau, Leo wanakuletea ahad nyingine mpya ya ujenz wa reli, afu tunawashabkia tena!!!! KAZI TUNAYO, mtaingizwa tena chaka
 
Acheni uongo nyie bavicha....reli tutajenga na mtayaona mabadiliko.

Tulisema tutatengeneza barabara kwa ajili ya basi za mwendo kasi...mlisema haiwezekani...mbona imewezekana?

M.a.lofa nyie.
 
kadri Kampeni zinavyozidi kupamba moto, tusishangae kusikia wakisema endapo tutawachagua, Mv Magogoni itavusha watu kuwapeleka Chanika!
 
Huyu ni kada wa CCM na alikuwa mwalimu wangu pale UDBS chuo kikuu UDSM. Jana alikiwakilisha chama chake cha ccm kwenye kipimajoto ITV.

Akadai wao kama CCM wamepanga kujenga RELI ZOTE KWA KIWANGO CHA LAMI. Hata alipoulizwa na mzee masako alirudia tena. Sasa jamani hawa watu wapo serious kweli?

Dr Francis mwezi uliopita aligombea ubunge jimbo la kigoma mjini kwa tiketi ya CCM lakini aliangushwa kura za maoni na Dr. Waridi Kaburu

Si hadaa za mchana kweupe?

Mhhh laana hizo za kutembea na mabint za watu na wake za watu, huyu Dr. mchafu sana anatumia nafasi yake akiwa kama mwalimu kutembea na wanawake pale chuoni.Sometime malipo ya maovu yanaanza hapahapa duniani
 
Huyu ni kada wa CCM na alikuwa mwalimu wangu pale UDBS chuo kikuu UDSM. Jana alikiwakilisha chama chake cha ccm kwenye kipimajoto ITV.

Akadai wao kama CCM wamepanga kujenga RELI ZOTE KWA KIWANGO CHA LAMI. Hata alipoulizwa na mzee masako alirudia tena. Sasa jamani hawa watu wapo serious kweli?

Dr Francis mwezi uliopita aligombea ubunge jimbo la kigoma mjini kwa tiketi ya CCM lakini aliangushwa kura za maoni na Dr. Waridi Kaburu

Si hadaa za mchana kweupe?

shida yao kubwa ni kuwa mwaka wa bajeti wanafanya upembuzi yakinifu!
 
Back
Top Bottom