Uchambuzi wa ahadi za mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Pombe Magufuli

mkafrend

mkafrend

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2014
Messages
3,055
Points
2,000
mkafrend

mkafrend

JF-Expert Member
Joined May 12, 2014
3,055 2,000
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amefungua pazia la kampeni za chama hicho kwenye Viwanja vya Jangwani katika tukio lililohudhuriwa na maelfu ya wananchi, huku akieleza mambo 25 atakayoyafanya iwapo Watanzania watamchagua kuwa Rais wa Awamu ya Tano.

Huku akitumia maneno: "Mimi kazi tu", "Tanzania ya Magufuli ni ya viwanda", Dk Magufuli aliyetumia dakika 53 kueleza sera zake, kuanzia saa 11.40 hadi 12.33 jioni alisema Watanzania wanataka kitabu kipya cha mabadiliko na yeye na mgombea mwenza, Samia Suluhu ndiyo wanaoweza kuyaletea.

Mgombea huyo wa urais wa CCM aliahidi kuanzisha mahakama maalumu ya kusikiliza kesi za rushwa na ufisadi, kumaliza tatizo la wanafunzi wa elimu ya juu kukosa mikopo, kuhakikisha mama lishe hawabughudhiwi, kusimamia haki za wasanii, kulinda Muungano na usalama wa nchi. Aliahidi kutoingilia utendaji kazi wa Bunge na Mahakama, kuheshimu mawazo ya vyama vingine vya siasa, kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama, wafanyabiashara wadogo na wakubwa wote kulipa kodi, kuendeleza kilimo, mifugo, uchimbaji wa madini, majisafi na elimu bora.

Nyingine ni kusimamia nishati ya gesi, ujenzi wa barabara, reli, kuboresha sekta ya utalii, kuimarisha uwekezaji, kuwasaidia walemavu na kusimamia uhuru wa habari.

Mkutano huo ulioanza rasmi saa 9.30 alasiri ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na CCM, wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete na marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa. Wengine ni Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba na Salim Ahmed Salim.

Ahadi alizotoa

Mgombea huyo alitoa ahadi mbalimbali ikiwamo ajira akisema: "Ninataka Watanzania wapate ajira, kazi ya Serikali itakuwa kukusanya kodi tu. Viwanda vinaweza kutengeneza ajira kwa asilimia 40 hasa kwa vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali nchini."

Kuhusu ubinafsishaji, alisisitiza: "Kuna viwanda vilibinafsishwa sasa wahusika wasipoviendeleza wajiandae kuvirudisha haraka."

Mbali na kurejesha viwanda vilivyobinafsishwa, alisema akipewa ridhaa hiyo atahakikisha chini ya uongozi wake, anajenga viwanda vingi vipya, akiainisha vile mahsusi kwa shughuli za kilimo, mifugo, kusindika nyama na madini.

Alitaja kipaumbele kingine kuwa ni kilimo na kwamba atahakikisha sekta hiyo ambayo ndiyo mhimili wa uchumi inaendelezwa.

"Tutaleta vitendea kazi, pembejeo na vifaa vingi vya kisasa na vya kutosha kwa wakulima… kama nilivyosema hapo awali, tutajenga viwanda kwa ajili ya wakulima pia.

Mbunge huyo wa zamani wa Chato alisema pia kipaumbele kingine katika Serikali yake ni kuhakikisha kuwa wananchi wa mjini wanapata majisafi na salama kwa asilimia 95 na wananchi wa vijijini wanapata maji kwa asilimia 85.

Kuhusu afya alisema: "Tutahakikisha tunakuwa na vituo vya afya, zahanati na hospitali katika maeneo mbalimbali kwa sababu tunaamini maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana kama wananchi hawana afya bora."

Kipaumbele kingine ni mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu akisema watakuwa wanapata mikopo kwa wakati bila kuchelewa na kwamba watajikita pia katika kujenga hosteli kwa wanafunzi wa vyuo.

"Mishahara ya walimu na wafanyakazi wote tutaishughulikia. Hata madereva haki zao za msingi lazima ziangaliwe," alisema huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.

Mgombea huyo alisema anafahamu kero ya msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam na kwamba maendeleo ya kweli yatapatikana kama changamoto hiyo itafanyiwa kazi.

"Tutaunganisha mikoa yote kwa barabara zenye viwango vya lami na pia tutajenga barabara za juu saba jijini hapa," alisema Magufuli.

Alisema akipewa ridhaa hiyo itashughulikia suala la reli kwa kujenga reli ya kisasa kwa viwango vya Standard Gauge" na kuboresha bandari na usafiri wa anga.

Kuhusu maliasili, alisema ni kipaumbele katika Serikali yake endapo akipewa ridhaa ya kuongoza nchi huku akieleza kukerwa na ujangili... "Ninapata shida sana ninapoona meno ya tembo yanauzwa Ulaya halafu unaambiwa yanatoka Tanzania… sasa unajiuliza yanapitaje?"

Alisema ili kushughulikia suala hilo atahakikisha watendaji wa sekta hiyo wanaboreshewa masilahi yao ili wachangie mapato ya nchi.

Aliahidi Serikali yake kuwa rafiki wa wawekezaji na kwamba italinda masilahi ya wafanyabiashara.

Mgombea urais huyo aliahidi kuwa atalinda uhuru wa habari na atafanya kazi na waandishi wa habari siyo tu wakati wa kipindi cha kampeni, bali hata baada.

Katika ahadi zake, Dk Magufuli hakuwaacha wasanii, alisema atahakikisha wanapata hakimiliki na kuhakikisha wao pamoja na wanamichezo wanaanzishiwa mfuko kwa ajili ya kuwasaidia katika mambo mbalimbali.

Baada ya kupitia hotuba hiyo numegundua kasoro nyingi sana kama ifuatavyo
  • Amesema kuwa ataanzisha mahakama maalum ya kushughulikia ufisadi, Je, Tanzania tunashindwa kuwawajibisha mafisadi sababu ya kukosa mahakama au ni mfumo uliopo wa kulindana? Kwani kwa issue kama ya ESCROW watuhumiwa mbona wanajulikana na wengine walikubali kuchota fedha zetu!
  • Kuhusu elimu ya juu, amesema anashangazwa na mfumo uliopo sasa hv mfumo huu si umeanzishwa na kulelewa na CCM? Sasa yeye atatumia nguvu ipo isiyoandikwa kwenye Ilani ya Chama chake!
  • Amesema kuhusu ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na hospitali za rufaa, Je, hajui kwamba miundombinu hiyo ipo ingawa haina dawa na watumishi sasa kama marais 4 waliopita hawakumaliza tatizo la afya yeye atatumia mwarobaini gani tatizo liishe Mfano: Atafanya nini kuondoa matumizi yaliyopindukia kwenye serikali mfano: rais analipwa dola 192,000/= kwa mwezi, wabunge tsh 12,000,000/= na wengine wengi sasa Magufuli haya atayashughulikia aweze akiwa CCM?

Kwa ufupi naona mashaka na ahadi 25 alizootoa!

Sera za Magufuli zitakwamisha ushindi wa wagombea Ubunge CCM

Mimi naona Maghufuli ajitambui kabisa.. kuwa anagombea uraisi kupitia chama tawala kilichoongoza nchi miula yote. na yeye akiwa ni kiongozi ngazi ya uwazir ktk miula mitatu.

Lakini ukitafakari sera za maghufuli ni kama vile ameamuwa kila mtu afe na mzigo wake.. sbb hotuba zake zote zinaingelea madhaifu yanayotendeka ndani ya serikali akigusia kila idara...

1. Kalamu sana kufa kwa viwanda... ila hiyo mikoa yote ambayo viwanda vimekufa,mingi inashikiliwa na ccm.. na ni serikali hihi ambayo imeuwa viwanda.. sasa hao wabunge wa ccm walikuwa wapi miaka yote kulipigia kelele bungeni.. je serikali awamu yote ilikuwa wapi??? waziri wa viwanda utaongea nini kwa watanzania

2. Elimu bure kuanzia la kwanza mpaka kidato cha nne - hivi kwautajiri tuliokuwanao wote... nilitegemea angesema mpaka kidato cha sita bure..na hii ilikuwa sera ya chadema japo chadema ilisema elimu itakuwa bure kwa ujumla. sasa hayo mabunge ya ccm yalikuwa wapi sikuzote kulipigia kelele swala la elimu kutolewa bure...au serikali kwa ujumla. waziri waelimu ambaye ni mbunge wa ccm,kazi unayo.

3. Afya - maghufuli anawatuumu manesi na madaktari kuchochea kuzorota kwa uduma ya afya tena kwa kuwatuumu ktk uwibaji wa dawa.ktk ili nilijuwa atakwenda kuongelea mzizi wa tatizo .. kulipwa kwa deni la msd, mishahara yao kuboreshwa.. kuliko kukaa na kuwatuumu.. hii inaonyesha wazi waziri wa afya hakuwa mtendasi mzuri.. mpaka anaruhusu wizi kutendeka au na yeye ni mwizi na uwenda hata ili deni la msd ni waziri katafuna pesa zetu kwa madawa ambayo yaliuzwa wanapojua wao.

Ni mengi sana yakuandika ila na malizia kwa kusema kweli nyani haoni kundule... ufisadi uliyofanyika ktk daraja la kigamboni hajagusia,nyumba zetu alizouza kwa bei ya kutupa na kujenga nyengine kwa ghala za juu,na uku watumishi wengi wakibakiwa bila makazi, amekaa kimya.

Maghufuli unaitaji wabunge wa CCM kuongoza nchi, badilisha hotuba zako.

Bye bye.
 
ONTARIO

ONTARIO

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2013
Messages
1,892
Points
2,000
ONTARIO

ONTARIO

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2013
1,892 2,000
Mvi atasaga meno sana, kodi yetu haiwezi kuliwa kirahisi rahisi... He'll rest behind bars. Subiri tu.
 
saidyakub

saidyakub

Senior Member
Joined
Aug 26, 2010
Messages
168
Points
225
saidyakub

saidyakub

Senior Member
Joined Aug 26, 2010
168 225
"nitaunda mahakama maalumu kwajili ya kushughulikia mafisadi na majizi"
hii itawatia adabu watu wote waliohujumu mali za umma.
# hapa kazi tu
Kishaanza uwongo tayari! Anaweza kujifungulia mahakama na kujitia adabu?
Kutuletea kivuko cha Dar Bagamoyo kwa bil9 hali akijua ni wizi na kwamba kitajiendesha kwa hasara . Wallah aanze kujifunga mwenyewe! Itawezekana kweli? Hakika Itawezekana endapo tu ewe mwananchi utachagua UKAWA
 
Amavubi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Messages
30,105
Points
2,000
Amavubi

Amavubi

JF-Expert Member
Joined Dec 9, 2010
30,105 2,000
...............ataanzisha mahakama ya mafisadi-watu makofiiiiiiiiiii
 
Gor

Gor

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Messages
2,794
Points
1,195
Gor

Gor

JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
2,794 1,195
magufuli huwezi kuleta uwajibikaji,uwazi,na utawala wa sheria maana kwanza wewe mwenyewe umetuthibitishia kuwa haueshimu sheria kwa kujiongezea muda wa kampeni hadi saa 12.35 jioni
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,842
Points
2,000
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,842 2,000
Mpe kura Magufuli hayo uliyojiuliza utapata majibu yake. Tingatinga halishindwi. Hata sisi CCM tuna imani naye. Atarekebisha kwa vile ameanza vema. Hana madeni nyuma
 
L

Le Grand

Member
Joined
Jul 28, 2012
Messages
73
Points
95
L

Le Grand

Member
Joined Jul 28, 2012
73 95
Yule dingi mfupi mara nyingi ni mtata sana kwa kauli zake jana sio mara yake ya kwanza kuwatusi WaTz ila sometimes ni kweli most of them especially wale wanaohudhuria mikutano ya ccm na kukenua mimeno kama mazuzu na kupiga makofi kuabudu utapeli uleule miaka yote, haiwezekani limtu linnasema litashugulikia majizi, mafisadi wakati hao hao ndo wamelibeba mgongoni atuambie hao mafisadi ni kina nani maana anawajua na wenzake waliwashindwa vp mpaka yeye awaweze ni UPUMBAVU kuamini kauli za KILOFA kama hizi, wenzako waliuza we unajiumauma eti utavirudisha viwanda na majitu yanakenua mimeno kama vile Mazuzu kushangilia!! Yule mzee anaposema hayo maneno machaf anamaanisha Wewe unaekubali upumbavu uleule wa miaka nenda rudi....! The silly season for silly people has began!!
 
Mchuja Nafaka G

Mchuja Nafaka G

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2014
Messages
764
Points
225
Mchuja Nafaka G

Mchuja Nafaka G

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2014
764 225
azitekelezeki labda kama safari hii wenye nchi (makada waandamizi ccm) wakubali kupunguza matumizi.
Safari
Mishahara mikubwa
Posho za vikao
Posho za safari
Posho za mawasiliano
Burudani
Mbio za mwenge

Na saizi wameshaanza kuwagasi wafanya biashara wachangie gharama Dr. Magufuli anavyotembelea katika wilaya zao
 
Mchuja Nafaka G

Mchuja Nafaka G

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2014
Messages
764
Points
225
Mchuja Nafaka G

Mchuja Nafaka G

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2014
764 225
Kupunguza baraza la mawaziri kutoka 62 hadi walau 30 itapunguza karibia bilioni moja kwa mwezi
 
Joseph Mshinga

Joseph Mshinga

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2014
Messages
232
Points
195
Joseph Mshinga

Joseph Mshinga

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2014
232 195
CCM HAINA TENA WABUNIFU NA ILANI YAKE IMEDHIHIRISHA KUCHOKA KWA CCM.


TUIPUMZISHE.

katika taasisi yoyote lazima kuwepo na magwiji wa ubunifu,mikakati mizito na stadi. hawa kwa kimombo wanaitwa THINK TANKS.

kwa mara ya kwanza kabisa nimeshuhudia CCM ikifeli kwa kila kitu.

kuanzia kauli mbiu ya CCM mwaka huu. nimeona Magufuli akisema wao ni KAZI TU.


ilani ya CCM kwa kadri ilivyoelezwa.

ELIMU:
Itakuwa bure kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne.

hakuna matumaini ya kuifanyia mapinduzi elimu yetu iliyodorora kabisa huku ikikumbwa na matatizo lukuki kama ukosefu wa mazingira stahiki ya kujifunzia na kujisomea, ukosefu wa mabweni mashuleni, ukosefu wa maji mashuleni, ukosefu wa vifaa vya kujifunzia ikiwemo vitabu na vifaa vya maabara,ukosefu wa umeme mashuleni.

eti CCM imeishia kuahidi elimu bure mpaka kidato cha nne katika mazingira hayahaya ya shule za kata ambazo hazina umeme,hazina mabweni,hazina vitabu, hazina maji, hazina nyumba za walimu nk.

CCM haina tena magwiji wenye uwezo wa kulisaidia taifa hili.

elimu nchini Tanzania ipo katika mdororo usioelezeka na kunahitajika mipango madhubuti ya kuifanyia mapinduzi elimu yetu ili iwe ya kisasa zaidi na yenye kuakisi ubora wa juu kabisa ndani ya miaka kumi ijayo. CCM imefeli kabisa na kudhihirisha kuwa imechoka sana kwa ilani hii ninayodiriki kuiita kuwa ni ilani isiyostahili kupelekwa kwa wananchi.

UCHUMI.

nchi kwa sasa inahitaji mipango na mikakati makini ya kulifanya taifa lipige hatua kubwa katika maswala ya TEKNOLOJIA NA VIWANDA ili kulifikisha taifa katika mapinduzi ya viwanda katika miaka isiyopungua 30 ijayo. naona hapa ccm haina kabisa mpango wala mkakati wowote wa kueleweka.

mimi Joseph Mshinga sipo tayari na sitakuwa tayari kuunga mkono ilani yoyote katika kipengele cha UCHUMI ikiwa hakuna mpango wenye matumaini ya kulifanyia mapinduzi ya viwanda taifa letu. Hatuwezi kuwa taifa la kuombaomba miaka yote. CCM katika kipengele hiki wanaomba wapewe kuiongoza nchi kwa staili ileile ya kuombaomba na kukopa. Kibaya zaidi wanaendeleza mazingira ya kulifanya taifa letu liendelee kuwa la kuombaomba,kukopa na tegemezi ili tuendelee kuuza madini na kila aina ya utajiri wetu kwa mikataba ya bei ya pelemende kwa kuwa hatuna teknolojia. CCM mpaka sasa ni chama cha ujamaa lakini katika ilani yao hakuna ujamaa uliowekwa na wala hakuna ile kauli maarufu ya ujamaa na kujitegemea lakini naona hapa ccm inatuhakikishia kuendelea kulifanya taifa letu kuwa tegemezi badala ya kujitegemea. #HILI HALIKUBARIKI# kwa manufaa ya taifa na vizazi vijavyo tuikatae katakata CCM isiendelee kutuharibia taifa letu.

sisi tunahitaji taifa ambalo ifike muda madini yetu tuchimbe wenyewe kwa teknolojia yetu wenyewe, tutengeneze bidhaa zetu wenyewe kutokana na raslimali asili zetu kwa teknolojia yetu na kwa viwanda vyetu. CCM haina kabisa think tank kwa sasa. Ilikuwa miaka ya 70(1970s) wakati ambapo viongozi wa wakati ule waliamua kuanzisha viwanda vya kila aina katika kila kona ya nchi ili kuuishi uchumi halisi. leo ccm haina tena uwezo huo na wala historia hawaikumbuki tena.


CCM THINK TANK HAS BROUGHT THIS VERY POOR MANIFESTO EVER SEEN IN TANZANIA GENERAL ELECTION.

hotuba ya Magufuli imejikita katika kuongelea matatizo madogomadogo ambayo ni ya kiutendaji na majibu ya kutaka na kutatua matatizo ya watanzania hayamo katika ilani ya CCM. TUIKATAE CCM.

tunahitaji uchumi imara utakaofanya yafuatayo.

1.uchumi utakaoruhusu darasa la saba kuwa na ajira zinazoendana na elimu yao kwa kuwa siyo kila mtanzania atasoma zaidi ya darasa la saba.

2.uchumi utakaoruhusu na kuwahakikishia wenye elimu ya kidato cha nne nao kupata ajira kulingana na elimu yao maana si kila mtanzania ana ndoto za kusoma zaidi ya kidato cha nne. Wengine elimu ya form four inawatosha kwa matakwa yao lakini lazima tuwe na uchumi unaowahakikishia kundi hili ajira ili waweze kuendelea na maisha yao.

3.uchumi utakaowahikishia kidato cha sita kupata ajira zinazolingana na elimu yao na ujira unaolingana na elimu yao. siyo lazima kila mtanzania afike chuo kikuu lakini tuna wajibu kama taifa kuhakikisha kila kiwango cha elimu kinaingia kwenye mfumo wa ajira kwa kulihakikishia kundi husika kupata kazi/ajira ili kila mtu aishi kwa kazi yake.

4. uchumi utakao wahakikishia wenye elimu ya chuo kikuu kupata ajira na ujira unaolingana na elimu yao.Kwa mazingira ya sasa hata wenye degree hawana uhakika wa kupata ajira. kwa mantiki hiyo hata wenye elimu ya chini wengi wanalazimika kujitahidi wafike chuo kikuu ili kwa kiasi fulani waweze kupata jira lakini bado hata degree haimhakikishii mtanzania kupata ajira hata ile ya kinyonyaji. Tunahitaji uchumi wa kutoa ajira kwa kila kundi.

5.tunahitaji uchumi wa kulifanyia mapinduzi taifa katika sekta ya elimu,afya, miundombinu nk.

uchumi ukiwa imara watanzania watafanya mambo mengine wao wenyewe kupitia vipato vyao halali.


mfano.
#mtu mwenye kazi na mshahara hahitaji kusomeshewa mtoto wake bure. kwa hiyo wazazi wengi wakiwa na kazi zao wanaweza kuwapeleka watoto wao shule kwa gharama zao. Umasikini ndio unawafanya watanzania wahitaji usaidizi kutoka serikalini katika kusomesha watoto wao lakini kama wakiwa na kazi kila mtu ataweza kumsomesha mtoto wake na kumudu gharama zinazohitajika.

#wakiwa na kazi kila mtu anaweza kumudu kujenga nyumba yake ya kawaida na kuishi maisha anayoyataka.


nk nk nk nk.

kwa sasa ni sahihi kuwa baadhi ya mambo yanahitaji usaidizi wa serikali kabla uchumi haujasimama na kumuwezesha mtanzania kugharamia mwenyewe gharama hizo kupitia ajira yake. Mambo hayo ni pamoja na kuifanya elimu kuwa ya bure mpaka chuo kikuu ili kila mtanzania mwenye uwezo na nia ya kuifikia elimu ya juu asome na kufika huko bila kujali kama ni watoto wa matajiri ama wa masikini. kwa mantiki hii elimu ya bure bado ina umuhimu mkubwa katika mazingira ya sasa.

TUIKATAE CCM ILI KULIOKOA TAIFA.

NA:
JOSEPH NGIKILI MSHINGA
@(visioned to industrial revolution)@
 
yadodo

yadodo

Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
21
Points
45
yadodo

yadodo

Member
Joined Jul 28, 2015
21 45
Hapo hakuna lotakalofanyika ni kupendezesha jukwaa tu ili tumpe kula hana jipya huyo
 
sifongo

sifongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2011
Messages
4,801
Points
2,000
sifongo

sifongo

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2011
4,801 2,000
Hayo mtu yyt anaweza kuyasema, hata lusinde hashindwi kuyasoma akiandikiwa......wasiwasi wangu ni utekelezaji, CCM musahaahidi sana tangu napata akili za kujua mema na mabaya, wazazi wangu wameniambia washaahidiwa sana na hakuna lililofanyika.
 
kulangwa22

kulangwa22

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2015
Messages
720
Points
500
kulangwa22

kulangwa22

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2015
720 500
Ata kikwete alikuja ivi akatoa adi no za sm apigiwe kama kuna rushwa au tatizo ila akuna cho2te kila kitu kwa maisha ya watanzania wachini yamepanda bei
 
B

Bukyanagandi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2009
Messages
7,775
Points
2,000
B

Bukyanagandi

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2009
7,775 2,000
Kupunguza baraza la mawaziri kutoka 62 hadi walau 30 itapunguza karibia bilioni moja kwa mwezi
Mkuu hata Mawaziri 30 ni wengi mno, kwa nini hatuigi Taifa kubwa lenye utajiri kama Merikani ambalo idadi ya Mawaziri ni ndogo sana, Mh.Magufuli suala hilo anapaswa kulifanyia kazi fasta -apunguze vile vile vitu vya anasa especially magari ya kifahari na safari za nje zisizo kuwa na kichwa wala miguu, makongamano yasiyo kuwa na tija kwa Taifa letu - mwisho afanye juu chini kufufua viwanda nchini, wale wote walio uziwa viwanda vyetu wakavigeuza ma Godown wafunguliwe mashtaka na kufilisiwa.
 
K

kabombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Messages
20,436
Points
2,000
K

kabombe

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2011
20,436 2,000
mkafrend una ushahidi gani Rais kupokea dola 192,000? Hiyo mishahara ya wabunge uliotaja ni wabunge wa ukawa ndio walipendekeza na pisho wanachukua
 
M

magufuliforpresident

Senior Member
Joined
Aug 18, 2015
Messages
156
Points
0
M

magufuliforpresident

Senior Member
Joined Aug 18, 2015
156 0
Kishaanza uwongo tayari! Anaweza kujifungulia mahakama na kujitia adabu?
Kutuletea kivuko cha Dar Bagamoyo kwa bil9 hali akijua ni wizi na kwamba kitajiendesha kwa hasara . Wallah aanze kujifunga mwenyewe! Itawezekana kweli? Hakika Itawezekana endapo tu ewe mwananchi utachagua UKAWA

duniani kila mtu anamapungufu yake btw ......tunahitaji mtu atleast anaeweza simama kutuongoza wazungu wanasem somethng is btr than nothing ................................kwa mamvi bado kwakwel.....hatushawishi hata kidogo
 
gnassingbe

gnassingbe

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2015
Messages
4,218
Points
2,000
gnassingbe

gnassingbe

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2015
4,218 2,000
Kishaanza uwongo tayari! Anaweza kujifungulia mahakama na kujitia adabu?
Kutuletea kivuko cha Dar Bagamoyo kwa bil9 hali akijua ni wizi na kwamba kitajiendesha kwa hasara . Wallah aanze kujifunga mwenyewe! Itawezekana kweli? Hakika Itawezekana endapo tu ewe mwananchi utachagua UKAWA

duniani kila mtu anamapungufu yake btw ......tunahitaji mtu atleast anaeweza simama kutuongoza wazungu wanasem somethng is btr than nothing ................................kwa mamvi bado kwakwel.....hatushawishi hata kidogo
Hakushawishi wewe na nani?Au ni wewe mwenyewe unataka kuionyesha hadhira mko wengi.
 
lusungo

lusungo

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Messages
19,738
Points
2,000
lusungo

lusungo

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2014
19,738 2,000
Nimepita ongeza idadi ya comment.....
 

Forum statistics

Threads 1,304,902
Members 501,583
Posts 31,531,222
Top