Dr. Francis wa CCM: Tutajenga reli kwa kiwango cha lami

Dr. Francis wa CCM: Tutajenga reli kwa kiwango cha lami

Kiwanda cha Azam cha tazara zamani ilikuwa ndio makao makuu ya NMC. Inasemekana Azam alipewa hapo kama compansation baada ya serekali kutakiwa kumlipa SSB kutokana na serikali kumwaga shehena zake za ngano na Michele kwa kisingizio Kuwa shehena hiyo ilikuwa na vyakula feki. Aliposhitaki mahakamani serikali ilitakiwa kumlipa ndio nasikia akapewa NMC ambayo kipindi hicho alibaki mkurugenzi na walinzi tu na hakukuwa na uzalishaji wowote.

aliosababisha hasara hiyo ni sumay akiwa waziri mkuu
 
Pengine tumweleweshe kidogo dk kuhusu reli maana yawezekana akiona mawe ( ballast) relini anadhani hiyo ni lami, ni hivi dk, reli imejengwa kwa mataluma (sleepers) na reli (rails) na kuunganishwa na vifungio (fittings and fastenings) ambazo ni boliti na nati (bolts and nuts) pamoja na chuma mbili (fishplates), ukishafunga hivyo unaiimarisha kwa kuipigilia (packing) aidha kwa udongo (earth ballast) au kwa kokoto (stone ballast) ambazo ukubwa wake si chini ya nchi moja na si zaidi ya nchi mbili na nusu, hivyo dk hakuna uhusiano wowote wa njia ya reli (rail track) na lami (tarmac) kwani ukiweka lami relini utashindwa kuipigilia (packing),pengine huwa unaona kitu kama lami relini, hiyo huwa siyo lami ni aidha dizeli au oili inayovuja kutoka kwenye engine.
 
Huyu ni kada wa CCM na alikuwa mwalimu wangu pale UDBS chuo kikuu UDSM. Jana alikiwakilisha chama chake cha ccm kwenye kipimajoto ITV.

Akadai wao kama ccm wamepanga kujenga RELI ZOTE KWA KIWANGO CHA LAMI. Hata alipoulizwa na mzee masako alirudia tena. Sasa jamani hawa watu wapo serious kweli?
Dr Francis mwezi uliopita aligombea ubunge jimbo la kigoma mjini kwa tiketi ya ccm lakini aliangushwa kura za maoni na Dr Waridi Kaburu

Si hadaa za mchana kweupe?
Hiyo ni kawaida ya CCM, Ndio wakati mwingine tunakuwa na wasiwasi na vyeti vyao endapo ni halali au vya kughushi. Si unakumbuka waziri mzima wa serikali hii hii ya CCM aliwahi kusema kwamba Tanzania imetokana na muungano kati Tanganyika na Zimbabwe! Hii ndio Tanzania bwana, mojawapo ya maajabu ya dunia. Yasiyowezekana kwenye nchi nyingine zote yanawezekana hapa kwetu, hii ikiwa ni pamoja na watu wanaotarajiwa kuwa na weledi wa hali ya juu kuongea pumba. Ni hapa tu ndipo unakuta mtoto amefaulu kwenda form one wakati hata kuandika jina lake hajui. Kweli nchi yetu ni moja ya maajabu ya dunia, na yasiyowezekana kwa wengine yanawezekana hapa kwetu.
 
Kweli Dr alichemka sana. Dah siasa zetu zinachekesha sana.
 
Mgombea wa UKAWA anapokosea hamyaoni juzi kakosea kasema ccm oyee hamkuona ila wa ccm akikosea inakua kosa humu JF zuri lifanywe na UKAWA wakifanya wengine utashambuliwa kweli 25 Oct si mbali heshima italudia mkondo wake
 
matatizo tuliokuwa nao watanzania tunadhani professors wote ni waelewa bila kutizama amespecialize kwenye nini, inaelekea hata hajui technology mpya za treni hadi anafananisha na lami,makosa ni yetu vijana tunakazana kuwapigia debe wazee wenye mawazo ya karne ya 20 ndani ya karne ya 21,hii ni aibu kwa mtu msomi kushindwa kujua magnetic-levitation-trains ambayo ndiyo technology ya sasa na kutoa hoja bila utafiti.
Hapo kwenye red sikuungi mkono, huhitaji elimu yoyote kujuwa tofauti ya reli na barabara. Tatizo ukiwa ccm akili zinahamia kwenye ESCROW,
 
Kumbe watu wako makini kweli niliiona live jana,, reli kiwango cha lami!!!
 
Ndio maana nasema kama chama hiki kikipoteza mwaka huu kurudi itakuwa ngumu sana maana hawana hoja za kurudisha imani kwa wananchi wao, wamezoea kupeana tu ulaji kimagumashi.
 
Hata Magufuli alipokuwa Mtwara alisema serikali imejenga kiwanda cha Dangote.
 
Mkiambiwa ccm waongo hamwamini.itakula kwenu.
 
Jamaa bishi...alipewa 3 mnts kazitumia ovyooo still akawaonea wivu wenzie..alipopewa mda ndo hivyo reli kipita juu ya lami....viwanda vingi vya azam...uchumi ukaua kwa kasi akijubu swali la kwa nini maisha magumu.
 
Nyie bavicha na propaganda zenu za uongo....alisema hivyo na palepale akarekebisha si kwamba alikusudia bali ulimi uliteleza na kwa haraka akaendelea na maelezi mengine....ila kwakuwa bavicha haziwatoshi mliona hilo tu...

Mbona hamumsemi Prof. Kitila Mkumbo aliyesema kuwa CHADEMA wanaogopa kuusema ufisadi kwakuwa wamekumbatia mafisadi?

Dr. Francis alimbana Mnyika hadi akatoa povu...
 
CCM walifanya uchaguzi sahihi wa kumpeleka Dr. Francis pale...maana alikuwa akifafanua kwa data hadi unafurahi..sio blablah za Mnyika alizokuwa akipiga anazunguka weee kuelezea katiba ya chadema wakati walikuwa wakijadili ilani za vyama.
 
Kiwanda cha Azam cha tazara zamani ilikuwa ndio makao makuu ya NMC. Inasemekana Azam alipewa hapo kama compansation baada ya serekali kutakiwa kumlipa SSB kutokana na serikali kumwaga shehena zake za ngano na Michele kwa kisingizio Kuwa shehena hiyo ilikuwa na vyakula feki. Aliposhitaki mahakamani serikali ilitakiwa kumlipa ndio nasikia akapewa NMC ambayo kipindi hicho alibaki mkurugenzi na walinzi tu na hakukuwa na uzalishaji wowote.

Na mbaya zaidi huo mchele ulimwagwa kisiasa na sio kuwa ulikuwa mbovu. Kisa eti alikuwa upande wa CUF! Yaani tamaa ya ccm kubaki madarakani ikatupotezea National Milling yetu! To hell ccm
 
Mgombea wa UKAWA anapokosea hamyaoni juzi kakosea kasema ccm oyee hamkuona ila wa ccm akikosea inakua kosa humu JF zuri lifanywe na UKAWA wakifanya wengine utashambuliwa kweli 25 Oct si mbali heshima italudia mkondo wake

Naomba uweke video.
 
Back
Top Bottom