MIAFRIKA JAMANI?....
Hivi kweli kuna mtuanaweza kunipa sifa za Asha Rose Migiro kama kiongozi?..Kumbukeni tu kwamba Uongozi wa nchi ni kipaji ambacho hakina sifa ya darasa wala ujuzi..Halafu tujiulize - nini msimamo wake kuhusu Mafisadi na Azimio la Zanzibar, Katiba Mpya, Muungano, Uwekezaji, Uhamiaji, madini, Usalama wa Taifa, Umiliki wa Ardhi, Ajira, Elimu, AFYA na Maisha bora kwa wananchi.
Msitake kumpamba mtu kama mlivyofanya wakati wa JK kumbe hakuwa na sifa ya Uongozi.. Je, kuchaguliwa Umoja wa Mataifa ndio sababu kubwa ilowavutia na jina lake? maanake toka awepo hapo UN hakuna lolote la maana kalifanya...Simchukii hata kidogo, she is good people - lakini ucheshi ama uzuri wa sura hakuimpi wala hakuongezi uwezo wake wa kuwa rais wa nchi.. Hizi habari za Usawa na uuwiano ktk hali tuliyopo haiwezi kuwa sababu wala kigezo cha kujivunia...
Toka kaingia yeye na Huyo macho madogo UN imekuwa chombo cha mabepari, wanapelekeshwa kama malaya, vikwezo kwa Syria lakini sio Bahrain. Majeshi ya NATO yanavamia nchi za watu na kuvunja sheria zote za Umoja wa Mataifa kuhusiana na sovereign immunity, jambo ambalo sisi hatuwezi kuwachagulia wao viongozi. Obama amegeuka kuwa mpenda vita kuliko hata Bush..Dunia ya leo vita kila kona duniani kutokana na uvamizi wa uwekezaji kujenga interest zao (Ukoloni mamboleo) - WHAT HAS SHE DONE FOR US LATELY?