Dr. Asha Rose Migiro: The next president?

Dr. Asha Rose Migiro: The next president?

Hizi ni zaidi ya tetesi. Kwa sasa hivi wakubwa wanajipanga vilivyo, na UWT ndio wataongoza msafara wa kumnadi mara kipengele kitapopulizwa. Kuna kitu ambacho bado hakijakaa sawa, huyu mwanamama anapiganiwa na kambi zote mbili yaani kambi ya EL inamtaka na kambi ya mkuu wa kaya nayo inamtaka. Na wote wamewekeza kwenye kisingizio cha JINSIA yake.

Kwangu mimi maswali ni haya; kwa jinsi ufisadi umeitafuna Tanzania na kulifanya taifa hili kuwa omba omba na kopa kopa, je Dr Migiro ndio jibu? Huyu mama kwa record tuliyonayo wakati akiwa waziri hapa, ana ubavu wa kupambana na matatizo tuliyonayo? Ana mshipa wa kufanya maamuzi magumu hata ndani ya chama chake let alone kwa nchi?

Tunauziwa mbuzi kwenye gunia?
Kwenye bold kweli mmejipanga kama mtoa hoja alivyosema(sio kawaida yenu), lakini ni ndoto kusema eti kambi mbili za mahasimu zinamkubali hiyo labda jaribu kuja vingine tifu tifu lenyewe bado ndiyo linatoa vumbi wewe unakuja na conclusion hapana.

Tanzania hatujawa na Indira Gandhi, hatuna Margaret Thatcher, hatuna Elen Sirleaf. Bado!

Watanzania hatutakubali kutawaliwa na kimada wa fulani. Inatosha

swali moja tu la kumuuliza Migiro kama anataka Uraisi.

Je anao uwezo wa kumtii mikononi mwa sheria JK na wengine wote ambao wameifikisha nchi hii hapa ilipo?
Kama ataweza kufanya hivyo basi anaweza kuingia kwenye list ya wagombea ambao tunataka.

Nchi hii sasa inahitaji mwanaume wa shoka atakayerudisha nidhamu na siyo kuuza sura na kuchekacheka.

Naamini kila mtu ukimuuliza atakwambia hivhivyo maana nchi imekosa mwelekeo ndani ya hii miaka 10 ya JK.

Kitu kingine ambacho haitakuwa kazi rahisi ni JK kututeulia mtu wa kumrithisha ili hali yeye anaiacha nchi iko hoi.

Kitu kingine ambacho kikowazi ni kutafuta mrithi ambaye atalinda masilahi ya kifisadi ambayo yataachwa na JK.
Je sisi tuko tayri kuona ufisadi unaendelea kulindwa na watawala kwa kuachiana madaraka? Hili ndiyo ndo swali la msingi la kujiuliza kabla hatuaachia ccm iendelee tena.

Lakini pia tunalo swali lingine la msingi la kujiuliza, Je ccm inaweza kutupa Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tz tena kwa hali iliyonayo sasa?

Tunahitaji kuanza upya period

Watanzania hatutakubali kutawaliwa na kimada wa fulani. Inatosha
Hasa sisi wanawake(samahani) 'siwezi kuongozwa na mwanamke mwenzangu'(inferiority complex) hiyo mentality bado ipo sana wasiidharau.

anavyolegea vile, atatusaidia nini watz? kama wanataka waangukie pua, wamlete huyo ******. kwa habari ya udini, sidhani kama adha rose mingiro ni mwislam, nilikuwa najua ni mkristo...kama kuna mwenye fununu atuelezee vizuri.

Mingiro hatashinda believe me or not nafikiri hamjui tabia za wanawake hasa wa kitanzania atazikosa kura zao usiniulize kwanini.

Si tu atazikosa kura za wanawake,bali hata za wanaume kwani maeneo mengi ya vijijini kuna nguvu kubwa ya mfumo dume!

Mhh waswahili wanasema Band moja miziki tofauti. Mhh mie Safari hii CCM hawapati kura yangu hata waseme sijui nini. tumechoshwa na uwongo wao.

Kwa mtu makini atabaini hizo jitihada za chini chini za kum-promote Dr. Migiro. Kama alivyosema mwandishi mmoja wa makala wa gazet la Raia Mwema, huyu mama mkwele atamnadi kwa gear ya 'sasa ni zamu ya akina mama' lakini nia iliyofichika ambayo watanzania wengi bado hawajaibaini ni 'udini'. Mkwele nimesoma nae namjua sana kuhusu eneo hili. Ngoja tusubiri tuone mambo.
wewe zezeta ungejua wala usingeandika hizi pumba zako hapa. Huo udini wa Kikwete ni upi? au wewe ndo mdini? sidhani huyo JK kama hata hizo swala 5 anazifuta. Ila sema tu kwa sababu ni muislam basi ni mdini. Ama kweli wewe ni Bwe.ge.

Sitawapa ccm kura yangu ht wamweke sitta,mwakyembe,magufuli,migiro Sijui nani kura yangu sitawapa ng'o sababu kubwa ni kutokua na imani na chama chao

Tusijidanganye mda haujafika kwa Tanzania kuongozwa na RAIS MWANAMKE TENA WA CCM, USPIKA UMETUSHINDA URAIS TUTAUWEZA?? LABDA UMAKAMU WA RAIS TN AWE ANATOKA UPINZANI.

Rekebisha hapo penye bold --Hebu sema ni kwanini muda bado? 50 yrs ya uongozi wa wanaume umetuletea nini?

Wanawake nao wana haki kushiriki uongozi katika ngazi yoyote. Huenda hata ufisadi ukapungua pale tutakapoongeza wanawake kwenye uongozi. Nikisema hivi sina maana kumshabikia ARM bali napinga hiyo kauli kwenye bold. Mwisho wa siku watanzania ndio wataamua wenyewe.

Si tu atazikosa kura za wanawake,bali hata za wanaume kwani maeneo mengi ya vijijini kuna nguvu kubwa ya mfumo dume!

mbona tunaongozwa na wanawake siku nyingi sana maana kama tungekuwa tunaongozwa na wanaume tusingekuwa hivi after 50 yrs of independent. bado tunaomba omba bado tunajigonga kwa ngozi nyeupe as if ni mabwana zetu!

kiongozi anayepanda madaraja ya uongozi kwa kubebwa hafai kupata uongozi wa juu kama urais,hataweza kufanya maamuzi kwa kuzingatia maslahi ya umma bali mabasha zake!

Sio kawaida yetu kubandika hapa mambo ambayo ni tetesi.Leo naomba iwe siku tofauti kwani zipo tetesi zingine ambazo zinakuwa “interesting” kupita kiasi…at least kwetu.Kuna tetesi kwamba Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr. Asha Rose Migiro,huenda akajitupa katika kinyang’anyiro cha kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Tetesi hizo zinatiliwa utambi na kinachoonekana wazi kwamba huenda sasa muda umefika kwa Tanzania kupata Rais mwanamke kwani upande wa kiumeni umeonyesha ulichoweza kwa miaka takribani 50 sasa tangu Uhuru.

If this is true then CHADEMMA kwishneei 2015
Karibu Migiro tutakupa wizara mpya ya kuboresha maendeleo ya wanawake!

Tunataka rais mwenye msimamo hasa katika kufanya maamuzi magumu..huyo mwanamke atatuletea giza kama Makinda...

Sio kawaida yetu kubandika hapa mambo ambayo ni tetesi.Leo naomba iwe siku tofauti kwani zipo tetesi zingine ambazo zinakuwa "interesting" kupita kiasi…at least kwetu.Kuna tetesi kwamba Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr. Asha Rose Migiro,huenda akajitupa katika kinyang'anyiro cha kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Tetesi hizo zinatiliwa utambi na kinachoonekana wazi kwamba huenda sasa muda umefika kwa Tanzania kupata Rais mwanamke kwani upande
wa kiumeni umeonyesha ulichoweza kwa miaka takribani 50 sasa tangu Uhuru.

If this is true then CHADEMMA kwishneei 2015

kama wewe hujadili majina na titles za watu! inshangaza kuona huna dalili hata chembe ya hatari inayoinyemelea tanzania! ungejua wala akili isingekutuma kuuliza habari za migiro na urais hapa!!

MIAFRIKA JAMANI?....

Hivi kweli kuna mtuanaweza kunipa sifa za Asha Rose Migiro kama kiongozi?..Kumbukeni tu kwamba Uongozi wa nchi ni kipaji ambacho hakina sifa ya darasa wala ujuzi..Halafu tujiulize - nini msimamo wake kuhusu Mafisadi na Azimio la Zanzibar, Katiba Mpya, Muungano, Uwekezaji, Uhamiaji, madini, Usalama wa Taifa, Umiliki wa Ardhi, Ajira, Elimu, AFYA na Maisha bora kwa wananchi.

Msitake kumpamba mtu kama mlivyofanya wakati wa JK kumbe hakuwa na sifa ya Uongozi.. Je, kuchaguliwa Umoja wa Mataifa ndio sababu kubwa ilowavutia na jina lake? maanake toka awepo hapo UN hakuna lolote la maana kalifanya...Simchukii hata kidogo, she is good people - lakini ucheshi ama uzuri wa sura hakuimpi wala hakuongezi uwezo wake wa kuwa rais wa nchi.. Hizi habari za Usawa na uuwiano ktk hali tuliyopo haiwezi kuwa sababu wala kigezo cha kujivunia...

Toka kaingia yeye na Huyo macho madogo UN imekuwa chombo cha mabepari, wanapelekeshwa kama malaya, vikwezo kwa Syria lakini sio Bahrain. Majeshi ya NATO yanavamia nchi za watu na kuvunja sheria zote za Umoja wa Mataifa kuhusiana na sovereign immunity, jambo ambalo sisi hatuwezi kuwachagulia wao viongozi. Obama amegeuka kuwa mpenda vita kuliko hata Bush..Dunia ya leo vita kila kona duniani kutokana na uvamizi wa uwekezaji kujenga interest zao (Ukoloni mamboleo) - WHAT HAS SHE DONE FOR US LATELY?

Mingiro hatashinda believe me or not nafikiri hamjui tabia za wanawake hasa wa kitanzania atazikosa kura zao usiniulize kwanini.

Naona mkuu wa kaya amekwama, anatapatapa. Migiro hana sifa kwa sasa kuwa rais wa nchi inayoelekea kuwa kama somalia economically.

Kuna nafasi za kufanya majaribio na zisizotakiwa kufanyiwa majaribio. Tumefanya majaribio mwaka 2005 tukaonja joto lake kisha wakachakachua tena mwaka 2010 tukaona moto wake. Hatukubali tena majaribio mengine 2015 nchi imechakaa sana inahitaji mtu makini na mzalendo na huyu hataweza kupatikana katika sisiem ya mfumo wa sasa.

Back
Top Bottom