Dr. Asha Rose Migiro: The next president?

Majasho

JF-Expert Member
Aug 4, 2009
413
220
Sio kawaida yetu kubandika hapa mambo ambayo ni tetesi. Leo naomba iwe siku tofauti kwani zipo tetesi zingine ambazo zinakuwa "interesting" kupita kiasi at least kwetu. Kuna tetesi kwamba Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr. Asha Rose Migiro huenda akajitupa katika kinyang'anyiro cha kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Tetesi hizo zinatiliwa utambi na kinachoonekana wazi kwamba huenda sasa muda umefika kwa Tanzania kupata Rais mwanamke kwani upande wa kiumeni umeonyesha ulichoweza kwa miaka takribani 50 sasa tangu Uhuru.

If this is true then CHADEMA kwishneei 2015
 
Kwa mtu makini atabaini hizo jitihada za chini chini za kum-promote Dr. Migiro. Kama alivyosema mwandishi mmoja wa makala wa gazet la Raia Mwema, huyu mama mkwele atamnadi kwa gear ya 'sasa ni zamu ya akina mama' lakini nia iliyofichika ambayo watanzania wengi bado hawajaibaini ni 'udini'. Mkwele nimesoma nae namjua sana kuhusu eneo hili. Ngoja tusubiri tuone mambo.
 
Hizi ni zaidi ya tetesi. Kwa sasa hivi wakubwa wanajipanga vilivyo, na UWT ndio wataongoza msafara wa kumnadi mara kipengele kitapopulizwa. Kuna kitu ambacho bado hakijakaa sawa, huyu mwanamama anapiganiwa na kambi zote mbili yaani kambi ya EL inamtaka na kambi ya mkuu wa kaya nayo inamtaka. Na wote wamewekeza kwenye kisingizio cha JINSIA yake.

Kwangu mimi maswali ni haya; kwa jinsi ufisadi umeitafuna Tanzania na kulifanya taifa hili kuwa omba omba na kopa kopa, je Dr Migiro ndio jibu? Huyu mama kwa record tuliyonayo wakati akiwa waziri hapa, ana ubavu wa kupambana na matatizo tuliyonayo? Ana mshipa wa kufanya maamuzi magumu hata ndani ya chama chake let alone kwa nchi?

Tunauziwa mbuzi kwenye gunia?
 
ccm watakubali mwanamke awe mwenyekiti wao?2015 mie nafikilia atatokea znz na cyo tanganyika
 
nadhani sisi wananchi tusiouza utu wetu kwa kipande cha khanga na kofia
ndiyo wenye uamuzi wa mwisho wa nani awe raisi, labda zitumike mbnu chafu kama
zilivyotumika uchaguzi uliopita ulio HALALISHA haramu na KUHARAMISHA halali
 
Hivi kwa mfumo dume uliojengeka Tanzania, kuna mtu anaweza kufikiria kwamba kusimamishwa kwa Dr. Migiro kutaimaliza CHADEMA? Sema tu kitakachomuwezesha ashinde ni hiyo publicity ambayo imeshaanza sasa hivi, pamoja na fedha za kifisadi ambazo Kikwete anajaribu kukusanya ziikomboe CCM 2015, kwa kuhofia isije ikafia mikononi mwake.

Lakini katika hali ya kawaida sitarajii kwamba Migiro anaweza kufurukuta mbele ya Slaa kwenye uwanja huru wa uchaguzi. Najua Slaa atakosa kura nyingi Zanzibar na mikoa ya Pwani ambako watu wanafikiria udini zaidi kuliko taifa. Vinginevyo, Migiro si kitu mbele ya Slaa.
 
Sio kawaida yetu kubandika hapa mambo ambayo ni tetesi.Leo naomba iwe siku tofauti kwani zipo tetesi zingine ambazo zinakuwa "interesting" kupita kiasi…at least kwetu.Kuna tetesi kwamba Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr. Asha Rose Migiro,huenda akajitupa katika kinyang'anyiro cha kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Tetesi hizo zinatiliwa utambi na kinachoonekana wazi kwamba huenda sasa muda umefika kwa Tanzania kupata Rais mwanamke kwani upande wa kiumeni umeonyesha ulichoweza kwa miaka takribani 50 sasa tangu Uhuru.

If this is true then CHADEMMA kwishneei 2015

Utopian thinker.
 
Sio kawaida yetu kubandika hapa mambo ambayo ni tetesi.Leo naomba iwe siku tofauti kwani zipo tetesi zingine ambazo zinakuwa "interesting" kupita kiasi…at least kwetu.Kuna tetesi kwamba Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr. Asha Rose Migiro,huenda akajitupa katika kinyang'anyiro cha kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Tetesi hizo zinatiliwa utambi na kinachoonekana wazi kwamba huenda sasa muda umefika kwa Tanzania kupata Rais mwanamke kwani upande wa kiumeni umeonyesha ulichoweza kwa miaka takribani 50 sasa tangu Uhuru.

If this is true then CHADEMMA kwishneei 2015

Nimeshasema sana humu JF kwamba CCM strategy ya communication ni failure kwasbabu wanatumia watu wao waliokulia kwenye siasa hizohizo chafu nikaonekana muongo...

sasa hebu cheki kwenye red... it is an ID used by more than one person, wanatumwa, wanajipanga na wanapeana shifts... and they are in teh payroll... WELL, MOST OF JF MEMBERS ARE NOT LIKE THAT

Ujumbe umefika, lakini it will be the biggest mistake to bring a person who doesnt have a strong grip in local dynamics... a person who is great but may end up be another vasco da gama, a vulnerable personality in trying times and a great woman to be just where she is now, mkimleta Tanzania sasa, atachafuka hata kabla ya kura za maoni za CCM hasa ukizingatia hoja za CCM kama udini, Ubara na Uzanzibara, Mtu mwenye uelewa wa ndani, Ufisadi, Magamba nk

All the best Asha, wameanza kukutafuta sasa... Maana pesa za Kaddafi zimeshindikana
 
Sina uhakika kama atapata uungwaji mkono sana na hasa kuanzia katika chama chao..
 
kama unafanya utafiti kwangu chukua majawabu yafuatayo, 1. simpigii kura mgombea yeyote kwa kuangalia jinsia yake 2. ni vigumu chama kilichofeli kunilaghai 3. siwezi kusahau sarakasi za ccm kwenye nishati, 4. bado naamini madini ya nchi yetu yanawanufaisha ccm na waambata wake. HIVYO BASI; KIONGOZI BORA WA NGAZI YOYOTE HAWEZI KUTOKEA CCM. KWANI HAWAYATENDI WAYAHUBIRIYO MAJUKWAANI, na hata wakianza leo hawainunui akili yangu na familia yangu, kwani ni ulaghai. na bibi kiroboto makindra atasaidia sana kutengeneza hasira kwa wale waangaliao jinsia kabla kupitisha mgombea au kumpigia kura.
 
Nchi imeharibika sana kama vile haina wenyewe. Huu sio muda wa kufanya majaribio katika nafasi nyeti kama urais. Tunahitaji mtu makini, tumeingia mkenge kwa hii miaka 10, awamu ijayo hatudanganyiki.
 
Tanzania hatujawa na Indira Gandhi, hatuna Margaret Thatcher, hatuna Elen Sirleaf. Bado!
 
Tusijidanganye mda haujafika kwa Tanzania kuongozwa na RAIS MWANAMKE TENA WA CCM, USPIKA UMETUSHINDA URAIS TUTAUWEZA?? LABDA UMAKAMU WA RAIS TN AWE ANATOKA UPINZANI.
 
Mingiro hatashinda believe me or not nafikiri hamjui tabia za wanawake hasa wa kitanzania atazikosa kura zao usiniulize kwanini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom