mwkjjj.
zumari limelia nasi tupo kulichezaaaaa.. mambo ya dowans natumai yatatupa picha nyingine ya uwezo wa serikali hiii katika kutendaaa maamuzi yake.
Hakuna lolote hayo ni kutupotezea muda waTanzania katika kudai KAtiba mpya ,Katiba ambayo haitakuwa na swahiba au haitakuwa na huyu ni mwenzetu ,haya mambo yanayoletwa na wafuasi wa Sltani CCM ni kutaka kutuchanganya WaTanzania ili baadae ionekane sote tulishiriki ,walilolikoroga waachwe walinywe wenyewe kama wewe ni MTanzania unaetaka mageuzi ya kweli ambayo yatakultea maendeleo huna budi kuachana na ubabaishaji huo ambao unaonekana kusukwa ili waingie waliokuwemo na wasio kuwemo.
Madai ya Mtanzania yeyote yule ambae ameamua kuondokana na umasikini hana budi kuyahamisha na kuyapeleka katika kudai KATIBA mpya,Katiba ambayo haitakuwa na nafasi kucheza na wababaishaji wanaowaburuza wananchi katika masuala nyeti wakati hakuna la maana hata moja litakalopatikana zaidi ya kupasiana majukumu na kuishia hewani.
WaTanzani ni lazima tuamke katika kudai mabadiliko makubwa ambayo yataendana na kufuata mfumo wa vyama vingi,kufuata matakwa ya wengi na sio kufuata yale ya ukichagua ndio ,ndio yeye na ukichagua hapana ,hapana mwengine isipo kuwa yeye ,huko ni kuburuzwa.
Sultani CCM na wafuasi wake wanajaribu kuyatwist mambo ili kuwazubaisha wananchi na kuzidi kuwapotezea muda wa kufikia maendeleo ya uhakika ,haya maendeleo ya kupigiwa kura wanaoua vikongwe na maalbino pamoja kuwatambua majambazi ni kuishiwa kwa sera za maendeleo kwa Sultani CCM na ni kuwadharau wananchi ,wananchi ambao kwa kauli za aina hii kutoka kwa wafuasi wa Sultani CCM ni za kuwakatisha tamaa juu ya maisha yao na vizazi vyao vya baadae.
Hakuna faida juu ya mambo haya ambayo ni madudu ya Sultani CCM yaliyofanywa na wafuasi wake ,na hayawezi kutatuliwa kwa kununua au kutonunuliwa ,zaidi ya kufanikisha ubabaishaji wao.
Mmoja wa wafuasi wa Sultani CCM ambae ndie kinara kila siku anasikika akisema nina majina,nina orodha nina hiki na kile akikusudia wanaohujumu uchumi,sio vibaya ni vizuri kabisa kuwa anafahamu wanaolihujumu Taifa ni ushahidi tosha hata wa yeye kufikishwa mahakamani (Wanasema anakinga),maana ukiwajua wahalifu na kuwahifadhi ni kosa na haswa pale unapojulikana kuwa unawajua ,seuze umesema unawajua ,inamaana kutowataja au kutowachukulia hatua ni kuwaachia waendelee kuhujumu,jamani umekwisha kuwajua unapoteza muda wa nini ? Kwa nini unawapa muda wezi mafisadi ? Unapata faida gani ? Eti wajirekebisheh !! Wezi wajirekebishe ,Taifa linaingia au limeingia hasara unasema wajirekebishe na ile hasara waliyoisababisha hata ukapatiwa orodha ndio basi ! tunaibeba wananchi ? Tunaibeba hasara iliyosababishwa na watu wanaojulikana ! Toka alipopatiwa orodha ,sijui kama kati yetu yupo anaejua mpaka leo ni muda gazi zaidi ya aliepeleka orodha hiyo ? Je ni rate gani Taifa limepata hasara kwa muda huo ?
Hii ni kesi ikiwa kinara wa Sultani CCM haelewi ,moja kwa moja inaweza kumpeleka mahakamani.Kwa kuwahifadhi wahujumu uchumi ,aliempelekea orodha alikuwa na imani Taifa litasimamishiwa hasara hiyo ,lakini wenzetu wameambiwa wajirekebishe.
Sasa hayo nasema ni ya Wafuasi wa Sultan CCM ,ni madudu ,ni mauzauza ni dharau ambazo zinafanywa na kutekelezwa na wafuasi wa Sultani CCM ni mambo yao ambayo yanalindwa na Katiba ya uongozi chini ya mfumo wa Chama kimoja.
Katiba ambayo haifai kwa muda huu tulionao haina budi kubadilishwa mara moja.