Wasibabaishe watu wote hao lao moja,wanajaribu kuzuga zuga ili wasidaiwe ,madai ambayo ni hatari kwao.
Utawala wa Sultani CCM upo kwenye kona ,kila siku nasema na nitaendelea kusema kuwa kunahitajika mabadiliko ya KATIBA ,Tume ya Uchaguzi ,mfumo wa Mahakama na kupunguzwa kwa nguvu za Raisi na viongozi wawepo chini ya sheria.
Haya malumbano ni yao wao kwa ukweli kabisa hayawahusu wengine ,wao ndio wenye serikali ,wao ndio wenye usukani, wengine ambao wanaingia kwenye kundi ni wale ambao wanampigia na kumshangilia mwendawazimu ,hivyo kila ukizidi kushangilia ndipo vituko vinapozidi.
Wale wote ambao hawaupendi mwenendo wa Sultani CCM ni lazima waungane ili kuiletea Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania mabadiliko makubwa ,kwa muda huu tulionao CCM waachwe kama walivyo wakiuza ,wakinunua ,wakiwatafuta majambazi kwa kupiga kura ,waachwe wafanye watakavyo kwani ,zote hizo ni dalili za kukata roho na kumalizika Utawala wa CCM Empire hapa Tanzania .
Mbio hizi za kufukuzana na kudhaniana wao kwa wao zisituvurugie lengo ni lazima muwasome kwani wananunua wakati na kupoteza nguvu za upinzani.
Fikiria tokea wakati tulipoanza kuwanadi kuwa ni wezi hadi leo ,ingelikuwa vifijo na mayoe na makelele ni kudai Katiba huru na tume huru leo hii tungelikuwa tumeshafikishana nao mbali.
Haya ambayo tunakwenda nayo kwa kweli hayatusaidii chochote na yanapelekwa kwa mwendo wa kinyonga au yanakwenda mwendo wa gegereka au kaa ,ndio maana yake mara yanapelekwa huku mara yanapelekwa huku.
Tunaona viongozi wanapoteza nguvu na kupoteza umaarufu wao kwa kupigizana na kubishana na wezi au mafisadi wa Sultani CCM. Jambo ambalo lilitakiwa sio kubishana nao bali ni kuelekea kwa wananchi na kuwaeleimisha mpaka wakafahamu maana kuzidi kuwafahamisha kila siku mwisho wake wangeelewa tu anachofanya Sultani CCM ,jamani kamba inakata jiwe halikadhalika maji yanapasua milima na majabali.
Kama tutakaa na kubishana na Sultani CCM juu ya unyama anaoutenda na anao ubariki ,siku zote tutakuwa kwenye malumbano ambayo tija yake ni dhaifu sana ,lazima nguvu hizi zielekezwe kwa wananchi na kuwaelewesha umuhimu wa Kuifanyia marekebisho Katiba ili iendane na mfumo wa vyama vingi jambo ambalo litakuwa na manufaa sana sana.