Dowans: Another Richmond in making?

kuwepo kwa mgawo wa nguvu...haimaanishi ni kwa sababu ya kutonunua mitambo ya Dowans...........inamaanisha sisi wananchi tunaendelea kufanywa WAJINGA na MABWEGE

No, kuwapo kwa mgao kunamaanisha sisi Miafrika ni Ndivyo Tulivyo, hatuna uwezo wa kutengeneza mitambo yetu wenyewe kwani tungekuwa na uwezo huo tungekuwa tumeshalitatua hili tatizo once and for all. Remember, necessity is the mother of all (or most) inventions.
 


moelex23......ulitaka Zitto ajiuzulu kutoka kwenye kamati?!!!.......ndio maana watu walitaka sana kujua msimamo wa yeye mwenyewe Zitto ni upi...
 
...................Across the country voters are shocked at the news stand to read that Zitto anataka sheria ibadilishwe kuwa accomodate Dowans! ...............

Kuhani,

Zitto anasema, mtafutieni hiyo sheria mnayodai kuwa inakiukwa!
 

waveche sana baba/mama...............aika mbe.........aika meku.........well done....nina hakika brother zitto ame print hii kitu na anaisoma kwa utulivu then kesho atameza matapishi yake kwa kisingizio cha kupotoshwa..........THIS IS TANZANIA.........teh,teh,teh......
 

Ogah,

Swala siyo chombo bali swali ni kwamba kwani TANESCO hawawezi kutangaza tender ya kununua mitambo mipya? Hivi option ya TANESCO ni kukodi mitambo kila kukicha?

Tendering process ya kukodi mitambo na tendering process ya kununua mitambo mipya inachukua same time. Mitambo hiyo iwe ya kukodi ama kununua bado itabidi isafirishwe kuletwa Tanzania na kuifunga ili kuiunganisha na grid ya taifa. Sasa hapo kuna tofauti gani kati ya option ya kununua mitambo mipya na kutangaza zabuni ya kukodi mitambo?

Tulishaumizwa kwenye kukodi mitambo ya IPTL, SONGAS, AGGREKO na mwishoni RICHMOND/DOWANS, hivi bado hatujajifunza kwamba option hiyo ndiyo inatuumiza kila kukicha na ndiyo maana mpaka leo hii tunaongelea capacity charges.

Mimi nilidhani option nzuri kwa TANESCO ni kutangaza tender ya kununua mitambo mipya badala ya hii idea ya kukodi mitambo. Wakinunua mitambo mipya ni ya kwao na ni ya kudumu na inaweza kukaa hata miaka 30 au zaidi. Lakini hii habari ya kukodi kila siku ndiyo imefanya umeme wa Tanzania uwe ghali na pia TANESCO wajiendeshe kwa hasara.

Je, kununua mitambo ya Dowans ndiyo option pekee? Kwanini tunaji-limit kwenye option ambayo ina-cast doubt mbele ya macho ya wananchi ambao tayari walishaumwa na nyoka na hivyo wakiguswa na unyasi wanaruka wakidhani nyoka karudi tena?
 
Kuhani,

Zitto anasema, mtafutieni hiyo sheria mnayodai kuwa inakiukwa!

Wamtafutie wakati yeye amekuwa akii-quote katika maelezo yake? Kui-quote tu ni ushahidi tosha kwamba anayo na alishaisoma sasa waiweke hapa ili iweje? Ichambuliwe ama tuangalie vipengele vya kufanyia marekebisho ili kuruhusu ununuzi wa mitambo chakavu?

Kuna magazeti yaliandika kwamba Mh. Zitto anapendekeza sheria hiyo ifanyiwe marekebisho ili tuweze kununua mitambo ya Dowans, kwa hiyo alishaipitia na anaifahamu vyema sana na anajua hata sehemu ambazo zinaweza kurekebishwa ili kulinusuru taifa lisiingie gizani. Lakini nadhani Mkuu Nentanyahu amemjibu vyema kwamba process ya kurekebisha sheria haiko rahisi kiasi hicho na haiwezi kuchukua muda mfupi na hasa kama kweli tuko kwenye dharura. Maana lazima marekebisho yaende Bungeni yawe discussed na yapitishwe.
 
Wataalam wa sheria naomba mnisaidie maana mimi ni kilaza wa sheria kabisa. Hivi serikali inapotaka kununua vitu huwa inatangaza zabuni ama na yenyewe inaruhusiwa ku-bid?

Nimeuliza hilo kwa sababu maelezo ya Mh. Zitto yanasema kwamba Tanesco wali-bid kununua mitambo ya Dowans baada ya kampuni hiyo kutangaza kwamba wanauza mitambo yao. Je, sheria inaruhusu ku-bid kwenye tender kama hizo? Achilia mbali uchakavu wa mitambo ya Dowans ninaongelea kwa ujumla. Maana sijawahi kusikia serikali ama shirika lake lime-bid kununua kitu kwa zabuni, ila mara nyingi huwa ninaona wao ndiyo wanatangaza zabuni ya kununua vitu.
 

Keil,

natambua kuwa TANESCO wana authority ku-execute procurement ikiwa kama Gvt parastatal........ninachojiuliza na kutokana na maelzo ya Mh Zitto ni HOW.......procurement procedures ziko wazi.....ndio maana nikauliza walifikiaje hatua ya kwenda ku-BID mitambo ya Dowans...how didi they reach there...?

nakubaliana na maelezo yako kwa sana, na hata ukiangalia mambo mengi uliyoeleza, nimeyasema hapo awali.......ninachojaribu kufanya ni kuchukua one statement after the other ya Mh Zitto...........ili tuichambue

Jibu la ile quotation toka kwa Zitto ni kuwa.......SI LAZIMA KUKODI MITAMBO.....TUNAWEZA KUNUNUA PIA

.....next alichosema Mh Zitto ni kuwa eti.......hiyo sheria ya manunuzi kuwa ni lazima tununue mitambo mipya iko wapi.......and i quote below

PART V sasa basi inawezekana waandishi wetu wa magazeti walim-quote vibaya Mh. lakini hicho ndicho alichokiandika hapa JF (yeye mwenyewe Zitto)......

tuendelee kujadili
 

Ukiangalia vizuri procurement Act......itakuwa inaelezea ni kwa jinsi gani procurement entity (kama TANESCO) inavyoweza ku-PROCURE i.e renting/leasing, purchasing/buying or acquiring services.....ndicho ninachokumbuka.......kuhusu serikali/TANESCO ku-BID.......mmmhh

hapo nyuma nilisema hivi


tuendelee kujadili
 
Mwanakijiji,

Naomba kujua mahojiano hayo yatarushwa saa ngapi ili niweze kuyasikiliza. Maana kwenye post yako umesema yatarushwa leo, ila muda ndo ambao hukusema.
 
mbona una wasiwasi, mimi siandiki maswali wala majibu yake, utasikia mwenyewe haya mambo ya kunukuliwa ndiyo niliyoyakwepa. Kama kuna maswali ya ziada baada ya wewe kusikia niandikie halafu tutamtafuta kumuuliza tena.

Yaweke basi hayo mahojiano na Ngeleja tunayasubiri kwa hamu kuu, unangoja nini tena!?
 
Within the hour.. yataweza kupatikana katika sites zote.. JF.. Mwanakijiji na Podomatic..
 
Inakuwa vipi waziri Ngeleja hajui hiyo Dowans inatoka wapi na inamilikiwa na nani? At the same time anataka kuingia nayo deal kubwa ya kununua mitambo? Wizi mtupu!
 
Yaani Waziri hajui hiyo Dowans ni ya nchi gani,lakini yuko radhi kuwapa tenda! hii ni ajabu!

Unajua kuwa na nia nzuri ni tofauti kabisa na kuitimiza hiyo nia kwa vitendo, pamoja na nia nzuri ya serikali je hii ndo njia bora ya kuondoa ama kupunguza tatizo la umeme nchini?, je option B iko wapi, option C je?
 
Last edited:
ZITO na SLAA mmenikatisha tamaa kupita kiasi katika hili,nikiwa mfuasi wa CHADEMA nasikitika kusema kuwa kwa mtaji huu ni heri ZIMWI TULIJUALO CCM,naona huu unaweza kuwa kama mwendo wa Zambia kumtoa KENNETH KAUNDA kumuweka madarakani fisadi FREDRICK CHILUBA,kweli " Mi-Wana-SiHasa-ya-Kiafrika-Ndivyo-Ilivyo".
 
Hivi hawa viongozi wetu wamekumbwa na pepo gani?... Yani Ngeleja anataka kutuambia nchi imekubali kabisa kuwa held hostage na predatory businessmen?...Nchi yenye dola kamili na balozi zimezagaa mataifa yote makubwa.

Ana maana gani kusema kuwa, serikali haiwezi kuwashindanisha Dowans eti sababu ni kuwa aliyetangaza tenda ya kuuza mitambo ni Dowans, kwa maana nyingine serikali yetu kwenye hili imegeuka kuwa ni bidder. Complete reverse of roles, yaani tutanunua kwa bei atakayotaka huyo vendor ambaye ni Dowans.

Halafu anaongelea best practices. Best practices za wapi za kusource such heavy infrastructure equipment kwa kumfuata vendor mmoja?... Ambapo utanunua kwa bei aliokupangia na utanunua mashine hizohizo huna alternatives za kufananisha, badala ya kushindanisha masupplier wengi ili uweze kupata the best possible deal....Siku zote kwenye such sectors za suppliers wachache(olygopolies), best deal utaipata kwa kuwashindanisha manufacturers wenyewe sio kina Dowans.

Anataka kutuambia kwa vile mtu unajua ATC wanamatatizo, unaenda ulaya unanunua dege lako, unakuja kuliweka JNIA pale, then ghafla unatangaza kuliuza kwa bei yako. Halafu unakua na certificate ya mtaalam flani kuwa ndege inaruka. Then serikali itakuja kusema the same porojo au vipi?...Kuwa tununue tu kwa vile mwenye dege kaamua kuliuza na uzuri limeshafika JNIA, na ATC ina matatizo. Kwahiyo ni kulinunua tu na kuanza safari. Manunuzi gani ya umma yanafanywa kwa style hii.

Atuambie if that is the case, serikali ingefanya nini au iliandaa nini kama Dowans wasinge tangaza kuuza mitambo yao?...Maana to me Dowans kuamua kuuza mitambo ni kitu adhoc kwa serikali. Wao walipanga nini in the first place kukabiliana na hilo giza linalopigiwa mayowe?....Yaani anataka tuamini kuwa ni mere coincidence kwamba crisis ya umeme imebite na Dowans wametangaza kuuza mitambo yao, as if hao Dowans wanategemea wateja wengine weengi apart from Tanesco...

Hii cheap talk ya kutuambia tusidhani kila mtu ni fisadi wala asituletee. Sijawahi kumsikia fisadi yeyote including waliokutwa na vijisenti na wakashindwa kuvitolea maelezo aliyewahi kukubali, ametuchezea mchezo mchafu. It will be pretty naive kwa mtu kuiamini tu kauli ya "mimi sina maslahi binafsi" wakati vitendo vyake mashaka matupu.
 
Unajua Mitanzania kwa 10% yaani wapo lazi wanunue hata kitu cha kutumia wiki 2 ila wao wanajali 10% kwa matumbo yao na hawajali kuwa baada ya wiki 2 hizo na wao watasuffer.Huku Kwetu Kigali tunatupilia mbali mutu kama hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…