Bob,
...tena kuna mtu hapa hapa JF alisema.......wakati ule tunajadili ile issue ya RDC........kuwa hii mitambo TUTAKUJA KUINUNUA.........na sasa inatokea..........wallahi sijui Tanzania tumeingiliwa na Kichaa gani.......damn!
Baada ya meneno mengi Mimi ningependa tuwe action oriented
hivi kutatua matatizo ya umeme Tanzania Sasa hivi option tulizo nazo ni Zipi?
Heheheheee....action what?
Option tuliyonayo ni kutengeneza mitambo na vifaa vya kuzalisha umeme sisi wenyewe. Swali, je tunao huo ubavu? Do we have what it takes? You be the judge...
Una maana Luhanga na Engineering yake Hawezi Kutengeneze? Basi tuwaulize wa Finnish lakini cha msingi sasa tuanze kufanya kitu
Kama Dowans ingekuwa contract yake haina ufisadi, tungeweza kuangalia kama tunaweza hata kuongelea uwezekano wa kudiscuss manunuzi.
Wadanganyika kwanza lazima tumjue huyu Idris Rashid ni nani katika vita yetu na hawa mafisadi.; huyu bwana ni mdau wa kampuni zote mbili anzia Richmond na sasa Dowans. Ubia wa Rashid katika kampuni hizi unapitia kwa watu wawili ambao ni partners wake kibiashara nao ni Rostam na Noni wa BOT ambao waliwekeza pamoja toka Vodacom na hata wakati fulani yeye Rashid akawa kinara wa Vodacom kwa muda mfupi!! Sasa katika biashara zao, hii mitambo yao ya Dowans wasipoiuzia Tanzania watakula hasara kibiashara kwahiyo lazima watafute kila hila waiuze hapa si kwa manufaa ya wadanganyika bali kwa kupunguza hasara zao. Sasa wanatumia hila through position ya Rashid Tanesco to create panic [fear factor] kwamba bila kuinunua hii mitambo, basi nchi itaathirika kiuchumi; kudhihilisha hilo Rashid anacreate artificial shortage ya umeme na kuanzisha load shedding as a way ya blackmail watu waamini kuwa bila kununua hii mitambo chakavu nchi haina alternative nyingine isipokuwa giza !! Hii nddio deal yao mpaka sasa wameishaiuza kwa wakina Zitto nao wameuvaa Mkenge!! Hawa mafisadi wabaya sana; Rashid kishatuibia kwenye Radar na Chenge wake leo huo uzalendo wa kutuonea huruma ameutoa wapi? Jamani tuamke huyu hatutetei sisi anatetea commission yake hapo!!
JF ni jukwaa muhimu sana na linaheshimika kwa wale 'middle class', ni eneo la kuchota taarifa na maarifa wakati mwingine.
Hapana. Mimi binafsi suala hili sio la lazima. Kwamba do or die. Hapana. Options zingine ziangaliwe pia au hata kutonunua kabisa Dowans bali tununue mtambo wa kuziba hii nakisi. TANESCO imekuwa despecified mwaka 2007 na hivyo kuweza kuwekeza na hata kukopa. These are facts and tuziweke facts mezani bila kuzipinda. Mjadala huu tusichukue sides. Tuelimishane na kwa sisi wawakilishi wenu Bungeni tukiona hoja hapa tunaibeba wazee. Tumefanya hivyo mara kadhaa. Tuweke hoja na tukate issues an hatimae kufikia hitimisho. Mtu mmoja adraft maazimio hapa na mwishowe tuseme, haya ni ya JF, Zitto peleka huko. Hapo JF itakuwa imesaidia Taifa. Hii kulalama lalama hapana!
Wakuu mimi hapa naona bado ni changa la macho.
Mitaambo hii wakati wa mchakato wa Richmond tuliambiwa ni kutoka "Pratt and Whitney" ambayo ni kampuni ya marekani halafu leo hii tunaambiwa kwamba eti kuna the so called "mtaalamu kutoka ujerumani" ameikagua na kuona ni safi hatuambiwi huyo mtaalamu ni kutoka kampuni gani, na je kampuni hiyo inatambulika na pratt & Whitney kama insperctors???????? Na after all huyo manayeitwa mtaalamu ana uzoefu gani na shughuli za ukaguzi wa mitambo kama hiyo.? Je is the guy insured kutokana na ukaguzi wake?
Well kuna hili la guarantee!!!! Guarantor wa hiyo mika kumi ni nani? na kama ni Dowans mbona kampuni yenyewe imekaa kisanii sanii, kwani ni wapi ina shughuli zingine kama hizi?
Halafu eti tunatishwa kwamba tusiponunua nchi itaingia gizani! wht a joke?????????? si kisingizio hiki hiki EL alitumia kuhalalisha Richmond?????? Hawa jamaa wamekuwa wapi miaka yote hii toka 2006?
Pia kuna hili la kuchekesha zaidi eti kwamba Tanesco inaidai Dowans kama USD 11m, na kwamba eti tukinunua hiyo mitombo tutakatana humo humo. Huu ni utani tena utani wa masuala ya nguoni!!!!!!!! Yaani ina maana Tanesco inaogopa kumdai Dowans ambaye ana mitambo kwenye yadi ta Tanesco???????? Deni ni Deni hata Tanesco isiponunua hiyo mitambo bado Dowans anadaiwa.
Halafu juzi nimemsikia yule Mkurugenzi Idris aking'aka kwamba mitambo lazima inunuliwe na eti watu wengine wanafikiri wengine hawakwenda shule. Hv huyu jamaa anafahamu kwamba ana questionable credibility?
Hivi hawa wakulu wanatuonaje watanzania?????? Wanatuona sisi mafala sana eeh??? Wanatuona sisi ni kuku????
Pia nashindwa kumshangaa mtu nayemuheshimu Zitto kushabikia ununuzi huu. Yeye ni mwanasiasa anafahamu nini kuhusu mitambo ya umeme? These people should know kwamba huwa tunawasapoti pale wanapokuwa na facts na si kwamba we have just aligned to them. When they are wrong wanapaswa kukosolewa!!!!! Na katika hili nnaamini opinion ya Zito si sahihi!!!!!!
Ochu, heshima mbele mkuu
Asante kwa analysis yako but with due respect I have to differ with your opinion.
Kama sheria ya Tanzania ndio imeanishwa kutumika katika huo mkataba basi uchambuzi wa sheria hapo juu waweza kuchukua mkondo wake.
Lakini, as i can feel it, this was a kind of International Business Transaction na inanifanya nichelee kukubaliana na wewe kuhusu hizo principles ulizoweka hapo juu unless umeona mkataba unasimamiwa na sheria ya nchi gani au kanuni zipi; yote yanawezekana, unaweza kuta Tanzania courts do not have jurisdiction on the matter na kwamba ikitokea kukiwa na msuguano wa mkataba, labda Iternational Arbitration will take over mfano mzuri ni Kesi ya IPTL na TANESCO ambayo ilifanyika hapa marekani.
Deal kubwa kama hiyo, I am sure jamaa watakuwa wameweka kifungu kinachoonyesha sheria ya nchi gani itatumika au vitu kama Incoterms au UCP.
Kwa hiyo tukiupata huo mkataba itakuwa vema na rahisi kuuchambua otherwise we are just dealing with some kind of speculation.
**************
Inavyoonekana Mawakala wa mafisdadi hawakosekani. Wako kila mahali, watajaribu kuweka uhalali katika kila haramu, wataliita giza kuwa mwanga, watachimbua kila sheria, watachunguza kila kipengele, kanuni, taratibu -- watatembea kila urefu wa kilometre hapa duniani na hata ahera ili tu watafute kisingizio cha kuwaibia Watanzania masikini.
INAONEKANA KAMA VILE HAKUNA SERIKALI HAPA KUZUIA HII. SERIKALI INAYO KILA HAKI KUSTOP -- KWANI LAZIMA??? WANANCHI TUSIKUBALI MAFISADI WATUZIDI KETE, TUSIKUBALI KABISAAAAAAAAAAA!