Dowans: Another Richmond in making?

Dowans: Another Richmond in making?

Naomba niulize: suluhisho pekee, bora, na linalowezekana kuzuia matatizo ya umeme nchini ni kununua mitambo ya Dowans? Kwamba katika kufikiria kwetu kote tumebakia na Dowans as the only and absolute option?

Naomba TANESCO watuambie wanahitaji mitambo yenye sifa gani, and I promise you I can get a better deal!!
 
Naomba niulize: suluhisho pekee, bora, na linalowezekana kuzuia matatizo ya umeme nchini ni kununua mitambo ya Dowans? Kwamba katika kufikiria kwetu kote tumebakia na Dowans as the only and absolute option?

Naomba TANESCO watuambie wanahitaji mitambo yenye sifa gani, and I promise you I can get a better deal!!

Mkuu mbona Dr Idrisa Rashid (Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco) alishasema kuwa hawana njia nyingine ila kununua mitambo ya Dowans? Hapo ndipo napata kizunguzungu! Kwamba ama tununue mitambo ya Dowans tuepuke giza au tuingie gizani. Tumerushiwa kitanzi tujinyonge wenyewe.
 
Idrissa , anajaribu kusema eti kuagiza mitambo itachukua miezi sita kupata mitambo kutoka China.

Anasema kama tusiponunua mitambo ya Dowans na kwanza ni lazima sheria ya manunuzi ibadilishwe ndipo tuweze kununua mitambo hiyo ili sheria iruhusu kununua mitambo chakavu.

Anasema zinatakiwa dola milioni 90 kununu mitmbo hiyo yenye megawat 90, sasa hapa anazidi kunichanganya zaidi kwani kama kuna suala la kubadilisha sheria ,itachukua muda gani?kujitisha Bunge na kupitisha marekebisho ya sheria ili tuu mitambo ya Dowans inunuliwe.?

Kama hali ndio hii inaonekana kuna kitu zaidi ya kununua mitambo, kwani Dowans si waiuze nchi nhyingine? Kwani lazima sisi tununue mitambo chakavu?
 
Naomba niulize: suluhisho pekee, bora, na linalowezekana kuzuia matatizo ya umeme nchini ni kununua mitambo ya Dowans? Kwamba katika kufikiria kwetu kote tumebakia na Dowans as the only and absolute option?

Naomba TANESCO watuambie wanahitaji mitambo yenye sifa gani, and I promise you I can get a better deal!!

Mitambo ya Dowans inaweza kuzalisha megawatt 100, hivyo fuatilia kama kununua mitambo ya kuzalisha umeme wenye megawatt hizo unagharimu pesa nyingi kiasi hicho.
 
Idrissa , anajaribu kusema eti kuagiza mitambo itachukua miezi sita kupata mitambo kutoka China.

Anasema kama tusiponunua mitambo ya Dowans na kwanza ni lazima sheria ya manunuzi ibadilishwe ndipo tuweze kununua mitambo hiyo ili sheria iruhusu kununua mitambo chakavu.

Anasema zinatakiwa dola milioni 90 kununu mitmbo hiyo yenye megawat 90, sasa hapa anazidi kunichanganya zaidi kwani kama kuna suala la kubadilisha sheria ,itachukua muda gani?kujitisha Bunge na kupitisha marekebisho ya sheria ili tuu mitambo ya Dowans inunuliwe.?

Kama hali ndio hii inaonekana kuna kitu zaidi ya kununua mitambo, kwani Dowans si waiuze nchi nhyingine? Kwani lazima sisi tununue mitambo chakavu?

Mkuu Kiranja,

Naenda kupumzika ila roho inaniuma sana. Naona hata Mh Dr Slaa amezidisha kunichanganya. Labda nimemuelewa vibaya na labda pia sijamuelewa Zitto. Siamini kama kuna mtu kati ya hao (nawaheshimu sana) angeweza kuonesha hata dalili za kuunga mkono ununuzi wa mitambo ya Dowans. Hata kama nchi ingekuwa inaungua moto na mitambo hiyo ni maji ya kuzimia huo moto. Hivi unaanzia wapi kujadiliana na mtu ambaye ulimwita (na wengi tunaamini bila shaka lolote) kuwa ni mwizi? Na siyo mwizi tu (kama vibaka wa mtaa wa Kongo) ni fisadi mkubwa aliyekwiba pesa zetu kwa mabilioni, yaani million 1000 mara makumi kibao! Sina hamu na kila kitu, ngoja nikalale.😕
 
Kuna taarifa kuwa wageni wengi wanaofanya kazi kama meneja wa hoteli nyingi za kitalii nchini especially in our national parks wanawashauri watalii kutotembelea Tanzania maana is the most expensive destination,Je kuna mtu ana more datas about it?
 
1229518579_waziriwanishati.jpg


[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]“Serikali imetafakari maoni ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na imejiridhisha kwamba ni vema TANESCO wasishiriki kwenye zabuni ya ununuzi wa mitambo ya Dowans.

“Serikali tayari imekwishaiagiza TANESCO kutoshiriki kwenye zabuni hiyo. Wizara ya Nishati na Madini na Serikali kwa ujumla tuna imani kubwa na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Bunge kwa ujumla. “Kwa kuzingatia maslahi ya Taifa pamoja na sababu zetu ambazo tuliziona ni za msingi katika nia ya kushiriki kwenye zabuni, tumeona ni vema TANESCO isishiriki zabuni hiyo,” alisema
[/FONT][FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]William Ngeleja, [/FONT][FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Waziri wa Nishati na Madini, [/FONT][FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sasa cha zaidi nini hapa?
[/FONT]​

Tatizo ni kuwa dalili zimanza kujitokeza kuw Ngeleja (serikali) inataka kukiuka kauli hii iliyoitoa siku si nyingi zilizopita
 
Kuna taarifa kuwa wageni wengi wanaofanya kazi kama meneja wa hoteli nyingi za kitalii nchini especially in our national parks wanawashauri watalii kutotembelea Tanzania maana is the most expensive destination,Je kuna mtu ana more datas about it?

Logic inakataa... hawawezi kuukata mkono unaowalisha.

Hata hivyo Tz utalii ni gharama nafuu kuliko nchi zingine (but needs data to justfy).
 
Hatimaye Rostam Ametushinda kwenye DOWANS?
Dowans bado hajatushinda...

Angalia vipengele vifuatavyo..

3.10 Decomission...Lazima mitambo iondolewe ndani ya miezi mitatu na mahala palipokuwa pamefungwa mitambo hiyo parusidishwe kwenye hali yake ya mwanzo... Mapaka leo mitambo hii haijaondolewa wala mahala hapo hajatengenezwa kama mkataba unavyotaka..

4.4 Inataka Tanesco walipwe $10, 000 kwa siku kwa kutoiondoa mitambio hiyo, je wamelipwa, wanalipwa au watalipwa?

5.1. Inasema Richmond shall exist under Tza LAW... na ukiangalia sheria zetu, Richmond do not exist because of misrepresentation of facts and fraud by Richmond, hii pekee inafaa kuwaondoa Richmond hiyo mitambo...

5.1 (b) INASEMA supplier not to violate laws of Tanzania... yako wapi sasa mbona Richmond hawajabanwa katika Hili? Hivi hawa akina Ngereja walikwenda shule au walikimbia umande?

14.1 & 14.1 (b)inazungumzia Arbitration.. Hii pia iko kwenye TZA favour kwani Arbritration au ICC ni Lazima iwe Tanzania ni si vinginevyo...

14.2 Choice of law.. pia hii inasema kwamba ni lazima sheria ya Tanzania itumike, sasa kama ndo hivi shida iko wapi?
 
Inawezekana ikawa ghali,mfano kuna tofauti ya dollar zaidi ya 300,kwenye ticket moja ya kutoka Amsterdam Kilimanjaro,compare to jomo kenyata,pia serengeti ni ghali mara mbili zaidi ya masai mara,au kruger national park,na lodges pia ni ghali zaidi Tz
 
Here's the Bottom Line,

Tulikuwa kwenye GIZA na MGAO kabla RICHMOND haijapewa kazi, wakatuzungusha kwa miezi kadhaa mpaka walivyojitoa.

ATHARI KWA UCHUMI: JK alisema hakuna loss yeyote kwa uchumi wakati wote wa mgao.

SOLUTION FOR NOW: Tuko tayari kukaa gizani kwa miezi mingine 10 mpaka mitambo mingine mipya inunuliwe. Sisi sio watoto tena. Kama ni urgency, ipo wakati wote lakini kwa sababu kila mrija wa CCM umefungwa, wanataka kutudanganya tena, NO MORE!!

Its time for all wananchi to wake up and stand for our country and not this nonsense.

Bwana Idrissa hana uhalali wowote wa kuwa na wadhifa huo kutokana na madudu aliyoyafanya na mafisadi wenzake.

Hiyo mitambo kama ilinunuliwa na RICHMOND (Pesa za walipakodi), kesi iko mahakamani, mitambo bado ni ushaidi wa kesi hakuna kuinunua.
 
Waheshimiwa Dr. Slaa na Zitto naona hata aibu kwa jinsi mlivyoingia kwenye hili suala bila kufikiria kwa undani, and the only Conclusion ni kuwa SOMETHING IS FISHY and I have to go even further and look at the possibility of Corruption.

Tanzania kuwa na uhaba wa umeme in few months is a valid point and should have been a starter point of what to do. U guys want to force the issue and say Dowans is the only option of preventing Tanzania from Total darkness?? Really?? So if dowans generators explode accidentally, as a NATION WE ARE DOOMED!!!

Zitto na Dr SLaa, this is the end of upinzani tanzania sababu mmeingia kwenye suala ambalo mnakuwa mnawapa Mtandao nguvu kupitia jasho na damu ya wananchi iliyolipwa ili kuliokoa taifa letu. Shame on U guys, halafu mnajifanya mnaongea kwa undani na maneno mengi.

Point, Tanesco waseme :: Je dunia hii sasa hivi kuna kampuni kubwa kama GE au Wartsila ambazo zinaweza kuleta Generators mpya Tanzania za 100MW in 6 months @ a cost of USD $80 million????

Jibu litakalopatikana hapo, ndio tuanze kuangalia what is next.

Sasa nyie mnaongea eti tunataka mitambo ya dowans, as if mitambo ya dowans ndio issue wakati issue ni Tanesco wanahitaji 100MW in few months!!!

Zitto na Dr. Slaa, ningependekeza also mjiuzulu JF tubaki wenyewe sababu hapa inabidi nifuatilie kwa undani inaelekea lazima kuna blackmail toka kwa wakuu wa mtandao imetembea!! ( This is just me thinking out loud, what will push U guys into this corner of Publicly supporting Lowassa and Rostam @ a very high and suicide political cost??).

Rostam & Lowassa are our leaders, na ninapendekeza wananchi wa Tanzania tupledge allegiance kwao, sababu kama hata Dr. Slaa na Zitto wamekuwa spokepersons wao, we are doomed.

Rostam & Lowassa, I ................ will like to ask U guys if U can help our nation since U now have ABSOLUTE CONTROL of judiciary, Government & Parliament.

May God BLESS TANZANIA, May God Bless the powerless in our villages and May God Destroy those who Support Mtandao.
 
Tatizo ni kuwa dalili zimanza kujitokeza kuw Ngeleja (serikali) inataka kukiuka kauli hii iliyoitoa siku si nyingi zilizopita

Dalili gani zimeanza tena toka watangaze wameghaili hii mipango? Zaidi ya madai yaliyoibuliwa ( sio na Waziri ) kwamba tununue mitambo ya Dowans kwa sababu mwezi April, mwezi wa masika, umeme utakatika kuna nini kingine? Ndio hizo dalili za mvua za April tunazoongelea au kuna lingine?
 
Jamani waacheni wanunue, fedha wanazo, sababu wanazo na uwezo wanao!! Tukubali wanunue yaishe!!
 
Kiranja,
Mitambo ya Dowans inaweza kuzalisha megawatt 100, hivyo fuatilia kama kununua mitambo ya kuzalisha umeme wenye megawatt hizo unagharimu pesa nyingi kiasi hicho.
Unajua mkuu hawa wanasiasa wanataka kutuchezea akili zetu wakati sisi wengine hapa biahsra ndio zinatuweka duniani..
Swala lka kufikiria gharama hadi kesho nitalipinga sana na sababu nitazitoa kutoka mfano mdogo wa biashara zetu za nyumbani..
Mathlan mtu unakodisha bus (lease) la Scandinavia kufanya biashara ya safari za kwenda Mbeya..
1. Tatizo linalojitokeza ni ubovu wa mkataba wa awali, kwanza unagundua kuwa bus hilo hata hao Scandinavia wamelikodisha hviyo hawana gharama zaidi ya kucheza mchezo ya kati, mchezo ambao unakuigharimu ulipe shilingi 80 kwa kila 100 unayotengeneza...
Hivyo unapoamua kuvunja mkataba huo ni ujinga kufikiria kununua bus la Scandinavia kwani utakuwa unalipia gharama zao + interest...na pili ni lazima wataweka chochote mbali na kwamba umewaponyesha kurudisha deni lao..+ interest ya kila mwezi au mwaka ambayo wamekubaliana na financer (mtoa mkopo)..

Kwa mfanya biashara yeyote atafahamu kwamba huhitaji middleman ikiwa unaweza ku lease bus wewe moja kwa moja kutokana na sababu zilizotangulia., In this case nitarudi kwa ktk utata wa Richmond deal..

2. Tatizo jingine sio ukubwa wa bus kuweza kuchukua abiria 50 isipokuwa ni hali ya bus lenyewe!.. huwezi kuacha kununua bus jipya kwa kigezo kuwa hili bus linachukua abiria 50 kisha ukatazama gharama yake wakati kuna ma bus yanayoweza chukua abiria chini au zaidi ya hizo 50..kwa hiyo kigezo cha uwezo na gharama ya bus sio chanzo kinachoweza kutumika kama sababu..
Unataka kununua hilo bus kwa sababu nje kabisa ya uwezo na gharama kwani ni ujinga kufikiria gharama au kupoteza asilimia 80 ya pato la awali kwa Scandinavia ikiwa pato hilo linaweza patikana pia ukinunua bus jipya ambalo vipengele vyake kuhusiana na interest, guarantee, maintanance, spareparts (vipuli) vyote utavipata under Your name badala ya mafundi wa kubabaisha wa Scandinavia..

3. Kama kuna sababu ya kunyang'anywa bus tusiponunua, hii wazi inatokana na kuchachamaa kwa Scandinavia sio uwezo wa mnunuzi!.hii ndio point yangu, ina maana tu Scandinavia wanataka ununue bus lao kutokana na mkataba wa awali hasa pale kisheria unaposhindwa kumsimamisha ndugu yako aliweka sahihi mahakamani kama mkosa!..Kama msahihi hana makosa kisheria iweje mkataba wa Richmond au Dorwans uwe na makosa ya kughushi!

Wakuu hapa hakuna hadithi, Lowassa na Karamagi walituingiza mkenge, na sababu kubwa ya kutowasimamisha hawa watu mahakamani wakaonekana kuwa na makosa ndicho kinachoweza kutumika na Dorwans kuwa mkataba wao ni halali na sasa hivi tunataka kujificha nyuma ya madhambi yetu wenyewe..
Kama Dorwans wamefikisha kesi hii ktk mahakama za kimataifa, kilichotakiwa sisi kufanya ni kuwaweka Lowassa, Rostam, na Karamagi hatiani kisha ushahidi huo ukatumika kuvunja mkataba wa Richmond.
Sisi tumechukua sheria mkononi kuvunja mkataba, tunametaka kuwapiga bao Dorwans bila kutumia vyombo vya sheria kutengua mkataba kwa sababu ya kinga kwa baadhi viongozi wetu, well ndio malipo yake haya!..
Sasa wasije na hadithi za SIASA kutufungia kanya boya hapa..maamuzi mabaya yametokana na siasa nyingi ktk utekelezaji...
 
Kuwe na shida ya umeme au kusiwe na shida ya umeme, mitambo ya Dowans tutanunua. Tusiponunua nani mwingine anunue? Hata huyo mwingine akinunua tutaishia kununua umeme kutoka kwake, so kwanini tusinunue tu hata kwa ajili akiba.

Tatizo ni kuwa mitambo hiyo haiwezi kukaa bila kutumiwa, haiwezi kurudishwa kwa muuzaji wa mwanzo, n.k. Watu pekee wa kuinunua ni serikali ya Tanzania. Sijui kwanini hatutaki. Hela ipo na sababu ipo!
 
Kuwe na shida ya umeme au kusiwe na shida ya umeme, mitambo ya Dowans tutanunua. Tusiponunua nani mwingine anunue? Hata huyo mwingine akinunua tutaishia kununua umeme kutoka kwake, so kwanini tusinunue tu hata kwa ajili akiba.

Tatizo ni kuwa mitambo hiyo haiwezi kukaa bila kutumiwa, haiwezi kurudishwa kwa muuzaji wa mwanzo, n.k. Watu pekee wa kuinunua ni serikali ya Tanzania. Sijui kwanini hatutaki. Hela ipo na sababu ipo!

Tatizo lako ni kutawaliwa na falsafa ya ujamaa. kwanini unaamini anayeweza kununua ni serikali peke yake? na kwanini Dowans wasiuze mitambo hiyo kokote kwingine duniani kama mitambo inafaa. Bidhaa yanye kiwango cha kutosha haiwezi kuwa na mteja mmoja!!!
Ununuzi ufanyike iwapo tu wataalam wa fani ya umeme na sheria za manunuzi ya serikali wataridhika na viwango vya mitambo na si vinginevyo. Haya mambo ya kitaalam inabidi msiyashabikie kisiasa.
 
Date::2/27/2009
Kununua mitambo Dowans si ufisadi
Na Ramadhan Semtawa

WAKATI Bunge la Jamhuri ya Muungano likiwa limenawa mikono katika mpango wa kununua mitambo ya kufua umeme wa dharura ya kampuni ya Dowans, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ameonyesha msimamo kutetea mpango huo, akisema si wa kifisadi.

Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ilishashauri kuwa serikali isinunue mitambo hiyo kutokana na kuwa imeshatumika, ikieleza kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria ya manunuzi ya umma, lakini serikali imeonekana kupitia mlango mwingine na kuwasilisha mpango huo kwenye kamati nyingine ya bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, ambayo iliomba kamati hizo zikutanishwe ili kutoa uamuzi kuhusu mpango huo.

Hata hivyo, katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah alisema hakuna haja ya kamati kukutana kujadili suala hilo kwa kuwa bunge halina uwezo wa kuilazimisha au kuikataza serikali kufanya manunuzi kama inavyokuwa wakati ikinunua magari yake na vitu vingine.

Kwa sasa mitambo hiyo inashikiliwa na Tanesco, ambalo linadai kuwa itatumika kama fidia iwapo shirika hilo litashinda kwenye kesi ambayo Dowans imefungua dhidi ya Tanesco kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Biashara iliyo Paris, Ufaransa.

Lakini jana, Waziri Ngeleja aliiambia Mwananchi katika mahojiano ofisini kwake kuwa kununua mitambo hiyo hakutakuwa na chembechembe zozote za ufisadi ingawa wengi wanahisi hivyo.

"Nchi haiongozwi kwa hisia," alisema Ngeleja, ambaye alitetea sana mpango wa kununua mitambo hiyo wakati akiongea na waandishi kuhusu uamuzi wa serikali kukubaliana na ushauri wa kamati ya bunge wa kuzuia kununuliwa kwa mitambo hiyo.

"Ni hatari kuacha kujadili mambo muhimu ya nchi yanayozingatia maslahi ya taifa, na badala yake kuendekeza hisia zisizo na mantiki,"alisema.

Ngeleja alisema kitendo cha watu kuhisi kuna kuna ufisadi katika mpango huo wa kununua mitambo hiyo, hakina mantiki, akisema kuwa serikali iko makini na haiwezi kukubali matokeo kama ya Richmond, ambayo ilipewa zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa mazingira tata na kusababisha Bunge kuingilia kati na kufanya uchunguzi uliosababisha Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa uwaziri mkuu na baadaye kufuatiwa na mawaziri wawili.

Ngeleja alisema vipo vyombo vya serikali vinavyosimamia sheria na vinafanya kazi kwa umakini na akahoji: "Hivi watu hawaoni vigogo wanavyoburuzwa mahakamani, sasa watu wanafikiri serikali imelala, kwanini tuendeshe nchi kwa hisia."

Alipoulizwa kama kuna msukumo wowote kutoka kwa watu ambao walituhumiwa kuhusika katika mpango wa kuifanikisha Richmond kushinda zabuni ya ufuaji umeme wa dharura, Ngeleja alijibu: "Umeangalia maslahi ya taifa tu."

Ngeleja alisema msukumo wa kutaka kununua sasa mitambo hiyo unatokana na kuangalia ukuaji wa uchumi, ambao mahitaji yake ya umeme yanaongekeza kwa asilimia kati ya 10 hadi 15 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi 2012.

"Utafiti uliofanywa katika Power System Master Plan (mpango wa kuendeleza sekta ya umeme) unaonyesha mahitaji ya umeme yanakua kwa wastani wa asilimia 10 hadi 15 kila mwaka katika kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi 2012," alisema.

Alisema changamoto ni kwamba mipango iliyopo ya kuongeza uzalishaji haitaweza kuziba pengo kati ya uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme na mahitaji ya umeme yanayotarajiwa kati ya mwaka huu na mwaka kesho, baada ya miradi ya dharura kuondolewa.

"Hii inatokana na ukweli kwamba, ni vigumu kubuni mradi unaoweza kukamilika kabla ya mwaka 2009 kuisha," alisisitiza.
Kuhusu bunge kushauri mitambo hiyo ya Dowans isinunuliwe kutokana na kwenda kinyume na sheria ya manunuzi ya umma, Ngeleja alijibu: "Ninachokumbuka, bunge lilijadili na kupitisha azimio kuhusu uhalali wa mkataba wa Richmond.

"Hakuna mtu anayepinga... mkataba wa Richmond ulibainika kuwa tata na serikali ilichukua hatua. Serikali haiwezi kuzembea wala kufumbia macho vitendo vya kifisadi.

"Juni 28, 2008 serikali ilitoa tamko la kusitishwa mkataba huo ifikapo Agosti mosi na kweli ilifanyika... hatua hiyo ilichukuliwa na serikali lakini pia kwa kuzingatia maelekezo ya bunge," alifafanua.

Alipoulizwa sababu za kung'ang'ania kununua mitambo hiyo kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umme ambayo inazuia taasisi za serikali kununua mitumba, Ngeleja alihoji: "Mbona watu wanasema tununue mitambo ya IPTL.

"Ni kweli sheria ya PPRA inatakaza ununuzi wa vitu vilivyotumika, lakini yapo maeneo ambayo kutokana na mazingira halisi ya kisekta si lazima kinachonunuliwa kiwe kipya.

"Angalia, ATC leo hii inaweza kununua au kukodi ndege lakini si lazima iwe mpya. Tuangalie maeneo ya msingi, jambo kubwa ni watalaamu kuthibitisha ubora na uwezo wa kukidhi mahitaji ya nchi. Mitambo ile unaweza kuifunga leo hii katika toroli na kuipeleka mkoa wowote wenye uhaba wa umeme."

Kuhusu gharama za kununua mitambo mipya kulinganisha na gharama za mitambo ya mitumba ya Dowans, Ngeleja alijibu: "Tuliwahi kupata mtaalamu akasema hii ya Dowans ni kati ya dola 58 hadi 60 milioni, wakati mipya ni kati ya dola 120 milioni... mara mbili ya hii."

Alisema uamuzi huo wa kutaka kununua mitambo ya Dowans, hauna msukumo wala mkono wa mafisadi kwani unalenga kuikoa nchi katika tatizo la mgao wa umeme.

"'Sasa hapa, utaona kwamba uamuzi huu hauna msukumo wala mkono wa mafisadi," alisema.

Utata wa mitambo hiyo ya Dowans sasa unaendelea kama sakata la zabuni ya ufuaji umeme wa dharura lilivyoanza. Dowans ilirithi mkataba wa Richmond iliyobainika kuwa haikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme huo wa dharura.

Matokeo ya uchunguzi wa kamati hiyo ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge Harrison Mwakyembe ulisababisha Lowassa kujiuzulu baada ya kutuhumiwa kuingilia mchakato wa zabuni na kushauriwa atumie busara kuamua juu ya ushiriki wake katika suala hilo.

Hali mkataba wa Dowans ukiwa umeshaisha, kampuni hiyo imewasilisha mashtaka Mahakama ya Kimataifa ya Biashara dhidi ya Tanesco, ambayo nayo imeshikilia mitambo ya Dowans ikisema kuwa itatumika kama fidia iwapo shirika hilo la serikali litashinda kesi hiyo.
 
ZeMarcoPolo,
Tatizo lako ni kutawaliwa na falsafa ya ujamaa. kwanini unaamini anayeweza kununua ni serikali peke yake? na kwanini Dowans wasiuze mitambo hiyo kokote kwingine duniani kama mitambo inafaa. Bidhaa yanye kiwango cha kutosha haiwezi kuwa na mteja mmoja!!!
Ununuzi ufanyike iwapo tu wataalam wa fani ya umeme na sheria za manunuzi ya serikali wataridhika na viwango vya mitambo na si vinginevyo. Haya mambo ya kitaalam inabidi msiyashabikie kisiasa.
Mkuu samahani, nadhani mwenye tatizo hapa ni wewe kwa sababu huelewi biashara hii kabisa!.. Hakuna nchi inawezza kununua mitambo iliyokwisha tumika unless nchi hiyo inaendeshwa kama yetu - Ufisadi..
Pili, sio swala la Ujamaa kuwa na chanzo cha umeme kushikiliwa na serikali. Nchi zote za kibepari chanzo cha uzalishaji umeme kinaendeshwa na serikali kisha suppliers ndio utawakuta watu binafsi.. Kama unakumbuka mwaka 2003, huko Marekani umeme ulikatika miji ya New York, hadi miji ya Canada na tuliona jinsi serikali hizi mbili wakitumia kila uwezo wao kuhakikisha Umeme unarudi kwa sababu hawa wote wana control uzalishaji na usambazaji ktk grid zao. Na ukiona shirika binafsi sehemu hizi basi wapo under contract kuendesha uzalishaji huo lakini sio wamiliki kama tunavyofanya sisi kinyume kabisa cha kuelewa umuhimu wa miundombinu na umiliki wake..
Ndio maana leo tunatishiwa tusiponmunua mitambo ya hawa jamaa tutakosa umeme, na kifupi na hatua jinsi kwa sababu ya Ufisadi!..
 
Hizi kauli za Waziri Ngeleja mbona zinanichanganya....au ndio waandishi wetu wanatupa habari nusu nusu?.....mara hatununui mitambi michakavu.......mara tunanunua mitambo michakavu..........
 
Back
Top Bottom