Kwa muda sasa wa zaidi ya majuma mawili kumetokea maneno mengi sana ambayo Kamati mbili za Kudumu za Bunge zimekuwa zikisema kuhusiana na ununuzi wa mitambo chakavu ya Dowans , ambayo ni masalia ya Richmond.
Kamati ya Nishati na madini inayoongozwa na Mh. Shelukindo ambaye ni miongoni mwa wabunge wakongwe na wasiokuwa na madoa ya ufisadi yanayoonekana wazi wakipinga TANESCO kununua mitambo hiyo chakavu kwani ni kinyume na sheria za manunuzi ya umma .
Na sababu ya pili wakitoa kuwa mitambo hiyo bei yake imeongezwa maradufu na wamiliki wa Dowans yaani price imekuwa infleted.
Kamati hii ambayo ndio yenye wajibu wa kusimamia masuala ya kisera kuhusiana na mambo ya Nishati na madini , ikiwa na msimamo huo ambao kwangu nauona kuwa ni sdahihi na unalinda masilahi ya Taifa letu ili kutokuendelea kuangamizwa na wezi hawa ambao tunakumbuka jinsi walivyoliingiza Taifa kwenye matatizo makubwa na hata kufikia mahali Taifa letu likakaa siku nne bila kuwepo kwa Serikali.
Kamati nyingine ya Hesabu za Mashirika ya Umma inayoongozwa na mbunge kijana wa Kigoma Kasikazini Zitto imejitokeza na kuwa kama wasemaji wa Dowans na kuitaka serikali inunue mitambo hiyo chakavu na kwa bei ambayo inasemekana kuwa imeongezwa makusudi na wamiliki wa Dowans .
Kamati hii ya Zitto kwa mujibu wa kanuni za Bunge toleo la 2007 ina majukumu yafuatayo,
1.kushughulikia taarifa za kila mwaka za hesabu zilizokaguliwa za mashirika ya umma .
2.kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za Mashirika ya Umma yaliyoainishwa katika taarifa za kila mwaka za hesabu zilizokaguliwa za mashirika hayo na kutoa mapendekezo na ushauri wa namna ya kuyaondoa matatizo hayo.3.kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyokwishatolewa na kamati hiyo ili kuondoa matatizo hayo.
4.kutathimini ufanisi wa mashirika ya umma .
5.kufuatilia utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma .
Nimeona ninukuu vifungu vya kanuni za Bunge ili kuweka hoja yangu iweze kueleweka kwa wengi .
Wakati kamati ya Zitto ikitakiwa kushughulikia mashirika yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha kama lilivyo shirika letu la Tanesco na kutafutia ufumbuzi , Kamati hiyo sasa imegeuka na kusahau majukumu yake na kuanza kuwa wasemaji wa Dowans na sasa wanataka kuliingiza shirika hilo kwenye matumizi mabaya ya fedha za umma na hata kununua mitambo chakavu kwa bei iliyoongezwa.
Kamati hii ya Zitto imepewa nini?
Nini kinamsukuma Zitto hata kufikia mahali pa kusahau majukumu ya kamati yake ?
Je?kinachomsukuma ni sawa na kile walichofanya wakina Karamagi na Msabaha badala ya kuwa wasemaji wa serikali wakawa wasemaji wa Richmond?
Nini kinaendelea kwenye suala hili?
Zitto ana masilahi binafsi kwenye suala hili?
Je?ni kweli kuwa anasimamia masilahi ya Taifa kwenye hili hata kama ni kwa kununua mitambo chakavu?
Nimeuliza maswali haya ili kuweza kumrudisha mbunge huyu kijana kwenye mstari kwani ununuzi wa mitambo hii ni mkakati maalum wa kujipatia fedha za kampeni kwa wanamtandao hapo mwakani 2010.
Nitaweka mengine hapa hapo baadae.
Kiranja,
Asante kwa maswali yako mazuri sana. Nadhani hoja yako inakosa kwa misingi kadhaa:-
i) Hoja yako na maswali yamejikita katika Kifungu cha 2 cha Majukumu ya Kamati ya Mashirika ya Umma kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge ambayo umeinukuu. Kwa bahati mbaya hapa nilipo sina Kanuni hivyo ninategemea umeinukuu vizuri hadi ukatuwekea hapa. Lakini-
a) hukugusia kabisa majukumu ya Kanuni kama yalivyo kwenye kipengele cha 3, 4, na 5.Vipengele hivyo vyote vinatoa nafasi kwa Kamati ya Mashirika ya Umma kushughulikia utekelezaji wa Maelekezo ya Kamati ( ingelikuwa busara ungelianzia kwa utafati kama Kamati hiyo iliwahi wakati wowote ilipokuwa inapitia mahesabu imewahi kutoa Mapendekezo yeyote ili kuinusuru hali waliyoikuta wakati wa utekelezaji wa jukumu lao. Ni jukumu lao sasa kufuatilia "utekelezaji wa maagizo yao". Generalization ni hatari sana. Hivyo vyema, kama unazo taarifa kuhusu mapendekezo hayo ungelituwekea hapa ili tufahamu hisia inayoanza kujengeka. Ni vyema Tanzania tusiruhusu "hisia" katika mambo makubwa kama haya.
b)Kifungu cha 2 cha Kanuni uliyoinukuu hapo juu kinazungumzia "tathmini ufanisi". Ni mpaka utakaponiambia kuwa Kamati ya Mashirika ya Umma haijafanya "tathmini" na au haina mamlaka ya kufanya tathmini ya ufanisi wa Tanesco, ndipo nitakapoona kuwa hoja yako ina msingi. Lakini iwapo Kamati katika taratibu zake za kawaida imefanya Tathmini ya shirika la Tanesco, basi ni vizuri "tathmini" hiyo ikafanyiwa mjadala kwa hoja zake bila kuunganishwa na chochote kinachohusiana na maswala ya Richmond/Dowans. Iwapo Kuna mambo ambayo Kamati ya Mashirika ya Umma imeyagundua ambayo ni kwa maslahi ya Taifa, sidhani ni vyema kuyakataa kwa vile tu Kamati nyingine imekwisha kufanya uamuzi. Ndiyo msingi wa hoja ya Kamati mbili kukutana ili mambo mapya yaliyojitokeza yafanyiwe kazi. Mimi nafikiri this is where our system becomes healthy, and with checks and balances. Hatuwezi kuyakataa mambo ambayo Kamati imegundua kwa kuwa tu tumefanya uamuzi, hata katika system ya Mahakama, kuna flexibility katika mazingira fulani fulani. Kama nimesoma sahihi ni kuwa Kamati ya Nishati na Madini ilikuwa haijawahi kuisikiliza TANESCO kama TANESCO . Hatuwezi kuadhibu Taifa kutokana na Technicalities na grounds ambazo hazina tija kwa maoni yangu. Iwapo Kamati mbili zitakaa kwa manufaa ya Taifa, mimi ninaamini kabisa mawazo ya watu wengi yana tija zaidi daima.
c) Kanuni ya 5 uliyonukuu inazungumzia Kufuatilia "utekelezaji wa Sera..." hivyo sioni kabisa mantiki ya hoja yako kwani huwezi kufuatilia utekelezaji wa Sera bila pia kutazama maswala yanayohusu capacity ya Taasisi husika.
2)Kiranja, Wakati nakubaliana nawe kuwa ununuzi wa mitambo hii inaweza kuwa mbinu mmoja ya Wanamtandao kupata fedha za uchaguzi kwa 2010, lakini hoja hii bado ni dhaifu sana, kwani huwezi kuadhibu Taifa zima likakosa umeme kwa sababu za kisiasa. Kuna njia nyingi zaidi za kudhibiti wanamtandao kuliko hii. Hivyo, objective debate na kupata definitive solution kwa maswala ya athari ya ukosefu wa umeme yasichanganywe na maswala ambayo kwangu yanahitaji majibu na hatua za aina tofauti kabisa. Let us sit down and think, and think aloud for the good of our country and avoid simplistic answers to complicated issues as this one.
4) Hoja ya kuwa TANESCO ilizembea kuagiza mtambo unaostahili tangu azimio la Bunge, kwangu pia is non issue. Uzembe wa uongozi wa TANESCO uwe dealt with squarely, bila kuhusisha na maswala ya msingi.
5) What I dont like is having double standards in our country. Tumeruhusu Serikali ijadiliane na IPTL kununua mitambo ya IPTL ambayo imetusumbua kwa zaidi ya miaka 15 sasa, na ni chakavu zaidi kuliko mitambo ya Richmond /Dowans at least one kama ilivyoripotiwa kwenye vyombo vya Habari. I have no problem kama issue ni kufanya independent assesment ya Wataalamu, hata kama inamaanisha kuingia gharama ya kuwapata wataalamu hao, iwapo tu tutathibitishiwa kuwa mitambo hiyo ni cheaper kuliko ku import mitambo ya aina hiyo hiyo au mipya kabisa. Wakati huo huo tunakataa kununua mitambo ya Richomond/ Dowans.
6) Maswala ya kijinai ya Richmond/Dowans yashughulikiwe kwa utaratibu wa Kawaida, na tunaweza kabisa kutenganisha maswala haya.
7) Swali la kwamba Serikali iliisha kulipa Richmond Dowans advance ya US$ 35 Million appears to me as a new revelation. But this is a separate issue and I think at this stage we need the Government to tell us the full story about its relations na watu hawa.Hata Bunge halikupewa Taarifa hii, and if this is true, this is very serious in my opinion. Hatujaambiwa pia kwanini Dowans hawajalipa hadi leo US $ 10 million ambazo wanatakiwa kutulipa kwa kila siku waliyochelewesha kuingiza umeme kwenye National Grid. Let us discuss the matter soberly na tutafikia ukweli na solution kuliko kujenga hisia.