Mkuu inawezekana na mimi nina mapungufu yangu lakini sidhani kama ni vibaya kusema kile ninachoamini! Tushindane kwa hoja sio ku-attack personalities!
Nimeona sasa hivi mmeshaanza kugeuza mjadala na kunijadili mimi badala ya hoja iliyoko mezani! Jadili hoja yangu zaidi ili tusaidia kujenga nchi yetu! Who knows? Unaweza kunishawishi nikabadili mawazo niliyo nayo na kuwa na mtizamo mpya, na ndio maana tuko hapa Jukwaani!
Na huo "undumila kuwili wa Watanganyika" unaousema ndio upi? Unasema hivyo kwa ajili ya "ku-balance equation" au namna gani? Mbona hutoi detail? Au ndo juhudi za ku-divert mada?
Tukianzia kwa wakati wa Utawala wa Abeid Karume hamkuwahi kumuuliza namna gani aliiendesha nchi yake ambayo mnadai kuwa si nchi wakati ikitawaliwa na mwenye nchi atakavyo.
Tatizo lenu wengi mliomo humu hamuujuwi muungano ulivyokuwa huko nyuma. Huko nyuma Mtanganyika akijijuwa Mtanzania tu bila ya kujuwa kuwa neno Tanzania limetokana na muungano na ndio maana wengi wenu mnashindwa kutofautisha uwepo wa mataifa haya mawili, Tanganyika na Zanzibar
Undumila kuwili wa Watanganyika unajionyesha pia katika wakati wa chama kushika hatamu, hamkuwahi hata siku moja kuuliza wala kudai kuwa mnanyimwa haki Zanzibar kwa vile Nyerere aliwafadhili wahafidhina wa Zanzibar chini ya CCM. Ni wakati huu ambao SMZ iliunda vikosi mbali mbali vya ulinzi chini ya Rais wa Zanzibar. Undumila kuwiliwa Watanganyika ulionekana mlipoungana na serikali ya SMZ kwenye mauwaji ya Zanzibar kwa kupeleka vikosi na viongozi wa Tanganyika kupongeza mauwaji hayo ambapo harakati zilipobadilika sasa mnalaani vitendo kama hivyo. Sijui unataka undumilakuwili gani zaidi ufahamishwe?