Double Standard Kuhusu Kauli ya "Zanzibar Sio Nchi!"

Double Standard Kuhusu Kauli ya "Zanzibar Sio Nchi!"

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Posts
13,192
Reaction score
1,976
Wakuu,

Si mara ya kwanza kwa Pinda kutamka kuwa "Zanzibar Sio Nchi" halafu kukazua mtafaruku mkubwa sana hadi tukaona purukushani za kubadili Katiba ya Zanzibar, 1984 ili ku-create "nchi" iitwayo "Zanzibar!"

Ni siku za nyuma tuliona aliyekuwa Jaji Mkuu, Augustino Ramadhan, pamoja na Majaji wengine wakitamka katika Hukumu ya Mahakama ya Rufani-Kesi ya Uhaini (Machano Hamis and others vs R case) kuwa "Zanzibar Sio Nchi" na kwamba "Uhaini hauwezi kufanywa dhidi ya Rais wa Zanzibar" kwa kuwa "Zanzibar Sio Nchi!" Hukumu hiyo haikuleta hasira yoyote kwa Wazanzibari lakini aliponyanyua mdomo "Mtoto wa Mkulima" kukawa na mzozo mkubwa sana ambao kila mmojawetu anaujua!

Swali ni kwamba kwa nini Wazanzibari hawakukasirishwa na kauli ya Jaji Mstaafu Agustino Ramadhan wakaja kukasirishwa na kauli ile ile lakini ikasemwa na Pinda? Why double standard? Au ni chuki tu kwa watu wa bara/ Tanganyika? Juzi tena Pinda "kazungumzia kuwa wanaotaka Tanganyika waeleze ni Tanganyika ipi waitakayo!"

Hili nalo limeleta "hasira" kwa Wazanzibari hapa JF utafikiri alikuwa anazungumzia kuhusu "nchi" yao! Hawa watu huwa siwaelewi kabisa! Ila wakipewa vyeo huku Bara kwenye Wizara ambazo si za Muungano wako kimya kama wamemwagiwa maji ya baridi! Lakini utasikia eti "Waziri Mkuu Pinda mwisho wake ni kisiwa cha Chumbe!" Hatusikii wakisema Makamu wao wa Kwanza wa Rais ambaye hata Katiba ya JMT, 1977 haimtambui mwisho wake wapi!

Wao wenyewe wame-acquire ardhi na kuishi Tanzania Bara bila bughudha yoyote! Hao ndo Wazanzibari bwana!!!

====================================
ADDITIONAL
====================================
Hivi ndivyo alivyosema Jaji AGUSTINO RAMADHANI, pamoja na Majaji wenzake katika Kesi ya SMZ v. Machano Hamisi and 18 others:

"After the above exposition, we have no difficulty at all to answer that question in the negative. The International Persons called Tanganyika and Zanzibar ceased to exist as from 26[SUP]th[/SUP] April, 1964 because of the Articles of Union. The two states merged to form a new international person called the United Republic of Tanzania.
The Rt. Hon. The Earl of Birkenhead has said at page 36: "A nation cannot indefinitely surrender the treaty-making power to another, and at the same time retain its existence as a sovereign state". We concur with this contention and we wish to point out that both Tanganyika and Zanzibar, and not Zanzibar alone, surrendered their treaty-making powers to the United Republic of Tanzania.
Thus, Zanzibar, just like its sister Tanganyika, is neither a state nor is it sovereign. The state and the sovereign is the United Republic of Tanzania."
 
wazanzibari wanawanyonya watanganyika, na kusema ukweli kwa mujibu wa katiba iliyopo Zanzibar siyo nchi,pamoja na kurekebisha katiba yao lakini ukweli una baki palepale si nchi
 
Nyinyi watu vipi??

Sasa kama wanataka nchi yao kwanin muwalazimishe wafuate matakwa yenu??

Tume ya jaji warioba si imeshaweka wazi kila kitu??waachen waende zao,tatizo liko wapi??

Hovyo sana watu kuwa ving'ang'anizi namna hii
 
Tunajadili juu ya "double standard" wewe unajadili juu ya "ung'ang'anizi!" Tutafika kweli?
 
Wazanzibari ni vipanga kuliko watanganyika. Kwa kutumia mbinu ya kulalamika na kukosoa muungano wa sasa wameweza kututawala na kunufaika na muungano kuliko watanganyika.

Wao wanaweza kuongoza wizara za Tanganyika, wanamiliki ardhi na biashara huku Tanganyika lakini bado wanalaumu muungano. CHETU CHA WOTE CHAO CHA KWAO PEKE YAO.
 
wazanzibari wanawanyonya watanganyika, na kusema ukweli kwa mujibu wa katiba iliyopo Zanzibar siyo nchi,pamoja na kurekebisha katiba yao lakini ukweli una baki palepale si nchi

Kama wanawanyonya basi muwaachie nchi yao

Mnalalamika nini ili hali wao washasema wanataka zanzibar yao??ajabu nyinyi hamuitaki tanganyika yenu
 
Wazanzibari ni mwiba wa kooni kwa Watanganyika.

Issue sio kuwa "mwiba!" Naona tukianza kujadili juu ya suala la Muungano watu huwa mnachanganyikiwa! Haya tukikubaliana na hoja yako ya "mwiba" toa maelezo juu ya huo "Umwiba wa Wazanzibari!"
 
Buchanan

Mkuu, haujamtendea haki PM wetu Mizengo Pinda, umemeuita kama hana cheo chochote.
 
Tunajadili juu ya "double standard" wewe unajadili juu ya "ung'ang'anizi!" Tutafika kweli?

What the hell is double standard nyinyi??acheni unafiki wenu...!!

Watu mmekaa kushingilia jambo moja kila siku kwa maslahi yenu huku mmeweka pamba maskion ndio nin sasa??

Kama wao wazanzibar wenyewe wanataka taifa lao iweje nyinyi muendelee kuwawekea ngumu na kuwatolea kauli za kejeli?

What is double standard wakati watu wameweka nia yao mbele na inaonekana?
 
Hili suala la muungano nina uhakika halitatatuliwa na hili bunge la katiba.
 
Kama wanawanyonya basi muwaachie nchi yao

Mnalalamika nini ili hali wao washasema wanataka zanzibar yao??ajabu nyinyi hamuitaki tanganyika yenu
Kwa nini tuiachie Zanzibar wajukuu wa sultani! Mnadhani Watanganyika wajinga waache ndugu zao warejeshwe kwenye utumwa?
 
What the hell is double standard nyinyi??acheni unafiki wenu...!!

Watu mmekaa kushingilia jambo moja kila siku kwa maslahi yenu huku mmeweka pamba maskion ndio nin sasa??

Kama wao wazanzibar wenyewe wanataka taifa lao iweje nyinyi muendelee kuwawekea ngumu na kuwatolea kauli za kejeli?

What is double standard wakati watu wameweka nia yao mbele na inaonekana?

Kwa nini Jaji Mstaafu Agustino Ramadhan alipodai kuwa Zanzibar sio nchi hamkukimbilia kubadili Katiba ya Zanzibar?
 
Sioni wa kulitatua kwasababu waliolianzisha hili tatizo hawapo na bahati mbaya wanaotakiwa kulitatua hawako tayari kwasababu kwanza wanaangalia maslahi yao ya kisiasa zaidi hasa uchaguzi wa mwaka 2015 badala ya kuangalia suala la muungano katika maono ya muda mrefu hasa ukitilia maanani EAF.

Ngongo hili suala nani atalitatua kama bunge la katiba haliwezi?
 
Sioni wa kulitatua kwasababu waliolianzisha hili tatizo hawapo na bahati mbaya wanaotakiwa kulitatua hawako tayari kwasababu kwanza wanaangalia maslahi yao ya kisiasa zaidi hasa uchaguzi wa mwaka 2015 badala ya kuangalia suala la muungano katika maono ya muda mrefu hasa ukitilia maanani EAF.

Kwa nini Wazenj wana "Double Standard," linapokuja suala la "Zanzibar Sio Nchi?"
 
Back
Top Bottom