Bwana Buchanan, sijui ulitaka kuelimishwa au kujibiwa shutuma zako juu ya haki a Wazanzibari. Nitajaribu kufanya yote mawili.
1. Fahamu kuwa matamshi mawili unayoyanukuu yana sababu tofauti, La kwanza ni jitihada ya Wazanzibari katika hizo harakati za kuigombea hiyo Zanzibar kutokana na dola la Zanzibar chini ya SMZ ilipokuwa ikipingana na jitihada hizo za kudai Utaifa wa Zanzibar. Waliokuwa mahakamani hawakuwa na kesi bali walikuwa wakipinga maovu ya kutawaliwa. Hivyo basi lolote ambalo lingesaidia katika harakati hizo ingekuwa rahisi kupotelezewa kama ilivyofanywa kwa kauli ya Jaji Augustino
2. Kauli ya Pinda ni muendelezo wa kuidhalilisha Zanzibar, jambo lililofanya Wazanzibari wapinge. Harakati ni zile zile kama hapo mwanzo ni kutaka uhuru wa Zanzibar.
Kuhusu swali la ktukejeli, nafikiri akili ya mtu alie sawa itamwambia kuwa mtu ujivune na upiganie chako na hivyo Wazanzibari kupigania nchi yao si vibaya ubaya ni kukukatalieni nyie kuwa na nchi yenu, lakini kwa vile hamuitaki isiwe lazima tutuburuza mnavyotaka. As far as hili la utambuzi, hiyo ni hiyari yenu mnapoona kuwa muwape rushwa baadhi ya Wazanzibari ili iwe kigezo cha kutafuta uhalali wa kutumeza. Rushwa ni rushwa ni si Wazanzibari tu bali hata nyinyi tunawaona Makamanda wanaingizwa kwenye kamati za POSHO na kutoka na maazimio ya muafaka na CCM.
Hili la Makamo wa pili kufika Tanganyika huwa hafiki Kiserikali na hahudumiwi na SMT na hivyo si vibaya na Pinda nae kuambiwa mwisho Chumbe.