Double Standard Kuhusu Kauli ya "Zanzibar Sio Nchi!"

Double Standard Kuhusu Kauli ya "Zanzibar Sio Nchi!"

Punguza jazba na chuki za kuwazushia mambo wa Znz.

Zanzibar hawahitaji Serikali 2 au 3 au hata 10. Kinachotakiwa ni kuwa na Znz huru kwa maana nchi yenye mamlaka kamili. Kama Znz itaweza kuyapata haya katika Serikali Moja au Mbili au Tatu au hata 7 hiyo sio Tatizo.

Jaribu kuwasoma nini wa Znz wanachotaka na sio kuendeshwa na hisia na chuki dhidi yao.

Lakin japo ni Mod naweza kukuuliza suala hapa. JE UNAJUA TOFAUTI ZA DOLA NA NCHI?

Naomba jibu lako ili tukupe mwanga kama upo kizani.

Mkuu sina jazba yoyote wala chuki, niko fiti kwa kile ninachosimamia, wala usinipe pole kwa kuwa sijakwazwa au kuumia popote kwenye mjadala huu! Unaposema Wazanzibari hawataki Serikali 2 au zaidi umenukuu kauli ya nani? Mimi nimewanukuu akina Amani, Jumbe na kuhusu Sera za CUF.

Kwa kuongezea tu CCM Zanzibar walimvua uanachama Mbunge kwa kudai Serikali 3, akanyang'anywa Kadi na kuambiwa kuwa hiyo sio Sera ya CCM! Sasa wewe uko nchi gani mwenzetu?

Kwa habari ya Dola vs Nchi, mimi sijazungumzia Dola, kama unataka mjadala wa kama Zanzibar ni Dola au la anzisha tu tutatoa mawazo yetu!
 
Umejitahidi sana kuuhalalisha ubovu wa muungano tulionao lakini ukweli utabaki kuwa jinsi ulivyo, kwamba Muungano uliundwa ukiwa na kasoro zake tokea mwanzo. Huwezi ua nchi moja kabisa halafu nyingine ukaiacha kama ilivyokuwa na ukadai kwamba mmeungana kwa usawa na sasa nchi yenu ni moja. Kama ni kufa zife zote ndipo izaliwe nchi hiyo moja mnayotaka kuiunda, kama ni kubaki zibaki zote ili mjue hamjaungana bali mmeunda Jumuiya kama zilivyo SADC, EAC, etc.

Hakuna "ndoa" isiyopita kwenye misukosuko hata kidogo na misukosuko ndiyo inayoiimarisha! Hata hivyo wazo lako la Serikali moja ni jema na aliwahi kulitoa PM Pinda nalo halikuwafurahisha baadhi ya watu!
 
Nataka nimdarsishe kidogo hapo kwani Hata Mahakama katika kesi hiyo haijatamka kuwa Znz sio nchi bali walisema Znz sio Doula.

Nafikiri anajichanganya na kukurupuka mwenyewe katika maneno hayo na ukiongezea na chuki na hisia zake ndio zinampeleka pabaya.

Tuvute subra kusubiri jibu lake.

"Zanzibar is NOT a Sovereign State" maana yake ni nini? Juzi juzi nimemsikia Jaji Mstaafu akirudia kauli yake kuwa "Zanzibar Sio Nchi" na akadai kuwa wa kulaumiwa hakuwa PM Pinda bali ni yeye mwenyewe Jaji Ramadhan kwa kutangulia kusema kuwa "Zanzibar Sio Nchi" na si PM Pinda!
 
attachment.php
 
Ngongo,

Achana kabisa na hawa wanasheria unaowataja kwani wote ni wachumia tumbo na wanafiki wakubwa.JIULIZE KWANINI WALISHINDWA KWENDA MAHAKAMANI KUDAI HAKI YAO YA KIMSINGI KABISA YA UVUNJWAJI HUO WA SHARIA NA KATIBA YA NCHI.

Ndio maana tunaita wachumia tumbo na wanafiki tu.

Pole sana.

"Sharia" ya nchi gani ilivunjwa mkuu?
 
Hakuna safari ndefu kwani sasa mambo yapo katika ncha. LAAZIMA ZNZ HURU YENYE MAMLAKA KAMILI IPATIKANE. Na waZnz wanataka kupumua sasa.

Laazima kieleweke huko Dodoma
.

Tunaomba maamuzi yatakayotoka Dodoma yamalize hizi kelele watu wachape kazi kila siku muungano, muungano kitu gani tafuteni maendeleo.
 
Undumilakuwili kama unaouonyesha wewe wa kuwaita wenzako wazanzibar double standard wakati nawe ni walewale.
Undumilakuwili wa watanganyika ni kuwa ng'ang'ania wazanzibar waliojipambanua wazi hawataki muungano. Unataka detail ya wanaong'ang'ania muungano au detail gani mkuu!?
you are right mkuu CHAMVIGA. huwezi kumlazimisha mtu kula chakula asichokipenda tu kwa sababu wewe unadhani kipo na ladha nzuri. Kufanya hivyo ni uwendawazimu. Wazanzibari wanahisi kwao wao muungano basi, imetosha! sasa kwa nini walazimishwe? Mi nadhani wangeachwa tu wakajiondowa katika huu muungano kwa slama na amani, matokeo yoyote watakayokumbana nayo hapo baadae ikiwemo kufa njaa, kukosa ardhi ya kuishi nk ni juu yao wenyewe.
kuendelea kuwashupalia kuwemo katka muungano wanaoamini kutokuwa na manufaa kwao ndio double standard hasa. Jitambueni Watanganyika, ioneni thamani ya nchi yenu kama vile Wazanzibari wanavyojitambua na kuiona thamani ya nchi yao.
 
Msugua CD wa CHADEMA ana faida gani kwa nchi?

sasa habari ya Chadema imekuja vipi hapa kwenye topic ya Muungano? Huo ndo ujuha. Ili kuweka kumbukumbu sawa tuambie ziara hata moja ya PM huko Zanzibar ilikuwa lini tangu awe PM?
 
Tunaomba maamuzi yatakayotoka Dodoma yamalize hizi kelele watu wachape kazi kila siku muungano, muungano kitu gani tafuteni maendeleo.

Nchi hii haitaisha "kelele" mkuu, tukimaliza hili tutajadili mgogoro na Malawi, likiisha hilo ni mgogoro na Rwanda, huo ukiisha unakuja ule wa EAC! Tukimaliza mambo ya nje, tunaingia ndani, migogoro ya Wakulima na Wafugaji, posho za Wabunge, nk! Kifupi hii ni nchi inavyokwenda kwa matukio! Huwezi ukakuta mwezi umepita bila kuwa na tukio jipya!
 
you are right mkuu CHAMVIGA. huwezi kumlazimisha mtu kula chakula asichokipenda tu kwa sababu wewe unadhani kipo na ladha nzuri. Kufanya hivyo ni uwendawazimu. Wazanzibari wanahisi kwao wao muungano basi, imetosha! sasa kwa nini walazimishwe? Mi nadhani wangeachwa tu wakajiondowa katika huu muungano kwa slama na amani, matokeo yoyote watakayokumbana nayo hapo baadae ikiwemo kufa njaa, kukosa ardhi ya kuishi nk ni juu yao wenyewe.
kuendelea kuwashupalia kuwemo katka muungano wanaoamini kutokuwa na manufaa kwao ndio double standard hasa. Jitambueni Watanganyika, ioneni thamani ya nchi yenu kama vile Wazanzibari wanavyojitambua na kuiona thamani ya nchi yao.

Juzi juzi kuna mtu kavuliwa uanachama na Wazanzibari kwa kutaka Serikali 3! Msiwachukie watu wengine bure jamani wakati nyie wenyewe ndo mnang'ang'ania mambo huku mkifanya kama hamtaki!
Niwape changamoto wang'ang'ania Muungano wa Zanzibar: ukipewa Cheo chochote na JK, whether kwenye Taasisi ya Muungano au la ukatae kwa kuwa wewe hutaki Muungano! Otherwise ni unafiki hutaki samaki huku unakunywa mchuzi wake!
 
Kwa staili hii mkuu sisi tutabaki tunashangaa tu wenzetu wanafanya mambo sisi tutabakia kushikana uchawi tu.

Znz nchi au sio nchi kama watu hawana ajira, elimu duni kuwa nchi au la inasaidia nini?!
 
you are right mkuu CHAMVIGA. huwezi kumlazimisha mtu kula chakula asichokipenda tu kwa sababu wewe unadhani kipo na ladha nzuri. Kufanya hivyo ni uwendawazimu. Wazanzibari wanahisi kwao wao muungano basi, imetosha! sasa kwa nini walazimishwe? Mi nadhani wangeachwa tu wakajiondowa katika huu muungano kwa slama na amani, matokeo yoyote watakayokumbana nayo hapo baadae ikiwemo kufa njaa, kukosa ardhi ya kuishi nk ni juu yao wenyewe.
kuendelea kuwashupalia kuwemo katka muungano wanaoamini kutokuwa na manufaa kwao ndio double standard hasa. Jitambueni Watanganyika, ioneni thamani ya nchi yenu kama vile Wazanzibari wanavyojitambua na kuiona thamani ya nchi yao.

Wazanzibar hawana haja ya kutishiwa kuhusu jambo lolote. Hawa walipotafuta uhuru wa taifa lao walikuwa wanajua kuhusu kuongezeka kwa number yao, walikuwa wanafahamu kuhusu kuendesha serikali yao pia kunaitaji gharama kwahiyo wao tuwape uhuru wanaoutaka. Hata Uholanzi kijieneo chao kilikuwa hakitoshelezi wakafanya land reclamation na eneo likawa kubwa. Wakishakuwa na nchi yao pia matatizo yao watajua jinsi ya kuyatatua.
 
Juzi juzi kuna mtu kavuliwa uanachama na Wazanzibari kwa kutaka Serikali 3! Msiwachukie watu wengine bure jamani wakati nyie wenyewe ndo mnang'ang'ania mambo huku mkifanya kama hamtaki!
Niwape changamoto wang'ang'ania Muungano wa Zanzibar: ukipewa Cheo chochote na JK, whether kwenye Taasisi ya Muungano au la ukatae kwa kuwa wewe hutaki Muungano! Otherwise ni unafiki hutaki samaki huku unakunywa mchuzi wake!
sasa unakosa logic ya mjadala wako. kwa nini unataka kugeneralize wazanzibari wote kwa vitendo vya watu wachache walafi wa madaraka na tamaa za maisha? kama upo serious kweli, unadhani ikapigwa kura ya maoni leo hii ya kukubali au kukataa muungano zanzibar, matokeo unahisi yatakuwaje?
Nashangaa sana unakuja na mjadala wako baadae unataka watu waelekee katika kuungana na hoja yako. Umesoma chuo gani wewe? na umefundishwa na nani?
 
hivi kwanini tunawang'ang'ania wazenj wakati wao hawatutaki? milipuko ya jana laiti ingetokea msikitini ndio tungejua balaa lake
 
Issue sio kuwa "mwiba!" Naona tukianza kujadili juu ya suala la Muungano watu huwa mnachanganyikiwa! Haya tukikubaliana na hoja yako ya "mwiba" toa maelezo juu ya huo "Umwiba wa Wazanzibari!"

Si mwiba tu bali ni luba vilevile....kwani wanapenda sana kupigania haki...kila kitu fifty-fifty, lakini inapokuja Wajibu, hasa katika kuchangia sawa gharama za muungano, wanaruka kimanga...mara kanchi kao kadogo na watu ni wachache!!!

Dawa ni kuwa na muungano wa nchi moja fullstop...ikishindikana ni wa nchi tatu km tume ya warioba ilivyopendekeza...wasipotaka basi turudi, kwa kinyongo, serikali mbili, lakini kila upande ugharimie gharama za uendeshaji pasu kwa pasu na kusiwe na visingizio vya aina yeyote wala mipaka ya kijinga.
 
sasa unakosa logic ya mjadala wako. kwa nini unataka kugeneralize wazanzibari wote kwa vitendo vya watu wachache walafi wa madaraka na tamaa za maisha? kama upo serious kweli, unadhani ikapigwa kura ya maoni leo hii ya kukubali au kukataa muungano zanzibar, matokeo unahisi yatakuwaje?
Nashangaa sana unakuja na mjadala wako baadae unataka watu waelekee katika kuungana na hoja yako. Umesoma chuo gani wewe? na umefundishwa na nani?

Hata hao wachache sio Wazanzibari? Kwani nilisema WOTE?
Hilo la kura tutaliona huko Dodoma, sidhani kama kuna room nyingine ya kura za maoni!

Kuhusu vyuo nilivyosoma ni vingi na nimefundishwa na Wahadhiri wengi! Kwani tatizo liko wapi hapo? Kama kuulizana vyuo tulivyosoma na walimu waliotufundisha tuwataje, naomba uanze wewe mkuu!
 
hivi kwanini tunawang'ang'ania wazenj wakati wao hawatutaki? milipuko ya jana laiti ingetokea msikitini ndio tungejua balaa lake

Wazanzibari ndio wanaong'ang'ania Muungano, usipochunguza kwa makini hutalielewa hili!
 
Back
Top Bottom