Double Standard Kuhusu Kauli ya "Zanzibar Sio Nchi!"

Double Standard Kuhusu Kauli ya "Zanzibar Sio Nchi!"

Mimi ni mtanganyika halisi ninapenda haki itendeke kwa watu wote. Dhulma si jambo jema na kumsaidia/kumnusuru ndugu aliyedhulumiwa ni jambo la heri mbele za Mungu.

Mtu anayejiita mtanganyika wakati unaona zanzibari haitendewi haki wakati ina serekali yake wakati tanganyika haina serekali yake unaona poa tu ni mzanzibara. Napenda kukutaarifu tanganyika yetu ikirudi tutakutimua urudi kwenu zanzibar na makunguru yenu maana nyie wazanzibar na kungururu wennu mnafanana kwa uroho.
 
Mkuu inawezekana na mimi nina mapungufu yangu lakini sidhani kama ni vibaya kusema kile ninachoamini! Tushindane kwa hoja sio ku-attack personalities!

Nimeona sasa hivi mmeshaanza kugeuza mjadala na kunijadili mimi badala ya hoja iliyoko mezani! Jadili hoja yangu zaidi ili tusaidia kujenga nchi yetu! Who knows? Unaweza kunishawishi nikabadili mawazo niliyo nayo na kuwa na mtizamo mpya, na ndio maana tuko hapa Jukwaani!

Na huo "undumila kuwili wa Watanganyika" unaousema ndio upi? Unasema hivyo kwa ajili ya "ku-balance equation" au namna gani? Mbona hutoi detail? Au ndo juhudi za ku-divert mada?

Undumilakuwili kama unaouonyesha wewe wa kuwaita wenzako wazanzibar double standard wakati nawe ni walewale.

Undumilakuwili wa watanganyika ni kuwa ng'ang'ania wazanzibar waliojipambanua wazi hawataki muungano. Unataka detail ya wanaong'ang'ania muungano au detail gani mkuu!?
 
Wakuu,

ukasirishwa na kauli ya Jaji Mstaafu Agustino Ramadhan wakaja kukasirishwa na kauli ile ile lakini ikasemwa na Pinda? Why double standard? Au ni chuki tu kwa watu wa bara/ Tanganyika? Juzi tena Pinda "kazungumzia kuwa wanaotaka Tanganyika waeleze ni Tanganyika ipi waitakayo!"

Wao wenyewe wame-acquire ardhi na kuishi Tanzania Bara bila bughudha yoyote! Hao ndo Wazanzibari bwana!!!

Wazanzibari ni watu werevu sana na inabidi uwapongeze kwa hilo. Hukumu ya mahaka iliposema Zanzibar si nchi ilikuwa ni kwa context ya uhaini kwa vile dola ni swala la muungano. Kimantiki huwezi ukaipindua ZNZ kwa vile vyombo vya ulinzi ni vya muungano.

Wazanzibari pia wakati ule walikuwa wanataka wenzao watoke nje ya dhulma kwa hiyo haikuwa wakati muafaka kwa wao kufanya chochote ambacho kingwezza kuhatarisha ustawi wa maisha ya ndugu zao.

Hakuna double standards ni uelewa tu wa importance-urgency matrix! Ninini ufanye ni kwa wakati gani!

Zanzibar ni nchi. Nukta.
 
Mtu anayejiita mtanganyika wakati unaona zanzibari haitendewi haki wakati ina serekali yake wakati tanganyika haina serekali yake unaona poa tu ni mzanzibara. Napenda kukutaarifu tanganyika yetu ikirudi tutakutimua urudi kwenu zanzibar na makunguru yenu maana nyie wazanzibar na kungururu wennu mnafanana kwa uroho.

Possibly wewe na mimi niwa moja katika mawazo. Mimi nataka serikali yangu ya Tanganyika na hao wazanzibar wasiotaka kuwa nasi tuwape haki yao. Kwanini tuwang'ang'anie watu wasiotaka kuwa nasi?
 
Mkuu mimi nazungumzia maslahi ya nchi, sio u-CHADEMA wala u-CCM. Hilo la external influence liko wazi kabisa wala halihitaji speculations! Soma taarifa ya Siri ya CIA juu ya Mapinduzi ya Zanzibar, 1964 in context ndio utaelewa namaanisha nini hapa!

Kwa taarifa yako hata Constitutional Review Commission (CRC) ya akina Warioba walilijadili hili kwa kirefu sana!

Ukweli ndo huo, wewe baki na "CHADEMA/CCM Politics," dunia inaendeshwa kwa underground movements kwa kiasi kikubwa!

utaumiza kichwa bure kupigizana kelele na watu humu.

Mpaka mtu uwe na taarifa sahihi kama wewe ndio utafanya maamuzi sahihi.Vinginevyo utaona tu watu wanapiga kelele bila kujua ujasiri huo unatoka wapi! Kelele na ujasiri wa serikali ya CCM kukataa kuvunja muungano zina source yake wanakopata kiburi. Pia kelele za wazanzibar kuvunja muungano zina source yake.

Haya tuyaonayo ni matokeo tu ya hizo underground movements. CCM kwenye hili sio wajinga,wanajua wanachopambana nacho. Tunapambana kutetea different ideologies tulizoletewa na wakoloni. Wabara na ideologies za mzungu,wazanzibari na ideologies za mwarabu. Hapa ndipo vacuum ya "national identity" inapoonekana.

Nyerere aliona mbali sana na ujamaa wake. Waafrika ni ndugu kabisa, lakini tazama tunavyotoana ngeu kama vile ni viumbe tofauti toka sayari tofauti. Only because kuna mtu anataka ideology yake itawale vichwa vya watu ili awatumie for economic purposes. Na sisi tumekubali kabisaa! Ningekuwa mtaalam wa geneology, ningefanya research kubwa sana on our DNAs!
 
Tatizo sio Wazanzibari bali ni viongozi wa Tanganyika wanoing'ang'ania Zanzibar isijitenge na kujitegemea.

Kwa ufupi tatizo la muungano lipo kwa Tanganyika zaidi kuliko Zanzibar kwakuwa yenyewe imeshajitambulisha kama nchi ikwa na vigezo vyote vya nchi. Sasa Tangayika ipo wapi? Hakuna viongozi waoga kama wale wanaotokea Tanganyika. Mtu atatolewa Zanzibar na kupewa wizara ya Tanganyika wote wanafyata mikoa. Hebu hilo lifanyike Zanzibar uone cha moto. Hata rais anateua wazanzibar kushika wizara zisizo za muungano ili kujibembeleza tu hakuna mantiki yoyote.

Viongozi wa Tanganyika wanakabiliwa na kitu kinachoitwa "fear oa unknown" kwamba hivi leo Tanganyika ikirudi itakuwaje? Tutaitawala vipi maana hatuna uzoefu wa kuendesha nchi yetu wenyewe, je mimi nitakuwa nani nk nk. Wazanzibari hawana shida kwani tayari wanaserikali yao na system ya uongozi inayofanya kazi.

TANGANYIKA BILA ZANZIBAR INAWEZEKANA. WAKE UP TANGANYIKANS!

Mkuu wanaokerwa na Muungano ni Wazanzibari zaidi ya Watanzania KUumbuka Suala la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Amani Karume alipouita Muungano kuwa ni kama "koti" unaloweza kulivua, Rais aliyejiuzulu kwa "machafuko ya hali ya hewa ya kisiasa," Aboud Jumbe Mwinyi, alipodai "greater autonomy" kwa Zanzibar, CUF ambayo ina mizizi yake huko Zanzibar ilianzisha hoja ya Serikali 3!

Malalamiko ya Watanganyika ni "reaction" baada ya malalamiko ya Wazanzibari ya muda mrefu! Remember, action and reaction are equal and opposite!!

Sasa hivi Wazanzibari wanageuka kidogo kidogo "kuubembeleza" Muungano, tena wa Serikali 2 uendelee! Ni kama walikuwa wanajaribu kina cha maji kwa mguu, walipoona wanakaribia kutumbukia ndo wanaomba msaada!
 
hatuwezi kuamini hicho unachokisema kwamb ni "double standard" Wazanzibar kauli yao tumeiona kweny takwimu za Jaji Warioba, na huo ndio msimamo wao unaotambulika kisheria!!

Inasemekana takwimu za Warioba zilikuwa na mushkeli...kisa...maswali waliyoulizwa wahusika yalikuwa ya wazi mno (very open question). hakukuwa na standadi ya maswali ambayo yanaweza kukupa nguvu ya kutamka watu kadhaa walitaka hiki ndani ya Katiba mpya....

Hebu fikiria watu mnaenda kutoa maoni kwanza mnatengwa kwenye makundi ya watakaozungumza maswala ya muungano, watakozungumza maswala ya rasilimali za nchi nakadhali na kadhalika...ndiyo maana nasisitiza Wazanzibar wengi wanataka muungano tena wa serikali moja...ila baadhi ya viongozi huko serikali ya mseto ya Zanzibar na wengine walioko Tanzania Bara (baadhi ya wapinzani na serikali), kwa sababu wanazozijua wao, ndiyo wanajitahidi kuhujumu maoni ya wazanzibari wengi eti wazanzibar hawatakubali serikali moja ya Tanzania.

Kwenye Mada;

Kwamba kwanini Wazanzibar wana'double' standard... mkuu si wazazibari wote bali ni wachache...na fuatilia hasa waliotoa kauli hizo mwanzoni na baadaye kuendela kuishupalia kauli ya Pinda...karibu wote ni baadhi ya viongozi...na sababu ya kufanya hivyo...ni kama nilivyoeleza hapo juu.
 
Possibly wewe na mimi niwa moja katika mawazo. Mimi nataka serikali yangu ya Tanganyika na hao wazanzibar wasiotaka kuwa nasi tuwape haki yao. Kwanini tuwang'ang'anie watu wasiotaka kuwa nasi?

Mkuu ulikuwa unaongea kwa jazba sikuwa nakuelewa, leo una point za msingi! We just let them go comeon! Yasije yakaanza kutokea mengine tukawa jalala la kutupia tàka!
 
mwakani Scotland watapiga kura kuamua kama wanataka Uhuru wao au waendelee kuwa chini ya uingereza nadhani wazanzibari wangefuata mkondo huo kuliko kukaa wakipiga kelele kama wanaona wamebanwa kwa Tanganyika tupo neutral lolote tutalipokeea na hatutapungukiwa na kitu, Mwalimu alituasa tusiwe wa kwanza kuwatenga wenzetu dhambi hiyo itatutafuna na ndio maana tupo kimya pamoja na matusi dharau na kejeli toka kwa wenzetu Hawa.
 
Buchanan,

Kama utakataa kuendeshwa na hisia zako na chuki dhidi ya Znz na WaZnz unaweza kujifunza mengi kutoka katika huo mnaouita Muungano.

Lakin naomba nikusaidie japo kiduchu.
KUNA TOFAUTI KATI YA NCHI NA DOULA.

Kama utasoma Ibara a Kwanza kabisa ya Katiba ya Znz imebainisha wazi kuwa ZNZ NI NCHI na imetaja mpaka mipaka ya nchi hiyo.

Lakin vile vile vigezo muhimu vya nchi kisharia karibu vyote Znz inavyo kuanzia Rais, Bunge (baraza la wawakilishi), Mahakama, Wmbo wa Taifa, Nembo ya Taifa N.k

Lakin kubwa ambalo wewe na wengine toka upande wa pili mlipaswa kujiuliza ni hili: Tanganyika ina ukubwa wa 885,800 SqKm na Znz ina 2,000 SqKm, Lakin pia Populationa ya Tanganyika ni 45,912,768 na Ile ya Znz ni 1,542,763.

Je kwa kigezo hichi utajiuliza, je nchi hizi zinaweza ungana kweli, tena Muungano wa pasu kwa pasu?

Pole sana Moderator.

 
tujue kuwa wazanzibar hawatupendi, wanatubagua, sio watu wazalendo kabisa
kwanini maneno hayohayo aliyosema ya kuwa zanzibar sio nchi alyosema ramadhan wasichukie waje kuchukia aliposema mtoto wamkulima ujue kuwa tangia zamani hawa wazanzibar wanatuchukia na hawana la kufanya juu yetu sisi watanganyika ndo mana tunataka tuwe na serikali yetu katiba yetu ya wtanganyika itakayotutambua na kutatua kero zetu kabisa kwani tunagandamizwa sana


hichi ndo kilio chetu watanganyika tuwe na serikali yetu na katiba yetu kama wao
 
Buchanan,

JAJI Mkuu mstafu Bwana A. Ramadhani amesema SERIKALI 3 ni JAMBO lazima kama tunahitaji MUUNGANO huu uwepo.

KWA NINI WALIFIKIA UAMUZI WA SERIKALI 3.

Jaji Ramadhani alisema kwa mazingira yaliyopo sasa, waliona ni busara kuwa na muundo wa Serikali tatu, kwani tayari Zanzibar imefanya Mabadiliko ya Katiba yake ya mwaka 2010 ambayo yalieleza wazi kuwa Zanzibar ni nchi.

Alisema pia walifanya mabadiliko ya kisheria ambapo sasa sheria zitakazokuwa zinapitishwa na Bunge la Muungano kabla ya kutumika Zanzibar ni lazima tena zipitie Baraza la Wawakilishi na ndio zipitishwe.

Alisema pia licha ya kuundwa tume na kamati kadhaa kupitia masuala ya Muungano matatizo mengi yameshindwa kufikiwa mwafaka. Jaji Ramadhani alisema, hata Bunge la Jamhuri ya Muungano, limekuwa likitumia muda mrefu kujadili masuala ya Tanganyika pekee na siyo ya Muungano.

Awataka wanasheria(TLC) kutoa elimu Hata hivyo, Jaji Ramadhani aliwataka mawakili na wanasheria nchini, kutumia taaluma yao, kusaidia wananchi katika mjadala wa upatikanaji Katiba iliyo bora.
 
Wazanziba haelewi maana ya nchi, wakasome nn maana ya nchi, ngoja niwape sababu moja tu kubwa wanayoisahau

Nchi haijatangazi yenyewe bali inatambuliwa, je Zanzibar inatambuliwa na nchi gani hapa duniani? Niambieni kama kuna taifa lenye balozi wa Zanzibar. Mstumie nguvu nying kujiita nchi eakati kanuni na shelia ya wewe kuwa nchi huna.

Naomba muendelee kutoa sababu zingine kwanini Zenji c nchi
 
Bwana Buchanan, sijui ulitaka kuelimishwa au kujibiwa shutuma zako juu ya haki a Wazanzibari. Nitajaribu kufanya yote mawili.

1. Fahamu kuwa matamshi mawili unayoyanukuu yana sababu tofauti, La kwanza ni jitihada ya Wazanzibari katika hizo harakati za kuigombea hiyo Zanzibar kutokana na dola la Zanzibar chini ya SMZ ilipokuwa ikipingana na jitihada hizo za kudai Utaifa wa Zanzibar.Waliokuwa mahakamani hawakuwa na kesi bali walikuwa wakipinga maovu ya kutawaliwa. Hivyo basi lolote ambalo lingesaidia katika harakati hizo ingekuwa rahisi kupotelezewa kama ilivyofanywa kwa kauli ya Jaji Augustino

2. Kauli ya Pinda ni muendelezo wa kuidhalilisha Zanzibar, jambo lililofanya Wazanzibari wapinge. Harakati ni zile zile kama hapo mwanzo ni kutaka uhuru wa Zanzibar.

Kuhusu swali la ktukejeli, nafikiri akili ya mtu alie sawa itamwambia kuwa mtu ujivune na upiganie chako na hivyo Wazanzibari kupigania nchi yao si vibaya ubaya ni kukukatalieni nyie kuwa na nchi yenu, lakini kwa vile hamuitaki isiwe lazima tutuburuza mnavyotaka. As far as hili la utambuzi, hiyo ni hiyari yenu mnapoona kuwa muwape rushwa baadhi ya Wazanzibari ili iwe kigezo cha kutafuta uhalali wa kutumeza. Rushwa ni rushwa ni si Wazanzibari tu bali hata nyinyi tunawaona Makamanda wanaingizwa kwenye kamati za POSHO na kutoka na maazimio ya muafaka na CCM.

Hili la Makamo wa pili kufika Tanganyika huwa hafiki Kiserikali na hahudumiwi na SMT na hivyo si vibaya na Pinda nae kuambiwa mwisho Chumbe.
 
Wazanzibari ni watu werevu sana na inabidi uwapongeze kwa hilo. Hukumu ya mahaka iliposema Zanzibar si nchi ilikuwa ni kwa context ya uhaini kwa vile dola ni swala la muungano. Kimantiki huwezi ukaipindua ZNZ kwa vile vyombo vya ulinzi ni vya muungano.

Wazanzibari pia wakati ule walikuwa wanataka wenzao watoke nje ya dhulma kwa hiyo haikuwa wakati muafaka kwa wao kufanya chochote ambacho kingwezza kuhatarisha ustawi wa maisha ya ndugu zao.

Hakuna double standards ni uelewa tu wa importance-urgency matrix! Ninini ufanye ni kwa wakati gani!

Zanzibar ni nchi. Nukta.

Context ni ile ile mkuu, PM alipozungumza "Zanzibar sio nchi" aliweka suala la uhaini pembeni? Tunapozungumzia nchi tunajumuisha mambo yote na sio kumega vitu kidogo kidogo!

Sasa kama "kiuhaini" Zanzibar sio nchi, itakuwa nchi kwa jambo lipi? "Nchi" ikikosa sifa moja zingine zinaweza kusimama?

Ni sasa na pombe ikitolewa alcohol haibaki tena kuwa pombe!

Tuki-assume kuwa Zanzibar ni nchi kama unavyolazimisha wewe kwa nini mnataka "kurudishiwa nchi" yenu wakati kumbe mnayo? Mbona Kenya, Uganda, nk hawalii "kurudishiwa" nchi zao, japokuwa wako kwenye EAC?

Nionavyo mimi ni double standard, tena kauli hiyo ingewafanya mkasirike sana kwa kuwa ilimshusha hadhi Rais wenu na kumfanya kuwa hana tofauti na Mkuu wa Mkoa ambaye hawezi kupinduliwa! Afadhali tu Pinda alidai kuwa Zanzibar Sio Nchi tu basi kuliko yule aliyegusa hata Kiongozi wa nchi!
 
Kwa nini tuiachie Zanzibar wajukuu wa sultani! Mnadhani Watanganyika wajinga waache ndugu zao warejeshwe kwenye utumwa?
Mkuu kauli yako imenichoma sana.Hakika hiki kisiwa kwa gharama yoyote lazima kiwe chini ya Tanganyika hata kwa mtutu wa bunduki kwa maslahi mapana sana ya wazalendo wote.
 
Mkuu wanaokerwa na Muungano ni Wazanzibari zaidi ya Watanzania KUumbuka Suala la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Amani Karume alipouita Muungano kuwa ni kama "koti" unaloweza kulivua, Rais aliyejiuzulu kwa "machafuko ya hali ya hewa ya kisiasa," Aboud Jumbe Mwinyi, alipodai "greater autonomy" kwa Zanzibar, CUF ambayo ina mizizi yake huko Zanzibar ilianzisha hoja ya Serikali 3! Malalamiko ya Watanganyika ni "reaction" baada ya malalamiko ya Wazanzibari ya muda mrefu! Remember, action and reaction are equal and opposite!!

Sasa hivi Wazanzibari wanageuka kidogo kidogo "kuubembeleza" Muungano, tena wa Serikali 2 uendelee! Ni kama walikuwa wanajaribu kina cha maji kwa mguu, walipoona wanakaribia kutumbukia ndo wanaomba msaada!

Punguza jazba na chuki za kuwazushia mambo wa Znz.

Zanzibar hawahitaji Serikali 2 au 3 au hata 10. Kinachotakiwa ni kuwa na Znz huru kwa maana nchi yenye mamlaka kamili. Kama Znz itaweza kuyapata haya katika Serikali Moja au Mbili au Tatu au hata 7 hiyo sio Tatizo.

Jaribu kuwasoma nini wa Znz wanachotaka na sio kuendeshwa na hisia na chuki dhidi yao.

Lakin japo ni Mod naweza kukuuliza suala hapa. JE UNAJUA TOFAUTI ZA DOLA NA NCHI?
Naomba jibu lako ili tukupe mwanga kama upo kizani.

Pole sana Mod.

 
Context ni ile ile mkuu, PM alipozungumza "Zanzibar sio nchi" aliweka suala la uhaini pembeni? Tunapozungumzia nchi tunajumuisha mambo yote na sio kumega vitu kidogo kidogo!

Sasa kama "kiuhaini" Zanzibar sio nchi, itakuwa nchi kwa jambo lipi? "Nchi" ikikosa sifa moja zingine zinaweza kusimama?

Ni sasa na pombe ikitolewa alcohol haibaki tena kuwa pombe!

Tuki-assume kuwa Zanzibar ni nchi kama unavyolazimisha wewe kwa nini mnataka "kurudishiwa nchi" yenu wakati kumbe mnayo? Mbona Kenya, Uganda, nk hawalii "kurudishiwa" nchi zao, japokuwa wako kwenye EAC?

Nionavyo mimi ni double standard, tena kauli hiyo ingewafanya mkasirike sana kwa kuwa ilimshusha hadhi Rais wenu na kumfanya kuwa hana tofauti na Mkuu wa Mkoa ambaye hawezi kupinduliwa! Afadhali tu Pinda alidai kuwa Zanzibar Sio Nchi tu basi kuliko yule aliyegusa hata Kiongozi wa nchi!
Wewe tumia akili basi,

Yani unakuja hapa kusema kwamba Zanzibar hawana hoja ya kuitaka Zanzibar yao kwa kuwa tayari wanayo tena unatoa mifano kama Kenya na Uganda na kadhalika ili iwe na mantiq gani??

Kwani wewe unadhani nchi ni eneo tuh basi??nchi ni MAMLAKA,UTAWALA,SARAFU,JESHI,UHURU NA MAAMUZ YENYE UHALISIA USIO INGILIWA WALA KUPANGIWA NA YEYOTE YULE...

Then unakuja kusema kwa kejeli kudharau kina Mulugo, huoni jinsi mwenyewe ulivyo mweupe upstairs?
 
Back
Top Bottom