Lady niece,
Sisi hatuwachukii nyinyi kabisa bali tunachukia vitendo vyenu tokea baada ya kuasisiwa huu the so called Muungano 1964, mlianza na makubaliani ya katiba yenyewe kuyachakachua mpaka tukaja 1970 kutaka tufanye review mkawahada viongozi wetu na ni mwalimu mwenyewe aliwahadaa viongozi wetu ambao wengi wao walikuwa si wasomi.
Ingia miaka ya sabiini thru siasa za ujamaa na kujitegemea mukaandaa mikakati ya kuvunja mipango ya kiuchumi ya Zanzibar ya uchumi huria na soko huru na mkatumia viongozi wasaliti wa Zanzibar huru kwa kuwapa nafasi za uongozi Tanganyika ili kudhibiti uchumi wa nchi yetu (Israel style) na mkaanza kuibana koo kiasi ambacho Zanzibar kukazuka njaa ya hali ya juu na chini ya kivuli cha Muungano ikawa hata ukileta sembe kutoka Tanganika ilikuwa ni.dhambi matokeo yake Mzee Karume akasema Azimio la Arusha mwisho Chumbe. Action and counter reaction Karume kauwawa na waliopanga mauwaji yale walizuiwa Tanganyika kukimbia hukumu badala yake wakawa kisingizio waarabu ikaanza witch hunt, kamata chinja weka kizuizini piga uwa Serikali ya Muungano imefumbia jicho na vikosi vyake.ndio vilitumika kufanya huo ukandamizaji wa watu wasio na hatia hasa Pemba na haya yalifanywa kusudi kuwabaguwa Wazanzibari. Ingia Aboud Jumbe tricked into joining ASP na TANU 1977, Zanzibaris waliona hii ndio njia peke kukimbia madhila ya ASP wakaunga mkono whole heartedly muungano wa vyama hivi hasa Pemba. Ndipo Mwanzo wa Wapemba kuanza kuhamia Tanganyika ambako walijihisi wako salama. NEXT chini ya utawala wa Chama kimoja na Party Supremacy ndio Zanzibar ilipoanza kushuhudia kuporwa madaraka yake, utaifa wake na nguvu zake za kujitegemea wenyewe kiuchumi. Coincidentaly kuvunjika kwa kwa EAC 1977 ambapo Zanzibar ilikuwa independent member wakati huo. Ikavunjika East African Monetary Board na mafao ya kila member Zanzibar ikaingia ubia kibiashara na BOT kwa kutoa mafao yake ya EAC na kichangia 11,5% mtaji wa BOT sio mchango wa Muungano. Kuanzia hapo Zanzibar haijapata dividend kutokana na ujasiria mali huo (moja katika kero rasmi za muungano).
Ingia machafuko ya kisiasa 1982 kuuzuliwa A. Jumbe why he questioned the motive behind the Union and benefits of partneship. Muungano huo.
Com e Mzee (Rukhsa) A. H. Mwinyi interim president of SMZ na siasa zake za kurudishia hadhi yake Zanzibar in few days his leadership with his CM Maalim Seif Zanzibar new policies of Liberalization of Trade and Economy, Nyerere could not swalow that Zanzibar had shown the light and turned arround to be abooming xenter of trading, watu wakija kutoka mbali hata Madagascar kununua bidhaa rahisi. 1984 Uchaguzi wa Zanzibar Seif sharif mshindi against Abdulwakil He Mwalimu schemed ushindi akapewa Abdulwakil kutumia famous hotuba ya ugavi U-unguja na Upemba and kufungwa Seif Sharif at the same time tricked Zanzibaris by eti Yeye kujiuzulu na kumpa hatamu Mzee A. Mwinyi urais wa JMT well while wazanzibaris walimnasihi asikubali yeye sababu tulijuwa kuwa ule ni mpango mwengine wa Mwalimu nae hakusikia kilio chao. Ndio maana hadi leo Mzee Mwinyi anaonekana ni msaliti. Haya hivyo mukubali jina la Mzee Rukhsa mlimpa nyinyi waTanganyika kwa vile alihamasisha policy zile zile za kiuchumi za Zanzibar na akaruhusu mengi ambayo Mwalimu .alikuwa akiyazuia. Hilo nalo lilimkera sana Mwalimu wakati bado tukiwa ndani ya system ya chama kishika hatamu (Supremacy) tulishuhudia Mwalimu akimtukana Mzee Mwinyi hadharani tena matusi ya nguoni video clip ya tukio hilo hadi leo ITV wanaichezesha kila siku as kumbukumbu zake. Come mkapa Amiri jeshi mkuu. Salmin enters presidency na matokeo ya siasa za chuki Zanzibar JMT govt imefumbia macho again. Ingia Amani Karume under Mkapa govt Mauwaji ya Pemba. Come uchaguzi wa 2010 Ushindi CUF na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na CCM Dodoma kutokufurahishwa na maridhiano wakaanza kuleta mikwara na kutaka kura yq maoni kudhania itakuwa in their favour wataweza kuuvunja umoja wa wa-Zanzibari matokeo yake 66% wameunga mkono ndio maana mukona matokea ya maoni ya CRC ni 60% wanataka serikali ya Mkataba.
From that day tokea kuasisiwa SUK Dodoma kushirikiana na CCM Kisonge conservative wamekuwa wakipigana na umoja huu nyuma ya pazia na baadae kuonekana waziwazi hasa katika viriri vyao wanaposimama na kumtukana Maalim Seif matusi ya nguoni. Na bado vyombo vya dola (Muungano) havifanyi lolote kuwachukuloa hatuwa wachafuzi wa amani Zanzibar. Watu hao hao ndio wanaosema Wapemba wende kwao hata kutishia watu kuwa watawachoma kwenye matanuri kama walivyofanya 1964 kule Bambi, Mkoa wa Kusini Zanzibar na hao ndio wanaongoza UVCCM na juzi tu eti tunamwona mmoja wao anapigania Chairmanship ya Bunge la Katiba. (Muungano huo).
Tukirudi huko nyuma matokeo ya hivi karibuni, kuuuliwa Wachungaji na hujuma.za Tindikali, wakati tunajijuwa Zanzibaris wa kawaida hasa raia hatuna tabia ya kupigana ovyo seuze kuuwana ovyo kwa kitu kidogo kama shilingi mia sisi tunajuwa fika kama ndugu zetu wa Kikristo tumeishi.nao kwa makarne kupita hatukuwahi kubughudhiana kwa lolote wacha kupigana aua kuuwana, kwa hiyo haya matokeo ya karibu tunaona yanapandikizwa na vyombo vyenye nguvu kutoka Tanganyika ili kutupaka.matope tuonekane Waislam wenye Siasa Kali, pia tunaona kuwa sekta ya Utalii ya Zanzibar imekuwa maradufu so kuongeza mapato ya Zanzibar hence kuinua uchumi wetu; wasiwasi wetu Tindikali dhidi ya wale wasichana na timing yake tumeona ni false flag na kuwa lengo hapa ni kutuhujumu kiuchumi tu.
Jiulizeni kwanini FBI wameondoka kimya kimya Zanzibar bila ya kutoa ripoti ya walichokiona kuhusu mauwaji ya Padri Mushi?
Tunachokiona kuwa vyombo vya dola vimegeuza Zanzibar movement to reforms ni adui wa 'Tanganyikan' Colonisers in the name of the Union, tunachokiaona Tanganyika iliyojificha ndani ya Tanzania Bara inatukaba roho na kutufanya adui zake kisa tumeona na kuyatambuwa makosa yao katika huu Muungano usiotufalia. Msituite mzigo wala.msitutukane kama huyo jamaa hapo aneiita nchib etu Uchi na
Buchanan asimpe Ban. Sisi tunajivunia.nchi yetu, tulishawaonyesha zamani.njia ya kuidai Tanganyika yenu na Mtikila katusaidia leo mnatuona wabaya wenu tuacheni tutokane kwa salama. Kama huu muungano mnaita ni ndoa basi sisi ndio tuliowaowa maana from day one tumezuia serikali yetu kamili na instruments zake na structure zake, nyinyi mumetuzuilia hizo funguoa muhimu tu. Sasa tuko tayari tuwape talaka kama hamtaki kukaa na sisi kwa salama na usawa, kifupi Hatuwachukii HATUPENDI DHULUMA ZENU TU!