Double Standard Kuhusu Kauli ya "Zanzibar Sio Nchi!"

Double Standard Kuhusu Kauli ya "Zanzibar Sio Nchi!"

Ndugu yangu achana kabisa na watanganyika watakuudhi tu bora uchague jukwaa la kuchat sio hapa utatoka una stress nyingi kwani sisi tushapindika na tunataka kuwapinda na nyie
gombesugu,

huyu muanzilishi mwenyewe wa hii thread ametumia maneno mengi ya kejeli. Kuna mmoja amediriki kuita zanzibar ni uchi na buchanan amejidai kushangalia tu, tutarajie haki hapo?
 
Jamani e, mapenzi ni kati ya watu wawili waliopendana, huwa wanaungana kuwa mwili mmoja kwa imani au kuwa wawili kiserikali. Sasa mapenzi yanapokoma uhakika ni mmoja wapo huwa anakuwa hasikilizani na mwenzake kiasi kwamba inakuwa kero.
Sasa akiamua kuomba talaka kwa sababu mapenzi yamekoma na ni ya kunyanyasika na kuonewa, kuna mjadala kweli hapo???
Mbona walipendana kwa hiari na wanataka kuachana kwa hiari watu mnapiga kelele?
Mapenzi yakifika mwisho hayajengeki tena, Dawa yake Talaka...................................Pole unayesikitika, hujui maana ya mapenzi kukoma kwako kumekaa vema mnaelewana.
 
Averoes,

Nimekusoma ndugu yangu!

Watu wa aina hii wala wasituumize vichwa...nimejaribu kupitia takriban bayana zoote hapa jamvini...yaani ni chuki tu na kashfa/matusi ndo vimewatawala ndani ya hizo mbongo zao dhaifu!

Yaelekea huyu ni nguli wa story za vijiweni tu...si umeona katuletea khabar za kwamba ati CIA wana mkono kwa kupitia CCM ati kulazimisha hizo sera za Seriklai mbili,na utumbo mwangineo dhaifu tu!

Hizi ni theories tu,na zipo za aina kadhaa na tunazisikia na kuzifuatilia takriban kila siku!

Sasa hiyo hiyo bayana yake humu aloandika utumbo huo...tukimwambia atuletee ushahidi yakinifu hapa hapa jamvini,tena wenye kuthibitika tena kwa vigezo mubashar...nina hakika hana na atakuja na triangular excuses tu! Daah!...au labda vipande vya majarida ya udaku!? Teeh! Teeh! Teeh!

Kwa kifupi ndugu yangu,hawa jamaa ni majanga saana tu!

Ahsanta.

Nakusoma ndugu yangu gombesugu baereze baelewe.
 
Naomba tusipotezeane muda inajulikana kuwa Zanzibar sio nchi.tunagombaaana wakat aliyechanganya mchanga mchanga tayar ulishamfukia
 
JK alishasema ZNZ si nchi nje ya TZ

hilo linajulikana....

kabla ya kujadili ni nchi au sio nchi ni bora kwanza ujiulize nchi ni nini? nchi inaundwa na nini? components zake ni Zipi? then unakuja kufanya comparison kwa ZNZ ndo upate jibu ni nchi au laa...

Haya malumbano nafikiri ni kutafuta Faraja tu lakini kwa mtu mwenye akili na mwelewa anaelewa kipi ni kipi

Zanzibar katika components za nchi haina .international recognition na sovereignty .kuhusu international recognition haitambuliki UN WALA AU
 
Jamani e, mapenzi ni kati ya watu wawili waliopendana, huwa wanaungana kuwa mwili mmoja kwa imani au kuwa wawili kiserikali. Sasa mapenzi yanapokoma uhakika ni mmoja wapo huwa anakuwa hasikilizani na mwenzake kiasi kwamba inakuwa kero.
Sasa akiamua kuomba talaka kwa sababu mapenzi yamekoma na ni ya kunyanyasika na kuonewa, kuna mjadala kweli hapo???
Mbona walipendana kwa hiari na wanataka kuachana kwa hiari watu mnapiga kelele?
Mapenzi yakifika mwisho hayajengeki tena, Dawa yake Talaka...................................Pole unayesikitika, hujui maana ya mapenzi kukoma kwako kumekaa vema mnaelewana.

Unajifanyaaaa yesu mwenyewe eti unaongea kwa mafumbo
 
"NJE YA MUUNGANO HAKUNA ZANZIBAR BALI KUNA UNGUJA NA PEMBA" (J.K. Nyerere, 1995). wanadai wasichokijua hao. By the way, washanyonya sana lakini hawakui, waacheni wakajitegemee watatia akili.

Lakin Alisita Nyerere huyo huyo kusema kuwa NJE YA MUUNGANO HAKUNA TANZANIA BARA BALI KUTAKUWA NA UISLAM NA UKRISTO. Na hilo ndio changamoto aliyoipanda Nyerere kwa Tanganyika na kuificha dhana hiyo ndani ya Muungano na ndio maana yeye ndie aliyefunga safari kwenda Znz kuomba waungane ili afiche ukweli wa mambo ambao ni kovu la ukoloni kwa Tanganyika.

kwa kuwa huwezi kufucha ukweli SASA YANADHWIHIRI NA suala la NANI MWENYE MAMLAKA YA KUCHINJA mpaka leo halijapatiwa ufumbuzi zaidi ya kufunika kombe.

Mtafunika kombe mpaka lini?

Pasu pasu una uhakika? Haya mambo msiongee tu mkiambiwa kugharamia Jeshi tu mnaanza kuomba kubaki na Serikali 2!

Ni lini Znz waliambiwa wachangie jeshi wakashindwa? Au ilikuwa KIHEREHERE CHA NYERERE KWA KUJIPENDEKEZA KWAKE NA KUIUA NCHI YAKE KWA KUIZAMISHA KATIKA MVUNGANO.

Hivi wewe na akili inawezekana kweli nchi yenye watu milioni 45 ikaungane na nchi yenye watu milioni 2 tena 50% kwa 50% kiutawala je kuna chembe ya akili hapo iliyotumika?

nawapa pole sana. waache znz wapumue.

Zanzibar katika components za nchi haina .international recognition na sovereignty .kuhusu international recognition haitambuliki UN WALA AU

Je Tanganyika inatambulika?

Nikusaidie kidogo Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Znz. Nje ya Muungano hakuna Tanzania bali utapata Tanganyika na Znz.
 
Katiba mpya itatusaidia sana kuachana hawa makupe mazenji

Nafikiri kwenye bunge la katiba linaloendelea huko Dodoma. Si umemuona JUSSA YUPO NA TUNDU LISU WAMEKAA PAMOJA.

Sasa subiri kishindo chake. Lazima Znz huru ipatikane na Tanganyika ipatikane.

Hongera sana Jussa na Tundu Lissu

Kwani kwa Tafsiri yako Mwinyi ni ni wa wapi?
Halafu hili la kukataa kulitolea maelezo kuhusu hawa kina Pinda, Magufuli, Warioba na orodha ndefu iliyopo ya mawaziri wenu unalisemaje? Hawa wapo kwa ajili ya Zanzibar, sijui wanasaidia mkoa gani kule Zanzibar.
Kwa upanse wa Mawaziri kama Shamsi, Samia na wengine ambao wametoka Zanzibar mbona hawana Makao kule Zanzibar au Wete, Pemba kwani hizo ndio sehemu za Zanzibar.

Kwa tafsiri yangu mwinyi ni mzanzibar na wala si mtanganyika. kwa hiyo kama unafikiri ninalolisema si kweli fanya uchunguzi. Pili, hao mawaziri kama pinda na wengineo Hawako kwa ajili ya zanzibar wala Tanganyika, bali wako kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kwamba wanasaidia mkoa gani kule zanzibar ni kwamba wao ni viongozi wa kitaifa na wala si wa kimkoa. kwa hiyo wanalitumikia taifa kama taifa na wala si mkoa fulani iwe ni Zanzibar au Bara. Hali hiyo hiyo ndiyo iko hata kwa wazanzibar kama Mwinyi. Kwamba ni kwanini hawaishe zanzibar ni kwasababu wanatakiwa watumikie watanzania kutoka mahali ofisi zao zilipo na wala si kutoka vijijini kwao walikozaliwa. Hata pinda na magufuli si wenyeji wa Dar es salaam lakini wanatenda kazi zao kutokea hapo.
 
Je Tanganyika inatambulika?

Nikusaidie kidogo Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Znz. Nje ya Muungano hakuna Tanzania bali utapata Tanganyika na Znz.
Tunataka serikali moja....serikali ya Zanzibar ifutwa na Serikali ya Tanganyika isirudi.
 
Nafikiri kwenye bunge la katiba linaloendelea huko Dodoma. Si umemuona JUSSA YUPO NA TUNDU LISU WAMEKAA PAMOJA.

Sasa subiri kishindo chake. Lazima Znz huru ipatikane na Tanganyika ipatikane.

Hongera sana Jussa na Tundu Lissu

Mkuu,
Decision itafanywa kwa kura za wazi!
 
Ni lini Znz waliambiwa wachangie jeshi wakashindwa? Au ilikuwa KIHEREHERE CHA NYERERE KWA KUJIPENDEKEZA KWAKE NA KUIUA NCHI YAKE KWA KUIZAMISHA KATIKA MVUNGANO.

Hivi wewe na akili inawezekana kweli nchi yenye watu milioni 45 ikaungane na nchi yenye watu milioni 2 tena 50% kwa 50% kiutawala je kuna chembe ya akili hapo iliyotumika?

nawapa pole sana. waache znz wapumue.

Yaani mpaka waambiwe wachangie?
 
Lakin Alisita Nyerere huyo huyo kusema kuwa NJE YA MUUNGANO HAKUNA TANZANIA BARA BALI KUTAKUWA NA UISLAM NA UKRISTO. Na hilo ndio changamoto aliyoipanda Nyerere kwa Tanganyika na kuificha dhana hiyo ndani ya Muungano na ndio maana yeye ndie aliyefunga safari kwenda Znz kuomba waungane ili afiche ukweli wa mambo ambao ni kovu la ukoloni kwa Tanganyika.

kwa kuwa huwezi kufucha ukweli SASA YANADHWIHIRI NA suala la NANI MWENYE MAMLAKA YA KUCHINJA mpaka leo halijapatiwa ufumbuzi zaidi ya kufunika kombe.

Mtafunika kombe mpaka lini?

Nje ya Muungano kuna "Somalia" na "Somaliland!" Yetu macho, mtoto akililia wembe....!
 
Hata mimi sikubaliani kwamba Nyerere hakuwafundisha viongozi wetu Ujamaa na Kujitegemea. Tulifundushwa sote tena kwa kasi ya ajabu. nakumbuka kati ya 1972 hadi 75 kila shule ilikuwa na somo la SIASA toka msingi, viongozi nao Kigamboni, Nyerere aliandika vitabu vingi vyenye kila sura ya ubepari lakini wapi mshikaji sikio la kufa halina dawa. Tatizo kubwa la Ujamaa ni adhabu inayokuja nayo hasa baada ya vita ya Uganda. Watu wote tunakumbukia njaa ya miaka ya sitini baada tu ya kutangazwa azimio la Arusha na ile mwanzoni mwa 80. Nadhani labda naweza kusema siasa ilichukua sana nafasi pale utaalam wa kiuchumi ulipotakiwa na kwa bahati mbaya hatukuwa na wataalam wa kiuchumi ndani ya mfumo huo wa Ujamaa na Kijitegemea zaidi ya kuchanganya siasa na uchumi.

Wapizani wa Nyerere wakati wote hawakuwa na nia nzuri. Kwanza kabisa hawakukubaliana na malengo yetu kitaifa - UJAMAA na KUJITEGEMEA. Na kibaya kuliko yote hawa wapizani hawakuwa na vision yeyote nje ya Ujamaa na kujitegemea... They had nothing to sale..

Walipinga Ujamaa kwa sababu, uliondoa kabisa nafasi yao kuwa watawala weusi wenye uwezo wa kujilimbikiza mali na vyeo..

Ukija kwa hawa akina Judas, nadhani Mzee Es anaweza kutueleza zaidi kuhusu Mkapa na swala la IPTL wakati Nyerere alipokuwa akimfuata kuulizia swala hili na lile la rushwa. (Warioba report) Inasemekana kwamba Mkapa, kila mara alikuwa akisema - Mzee sasa hivi swala la rushwa linashughulikiwa kikamilifu na kuhusu IPTL, ni uwongo wa watu hakuna kabisa mpango wa kuuzwa. Hatuuzi mali ya Umma zaidi ya asilimia 50. Well, maneno ya Judas leo hii sijui kama bado yamesimama hivyo.

Warioba na JM walikuwa kati ya viongozi waliomshitua Nyerere kila mara kuhusu ubinafsishaji lakini mzee kisha chagua mrithi na hana asili ya kugeuka kukubali makosa.

Mwinyi, Mkapa na hata JK wote wamesoma Kigamboni na majumbani mwao wanazo kila nakala ya vitabu vya Nyerere kama vile misahafu lakini yote haya ni kamba tu.

naupinga Ubepari kwa sababu wao wanaamini kwamba waafrika tunachohitaji ni just basic survival..I strongly discredit the notion. Waafrika tunastahili zaidi ya kupunguza umaskini ama kuondoa Umaskini....tunahitaji kuwa na vision mbele...to be able to make choices; to decide to do basic things without constraint, to live in a predictable environment, and have some control over what happens around us.

Labda ulikuwa haujaelewa namaanisha kuwa Zanzibar so nchi kwasababu ipo ndan ya Tanzania na Tanzania ndio inayotambulika AU na UN
 
Back
Top Bottom