Done your proper research?! Kingereza cha ugoko cha Bashite

Sio sawa na broken English anayozungumza Bashite
Hapo hakuna broken, nyuma ya done your proper research kuna you've,kaiacha hiyo kaonesha ukomavu tofauti na kiingereza cha wabongo wengi wanaoongea kama wanasoma kitabu
 
Kingereza kibovu kinafunikwa na kujiamini, ukijiamini utaongea lugha hata kama ni mbaya ni mbovu hutaaminiwa umeongea vizuri
 
Kwa upande mmoja kwa mfano nikisema nakubaliana na hizo hoja zako zote,swali ni kuwa kwanini tunacheka sasa tunapomuona mtu anakosea kuongea kiingereza ikiwa hayo uliyoeleza ndio chanzo chenye kufanya watanzania wengi kushindwa kuongea vizuri kiingereza?
 
Kwa sababu hakuna haja ya kulazimisha kuongea Kingereza kibovu ukiwa ni kiongozi, kama hujui Kingereza ongea tu Kiswahil, vinginevyo utaonekana kuwa sio mtu serious kama Shilole au Dotto Magari.
 
Hiyo nayo ipo.Kuna watu wana vipaji na wepesi kujua lugha mbalimbali.Wepesi mnoo.Mfano mmoja ninao chini ya paa ninalooshi.Anaweza kuzungumza lugha za asili na za mataifa kadhaa tena kwa madaha sana.Ipo hivyo muda mwingine.
Sasa unaweza kukuta watu wa namna hiyo kwenye kiingereza kama somo akawa hafanyi vizuri lakini kwenye kuongea akawa anaongea tu vizuri, kama ambavyo unaweza kukuta mtu anafanya vizuri katika somo la kiingereza ila kwenye kuongea sasa ikawa shida.
 
Kwa sababu hakuna haja ya kulazimisha kuongea Kingereza kibovu ukiwa ni kiongozi, kama hujui Kingereza ongea tu Kiswahil, vinginevyo utaonekana kuwa sio mtu serious kama Shilole au Dotto Magari.
Hao viongozi mara zote hutumia kiswahili kwenye mazungumzo, ila wakiongea japo kidogo kama hivyo inakuwa bonge la issue watakaoongea vizuri watasifiwa na watakaokosea watachekwa.
Kwahiyo tatizo ni mitazamo yetu kuhusu kiingereza, maana hata hao wenye kuongea vizuri kiingereza pia tunawasifiwa hatuoni kama ni kitu cha kawaida tu kutokana ni lugha yenye kutumika katika elimu yetu hivyo hakuna cha ajabu kwa yeye kujua kuzungumza hiyo lugha.

Hao viongozi waliyosoma huko zamani ambako ndio tunasema elimu ilikuwa bora, ajabu ni wachache tu wenye kusifika kuweza kuongea vizuri kiingereza.
 
Hivi tujiulize kama kweli kutumika kwa kiingereza masomo yetu ndio kunaweza kumfanya mtu aweze kuongea kiingereza vizuri na kwa ufasaha sasa kwanini watanzania tuna shida ya kuongea vizuri kiingereza?
Moja waalimu, pili ntu mwenyewe, hasa baada ya uhuru
 
Kenya waliishobokea English sana ila tazama hivi sasa ENGLISH hawaijui na kiswahili pia hawakijui.
Wewe umekaririshwa kama kasuku. Ndugu Mtanzania, kutokujua kwenu Kiingereza ndo kunakofanya mshindwe kuchangamkia fursa zilizo nje ya nchi yenu.

Angalia jinsi Wanigeria na Wakenya wanavyojipatia ajira kiulaini huko Ulaya, Amerika na kwingine ukilinganisha na Watanzania.
 
Moja waalimu, pili ntu mwenyewe, hasa baada ya uhuru
Una maana ya kwamba moja ya sababu ya watanzania kushindwa kuongea vizuri kiingereza ni kwamba hatuna waalimu wazuri wa somo la kiingereza?
 
Wabongo tuna allergy na English. Imagine huyo ni waziri na ana degree! Professor Ndalichako akizungumza ndio utazimia kabisa.
Ila Prof Ndalichako, nilicheka sana ile siku, [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Halafu nimekuja kugundua watu wengi wakishaona kiingereza kinawapiga chenga wanaanza kusingizia kwamba kiingereza sio lugha yetu.... Sasa tunakiongea cha nini wakati sio lugha yetu... Kiingereza kikikupiga chenga kubali tu usilete visingizio.
Haswaaa!! [emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…