Dondoo za Bajeti 2016/2017, kujitegemea kwa asilimia zaidi ya 80

Dondoo za Bajeti 2016/2017, kujitegemea kwa asilimia zaidi ya 80

Mkuu ebu toa maelezo kidogo, kama sijakuelewa hivi.
Yaani Serikali ijitahidi kuleta Stability ya sh against other Currency ndiyo msingi hapa hatuwezi kusema Budget 30Trillion wakati sarafu yetu ni weak matumizi yanaongezeka zaidi kwa sababu ya Currency depreciation. Leo Unatumia USD 100,000 Kununua Landcruiser ambayo ni sawa na TZS. 200,000,000 Lakini baada ya miaka 7 Gari itakua inauzwa 120,000 Kwa Tzs. 3000 hili gari litacost Tzs. 360,000,000 wakati huo mtu anashabikia kuongezeka kwa Figure ya Budget.
 
Hivi ni kweli wachangiaji wa huu uzi ni vilaza kiasi hiki mbona sioni Public debt imefikia sh. ngapi halafu bado unakopa 7.5 Trillion watu mnasifia Ujinga
Tena mikopo yakibiashara!!!
 
Yaani Serikali ijitahidi kuleta Stability ya sh against other Currency ndiyo msingi hapa hatuwezi kusema Budget 30Trillion wakati sarafu yetu ni weak matumizi yanaongezeka zaidi kwa sababu ya Currency depreciation. Leo Unatumia USD 100,000 Kununua Landcruiser ambayo ni sawa na TZS. 200,000,000 Lakini baada ya miaka 7 Gari itakua inauzwa 120,000 Kwa Tzs. 3000 hili gari litacost Tzs. 360,000,000 wakati huo mtu anashabikia kuongezeka kwa Figure ya Budget.
Umesema jambo la msingi sana!
 
Mimi siongei kimbea kama wakina mama wa mtaani kwenu naongea ki Public Economics/ Public Finance zaidi mwalimu wa Kiswahili na Historia ni Vigumu kuelewa madhara ya Public Finance na sifa ya Uongozi ni kuangalia na vizazi vijavyo.
hahaaa, unanichekesha na hayo majivuno yako kiongozi, mimi nakuambia reality ya utawala wa Africa jinsi ulivyo, hawaangalii future, na kuna mifano lukuki ya kukupa, lakini wewe kama ni msomi unavyosema utakua unajua hili na haina haja ya kukuambia...
Africa plan zao hata miaka 5 mbele hazianhalii wewe unapopiga kelele eti kuhusu vizazi vijavyo unapoteza muda,
nishaligundua hili miaka kibao iloyopita ni mind maisha yangu sio ya taifa
 
Bajeti ya Mwaka 2016/17 ni fedha za kitanzania trilioni 29.5

Katika bajeti hiyo fedha za ndani ambazo zitakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ni fedha za kitanzania shilingi trilioni 17.8 trilioni.

Mikopo ya kibiashara itakayochukuliwa na serikali kwa ajili ya Bajeti kuu ni shilingi trilioni 7.5

Misaada ya wafadhili ni shilingi trilioni 3.6.

Matumizi ya kawaida ni shilingi trilioni 17

Matumizi ya Maendeleo 11.8 trilioni.
nice to be true
 
what do you care about vizazi man? hapa ni kuji take care wewe na familia yako, ukiwa unaangalia mambo ya vizazi vijavyo hapa Afrika utaishia kuumiza kichwa bure ukakosa hata raha
nyie ndo mnakuwaga mafisad soon mkipewa madaraka sasa hiyo tabia ya kujiangalia ww kama ww mbona ni hataree
 
nyie ndo mnakuwaga mafisad soon mkipewa madaraka sasa hiyo tabia ya kujiangalia ww kama ww mbona ni hataree
nauchujiakia sana ubinafsi na ufisadi mkuu, lakini kwa jinsi ninavyoona hakuna namna ya kukabiliana nao kwenye serikali zetu, hakuna kabisa, viongozi wabovu na bado wananchi wanawachagua, halafu wakifariki au kustaafu wanaachia watoto wao, sasa mimi kuwaza mawazo ya future ya hii nchi wakati walio in charge hawawazi, nitapata vidonda vya tumbo
 
Tatizo la hizi bajeti unaweza kufurahia figure hapo lakini mwisho wa mwaka wa fedha hela iliyopatikana unakuta hata robo tatu haifiki, kuna Taasisi moja ya Muhimbili walipangiwa 118Biln mpaka jana kamati ya bunge imepita pale hela waliyopata ni 1 Biln Taasisi nyeti kama Afya.
Mwaka huu hakuna kupanga bajeti isiyotekelezeka!
 
Kuna swali la msingi bila kujali ushabiki...

Je vyanzo vya mapato vimegusa maeneo nyeti kama vile sekta ya uwekezaji katika madini,wafanyabiashara wakubwa na makampuni ya simu au ataendelea kukamuliwa mfanyakazi?
 
Bajeti ijayo ni trilion 29.5
Tra watakusanya 17.8
Mkopo 7.5
Misaada 3.6

Kwa mwendo huu wa kujitegemea kwa asilimia zaidi ya 80 ni hatua kubwa .....eko Magufuli
Source kamati ya bajeti
Naona mkuu hisabati yakupiga chenga.17.8 kwa 29.5 sio 80%, ni 60% bado saana,twategemea 40%toka nje na huku tukijishaua kuhusu MCC....tutakoma.
 
*kwa nini maendeleo yasichukue 17tr, na matumizi yakawa 11tr.

Jiulize matumizi ya kawaida ni yapi. Halafu uchukue ukubwa wa serikali na taasisi zote zilizo chini yake ndio utajua kwanini matumizi ya kawaida ni makubwa kuliko ya maendeleo.
 
Si rahisi bajeti ya maendeleo kuizidi bajeti ya kawaida. Nakumbuka kipindi fulani Prof Lipumba alilielezea vizuri hili kwamba bajeti ya matumizi huwa kubwa kwa kuwa ndio inalipa watendaji wote na wawezeshaji wa hayo maendeleo tunayoyakusudia. Kwa hiyo bajeti ya matumizi ikiwa ndogo kuna uwezekano miradi ya maendeleo isifanyike maana haitawezekana kuwalipa waibuaji, watendaji, wafuatiliaji na waendelezaji wa hiyo miradi.

Kwa kuongezea hapo, unapojenga hospitali au shule hiyo ni bajeti ya maendeleo lakini baada ya kukamilika mishahara ya madaktari, manesi, waalimu ununuzi wa madawa, vitabu usafi n.k hiyo hutumia bajeti ya kawaida. Hivyo kila bajeti ya maendeleo huzalisha bajeti ya kudumu ya kawaida hivyo siku zote bajeti ya kawaida itakuwa kubwa vinginevyo miundombinu uliyoijenga itakufa.
 
Hivi ni kweli wachangiaji wa huu uzi ni vilaza kiasi hiki mbona sioni Public debt imefikia sh. ngapi halafu bado unakopa 7.5 Trillion watu mnasifia Ujinga
Naona wewe kichwani ndo haupo vizuri. Sasa kama umebaini issue ya public debt ndo wenzako waliotangulia kuchangia wawe hawana akili?

Mimi naamini ulitakiwa kuongezea kwa kusema kuwa mjadala huu ungetilia maanani deni la Taifa. Hapo ungewasaidia wenye ujuzi kuanza kuchangia.
 
Bajeti ijayo ni trilion 29.5
Tra watakusanya 17.8
Mkopo 7.5
Misaada 3.6

Kwa mwendo huu wa kujitegemea kwa asilimia zaidi ya 80 ni hatua kubwa .....eko Magufuli
Source kamati ya bajeti
MBONA MIMI SIONI HIYO ASILIMIA 80?TRILIONI 17.8 NI ASILIMIA 60.33 YA TRILION 29.5,NA WALA SIO ASILIMIA 80.
 
Akili ndogo sana hii budget ni sawa na Trillion 9 tuu Shilling ilivyokua imara kwa exchange rate ya 650.

Ni kweli. Hii itakuwa na maana tu ikiwa Magu atachukua hata nyingine za ziada ikiwemo kupiga marufuku matumizi ya dola katika miamala ya kawaida ya ndani ili sarafu pekee iwe Tshs. Hii leo hata nyumba ya kupangisha unahitajia dola!
 
*kwa nini maendeleo yasichukue 17tr, na matumizi yakawa 11tr.

Kwa sababu hujui tofauti ya Matumizi ya Maendeleo na ya kawaida. Usitafsiri maneno ya kiuchumi kwa kutumia kiswahili cha mitaani utavurugikiwa kichwa!
 
Back
Top Bottom