Dondoo za Bajeti 2016/2017, kujitegemea kwa asilimia zaidi ya 80

Akili ndogo sana hii budget ni sawa na Trillion 9 tuu Shilling ilivyokua imara kwa exchange rate ya 650.
Kaka pale umeambiwa ni kwa tsh sasa unaweza kui convate vipi au ndo mpingaji wa kila kitu
Ok wazo lako likoje
 
Bajeti ya Mwaka 2016/17 ni fedha za kitanzania trilioni 29.5

Katika bajeti hiyo fedha za ndani ambazo zitakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ni fedha za kitanzania shilingi trilioni 17.8 trilioni.

Mikopo ya kibiashara itakayochukuliwa na serikali kwa ajili ya Bajeti kuu ni shilingi trilioni 7.5

Misaada ya wafadhili ni shilingi trilioni 3.6.

Matumizi ya kawaida ni shilingi trilioni 17

Matumizi ya Maendeleo 11.8 trilioni.
we jamaa mwongo balaa unatungaa figure
 
Bajeti ijayo ni trilion 29.5
Tra watakusanya 17.8
Mkopo 7.5
Misaada 3.6

Kwa mwendo huu wa kujitegemea kwa asilimia zaidi ya 80 ni hatua kubwa .....eko Magufuli
Source kamati ya bajeti
Mpaka sasa tunadaiwa trillion 40 bado tunaongeza mkopo
Ndivyo kujitegemea sio?
CCM ni ile ile
 
Bajeti ya Mwaka 2016/17 ni fedha za kitanzania trilioni 29.5

Katika bajeti hiyo fedha za ndani ambazo zitakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ni fedha za kitanzania shilingi trilioni 17.8 trilioni.

Mikopo ya kibiashara itakayochukuliwa na serikali kwa ajili ya Bajeti kuu ni shilingi trilioni 7.5

Misaada ya wafadhili ni shilingi trilioni 3.6.

Matumizi ya kawaida ni shilingi trilioni 17

Matumizi ya Maendeleo 11.8 trilioni.
Ritz na GRAND MUFTI hivi zile Billion 179 alizoiba Swaiba wangu Ustaadh Ramadhan Dau zikirudishwa si bajeti itasogea sogea kidogo?
 
Tanzania imeonyesha inataka isimame yenyewe kitu ambacho mataifa makubwa awapendi kusikiaaa kwamba taifa linasimama peke yake.
Mfano mzuri Libya ilijitaidi kusimama bila wazungu wameitafutia zengwe sasa ivi ukienda pamekuwa magofu.
Mkuuu kusimama wenywe inawezekana sana. Hao wazungu hawana nguvu kama wakiwa hawana puppet ndani ya nchi anayevuruga na nchi ikisgajua hilo huyo mtu ni kutolwa roho.
 
Sasa ivi kilichobaki mueshimiwa ajalibu kufanya mchakato na makampuni makubwa kama Huawei, Toyota, Tecno, Suzuki na makampuni ya kusindika Nyama ya Ng'ombe, ngozi, na Maziwa
Maana Kuna pesa nyingi sana apa Tanzania ajalibu kuongea na Chinese na Japanese. Kuliko kutegemea mataifa ya magharibi yana majungu sana. Wewe upewe msaada kwa kukubali kudhalilishwa alafu bado wanakuwa kukuibia
Wachina sio wa kuwaamini.... wapo katika hatua za mwanzo za kutafuta masoko na uwekezaji wa nje... kwa faida ya nchi yao... mpango ni yoyote aje ila kwa matakwa yetu sisi kama wenye malighafi....
Sio muda wa kuchagua nani aje nani asije...
suala la msingi ni atakae kuja akute sheria na taratibu zimewekwa zitakazo leta maendeleo kwa taifa letu.
 
SERIKALI imewasilisha mbele ya wabunge wote Mapendekezo ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti kwa mwaka 2016/2017, inayotarajiwa kuwa ya Sh trilioni 29.539. Kiasi hicho cha bajeti ya mwaka ujao wa fedha, kinatofautiana na bajeti ya mwaka huu wa fedha unaomalizika kwa takribani Sh trilioni tano.

Katika bajeti ya mwaka huu unaoishia, jumla ya Sh trilioni 22.495 zilitengwa kwa ajili ya bajeti nzima kutoka vyanzo vya ndani na nje. Mapendekezo ya mwaka ujao, ambayo yametajwa na baadhi ya wadau wa masuala ya siasa kuwa ni hatua kubwa na nzuri ya serikali, yanaonesha Serikali inalenga kutumia Sh trilioni 15.105, sawa na asilimia 82 ya mapato ya ndani. Mapato ya kodi na yasiyo ya kodi ni Sh trilioni 2.693 na mapato kutoka halmashauri ni Sh bilioni 665.4.

Fedha za washirika wa maendeleo zinazotarajiwa ni Sh trilioni 3.600, ambayo ni sawa na asilimia 12 ya bajeti yote. Akiwasilisha mapendekezo ya ukomo wa bajeti hiyo katika mkutano wa wabunge wote jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango, alitaja vipaumbele vya bajeti hiyo kuwa ni utekelezaji wa awamu ya pili ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2016/2017 wa miaka mitano.

Viwanda, ulipaji madeni Alitaja vipaumbele vingine kuwa ni viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda, kufungamanisha maendeleo ya uchumi na rasilimali watu na mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara.

Alisema bajeti hiyo, pia itaweka mkazo zaidi katika ukamilishaji wa miradi inayoendelea, miradi mipya, ulipaji wa madeni yaliyohakikiwa na utekelezaji wa maeneo yote ya vipaumbele, yaliyoainishwa katika Mpango huo wa Maendeleo wa mwaka 2016/17.

Akizungumzia mfumo wa bajeti hiyo, Waziri huyo alisema pamoja na michango ya ndani, pia washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia Sh trilioni 3.600 sawa na asilimia 12 ya bajeti yote ambayo ni misaada na mikopo, inayojumuisha miradi ya maendeleo, mifuko ya pamoja ya kisekta na ya kibajeti.

“Pia Serikali inatarajia kukopa Sh trilioni 5.374 kutoka soko la ndani kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva pamoja na mikopo mipya kwa ajili kugharimia miradi ya maendeleo ya pamoja na kulipia malimbikizo ya madai yaliyohakikiwa.

Mkopo nje “Vilevile ili kuongeza kasi katika ujenzi wa miundombinu, Serikali inatarajia kukopa Sh trilioni 2.101 kutoka soko la nje kwa masharti ya kibiashara,” alisisitiza Dk Mpango.

Akichanganua mapendekezo hayo ya bajeti, alisema kwa upande wa matumizi katika mwaka ujao wa fedha, Serikali inapanga kutumia Sh trilioni 17.719 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh trilioni 11.820 kwa matumizi ya maendeleo sawa na asilimia 40 ya bajeti yote. Aidha kiasi cha Sh trilioni 8.702 ni kwa ajili ya fedha za ndani na Sh trilioni 3.117 ni fedha za nje.

Bajeti inayomalizika Katika bajeti ya mwaka huu unaoishia, jumla ya Sh trilioni 22.495 zilitengwa kwa ajili bajeti nzima kutoka vyanzo vya nje na ndani. Jumla ya Sh trilioni 8.987 zilikuwa ni makusanyo ya ndani, halmashauri zikijumuishwa, sawa na asilimia 97 ya makadirio ya kukusanya Sh trilioni 9.281 katika kipindi hicho.

Dk Mpango alifafanua kuwa katika bajeti hiyo, mapato ya kodi yalikuwa ni Sh trilioni 7.931 sawa na asilimia 99 ya lengo la kukusanya Sh trilioni 8.016 kwa kipindi hicho.

Alisema mapato yasiyo ya kodi, yalikuwa Sh bilioni 786.1 sawa na asilimia 86 ya lengo la kukusanya Sh bilioni 916.1. Mapato yaliyokusanywa na halmashauri, yalikuwa Sh bilioni 270 sawa na asilimia 78 ya makadirio ya Sh bilioni 347.9 kwa kipindi hicho.

Alisema kwa mujibu wa matarajio ya bajeti hiyo, washirika wa maendeleo waliahidi kutoa Sh trilioni 2.322 kama misaada na mikopo nafuu, lakini hadi kufikia Februari mwaka huu, walitoa jumla ya Sh trilioni 1.017 ambazo ni sawa na asilimia 62.5 ya malengo.

Alisema Serikali ilitarajia kukopa mikopo yenye masharti nafuu ya kibiashara kutoka vyanzo vya nje na ndani jumla ya Sh trilioni 6.175.

Alisema kutofikiwa kwa malengo ya mikopo ya kibajeti, kulitokana na baadhi ya washirika wa maendeleo kupunguza ahadi zao, kuweka masharti mapya na wengine kuamua kutotoa fedha walizoahidi kwa sababu ya kubadilika kwa sera za ndani za nchi zao zinazohusu misaada kwa nchi zinazoendelea.

Aidha alisema hadi kufikia Februari mwaka huu, Serikali ilishakopa cha Sh trilioni 3.688 ikiwa ni asilimia 101 ya kiasi kilichopangwa kukopwa katika kipindi hicho.

Kati ya kiasi hicho Sh trilioni 2.133 zilikopwa kwa ajili ya kulipia amana za Serikali zilizoiva na mikopo mipya ilikuwa ni Sh trilioni 1.554 sawa na asilimia 101 ya kiasi kilichopangwa kukopwa.

Akizungumzia mgawanyo wa fedha za bajeti hiyo inayoishia, Dk Mpango alisema Serikali ilitoa mgawo wa Sh trilioni 13.152 kwenda kwenye mafungu mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti hiyo sawa na asilimia 92 ya makadirio ya bajeti hiyo.

Alisema jumla ya Sh trilioni 10.595 zilitolewa katika eneo la matumizi ya kawaida, linalojumuisha mishahara na malipo ya deni la taifa wakati jumla ya Sh trilioni 2.557 zilitolewa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Dk Mpango alisema hadi kufikia Februari mwaka huu, deni la taifa linalojumuisha Serikali na sekta binafsi, lilifikia dola za Marekani milioni 19.9 ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 19.6 kwa kipindi kinachoishia Juni mwaka jana.

Alisema kati ya kiasi hicho, dola za Marekani milioni 17.5 zilikuwa ni deni la Serikali na dola za Marekani milioni 2.3 ni deni la sekta binafsi hivyo deni la Serikali liliongezeka kwa asilimia nne.

Aliyataja mafanikio ya bajeti hiyo kuwa ni kuendelea kukua kwa uchumi kwa asilimia saba, kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya ndani hadi kufikia asilimia 99 ya lengo, kuendelea kupungua kwa mfumuko wa bei na kufikia asilimia 5.6 na kutia kwa wakati fedha za miradi ya maendeleo yenye vyanzo mahsusi kama vile mfuko wa barabara, wakala wa nishati, mfuko wa maji na reli.

Mafanikio mengine ni kuendelea kujenga miundombinu katika sekta za nishati, barabara, mawasiliano na uchukuzi, kufanikisha uchaguzi mkuu mwaka jana kwa kutumia fedha za ndani, kupunguza malimbikizo ya madai ya watumishi, wazabuni na wakandarasi na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaonufaika na mikopo waliohakikiwa.

Waziri Mpango alisema katika mwaka ujao wa fedha Serikali imelenga kuhakikisha kuwa pato halisi la taifa linakua kwa asilimia 7.2 kutoka asilimia saba, kuendelea kudhibiti mfumuko wa bei, ukusanyaji wa mapato ya ndani na halmashauri kuongezeka na kufikia asilimia 14.8 na mapato ya kodi kufikia asilimia 12.6.

Aidha alisema pia Serikali inatarajia kuongeza matumizi kutoka asilimia 23.9 ya pato la taifa hadi kufikia asilimia 27 na kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne.

“Katika Serikali ya awamu ya tano tunatarajia mapato ya Serikali yataongezeka na kupunguza utegemezi wa misaada na mikopo nafuu kutoka kwa washirika wa maendeleo ambayo imekuwa haitabiriki kwa siku za karibuni,” alisisitiza.

Alisema katika mwaka ujao wa fedha Serikali itasimamia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia sheria ya bajeti na maelekezo ya viongozi wa juu wa Serikali, lengo likiwa ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuziba mianya ya uvujaji wa fedha za umma.

Alisema ili kufanikisha azma hiyo, Serikali imepanga kuwianisha matumizi na mapato halisi yatakayopatikana kwa kila mwezi, kuimarisha ufuatiliaji wa matumizi ya Serikali ili yatumike kama ilivyokusudiwa, kusimamia maagizo yaliyotolewa na Serikali kama ununuzi wa samani na magari, kuziunganisha halmashauri zote katika mfumo wa malipo ya kibenki.

Kwi kwi kwi kwi mkuu mbona bajeti yenyewe bado inategemea wafadhili kwi kwi kwi kwi
 
duh au mm sielewi matumizi ya kawaida t17, ya maendeleo 11.. yaan ktk maendeleo tunatumia kidogo, duh, anyway may b mtu anisaidie tafsiri sahihi ya matumizi ya kawaida, plz
 
Bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano itaizidi ya Serikali ya Awamu ya Nne kwa Sh7.1 trilioni baada ya Waziri wa Fedha kutangaza sura ya bajeti ya mwaka 2016/17 inayoonyesha kutakuwa na makusanyo na matumizi ya Sh29.5 trilioni.

Sura hiyo ya bajeti ya mwaka 2016/17 inatofautiana na iliyopita iliyokuwa ya Sh22.45 trilioni katika maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na kiwango cha fedha kitakachotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo, ambacho ni zaidi ya mara mbili ya fedha za eneo hilo katika bajeti iliyopita.

Waziri wa Fedha, Dk Phillip Mpango alisema wakati akiwasilisha mapendekezo ya kiwango cha ukomo wa bajeti jijini Dar es Salaam jana kuwa kati ya fedha hizo, Sh18.46 trilioni, ambazo ni sawa na asilimia 62.5 ya bajeti yote, zitatokana na jumla ya mapato ya ndani yanayohusisha na halmashauri.

Kiwango hicho kimezidi Sh3.64 trilioni ya bajeti iliyopita ambayo ililenga kukusanya Sh14.82 trilioni.

“Kati ya mapato hayo, Serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi ya jumla ya Sh15,105 bilioni, sawa na asilimia 82 ya mapato ya ndani,”alisema Dk Mpango.

Alisema makisio ya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi yameongezeka kwa kuwa kuna viashiria vingi vinavyoonyesha kwamba Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kushirikiana na wizara na taasisi zinazokusanya maduhuli, zina uwezo wa kukusanya kiasi hicho.

Alisema: “Kipaumbele cha kwanza cha Serikali kitakuwa ni kujizatiti katika ukusanyaji wa mapato kwa kubuni vyanzo vipya na kuendelea kudhibiti mianya mbalimbali ya ukwepaji wa kodi. Suala hili linahitaji ushirikiano wa karibu na wananchi ili tujiletee maendeleo ya haraka kwa kushiriki kulipa kodi na kuwafichua wakwepa kodi kwa kuwaona kama maadui wa maendeleo yetu.”

Kwa mujibu wa Dk Mpango, Sh17.72 trilioni zitakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, wakati Sh11.82 trilioni, sawa na asilimia 40 ya bajeti nzima, zimetengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Katika bajeti iliyopita, matumizi ya kawaida yalitengewa Sh16.7 trilioni, sawa na asilimia 74.3 wakati shughuli za maendeleo zilipangiwa Sh5.76 sawa na asilimia 25.9.

“Asilimia 40 kwenda kwenye mipango ya maendeleo, hili ni jambo jema,” alisema Freeman Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa Chadema na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, alipoongea na waandishi.

“Kwamba tumepunguza matumizi ya kawaida ya Serikali na kuelekeza fedha zaidi kwenye mipango ya maendeleo, nasema hili ni jambo jema kama litatekelezeka.”

Vipaumbele
Kwa mujibu wa Dk Mpango, shughuli zitakazopewa kipaumbele kwenye mipango hiyo ya maendeleo zimegawanywa katika maeneo manne ambayo ni viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda, kufungamanisha maendeleo ya uchumi na rasilimali watu, mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji na pia usimamizi wa utekelezaji wa mpango.

Dk Mpango alisema washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia Sh3.6 trilioni, ikiwa ni ongezeko la Sh1.7 trilioni kulinganisha na Sh1.88 trilioni zilizokuwa zinategemewa kwenye bajeti iliyopita.

Fedha hizo zitakuwa za misaada na mikopo nafuu kutoka nje ambayo ni pamoja na GBS, Basket Fund na miradi ya maendeleo.

Aidha Serikali inatarajia kukopa Sh5,374.3 bilioni kutoka soko la ndani kwa ajili ya kulipia hati fungani na dhamana za Serikali zinazoiva pamoja, wakati kutoka kwenye soko la nje kwa masharti ya kibiashara inatarajia kukopa Sh2.1 trilioni.

Awali Spika Job Ndugai alisema kwa mujibu wa utaratibu mapendezo hayo yalipaswa kuwasilishwa tangu Machi 11, lakini kutokana na ratiba za wabunge wengi kuwa kwenye majimbo yao, aliamua kuongeza siku.

“ Sasa ninawashauri wabunge wote kwenda kuyasoma mapendekezo hayo vyema ili mpate nafasi ya kuchangia fedha bajeti itakapowasilishwa bungeni. Pia mhudhurie kwenye vikao vya kamati zenu ili kujipanga vyema. Wale watakaokuwa hawaonekani kwenye vikao, tutawasilisha majina yao kwenye vyama vyao ili wachukuliwe hatua zinazostahili.”

Miradi ya maendeleo
Katika kuongeza wigo wa makusanyo ya kodi, Dk Mpango alisema sera za mapato kwa mwaka 2016/2017 itajielekeza kufanya tathimini ya mkupuo ya majengo ili kuongeza mapato.

Katika mpango wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, Dk Mpango alisema kipaumbele kitakuwa ni mradi wa magadi soda ulioko kwenye Bonde la Engaruka ambako utafiti umebaini kuna magadi ya mita za ujazo bilioni 4.68 ambazo huongezeka kila mwaka kwa mita milioni 1.9 za ujazo.

“Mradi utahusisha kiwanda cha kuzalisha tani milioni moja za magadi kwa mwaka kwa ajili ya matumizi ya viwanda, hususan madawa, vioo na sabuni,” alisema.

Mradi huo utakapokamilika utaliingizia taifa Sh 400 bilioni kwa mwaka.

Eneo jingine ni kufufua kiwanda cha General Tyre cha Arusha, ambacho kimetengewa Sh2 bilioni kwa kazi hiyo. Pia kiwanda cha viuadudu kilichopo Kibaha mkoani Pwani ambacho mradi wake utatekelezwa kwa awamu tatu, mbili za mwisho zikihusisha ujenzi wa kiwanda cha mbolea na cha virutubisho.

Pia mpango huo utahusisha uendelezaji wa viwanda vidogo mkoani Morogoro, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza.

Katika kufunganisha maendeleo ya uchumi na rasilimali watu, Serikali itaweka nguvu kwenye elimu na mafunzo ya ufundi, ikihusisha kuimarisha mifumo, majengo na miundombinu katika shule za awali, msingi na sekondari.

Pia itahusisha ukarabati, upanuzi na ujenzi wa vyuo vikuu, mradi wa upanuzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (Mkwawa, Duce, Udom na OUT, Ardhi, Mzumbe, Sokoine, Muhimbili, Ushirika, Chuo Kikuu cha Sayansi cha Mwalimu Nyerere na pia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Eneo hilo litahusisha uendelezaji ustawi wa jamii kwa kuangalia huduma za afya, maji, kazi na ajira, na uwezeshaji wananchi kwa kutoa Sh50 milioni kwa kila kijiji.

Mazingira wezeshi
Katika kujenga mazingira wezeshi, Serikali itaongeza uwezo wa uzalishaji umeme, usambazaji umeme mijini na vijijini, ujenzi wa kiwanda cha kupokea, kuchakata na kubadilisha gesi asilia kuwa katika kimiminika kwa ajili ya kusafirisha nje, ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha gesi asilia, ujenzi wa miundombinu ya usafiri, teknolojia ya habari na mawasiliano, miradi ya makaa ya mawe na mradi wa chuma wa Liganga.
 
Pumba tupu. Walimu wataendelea kuishi kwenye nyumba za majani huku wakishindia viwavi jeshi.
 
ni bajeti nzuri ikienda kma ilivyopangwa.......
tatzo la viongoz wanaoongozwa na mfumo uliioza wa ccm,...huwa porojo nyingi utekelezaji 0......
 
maeneo manne ambayo ni viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda, kufungamanisha maendeleo ya uchumi na rasilimali watu, mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji na pia usimamizi wa utekelezaji wa mpango.
Katika mpango wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, Dk Mpango alisema kipaumbele kitakuwa ni mradi wa magadi soda ulioko kwenye Bonde la Engaruka ambako utafiti umebaini kuna magadi ya mita za ujazo bilioni 4.68 ambazo huongezeka kila mwaka kwa mita milioni 1.9 za ujazo.
“Mradi utahusisha kiwanda cha kuzalisha tani milioni moja za magadi kwa mwaka kwa ajili ya matumizi ya viwanda, hususan madawa, vioo na sabuni,” alisema.
Mradi huo utakapokamilika utaliingizia taifa Sh 400 bilioni kwa mwaka
.
Katika kufunganisha maendeleo ya uchumi na rasilimali watu, Serikali itaweka nguvu kwenye elimu na mafunzo ya ufundi, ikihusisha kuimarisha mifumo, majengo na miundombinu katika shule za awali, msingi na sekondari.
Pia itahusisha ukarabati, upanuzi na ujenzi wa vyuo vikuu, mradi wa upanuzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (Mkwawa, Duce, Udom na OUT, Ardhi, Mzumbe, Sokoine, Muhimbili, Ushirika, Chuo Kikuu cha Sayansi cha Mwalimu Nyerere na pia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.
Eneo hilo litahusisha uendelezaji ustawi wa jamii kwa kuangalia huduma za afya, maji, kazi na ajira, na uwezeshaji wananchi kwa kutoa Sh50 milioni kwa kila kijiji
.
Katika kujenga mazingira wezeshi, Serikali itaongeza uwezo wa uzalishaji umeme, usambazaji umeme mijini na vijijini, ujenzi wa kiwanda cha kupokea, kuchakata na kubadilisha gesi asilia kuwa katika kimiminika kwa ajili ya kusafirisha nje, ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha gesi asilia, ujenzi wa miundombinu ya usafiri, teknolojia ya habari na mawasiliano, miradi ya makaa ya mawe na mradi wa chuma wa Liganga.
kwahiyo bajetri kma itatekelezwa itakuwa good/..........
na hasa serikali ikiwekeza sana kwenye magadi soda ambapo wataweza kutengeneza madawa kwa wingi,vioo kwa wingi na sabuni.
bajeti isiwe porojo tu ndo kitu cha msingi,......
na serikali ipigane kupandisha thamani ya shillingi
 
Yaani inakuwa aina tofauti na mzazi kakusomesha ukipata kazi. Anakupa wajibu wa kulea wadogo Zako na yeye atakama anao uwezo. Dunia ina fitina sana, tena pale unapoanza kusimama. Cha msingi kuwa makini wanaokufata kipindi ambacho kinaonyesha kwamba unataka kusimama
Ww kumbe akili za mbayuwayu ulitaka ukimaliza shule uanze kutumbua ? hakuna vya bure dunia hii
 
KODI YA BIDHAA NA HUDUMA INASHUKA KWA ASILIMIA NGAPI?! MASHIRIKA YANAYOTOA HUDUMA KAMA MAJI, UMEME NA AFYA YATASHUSHA KODI KWA ASILIMIA NGAPI?! MADINI KAMA DHAHABU, ALMASI, TANZANITE, BATI, MAKAA YA MAWE, CHUMA, ULANGA, NK, MAPATO YAKE YATAPANDA KWA KIWANGO GANI?! GESI YA ASILI MAPATO YAKE YANAPANDA KWA KIWANGO GANI?! UTALII: MBUGA ZA WANYAMA, MILIMA KAMA KILIMANJARO, NK, MAPATO YAKE YATAPANDA KWA KIWANGO GANI?! POROJO HATUTAKI.!

Reagan bwana
 
Bajeti ya Mwaka 2016/17 ni fedha za kitanzania trilioni 29.5

Katika bajeti hiyo fedha za ndani ambazo zitakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ni fedha za kitanzania shilingi trilioni 17.8 trilioni.

Mikopo ya kibiashara itakayochukuliwa na serikali kwa ajili ya Bajeti kuu ni shilingi trilioni 7.5

Misaada ya wafadhili ni shilingi trilioni 3.6.

Matumizi ya kawaida ni shilingi trilioni 17

Matumizi ya Maendeleo 11.8 trilioni.

=================================================

Shida yetu iko hapo!

Ni yapi haya matumizi ya Kawaida?
Yaani kwenye pesa zetu za ndani tunabakiwa na Bilioni 800 tu?.
Kama kweli Magufuli anataka tujikwamue haya matumizi ya kawaida yawe 11.8trilioni .Ila hata kama wafadhili na mikopo itakwama bado serikali yake itaweza kufanya shughuli ndogo ndogo za maendeleo.

Kama ni mimi hao wataalamu lazima waje na hesabu iliyohalisia. Yaani tunachokisanya yote matumizi ya kawaida?
Hatuko serious!
 
Back
Top Bottom