Serikali kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 62.33 kwa mwaka 2026/2027

Serikali kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 62.33 kwa mwaka 2026/2027

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,943
Reaction score
2,982
kwa mwaka2026/27 Serikali inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 62.33, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.3 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2025/26.

Mchanganuo wa Matumizi ya Shilingi Trilioni 54.5

Waziri wa Fedha amefafanua kuwa kiasi hicho cha fedha kimetengwa kwa ajili ya matumizi pasipo kujumuisha malipo ya mtaji wa deni la serikali, ambapo mchanganuo wake uko kama ifuatavyo:

  • Ruzuku: Shilingi trilioni 25.32
  • Stahiki za Watumishi (ikiwemo Pensheni): Shilingi trilioni 10.13
  • Malipo ya Riba: Shilingi trilioni 6.86
  • Gharama za Bidhaa na Huduma: Shilingi trilioni 5.22
  • Gharama Nyinginezo: Shilingi trilioni 3.63
  • Uwekezaji katika Maamuzi ya Kifedha: Shilingi trilioni 2.33
  • Mafao na Misaada ya Kijamii: Shilingi trilioni 1.01
Balozi Khamis Mussa Omar ameeleza kuwa kutokana na makadirio ya mapato na matumizi hayo, bajeti ya serikali inakabiliwa na nakisi ya shilingi trilioni 7.71. Ili kuziba pengo hilo, serikali imepanga kukopa jumla ya shilingi trilioni 15.54 kwa kuzingatia mkakati wa muda wa kati wa kusimamia deni la serikali (2025/26 hadi 2027/28).

Mchanganuo wa mikopo hiyo unajumuisha:

  1. Mikopo ya Ndani: Shilingi trilioni 6.56.
  2. Mikopo ya Nje yenye Masharti Nafuu: Shilingi trilioni 6.55.
  3. Mikopo ya Nje yenye Masharti ya Kibiashara: Shilingi trilioni 2.43.
Aidha, kando na mikopo hiyo mipya, Waziri amebainisha kuwa serikali inakadiria kutumia shilingi trilioni 7.84 kwa ajili ya kulipa malipo ya mtaji kwa mikopo yote ambayo tayari



 
Back
Top Bottom