Dondoo za Bajeti 2016/2017, kujitegemea kwa asilimia zaidi ya 80

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
20,051
23,499
Bajeti ya Mwaka 2016/17 ni fedha za kitanzania trilioni 29.5

Katika bajeti hiyo fedha za ndani ambazo zitakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ni fedha za kitanzania shilingi trilioni 17.8 trilioni.

Mikopo ya kibiashara itakayochukuliwa na serikali kwa ajili ya Bajeti kuu ni shilingi trilioni 7.5

Misaada ya wafadhili ni shilingi trilioni 3.6.

Matumizi ya kawaida ni shilingi trilioni 17

Matumizi ya Maendeleo 11.8 trilioni.

========================
SERIKALI imewasilisha mbele ya wabunge wote Mapendekezo ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti kwa mwaka 2016/2017, inayotarajiwa kuwa ya Sh trilioni 29.539. Kiasi hicho cha bajeti ya mwaka ujao wa fedha, kinatofautiana na bajeti ya mwaka huu wa fedha unaomalizika kwa takribani Sh trilioni tano.

Katika bajeti ya mwaka huu unaoishia, jumla ya Sh trilioni 22.495 zilitengwa kwa ajili ya bajeti nzima kutoka vyanzo vya ndani na nje. Mapendekezo ya mwaka ujao, ambayo yametajwa na baadhi ya wadau wa masuala ya siasa kuwa ni hatua kubwa na nzuri ya serikali, yanaonesha Serikali inalenga kutumia Sh trilioni 15.105, sawa na asilimia 82 ya mapato ya ndani. Mapato ya kodi na yasiyo ya kodi ni Sh trilioni 2.693 na mapato kutoka halmashauri ni Sh bilioni 665.4.

Fedha za washirika wa maendeleo zinazotarajiwa ni Sh trilioni 3.600, ambayo ni sawa na asilimia 12 ya bajeti yote. Akiwasilisha mapendekezo ya ukomo wa bajeti hiyo katika mkutano wa wabunge wote jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango, alitaja vipaumbele vya bajeti hiyo kuwa ni utekelezaji wa awamu ya pili ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2016/2017 wa miaka mitano.

Viwanda, ulipaji madeni Alitaja vipaumbele vingine kuwa ni viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda, kufungamanisha maendeleo ya uchumi na rasilimali watu na mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara.

Alisema bajeti hiyo, pia itaweka mkazo zaidi katika ukamilishaji wa miradi inayoendelea, miradi mipya, ulipaji wa madeni yaliyohakikiwa na utekelezaji wa maeneo yote ya vipaumbele, yaliyoainishwa katika Mpango huo wa Maendeleo wa mwaka 2016/17.

Akizungumzia mfumo wa bajeti hiyo, Waziri huyo alisema pamoja na michango ya ndani, pia washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia Sh trilioni 3.600 sawa na asilimia 12 ya bajeti yote ambayo ni misaada na mikopo, inayojumuisha miradi ya maendeleo, mifuko ya pamoja ya kisekta na ya kibajeti.

“Pia Serikali inatarajia kukopa Sh trilioni 5.374 kutoka soko la ndani kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva pamoja na mikopo mipya kwa ajili kugharimia miradi ya maendeleo ya pamoja na kulipia malimbikizo ya madai yaliyohakikiwa.

Mkopo nje “Vilevile ili kuongeza kasi katika ujenzi wa miundombinu, Serikali inatarajia kukopa Sh trilioni 2.101 kutoka soko la nje kwa masharti ya kibiashara,” alisisitiza Dk Mpango.

Akichanganua mapendekezo hayo ya bajeti, alisema kwa upande wa matumizi katika mwaka ujao wa fedha, Serikali inapanga kutumia Sh trilioni 17.719 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh trilioni 11.820 kwa matumizi ya maendeleo sawa na asilimia 40 ya bajeti yote. Aidha kiasi cha Sh trilioni 8.702 ni kwa ajili ya fedha za ndani na Sh trilioni 3.117 ni fedha za nje.

Bajeti inayomalizika Katika bajeti ya mwaka huu unaoishia, jumla ya Sh trilioni 22.495 zilitengwa kwa ajili bajeti nzima kutoka vyanzo vya nje na ndani. Jumla ya Sh trilioni 8.987 zilikuwa ni makusanyo ya ndani, halmashauri zikijumuishwa, sawa na asilimia 97 ya makadirio ya kukusanya Sh trilioni 9.281 katika kipindi hicho.

Dk Mpango alifafanua kuwa katika bajeti hiyo, mapato ya kodi yalikuwa ni Sh trilioni 7.931 sawa na asilimia 99 ya lengo la kukusanya Sh trilioni 8.016 kwa kipindi hicho.

Alisema mapato yasiyo ya kodi, yalikuwa Sh bilioni 786.1 sawa na asilimia 86 ya lengo la kukusanya Sh bilioni 916.1. Mapato yaliyokusanywa na halmashauri, yalikuwa Sh bilioni 270 sawa na asilimia 78 ya makadirio ya Sh bilioni 347.9 kwa kipindi hicho.

Alisema kwa mujibu wa matarajio ya bajeti hiyo, washirika wa maendeleo waliahidi kutoa Sh trilioni 2.322 kama misaada na mikopo nafuu, lakini hadi kufikia Februari mwaka huu, walitoa jumla ya Sh trilioni 1.017 ambazo ni sawa na asilimia 62.5 ya malengo.

Alisema Serikali ilitarajia kukopa mikopo yenye masharti nafuu ya kibiashara kutoka vyanzo vya nje na ndani jumla ya Sh trilioni 6.175.

Alisema kutofikiwa kwa malengo ya mikopo ya kibajeti, kulitokana na baadhi ya washirika wa maendeleo kupunguza ahadi zao, kuweka masharti mapya na wengine kuamua kutotoa fedha walizoahidi kwa sababu ya kubadilika kwa sera za ndani za nchi zao zinazohusu misaada kwa nchi zinazoendelea.

Aidha alisema hadi kufikia Februari mwaka huu, Serikali ilishakopa cha Sh trilioni 3.688 ikiwa ni asilimia 101 ya kiasi kilichopangwa kukopwa katika kipindi hicho.

Kati ya kiasi hicho Sh trilioni 2.133 zilikopwa kwa ajili ya kulipia amana za Serikali zilizoiva na mikopo mipya ilikuwa ni Sh trilioni 1.554 sawa na asilimia 101 ya kiasi kilichopangwa kukopwa.

Akizungumzia mgawanyo wa fedha za bajeti hiyo inayoishia, Dk Mpango alisema Serikali ilitoa mgawo wa Sh trilioni 13.152 kwenda kwenye mafungu mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti hiyo sawa na asilimia 92 ya makadirio ya bajeti hiyo.

Alisema jumla ya Sh trilioni 10.595 zilitolewa katika eneo la matumizi ya kawaida, linalojumuisha mishahara na malipo ya deni la taifa wakati jumla ya Sh trilioni 2.557 zilitolewa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Dk Mpango alisema hadi kufikia Februari mwaka huu, deni la taifa linalojumuisha Serikali na sekta binafsi, lilifikia dola za Marekani milioni 19.9 ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 19.6 kwa kipindi kinachoishia Juni mwaka jana.

Alisema kati ya kiasi hicho, dola za Marekani milioni 17.5 zilikuwa ni deni la Serikali na dola za Marekani milioni 2.3 ni deni la sekta binafsi hivyo deni la Serikali liliongezeka kwa asilimia nne.

Aliyataja mafanikio ya bajeti hiyo kuwa ni kuendelea kukua kwa uchumi kwa asilimia saba, kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya ndani hadi kufikia asilimia 99 ya lengo, kuendelea kupungua kwa mfumuko wa bei na kufikia asilimia 5.6 na kutia kwa wakati fedha za miradi ya maendeleo yenye vyanzo mahsusi kama vile mfuko wa barabara, wakala wa nishati, mfuko wa maji na reli.

Mafanikio mengine ni kuendelea kujenga miundombinu katika sekta za nishati, barabara, mawasiliano na uchukuzi, kufanikisha uchaguzi mkuu mwaka jana kwa kutumia fedha za ndani, kupunguza malimbikizo ya madai ya watumishi, wazabuni na wakandarasi na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaonufaika na mikopo waliohakikiwa.

Waziri Mpango alisema katika mwaka ujao wa fedha Serikali imelenga kuhakikisha kuwa pato halisi la taifa linakua kwa asilimia 7.2 kutoka asilimia saba, kuendelea kudhibiti mfumuko wa bei, ukusanyaji wa mapato ya ndani na halmashauri kuongezeka na kufikia asilimia 14.8 na mapato ya kodi kufikia asilimia 12.6.

Aidha alisema pia Serikali inatarajia kuongeza matumizi kutoka asilimia 23.9 ya pato la taifa hadi kufikia asilimia 27 na kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne.

“Katika Serikali ya awamu ya tano tunatarajia mapato ya Serikali yataongezeka na kupunguza utegemezi wa misaada na mikopo nafuu kutoka kwa washirika wa maendeleo ambayo imekuwa haitabiriki kwa siku za karibuni,” alisisitiza.

Alisema katika mwaka ujao wa fedha Serikali itasimamia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia sheria ya bajeti na maelekezo ya viongozi wa juu wa Serikali, lengo likiwa ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuziba mianya ya uvujaji wa fedha za umma.

Alisema ili kufanikisha azma hiyo, Serikali imepanga kuwianisha matumizi na mapato halisi yatakayopatikana kwa kila mwezi, kuimarisha ufuatiliaji wa matumizi ya Serikali ili yatumike kama ilivyokusudiwa, kusimamia maagizo yaliyotolewa na Serikali kama ununuzi wa samani na magari, kuziunganisha halmashauri zote katika mfumo wa malipo ya kibenki.
 
Si rahisi bajeti ya maendeleo kuizidi bajeti ya kawaida. Nakumbuka kipindi fulani Prof Lipumba alilielezea vizuri hili kwamba bajeti ya matumizi huwa kubwa kwa kuwa ndio inalipa watendaji wote na wawezeshaji wa hayo maendeleo tunayoyakusudia. Kwa hiyo bajeti ya matumizi ikiwa ndogo kuna uwezekano miradi ya maendeleo isifanyike maana haitawezekana kuwalipa waibuaji, watendaji, wafuatiliaji na waendelezaji wa hiyo miradi.
 
Bajeti ya Mwaka 2016/17 ni
tshs 29.5 trillions. TRA
watakusanya tshs 17.8
trilioni. Mikopo itachukuliwa
tshs 7.5 trilioni na Misaada ya
wafadhili 3.6 trilioni. Matumizi
ya kawaida tshs 17 trilioni na
Matumizi ya Maendeleo 11.8
trilioni.
Bajeti ya tshs 29.5 trilioni ni
hatua kubwa sana.
Akili ndogo sana hii budget ni sawa na Trillion 9 tuu Shilling ilivyokua imara kwa exchange rate ya 650.
 
Bajeti ya Mwaka 2016/17 ni tshs 29.5 trillions. TRA watakusanya tshs 17.8 trilioni. Mikopo itachukuliwa tshs 7.5 trilioni na Misaada ya wafadhili 3.6 trilioni. Matumizi ya kawaida tshs 17 trilioni na Matumizi ya Maendeleo 11.trilioni.Bajeti ya tshs 29.5 trilioni ni hatua kubwa sana.
Tatizo la hizi bajeti unaweza kufurahia figure hapo lakini mwisho wa mwaka wa fedha hela iliyopatikana unakuta hata robo tatu haifiki, kuna Taasisi moja ya Muhimbili walipangiwa 118Biln mpaka jana kamati ya bunge imepita pale hela waliyopata ni 1 Biln Taasisi nyeti kama Afya.
 
Bajeti ya Mwaka 2016/17 ni tshs 29.5 trillions. TRA watakusanya tshs 17.8 trilioni. Mikopo itachukuliwa tshs 7.5 trilioni na Misaada ya wafadhili 3.6 trilioni. Matumizi ya kawaida tshs 17 trilioni na Matumizi ya Maendeleo 11.trilioni.Bajeti ya tshs 29.5 trilioni ni hatua kubwa sana.
KODI YA BIDHAA NA HUDUMA INASHUKA KWA ASILIMIA NGAPI?! MASHIRIKA YANAYOTOA HUDUMA KAMA MAJI, UMEME NA AFYA YATASHUSHA KODI KWA ASILIMIA NGAPI?! MADINI KAMA DHAHABU, ALMASI, TANZANITE, BATI, MAKAA YA MAWE, CHUMA, ULANGA, NK, MAPATO YAKE YATAPANDA KWA KIWANGO GANI?! GESI YA ASILI MAPATO YAKE YANAPANDA KWA KIWANGO GANI?! UTALII: MBUGA ZA WANYAMA, MILIMA KAMA KILIMANJARO, NK, MAPATO YAKE YATAPANDA KWA KIWANGO GANI?! POROJO HATUTAKI.!
 
Wanaotupa msaada wa kuendesha budget zetu. Wakiona tunaaanza kusimama wataanza kukumbushia madeni yao. Hapo ndio inakuwa shida sana
 
Yaani inakuwa aina tofauti na mzazi kakusomesha ukipata kazi. Anakupa wajibu wa kulea wadogo Zako na yeye atakama anao uwezo. Dunia ina fitina sana, tena pale unapoanza kusimama. Cha msingi kuwa makini wanaokufata kipindi ambacho kinaonyesha kwamba unataka kusimama
 
Tanzania imeonyesha inataka isimame yenyewe kitu ambacho mataifa makubwa awapendi kusikiaaa kwamba taifa linasimama peke yake.
Mfano mzuri Libya ilijitaidi kusimama bila wazungu wameitafutia zengwe sasa ivi ukienda pamekuwa magofu.
 
KODI YA BIDHAA NA HUDUMA INASHUKA KWA ASILIMIA NGAPI?! MASHIRIKA YANAYOTOA HUDUMA KAMA MAJI, UMEME NA AFYA YATASHUSHA KODI KWA ASILIMIA NGAPI?! MADINI KAMA DHAHABU, ALMASI, TANZANITE, BATI, MAKAA YA MAWE, CHUMA, ULANGA, NK, MAPATO YAKE YATAPANDA KWA KIWANGO GANI?! GESI YA ASILI MAPATO YAKE YANAPANDA KWA KIWANGO GANI?! UTALII: MBUGA ZA WANYAMA, MILIMA KAMA KILIMANJARO, NK, MAPATO YAKE YATAPANDA KWA KIWANGO GANI?! POROJO HATUTAKI.!
Unajua maana ya makadirio ya bajeti au umeuliza maswali ambayo yanasubiria bunge kujadili mgawanyo wa kila wizara
 
Sasa ivi kilichobaki mueshimiwa ajalibu kufanya mchakato na makampuni makubwa kama Huawei, Toyota, Tecno, Suzuki na makampuni ya kusindika Nyama ya Ng'ombe, ngozi, na Maziwa
Maana Kuna pesa nyingi sana apa Tanzania ajalibu kuongea na Chinese na Japanese. Kuliko kutegemea mataifa ya magharibi yana majungu sana. Wewe upewe msaada kwa kukubali kudhalilishwa alafu bado wanakuwa kukuibia
 
Hivi ni kweli wachangiaji wa huu uzi ni vilaza kiasi hiki mbona sioni Public debt imefikia sh. ngapi halafu bado unakopa 7.5 Trillion watu mnasifia Ujinga
Unawaona watu ni vilaza ila huenda na wao wanakushangaa, kwani makadirio ya bajeti lazima yaainishe deni la taifa? Na sijui hiyo public debt ni kitu gani kwenye makadirio ya bajeti
 
Back
Top Bottom