Dondoo za Bajeti 2016/2017, kujitegemea kwa asilimia zaidi ya 80

Dondoo za Bajeti 2016/2017, kujitegemea kwa asilimia zaidi ya 80

So ni TZS. 45 Trillion halafu zitakopwa 7.5Trillion so deni litakua 52.5Trillion hili deni ni kubwa tatizo la deni la Taifa huathiri vizazi na vizazi.
what do you care about vizazi man? hapa ni kuji take care wewe na familia yako, ukiwa unaangalia mambo ya vizazi vijavyo hapa Afrika utaishia kuumiza kichwa bure ukakosa hata raha
 
Mimi sijaona lamaana hapo mbona deni linaendelea kukua haatima ya hilo deni itanakuwaje?
 
Haya yote maigizo tu.misaada +mikopo sawa na 12 trillion ambayo ni karibu nusu ya budget,bado public debt
HA HA HA HA.. wakawa ni kiboko aisee.. yaani 3.6+7.5=12????? kweli.. ha haha. yaani unalazimisha tu kwamba mikopo na ufadhili ni hela nyingi ili tu magufuli aonekane hana maana..

nyie mkae mtulie.. mwanaume yupo kazini. msubiri 2020,
 
Hakuna mwaka ambao wizara zilipata hela ya bajeti kwa asilimia 100, so hata wakisema tutajitegemea asilimia 100, ni namba tu hakuna uhalisia.
 
Deni la Taifa litafikia 54tril hadi mwakani
 
So ni TZS. 45 Trillion halafu zitakopwa 7.5Trillion so deni litakua 52.5Trillion hili deni ni kubwa tatizo la deni la Taifa huathiri vizazi na vizazi.
kweli deni litaongezeka sasa kwa utaalamu wako wewe unashauri nini kifanyike badala ya kukopa hizo trilioni 7?mtaalamu huwa halalamiki tu anaonyesha na mbadala.
 
Tatizo la hizi bajeti unaweza kufurahia figure hapo lakini mwisho wa mwaka wa fedha hela iliyopatikana unakuta hata robo tatu haifiki, kuna Taasisi moja ya Muhimbili walipangiwa 118Biln mpaka jana kamati ya bunge imepita pale hela waliyopata ni 1 Biln Taasisi nyeti kama Afya.
Huo ulikua ni wakati ule uliopita, let's hope for the best, pengine awamu hii itakua tofauti, tuombe Mungu manake mafanikio ndiyo yatakua mkombozi wetu
 
Sasa ivi kilichobaki mueshimiwa ajalibu kufanya mchakato na makampuni makubwa kama Huawei, Toyota, Tecno, Suzuki na makampuni ya kusindika Nyama ya Ng'ombe, ngozi, na Maziwa
Maana Kuna pesa nyingi sana apa Tanzania ajalibu kuongea na Chinese na Japanese. Kuliko kutegemea mataifa ya magharibi yana majungu sana. Wewe upewe msaada kwa kukubali kudhalilishwa alafu bado wanakuwa kukuibia
Hudhalilishwi mkuu ni kuwa unatunga sheria halafu ulitunga sheria xako mwenyewe huzifati kwa ulafi wa madaraka
 
Deni la taifa litaendelea kukua sijui tutapanga kuilipa lini, makusanyo ya trillion 17.8 sidhani kama itafika ila kujitegemea in real sense ni 17.8/29.5 utaona ratio siyo nzuri.Pia tusisahau hakuna bajeti ambayo iliwahi kupatikana kama ilivyopangwa almost bajeti zinazopelekwa sehemu husika inakadiriwa ni 40%.Hakuna haja ya kuweka figure kubwa ambayo itakayopatikana haifiki 20 trillion.
Nimemkumbuka Makongoro mahanga aliposema indicator ya serikali kubwa ni kuongezeka kwa budget ya mwaka unaofuata.Big up
 
Naam maadamu tutaendelea kuongeza mikoa mipya,wilaya mpya,taasisi na idara mpya za serikali matumizi ya kawaida yataendelea kuwa juu ya matumizi ya miradi ya maendeleo.Laiti Magufuli angezifuta baadhi ya taasisi na idara za serikali zisizo na tija,akafuta baadhi ya miradi isiyo na faida, akaondoa mfumo wa mikoa na kuunda mfumo wa kanda kwa kuiunganisha baadhi ya mikoa ingesaidia sana kupunguza matumizi ya kawaida ya serikali kwa kiwango kikubwa na hivyo fedha za matumizi ya miradi ya maendeleo zingeongezeka mara dufu.The current bloated system bleeds the taxpayers money dry, this doesn't bode well for the future of our beloved country.
Si rahisi bajeti ya maendeleo kuizidi bajeti ya kawaida. Nakumbuka kipindi fulani Prof Lipumba alilielezea vizuri hili kwamba bajeti ya matumizi huwa kubwa kwa kuwa ndio inalipa watendaji wote na wawezeshaji wa hayo maendeleo tunayoyakusudia. Kwa hiyo bajeti ya matumizi ikiwa ndogo kuna uwezekano miradi ya maendeleo isifanyike maana haitawezekana kuwalipa waibuaji, watendaji, wafuatiliaji na waendelezaji wa hiyo miradi.
 
Nchi yetu bado sana, inabidi tujenge haraka viwanda walau tuongeze pato, bado makusanyo yetu ni madogo sana, trion 17.8 kwa mwaka ni kidogo hata hatujamfikia dangote trion ambae ambae ana bil 18 usd ,zaidi ya trion 36 . Tufika uwezo wa kukusanya walau trion 2-3 kwa mwezi hao tutakuwa tumeanza kusimama. Lakini sio mbaya hata hii trion 17.8 kwa sababu ndo mwanzo, lakini hatua zaidi zichukuliwe kuongeza mapato.
 
Bajeti ijayo ni trilion 29.5
Tra watakusanya 17.8
Mkopo 7.5
Misaada 3.6

Kwa mwendo huu wa kujitegemea kwa asilimia zaidi ya 80 ni hatua kubwa .....eko Magufuli
Source kamati ya bajeti
Haya ni matarajio siyo hali halisi. Takwimu zinapendeza. Changamoto itakuwa kutimiza hayo malengo. Bila cash cushion kutoka kwa wafadhili ina maana tutakuwa tunatumia kadili tunavyokusanya (cash budget). Kuna hatari ya mfumo kukwama (kuwa bogged down). Matokeo yake mishahara italipwa imechelewa, wazabuni watalipwa wamechelewa, mikopo ya wanafunzi haitatoka wakati inapotakiwa, huduma za jamii zitakwama, n.k. Pamoja na kupambana na wakwepa kodi hofu yangu ni kuwa vyanzo vya kodi (tax base) haitaongezeka katika muda mfupi. Huenda ikapungua. Tumpongeze JPM lakini!!!!!!!!!!!!!
 
Magufuli aja na bajeti ya viwanda ya Sh. trilioni 26
  • NI ukomo wa bajeti ya serikali 2016/ 17, umejikita kwenye viwanda, elimu, afya. Wasomi wataka serikali itafute suluhu na wahisani, waanisha vitu vya msingi vya kutilia mkazo...Ukurasa 12.
WIZARA ya Fedha na Mipango leo inatarajia kuwasilisha mbele ya wabunge wote ukomo wa Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, inayokadiriwa kuwa takribani Sh. trilioni 26.

Coin%20Graph.jpg

Taarifa ambazo Nipashe ilizipata jana kutoka Wizara ya Fedha, ukomo wa bajeti ijayo unakadiriwa kufikia Sh. trilioni 26, huku kipaumbe kikubwa kitakuwa viwanda.

Vipaumbele vingine vitakuwa ni elimu na maji na suala la miundombinu ya umeme na barabara pia vitakuwa jambo la muhimu kwenye bajeti hiyo, lengo likiwa ni kusaidia viwanda viweze kufanya kazi ipasavyo.

“Viwanda vitakavyopewa kipaumbele ni vile vinavyotokana na rasilimali ambazo tunazo kama vile mazao ya kilimo, ngozi, pambana na vitu vingine, lakini kumbuka huwezi kuwa na viwanda bila umeme wa uhakika na rasilimali watu, vyote hivi ni vitu muhimu ambavyo vitaangaliwa kwa makini kwenye bajeti hii inayokuja ili kusaidia msukumo wa viwanda ambayo ndiyo ahadi kubwa ya Rais tangu kwenye kampeni,” kilisema chanzo cha habari kwa gazeti hili.

Bajeti hiyo ambayo itakuwa ya kwanza kwa serikali ya Rais John Magufuli tangu aingie madarakani, inazidi ile ya mwisho ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete iliyokuwa ya Sh. trilioni 22.5, ambalo ni ingezeko la takribani Sh. trilioni nne.

Mbali na bajeti hiyo ya mwisho ya Rais Kikwete ambayo ilijikita zaidi kufanikisha uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, bajeti ya mwaka 2014/15 ilikuwa Sh. trilioni 19.85 na mwaka 2013/14 ilikuwa Sh. trilioni 18.2.

Wakati wa Mkutano wa Bunge uliopita, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, aliwasilisha mwelekeo wa mpango wa maendeo wa mwaka 2016/17, ambao ulionyesha kuwa bajeti ya serikali itakuwa wastani wa Sh. trilioni 23.

Bajeti hiyo inakuja wakati ambapo baadhi ya wahisani wametangaza kukata misaada yao kwenye bajeti ya Tanzania, huku wengine wakiondoa fedha zao kwenye miradi mbalimbali waliyokuwa wakiifadhili kutokana na kutoridhishwa na uchaguzi wa Zanzibar.

Kwenye bajeti ya serikali ya 2014/15 wahisani walitarajiwa kuchangia Sh. trilioni 1.09, lakini wengi walikataa kutoa fedha kutokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.

Marekani imeshatangaza kuifuta Tanzania kwenye nchi wanachama wa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), hivyo nchi kukosa Sh. trilioni 1.03 ilizokuwa ipewe na shirika hilo kusaidia ujenzi wa barabara za pembezoni na kusambaza umeme vijijini.

Umoja wa Ulaya (EU) nao upo kwenye hatihati ya Sh. trilioni 1.56, unaendelea kusubiri hatima ya mazungumzo na hali ya Zanzibar itulie kabisa.

Pia baadhi ya mawaziri wa Uingereza nao wanaishauri serikali yao kumyima Tanzania msaada wa Sh. bilioni 622 kutokana hali ya Zanzibar.

Wizara ya Fedha na Mipango imeshatangaza wahisani 10 kati 14 wanaosaidia bajeti kuu ya serikali kujitoa, ambapo Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Servacius Likwelile, alisema waliobaki ni Benki ya Dunia (WB), Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Dernmark na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB).

Wahisani wengine ambao wamekuwa wakisaidia bajeti kuu ya serikali ni Uingereza, Canada, Finland, Ujerumani, Ireland, Japan, Norway na Sweden.

VIPAUMBELE VYA SERIKALI
Kwenye mkutano wa Bunge uliopita, Dk. Mpango alisema vipaumbele vya serikali kwa mwaka 2016/17 itakuwa ni pamoja na kukamilisha utekelezaji wa miradi inayoendelea ya awamu ya kwanza ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP I) na Mkakati wa Kukuza Uchumi awamu ya pili (Mkukuta II).

Alisema kipaumbele kingine kitakuwa ni uendelezaji wa viwanda vya kuimarisha ukuaji uchumi, utekelezaji wa miradi mikubwa ya kielelezo, kuboresha maeneo wezeshi kwa maendeleo ya viwanda yakiwemo nishati, ardhi, kilimo na miundombinu.

Vipaumbe vingine ni kuendeleza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na maendeleo ya ujuzi maalum ili kuongeza upatikanaji rasilimali watu wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya uchumi wa viwanda, kuendeleza huduma za fedha, biashara na masoko na uendelezaji wa huduma za jamii kama vile elimu, afya na maji.

MATUMIZI YA SERIKALI
Alisema pia matumizi ya serikali yanatarajiwa kupungua kutoka asilimia 23.9 ya pato la taifa mwaka 2015/16 hadi kufikia asilimia 21.5 mwaka 2016/17, kufuatia kukamilika uchaguzi mkuu mwaka jana.

Kupunguza nakisi ya bajeti (ikijumuisha misaada) kutoka asilimia 4.2 mwaka 2015/16 na kuendelea kupungua hadi chini ya asilimia 3 katika kipindi cha muda wa kati.

WACHUMI WANENA
Dk. Wilhelm Ngasamiaku, ambaye ni mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDS), aliliambia Nipashei kuwa, ili bajeti iweze kuwa na tija lazima rasilimali watu iwe moja ya kipaumbele.

Alisema rasiliamali watu ndiyo kila kitu na itaweza kuhakikisha ndoto ya Tanzania ya viwanda inafanikiwa.

Alisema pia kwamba, viwanda hivyo vinatakiwa kuwa vile vinavyogusa rasilimali zilizo ndani ya nchi na pia miundombinu ya umeme na barabara iangaliwe ili kufanya viwanda hivyo vifanye kazi na siyo kuwa mzigo kwa taifa.
Naye Mhadhiri na Mtafiti wa Masuala ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Haji Semboja, alisema kuwa bajeti itengenezwe kulingana na kiwango cha fedha kilichopo.

“Unashona suti kulingana na kitambaa ulichonacho, hivyo kama fedha ipo ndogo tutegemee bajeti ndogo,” alisema na kuongeza:

“Lakini kuna njia mbili inategemea Wamerekani walitoa fedha kwa ajili ya matumizi gani, kama fedha hizo zilikuwa zinatolewa kwenye bajeti ni za maendeleo na inajulikana zilikuwa zinakwenda kwenye maeneo muhimu.”

Alisema kutokana na suala hilo anaishauri serikali kutafuta utaratibu wa kukopa kwenye taasisi za fedha za ndani ama za nje ya nchi zenye riba nafuu ili kuendeleza miradi hiyo bila kusimama.

Aidha, alisema katika mtazamo wa pili ni kwamba kusitishwa kwa msaada huo wa fedha hakujaelezwa ni adhabu ya kudumu au la, jambo la msingi ni serikali kujiuliza ilipokosea mpaka wameamua kusitishiwa msaada huo.

“Serikali inatakiwa kujiuliza ilipokosea mpaka wenzetu wakatukosesha fedha hizo, tunaweza kuzungumza na wenzetu katika hali ya kibinadamu kwani suala la misaada linatoka kwa watu wanakatwa kodi zao kutoka Marekani ambao ni wafanyakazi wa kawaida na wengine ni masikini na fedha hizo zinaletwa kufanya shughuli za maendeleo,” alisema.

Hata hivyo, alisema haamini kama Wamarekani wapo tayari kuwaadhibu masikini kwa ajili ya mfumo wa kiurasimu wa serikali ya Kitanzania ambao wanaususia.

Alisema suala la vipaumbele tayari vimeorodheshwa, hivyo haviwezi kupata usumbufu na kukosekana kwa fedha hizo.
Prof. Semboja alisema vipaumbele vya serikali havijabadilika ni vile vile ikiwamo afya, barabara, elimu miundombinu na maji, vingine vitakavyopatikana ni vile vilivyopo katika sekta zote za maendeleo.

Mchumi na Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Donath Ulomi, alisema vipaumbele anavyoviona kulingana na hali ya nchi ilivyo vinavyohitaji kuwekezwa katika maeneo ambayo yatafanya nchi iondoe matatizo ya msingi yaliyopo ni pamoja na upatikanaji wa fedha.

“Tatizo moja wapo ni upatikanaji wa fedha kwa sababu unapozungumzia bajeti sio pesa pekee, bali ni programu ya kazi ya mwaka wa serikali inayotakiwa kuainisha ni jinsi gani itasimamia vyanzo vya mapato sambamba na kutafuta vyanzo vipya,” alisema.

“Ili bajeti ijitosheleze bila kutegemea wafadhili ni lazima serikali ikubali kuwa chanzo kimojawapo cha kuchangia pato la taifa ni kodi ya majengo ambalo ni eneo halijafanya vizuri. Majengo mengi Dar es Salaam hayajafanyiwa tathmini hivyo serikali ikiamua kufanyia kazi eneo hilo itaongeza mapato,” alisema.

Pia alitaja eneo jingine ni umiliki wa ardhi ambayo sehemu kubwa haijapimwa na hata ile iliyopimwa hakuna motisha ya upatikanaji wa hati.

“Eneo la tatu ni la ukusanyaji wa kodi na jingine ni lazima tuboreshe utendaji hasa katika sekta ya umma, sasa tunaona majipu yanatumbuliwa lakini ukiingia katika taasisi na wizara hata sekta binafsi ukiangalia mpangilio wa kazi wa majukumu, ufuatiliaji na uwajibishaji kwa ngazi zote upo dhaifu,” alisema na kuongeza:

“Matokeo yake mfumo wa usimamiaji wa watumishi wa uwajibishaji na uwajibikaji kama sio imara utajikuta unalipa gharama kubwa sana, gharama za watumishi wa serikali ni karibu nusu ya pato la taifa, karibu nusu ya kodi inaenda kulipa watumishi, kwa hiyo kama huwasimamii vilivyo inaleta tatizo kubwa kwenye uchumi,” alisema.

Dk. Ulomi alitaja eneo jingine linalohitaji kushughulikiwa kuwa ni elimu, ambayo inatakiwa iboreshwe kuanzia shule za chini, za sekondari hadi vyuoni kwa sababu bado ni janga linaloumiza kiutendaji.

Pia alisema sekta ya kilimo inahitaji nguvu ya uwekezaji katika kilimo cha umwagiliaji badala ya kile kinachotegemea mvua ili kuchangia pato la taifa.
 
Bajeti ya Mwaka 2016/17 ni fedha za kitanzania trilioni 29.5

Katika bajeti hiyo fedha za ndani ambazo zitakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ni fedha za kitanzania shilingi trilioni 17.8 trilioni.

Mikopo ya kibiashara itakayochukuliwa na serikali kwa ajili ya Bajeti kuu ni shilingi trilioni 7.5

Misaada ya wafadhili ni shilingi trilioni 3.6.

Matumizi ya kawaida ni shilingi trilioni 17

Matumizi ya Maendeleo 11.8 trilioni.
Kama tutafanikiwa kuwa na bajeti isiyotegemea misaada kwa asilimia 80 kama inavyokisiwa itakuwa mafanikio kwa taifa na funzo kwa nchi za kiafrika na zaidi sana mshangao kwa nchi wahisani.Pamoja na kuafiki mwelekeo huo naona uwezekano wa kufanikiwa zaidi iwapo sisi watanzania hatutaendelea na kasi tuliyonayo ya kuzaana.Bajeti hii itakuwa na maana pale ongezeko la watanzania kwa mwaka litadhibitiwa.Hongera JPM na serikali ya awamu ya tano kwa kuthubutu.
 
what do you care about vizazi man? hapa ni kuji take care wewe na familia yako, ukiwa unaangalia mambo ya vizazi vijavyo hapa Afrika utaishia kuumiza kichwa bure ukakosa hata raha
Mimi siongei kimbea kama wakina mama wa mtaani kwenu naongea ki Public Economics/ Public Finance zaidi mwalimu wa Kiswahili na Historia ni Vigumu kuelewa madhara ya Public Finance na sifa ya Uongozi ni kuangalia na vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom