Dondoo za Bajeti 2016/2017, kujitegemea kwa asilimia zaidi ya 80

Dondoo za Bajeti 2016/2017, kujitegemea kwa asilimia zaidi ya 80

KODI YA BIDHAA NA HUDUMA INASHUKA KWA ASILIMIA NGAPI?! MASHIRIKA YANAYOTOA HUDUMA KAMA MAJI, UMEME NA AFYA YATASHUSHA KODI KWA ASILIMIA NGAPI?! MADINI KAMA DHAHABU, ALMASI, TANZANITE, BATI, MAKAA YA MAWE, CHUMA, ULANGA, NK, MAPATO YAKE YATAPANDA KWA KIWANGO GANI?! GESI YA ASILI MAPATO YAKE YANAPANDA KWA KIWANGO GANI?! UTALII: MBUGA ZA WANYAMA, MILIMA KAMA KILIMANJARO, NK, MAPATO YAKE YATAPANDA KWA KIWANGO GANI?! POROJO HATUTAKI.!
Kila kitu kitapanda ili kupata above 17trillion, naona umepanic sana, wewe ndio unaleta porojo
 
hivi wamezungunzia performance ya bajeti iliyopita?
Ama tunaweza ikuta wapi tuisome panawezakanika kufuatilia kama ni kweli tufanye hivyo. Maana hii nchi bana inapaswa kuendeshwa kama kampuni ndio tutafika. Tupime kila tunachotarajia kama kimewezekana kwa kiwango gani. Tukishindwa tujue vikwazo ni vipi na nani hatimizi wajibu wake ipasavyo.
 
hahahhahah asije vurugikiwa kichwa. sawa mkuu hili agizo atazingatia.
Kwa sababu hujui tofauti ya Matumizi ya Maendeleo na ya kawaida. Usitafsiri maneno ya kiuchumi kwa kutumia kiswahili cha mitaani utavurugikiwa kichwa![/QUOTE
 
Bajeti ya Mwaka 2016/17 ni fedha za kitanzania trilioni 29.5

Katika bajeti hiyo fedha za ndani ambazo zitakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) ni fedha za kitanzania shilingi trilioni 17.8 trilioni.

Mikopo ya kibiashara itakayochukuliwa na serikali kwa ajili ya Bajeti kuu ni shilingi trilioni 7.5

Misaada ya wafadhili ni shilingi trilioni 3.6.

Matumizi ya kawaida ni shilingi trilioni 17

Matumizi ya Maendeleo 11.8 trilioni.

========================
Misaada ya wafadhili waiondoe kabisa!!!!
 
Kiini macho.... serikali iliyo pita mpaka mwaka wa fedha unaisha bajeti imeenda 20%..... ngoja tuone serikali hii itakuwaje... siwezi amini mpaka mwisho wa mwaka huu. ..
 
Akili ndogo sana hii budget ni sawa na Trillion 9 tuu Shilling ilivyokua imara kwa exchange rate ya 650.
Kuna msemo maarufu, CCM wanapenda number lakini hawazijui. Suala rahisi tu kujiuliza mwaka jana wakati kama huu exchange rate ilikuwa ngapi? Watagunduwa kuwa bajeti ya mwaka jana ilikuwa kubwa kuliko ya mwaka huu. Kuwaelimisha hawa jamaa itachukuwa karne nzima
 
12986945_222765471421731_1982928611565962961_n.jpg


matumizi ya kawaida 2015/2016
yalikuwa 7.9 trl
iwaje 2016/17 yapande mpaka 17 trl.
 
Back
Top Bottom