Dogo katolewa chumba cha mtihani na Mkuu wa Shule

Dogo katolewa chumba cha mtihani na Mkuu wa Shule

Na kwa nini awe mtoro? Huo mtihani anaufanyaje mtu ambaye ni mtoro? Hiyo dawa aliyoichukua Mkuu wa shule ndiyo nzuri! Ni kumtimua moja kwa moja akachekee kijiji cha Mtakanini!
Utoro ni sababu ya kumzuia mwanafunzi kufanya mtihani aliyesajiliwa tayari ?
 
Lete ushahidi, ukiacha ile ya Bukoba ya shule ya Kiislam ambayo bado ilikuwa kwenye upelelezi. Unajua jinai wewe. Kafanye fujo kituo Cha mtihani uone km utafanya pepa.
Nenda Bariadi pale manispaa waulize nenda wilaya ya Serengeti kaulize pia case 2 mbili zipo tarime. Kuna Ile ya mwaka Jana aliemuua Baba yake ipo ruvuma
 
Kwa vyovyote vile kosa liko kwa mkuu wa shule hiyo. Tuseme mwanafunzi alikuwa na mwenendo mbaya, kwa nini hakuchukua hatua mapema ikiwemo kumjulisha mzazi wake, kumwadhibu kwa suspension kwani arudipo huja na mzazi, kumpeleka mbele ya kamati ya shule nk? Kwa nini asubiri kwenye mtihani ndipo amfukuze?
Unabwabwaja tu. Natamani siku moja ungepewa mwezi mmoja tu kuwa mkuu wa shule ili uone magumu yake.

Unampa mtoto barua anachana. Ukipiga simu hapatikani. Tangu alete mtoto hajawahi kugusa tena shuleni.

Hatumi pesa ya matumizi kwa mtoto wala kuulizia tatizo. Mbaya zaidi ni mtu kambi popote.
 
Wanafunzi kibao wamefanyia pepa mahabusu wengine Hadi Kwa Kesi ya uuaji je wajua Hilo. ukishasajiliwa kupiga pepa ni asilimia kubwa
Pawe na taarifa za mapema. Mfano inafahamika kesi itaenda hadi tarehe za mitihani.
 
Mzazi alipoenda shule kuulizia akaambiwa mwanao alikua mtoro, lakini mama akasema tangu lini na madaftari ya mahudhurio yanaonyesha yupo shule na alikua anaishi bwenini? Lakini kwa maelezo ya dogo anasema alikuwa anaambiwa na Mkuu huyo wa shule kuwa asijisumbue kusoma kwa sababu hataruhusu amalize kwenye shule hiyo.[emoji3064]
Unategemea dogo ataeleza ukweli?
 
Kusajiliwa siyo tatizo,huwa wanasajiliwa around February.....inawezekana hakuwa anahudhuria shule kweli au kuna lingine
Nijuavyo mimi kila mkuu wa shule anawajibu kuhakikisha wanafunzi wote waliosajiliwa wanafanya mitihani. Iweje kama hakuna shida, mkuu amwondoe dogo?

Dogo kampanga mzazi tu, hapo kuna jambo kubwa. Tusubiri tuone.
 
Ili kumsaidia mdogo wako, nenda kwa afisa elimu mkoa , ilipo shule na mweleze shida hiyo. Pia unaweza kuwasiliana na mkurugenzi wa elimu( sekondari) wizara ya elimu na kuwasilisha mashtaka yako hapo. Ni vema ukipata msaada wa wanasheria huru kukusaidia, kama wale wanaojihusisha na haki za watoto. Shinikizo za kisiasa zisiue ndoto za mdogo wako. Msaidie.
Unanunua bunduki kuua panya. Tumia akili kidogo tu. Anzia na Afisaelimu Kata. Kesi itaenda hadi mahali panapofaa.

Hakuna asiyeogopa issue ya mtihani wa taifa. Ni miongoni mwa vitu hatari sana kwa mtumishi wa idara ya elimu.

Mkuu wa shule mwenyewe kama kweli alifanya hivyo, alishapata ushauri ngazi za juu yake. Asingeweza kuchukua hatua kubwa kama hiyo bila kuchukua tahadhari na kushikilia kanuni na sheria husika.

Narudia, mkuu wa shule amejiridhisha na hatua akizochukua pasi na shaka kuwa yuko sahihi na salama.
 
Unabwabwaja tu. Natamani siku moja ungepewa mwezi mmoja tu kuwa mkuu wa shule ili uone magumu yake.

Unampa mtoto barua anachana. Ukipiga simu hapatikani. Tangu alete mtoto hajawahi kugusa tena shuleni.

Hatumi pesa ya matumizi kwa mtoto wala kuulizia tatizo. Mbaya zaidi ni mtu kambi popote.
Wewe ndio unabwabwaja na hujui uongozi ni nini. Ni heri ubaki kula mihogo tu. Jifunze kwanza maana ya uongozi na mamlaka yake ndio uje kukomenti.
 
Akili kisoda sibishani nayo
Wewe hata akili unayo basi? You're a fool. Hujui hata mamlaka aliyonayo Mwalimu kwa mwanafunzi na mzazi. Kwa akili yako ndogo unadhani mwalimu hana powers za kutumia vyombo vingine kumwajibisha mzazi? Hiyo kamati ya shule ni ya mapambo? Iweje mwalimu asubiri wakati wa kufanya mtihani ndipo amfukuze mwanafunzi? Afu unaleta vijisababu vyo hovyo ukijihesabu mwenye akili? Eti labda alikuwa hahudhurii darasani, kwani utoro unashughulikiwa vipi kwa mujibu wa taratibu za elimu? Kwamba akitoroka aachwe tu iia akitokea kwenye mtihani afukuzwe? Mbona unataka kuharibu mfumo wa elimu?

Think
 
Unauliza na kujijibu mwenyewe.

Majibu rahisi ni kuwa mkuu wa shule alishachukua hatua ndiyo maana akasema kabla kuwa hatafanya mtihani.

Kwa akili yako unadhani mkuu alikurupuka?
 
Ndiyo, kwa mfano alisajiliwa na hakuhudhuria shule zaidi ya siku 90. Anakuwa amejifuta shule hata kama alisajiliwa kufanya mtihani.

Huyu siku ya mtihani hataruhusiwa
Muongozo huu unaweza kuambatanisha mkuu ?
 
Back
Top Bottom