Dogo katolewa chumba cha mtihani na Mkuu wa Shule

Gwaya Hk

Member
Joined
Sep 17, 2018
Posts
45
Reaction score
29
Brothers and sisters naombeni msaada, nini kifanyike au wapi naweza kupata haki?

Mdogo wangu alikua anasoma Form Two mwaka huu 2022 shule ya kata, lakini juzi kipindi wanaanza kufanya mitihani akiwa chumba cha mtihani Mkuu wa Shule alimfata na kumwambia atoke nje, alipotoka Mkuu wa Shule alimpa barua arudi nyumbani na kumwambia hastahili kufanya mitihani kwa sababu ataongeza zero katika shule yake!

Mzazi alipoenda shule kuulizia akaambiwa mwanao alikua mtoro, lakini mama akasema tangu lini na madaftari ya mahudhurio yanaonyesha yupo shule na alikua anaishi bwenini? Lakini kwa maelezo ya dogo anasema alikuwa anaambiwa na Mkuu huyo wa shule kuwa asijisumbue kusoma kwa sababu hataruhusu amalize kwenye shule hiyo.

Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kututhibitishia kuwa dogo hakuwa mtoro? Bila shaka mlimpa kichwa na kiburi kuwa we nenda kafanye pepa .

Tuachane na hayo mtihani alio kuwa ameanza kufanya ulikusanywa au uliharibiwa? Hapo awali hakuwa na barua yoyote ya kinidhamu? Ukijibu kwa usahihi utaoata msaada mkubwa hapa jf. Kila la kheri
 
Brothers and sisters Naombeni msaada Nini kifanyike au wapi naweza kupata haki! Mdogo wangu alikua anasoma Form Two mwaka huu 2022 shule ya kata. lakini Juzi kipindi wanaanza Kufanya mitihani akiwa chumba Cha mtihani mkuu wa shule alimfata na kumwambia atoke nje, alipotoka mkuu wa shule alimpa barua arudi nyumbani na kumwambia hastahili Kufanya mitihani kwa sababu ataongeza zero katika shule yake! Mzazi alipoenda shule kuulizia akaambiwa mwanao alikua mtoro lakini mama akasema tangu lini na madaftari ya mahudhurio yanaonyesha yupo shule na alikua anaishi bwenini.
Lakini kwa maelezo ya dogo anasema alikua anaambiwa na mkuu hyo wa shule kuwa asijisumbue kusoma kwa Sababu hataruhusu amalize kwenye shule hyo.

Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kututhibitishia kuwa dogo hakuwa mtoro? Bila shaka mlimpa kichwa na kiburi kuwa we nenda kafanye pepa .

Tuachane na hayo mtihani alio kuwa ameanza kufanya ulikusanywa au uliharibiwa? Hapo awali hakuwa na barua yoyote ya kinidhamu? Ukijibu kwa usahihi utaoata msaada mkubwa hapa jf. Kila la kheri
Kwani mtoto anapokuwa mtoro haruhusiwi kufanya mitihani kama kasajiliwa ?
 
Unaweza kututhibitishia kuwa dogo hakuwa mtoro? Bila shaka mlimpa kichwa na kiburi kuwa we nenda kafanye pepa .

Tuachane na hayo mtihani alio kuwa ameanza kufanya ulikusanywa au uliharibiwa? Hapo awali hakuwa na barua yoyote ya kinidhamu? Ukijibu kwa usahihi utaoata msaada mkubwa hapa jf. Kila la kheri
Baada ya kufatilia kwa kina inaonekana ashawahi kuwa mtoro miezi ya nyuma yaani mwezi wa tano hivi Kama sikosei hakwenda shule Kama wiki 2 hvi lakini mother alipogundua alilifix na kumuhamishia hostel tangu hapo aliishi bwenini mpaka siku ya mtihani lakini pia hakuwai kupewa barua yoyote ya onyo baada ya hapo.

Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
 
Brothers and sisters naombeni msaada, nini kifanyike au wapi naweza kupata haki?

Mdogo wangu alikua anasoma Form Two mwaka huu 2022 shule ya kata, lakini juzi kipindi wanaanza kufanya mitihani akiwa chumba cha mtihani Mkuu wa Shule alimfata na kumwambia atoke nje, alipotoka Mkuu wa Shule alimpa barua arudi nyumbani na kumwambia hastahili kufanya mitihani kwa sababu ataongeza zero katika shule yake!

Mzazi alipoenda shule kuulizia akaambiwa mwanao alikua mtoro, lakini mama akasema tangu lini na madaftari ya mahudhurio yanaonyesha yupo shule na alikua anaishi bwenini? Lakini kwa maelezo ya dogo anasema alikuwa anaambiwa na Mkuu huyo wa shule kuwa asijisumbue kusoma kwa sababu hataruhusu amalize kwenye shule hiyo.

Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
Shida iliyopo ni kuwa wazazi/walezi tupo mbali sana na walimu!!! Iaonekana kulikuwa na changamoto muda mrefu. Fuatilieni na myajenge
 
No, no, no, no, big NO.
Kwanza mkuu wa Shule haruhusiwi kabisa kuingia/ kusogelea chumba Cha mtihani, labda kuwe na critical issue. Huo ndo muongozo wa Baraza la mitihani Tanzania.

Kwanza afadhali umesema mapema kuwa ni shule ya kata. Wazazi wengi wa mazingira hayo hawajali Elimu ya watoto kabisa, na watoto wanatumia mwanya huo kuwa wakaidi ktk masomo.

Wazazi wengi wa mazingira hayo wamekuwa busy na masuala ya kiuchumi km kilimo, ufugaji, na uuzaji wa pombe za kienyeji. Hawana muda wa kufanya follow up juu ya mahudhurio ya watoto wao shuleni Wala kupitia daftari zao.

Umesema alikuwa boarding, ok, nani alikuambia boarding hakuna utoro. Unajua maana ya utoto? Wangapi miongoni mwetu wakati wengine wanaenda darasani tulibakia bwenini, hapo hujui Mwalimu wa darasa akiingia kuita majina utaitwa mtoro maana haupo darasani.

Muongozo wa Elimu uko wazi kuwa iwapo mwanafumzi atashindwa kuhudhuria shule mfululizo (consecutively) kwa siku 90 basi haesabiki km mwanafunzi tena. Kwa lugha nyingine atafutwa shule, hata uhamisho hapewi, ingawa hadi kumfukuza kuna hatua huwa zinafuatwa km kuita bodi ya shule nk. Hafutwi kiholela hata km ni private school.

Unasema alikuwa na daftari zimeandikwa. Kuwa na daftari zilizoandikwa sio kigezo. Wangapi kati yetu tulikuwa tunashinda vichakani au kubaki bwenini na wenzetu wanapomaliza vipindi saa 8 tulikuwa tunaomba darftari zao na kunakili hadi nukuta. Je huyo akikuonesha daftari utajua haingii darasani. Mwalimu wa darasa huita Majina darasani na anaowakuta ndio huesabika wamefika Shule siku hiyo. Unafikiri Shule ni danguro, kuwa mtoa huduma atamfuata Mteja alipo. Kwa maana Mwalimu akaite majina bwenini, au vichakani walikojificha. Km akiwa anaumwa na yuko boarding wenzie watatoa taarifa kwa Mwalimu na hatua zitachukuliwa maana shule sio wodi ya kulaza au kukaa na wagonjwa.

Ushauri, nendeni shule mtapewa si tu maelezo ya kina bali uthibitisho wa utoro wake kwa kuangalia daftari la mahudhurio ya darasani (class attendance) kwa kurejea maneno yangu hapo juu ( siku 90 consecutively).

Mwisho, tuwaheshimu walimu wetu maana walitutoa ujinga hadi leo naandika hapa hadi kuweka lugha ya malikia kwa sababu Yao. Respect to all teachers in the world, I personally appreciate your presence.
 
Sure but hakuwa mtoro wa kufikia siku 90 hii Ni baada ya Kufanya follow up kwenye madaftari ya mahudhurio lakini pia ishu Ni halali kutolewa chumba Cha mtihani na Kama sio anapata haki yake ya kuendelea na shule. Ovaa!
 
Mtoto hawezi kufanya mitihani kama hakusajiliwa tu.

Utoro hauwezi kumzuia kufanya mitihani.
Usipoteshe uma wewe. Nyie ndio wazazi mnaokimbilia kulalamika mitandaoni bila kujua mlifanyalo. Kwa nini unaongea kitu usichokijua? Au unatafuta kuchochea moto kwa alieleta mada ili aumbuke zaidi.

Yani unasema kabisa kinaga ubaga kuwa mtoto akisha sajiliwa ndo basi lazima afanye mtihani. Hivi unazijua taratibu za Baraza pamoja na miongozo mbalimbali ya Elimu Tanzania? Pia Unajua kuwa shuleni Kuna sheria na taratibu?

Ebu ngoja nikuulize
1) Mfano mtoto wa kike kapata ujauzito wakati keshasajiliwa na shule ikabaini na kadi ya clinic akaileta. Hapo vipi.
2) Mwanafunzi akamshushia kipigo Mwalimu tena siku ya mtihani kwa sababu yoyote Ile, iwe bangi tu za Mwanafunzi zimemsukuma kufanya hivyo au vyovyote. Kwa mfano, ilivyotokea kwa huyo dogo km angemdindia mkuu na wakazichapa. Hapo vipi.
3) Kabla au mtihani ukiwa unaendelea, Mwanafunzi kwa makusudi akaharibu mali za shule, kuchoma jengo, kuharibu samani nk. Hapo vipi.
4) Ukiwa mtihani unaendelea mwanafunzi akafumaniwa na mke/ mume wa mtu na kupelekwa kituo Cha police. Utampelekea Pepa police na msimamizi. Au hapo vip.
5) Mwanafunzi akifanya fujo shuleni zinazoweza kupelekea uvunjifu wa amani shuleni wakati mtihani unaendelea. Hapo vipi. Tena kwa sekondari kumbuka Kuna kuwa na police kulinda usalama.

Matukio ya kumfukuza Mwanafunzi hata km ameshasajiliwa ni mengi. Muhimu tu inategemeana na busara za shule (bodi ya shule, walimu na mkuu wao). Ila hayo niliyotaja na mengine yenye kufanana na hayo hayana excuse.

Umewahi kujiuliza kwa nini siku hizi sherehe shule za serikali hasa sekondari mahafali ( graduation) hufanyika kabla ya mtihani. Wakati zamani ilikuwa hata baada ya mtihani. Ukipata jibu, basi utakuwa umenielewa.
 
Brothers and sisters naombeni msaada, nini kifanyike au wapi naweza kupata haki?

Mdogo wangu alikua anasoma Form Two mwaka huu 2022 shule ya kata, lakini juzi kipindi wanaanza kufanya mitihani akiwa chumba cha mtihani Mkuu wa Shule alimfata na kumwambia atoke nje, alipotoka Mkuu wa Shule alimpa barua arudi nyumbani na kumwambia hastahili kufanya mitihani kwa sababu ataongeza zero katika shule yake!

Mzazi alipoenda shule kuulizia akaambiwa mwanao alikua mtoro, lakini mama akasema tangu lini na madaftari ya mahudhurio yanaonyesha yupo shule na alikua anaishi bwenini? Lakini kwa maelezo ya dogo anasema alikuwa anaambiwa na Mkuu huyo wa shule kuwa asijisumbue kusoma kwa sababu hataruhusu amalize kwenye shule hiyo.

Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
Eleza ukweli, umeleta umbea umeacha habari kamili.

Mkuu wa shule hawezi kuwa na kisasi na form two.

Wala si kichaa amtoe mtahiniwa darasani.

Lete habari kamili na kama hufahamu usidandie habari.
 
Back
Top Bottom