YESU NDIYE MUNGU ALIYEZIUMBA MBINGU NA NCHI:
Yohana 1:1, 14 – “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu... Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu.”
2. Yohana 20:28 – Mtume Tomaso alipomwona Yesu baada ya kufufuka alisema: “Bwana wangu na Mungu wangu!” Yesu hakumkemea bali alikubali sifa hiyo.
3. Wakolosai 2:9 – “Kwa maana ndani yake unakaa utimilifu wote wa Mungu kwa mwili.”
4. Isaya 9:6 – Nabii alitabiri kumhusu: “Na jina lake litaitwa... Mungu Mkuu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.”
5. Ufunuo 1:8 – Yesu anasema: “Mimi ni Alfa na Omega... Mwenyezi.”
UMEANDIKA
YESU NDIYE MUNGU ALIYEZIUMBA MBINGU NA NCHI:
MAJIBU
YESU HAJAUMBA CHOCHOTE HATA MBU HAJAUMBA
Yesu ananukuliwa katika Yohana 5:30, akisema:
“Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.”.
Katika Matendo 2:22, Paulo anandika:
“Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua.”
umeandika
Yohana 1:1, 14 – “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu... Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu.”
MAJIBU
Huenda ‘ushahidi’ wa uungu wa Yesu ulionukuliwa sana ni Yohana 1:1 na 14, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, na Neno alikuwa Mungu… Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.”
Hata hivyo, maelezo haya hayakutolewa na Yesu Kristo, wala hayakuhusishwa naye na mtunzi wa Injili kwa mujibu wa Yohana.
Hivyo, mistari hii haiundi ushahidi wa uungu wa Yesu, hasa hasa kuzingatia shaka inayoshikiliwa na wasomi wa Kikristo juu ya Injili ya Nne.
Wasomi wa Biblia waliotunga Injili tano: “Picha mbili zilizochorwa na Yohana na muhtasari wa injili (yaani Injili ya Mathayo, Marko na Luka) zote mbili haziwezi kuwa ubainifu wa kihistoria.
Neno lilohusishwa na Yesu katika Injili ya Yohana kimsingi inatofautiana na Injili nyingine tatu (Injili za muhtasari) kiasi cha kutilia shaka uhakika wake. Kwa mfano:
Nne limeundwa na wainjilisti kwa sehemu kubwa, na linaakisi mwendelezo wa lugha ya jamii ya Wakristo wa Kiyohana.
Neno la Kigiriki lilotumiwa na mtunzi wa Injili ya Nne asiyejulikana kwa “neno” ni logos. Kwa kufanya hivyo, huyo mtunzi anamtambulisha Yesu kwa logos la wanafalsa wapagani wa Kigiriki, neno ambalo lilikuwa na lengo takatifu na thabiti lililojitokeza ulimwenguni, huyo mtunzi akalipangilia neno hilo na kulipa mfumo na maana.
Wazo la logos katika fikra za Kigiriki huenda linarejea nyuma, kwa uchache hadi kwa mwanafalsafa wa karne ya sita BC, Heracleitus, aliyependekeza kuwa, kulikuwa na logos ulimwenguni anayetenda kwa mwanadamu kulingana na nguvu ya hoja. Baadaye, Stoics analitambulisha logos kuwa ni tendo, mantiki, na kanuni ya kiroho inayosambaa katika ukweli wote.
Mwanafalsafa wa Kiyahudi anayeongea Kigiriki, Judaeus Philo wa Alexandria (15 BC -45 CE), amefundisha kuwa logos alikuwa ni mpatanishi baina ya Mungu na ulimwengu, kwa kuwa na sifa mbili za uwakala wa Mungu na ulimwengu, na kuwa na sifa mbili za uwakala wa viumbe na wakala wa ambaye kupitia kwake akili ya mwanadamu inaweza kumfahamu Mungu.
Maandiko ya Philo yalihifadhiwa na kutunzwa na kanisa, na kueneza ufunuo kwa mafundisho ya kistaarabu ya tiolojia ya kifalsafa ya Kikristo. Aliacha mafundisho ya fikra za Kipilato wakichukulia logos (Neno) na kuliita “mtoto wa kwanza wa kuzaliwa na Mungu.”
Utambulisho wa Yesu kwa logos, uliendelezwa katika kanisa la kwanza ikiwa ni tokeo la majaribio yaliyofanywa na wanatiolojia wa kwanza wa Kikristo pamoja na watetezi kuielezea imani ya Kikristo kwa istilahi ambayo ingekuwa wazi kwa ulimwengu wa Wayunani.
Zaidi ya hayo, ilikuwa ni kuwavutia wasikilizaji wao na mtazamo wao kuwa Ukristo ulikuwa unashinda, au mrithi wa wale wote waliokuwa wanafalsafa bora wa kipagani. Kwa hiyo, katika kazi zao za utetezi na Wingi wake ni logoi nalo pia linamaanisha “hoja” au “mpango”.
Mapadri wa Kikristo wa kwanza wameeleza kuwa Yesu alikuwa ni logos aliyekuwepo hapo kabla.
Neno la Kigiriki lililotumika kwa maana ya ‘Mungu’ katika hiyo ibara ni “na Neno lilikuwa kwa Mungu,” lipo katika mtindo wa “definite form- yaani mtindo uliowazi, au unaofahamika” batheos, Linalomaanisha “Huyo Mungu, au Mungu maalum”.
Hata hivyo, katika ibara ya pili “na Neno alikuwa Mungu”, neno la Kigiriki lililotumika kwa maana ya ‘Mungu’ katika ibara lipo katika mtindo wa “indefinite form- yaani mtindo usiowazi, au usiofahamika” tontheos, Linalomaanisha ‘mungu yoyote, yaani mungu asiyejulikana, au mungu yoyote asiye maalumu’.
Kwa hiyo, Yohana 1:1, kwa uwazi zaidi ilipaswa itafsiriwe, “Hapo Mwanzo kulikuwa na Neno, na hilo Neno lilikuwa kwa Mungu, na hilo Neno lilikuwa mungu mwingine.”
Kwa hiyo, kama hilo neno lilikuwa mungu mwingine kwa ufahamu wa kifasihi, itamaanisha kuwa kulikuwa na miungu miwili na sio mmoja. Hata hivyo, katika lugha ya Kibiblia, neno ‘mungu – asiyefahamika’ linatumika kwa maana ya istiari ili kuashiria nguvu.
Kwa mfano, Paulo alimtaja shetani kuwa ni ‘mungu – asiyefahamika’ katika 2 Wakorintho 4:4, "ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu."
Pia, Musa alitajwa kama ni ‘mungu – asiyefahamika’ katika Kutoka 7:1, "BWANA akamwambia Musa, Angalia, nimekufanya wewe kuwa Mungu kwa Farao; na huyo ndugu yako Haruna atakuwa nabii wako.