Dodoso: Tatizo la Tanzania sio CCM

Dodoso: Tatizo la Tanzania sio CCM

Mimi naona tatizo kubwa ni kukosa watu wenye akili zinazofikiri kisawa sawa. Nasema kwamba tungekuwa na watu wenye akili tusingekuwa waoga namna hii. Huu woga ni dalili moja tu ya ukosefu wa akili.
Tanzania hii kila mtu analenga maslahi yake mtakuea pamoja mwanzoni mwa harakati akipata anachotaka anasaliti Kambi.
Katika mazingira haya huwezi pata mabadikiko sababu hakuna common agenda.
Hasa kizazi hiki ndio kibaya zaidi yaani chawa ni tabu kabisa, unaona kabisa mtu anapambania apate kitu na si alete mabadikiko.
Naamini kitakacjotutoa hapa tulipo ni kuwa na demokrasia imara ambayo sinlazima ifanani na ya marekani au Uingereza ila Ile ambayo itawezesha maonoli ya watu yaheshimiwe.
Hofu yangu hatuwezi kupata demokrasia imara kwani historia ya nchi yetu pia inaonesha tuliingia vyama vingi kishingo upande ili kuwaridhisha wakubwa wasitutenge. Hapa ndipo CCM wanapambana toka enzi na enzi sababu hawakukubali kihiari kuingia kwenye vyama vingi.
Watu wetu pia wameziea shida hawaoni kama Kuna Maisha zaidi ya haya ni namna gani mtu huyu atatamani kubadili mambo?
Tunahitaji watu wa kuwafungua watu wetu na kuwaonesha kuwa tunaweza kuishi maisha Bora kabisa ya hadhi ya binadamu na hapo ndipo tutaweza kubadili Hali kwani itakuwa rahisi kupata kuungwa mkono kea wingi.
Hivyo elimu ya kuzindua watu ni muhimu saana, itolewe bila kuchoka.
Pilato aliwasha taa mchana kuwazindua watu bado kazi inapaswa kuendele bila kuchoka.
 
Vyama na katiba vyote vinatengenezwa na watu,kwa Katiba hii hii mbovu kuna mambo mengi yanafanyika yasiyoendana na Katiba ni action gani tulichukua?
Tatizo kubwa la Watanzania ni yoga unaoyokana na ujinga,halafu hii ni kwa wote waliosoma na ambao hawajasoma.
Hakika mkuu hili ni tatizo tulilo nalo kuendelea kulikataa kuwa hatuna au halipo , hii hari hupelekea sisi kuendelea kulipalilia hili lizidi kumea zaidi.
 
Tatizo la uoga katika hii Nchi alilitengeneza Nyerere ili aubudiwe,katika jamii ambayo ilikiluwa imejaa wajinga wengi Nyerere alitumia mwanya huo huo kujenga misingi mibovu ya watu kutohoji.

By the way kwa sasa hayupo na watu angalau asilimia Fulani wameelimika lakini tatizo bado ni kubwa sana.
Kweli kabisa.
 
Sikubaliani na weye mkuu.Tatizo si UOGA.Tatizo ni MUDA.Ndiyo.Do not force a button!Waache Watanzania kwanza waipokee hali.Halafu waache waiishi hali.Na ndiyo walipofikia.Wanaiishi hali.Basi,uwaache hadi wapate kifu/waikinai hali hii wanayoiishi.Utafika tu muda na watapanga kuchagua moja.Kwamba,waendelee na hali hii waliyonayo au waikatae na kufanya maamuzi.Mto wanauona.Ni khiyari ya moyo kwenda kunywa maji au "ku-buy buy time"!Usiwalazimishe.Muda utawaelekeza njia ya uzima.
Sasa mpaka lini mkuu kama dunia ni moja na wezetu mfano US walikata haya wakapata uhuru miaka ya 1800 huko sisi tuwaache watu wetu mpk lini kama si kuwazindua angalau kwa kusema hapa hapako sawa hapa palipaswa kuwa hivi.
 
Tanzania tukipata wapigania haki kama Lissu 15 hivi,wanaweza kubadili kidogo upepo wa Watanzani sisi tuliojaa ujinga.
Hakika mkuu aina ya harakati za ukombozi ambazo Lissu kila uchwao amekua akisisitiza ndizo sahihi kwa mageuzi ya taifa hili.
 
Mkuu acha hoja za shombo kama huna hoja ni bora kukaa kimya,kuishi ughaibuni sio hoja viongozi wetu wangapi wamesoma na kuishi huko ughaibuni?,wangapi wameugua na kupewa matibabu katika hizo Nchi za mashoga.unaweza usimpende kibinadamu lakini Ku acknowledge jitihada zake katika jambo Fulani sio vibaya.
Kweli kabisa mpaka sasa lissu mchango wake katika taifa kuhusu mageuzi hata akifariki leo uta zungumzwa kizazi mpaka kizazi madhira aliyo pitia lissu ni magumu sana haya elezeki.
 
Sawa mkuu , inabidi kwa kweli tujitathimini kuhusu huu uoga tulio nao ambao unazidi kukomaa kizazi mpaka kizazi huku tukiliacha taifa likiangamia .
Kama iliwezekana kwa CCM kuweka mapandikizi upunzani kwa minajili ya kudhoofisha naona ni wakati sahihi sasa kwa wanaoipenda Tanzania kuingia CCM ili kuiondoa kwenye mstari
 
Tundu Lissu alijaribu kuwaamsha Wadanganyika kwa maandamano baada ya uchafuzi wa 2000. Alipoona uoga umezidi na hakuna aliyejitokeza, huyoo akapanda pipa kwenda kula maisha Ubelgiji na sidhani kama ana mpango wa kurudi. Inauma sana unapowapigania watu mpaka kuhatarisha maisha yako lakini unaowapigania wapo wapo tu hawajitambui.

Na kwa uoga huu CCM itatawala milele!
Wakati ule yule kichaa angeuwa wengi Sana! Yule alikuwa ni shetani!
 
Katiba mpya itafaa nini ikiwa iliyopo haiheshimiwi.

Maandamano na vurugu ndio njia sahihi ya kupata haki.
Lakini ndo ivo sasa sisi ni waoga kinoma, uoga umezaa ubinafsi wa kiwango kikubwa sana.
Kweli kabisa mkuu uoga ni sumu mbaya sana inayo tumaliza na ambayo itaendelea kutumaliza tusipo chukua hatua stahiki.
 
Mimi naona tatizo kubwa ni kukosa watu wenye akili zinazofikiri kisawa sawa. Nasema kwamba tungekuwa na watu wenye akili tusingekuwa waoga namna hii. Huu woga ni dalili moja tu ya ukosefu wa akili.
Tanzania hii kila mtu analenga maslahi yake mtakuea pamoja mwanzoni mwa harakati akipata anachotaka anasaliti Kambi.
Katika mazingira haya huwezi pata mabadikiko sababu hakuna common agenda.
Hasa kizazi hiki ndio kibaya zaidi yaani chawa ni tabu kabisa, unaona kabisa mtu anapambania apate kitu na si alete mabadikiko.
Naamini kitakacjotutoa hapa tulipo ni kuwa na demokrasia imara ambayo sinlazima ifanani na ya marekani au Uingereza ila Ile ambayo itawezesha maonoli ya watu yaheshimiwe.
Hofu yangu hatuwezi kupata demokrasia imara kwani historia ya nchi yetu pia inaonesha tuliingia vyama vingi kishingo upande ili kuwaridhisha wakubwa wasitutenge. Hapa ndipo CCM wanapambana toka enzi na enzi sababu hawakukubali kihiari kuingia kwenye vyama vingi.
Watu wetu pia wameziea shida hawaoni kama Kuna Maisha zaidi ya haya ni namna gani mtu huyu atatamani kubadili mambo?
Tunahitaji watu wa kuwafungua watu wetu na kuwaonesha kuwa tunaweza kuishi maisha Bora kabisa ya hadhi ya binadamu na hapo ndipo tutaweza kubadili Hali kwani itakuwa rahisi kupata kuungwa mkono kea wingi.
Hivyo elimu ya kuzindua watu ni muhimu saana, itolewe bila kuchoka.
Pilato aliwasha taa mchana kuwazindua watu bado kazi inapaswa kuendele bila kuchoka.
Hakika, hakika, hakika haya uliyo nena kupitia maandishi mkuu hayana pingamizi lolote lile.
 
Sasa mpaka lini mkuu kama dunia ni moja na wezetu mfano US walikata haya wakapata uhuru miaka ya 1800 huko sisi tuwaache watu wetu mpk lini kama si kuwazindua angalau kwa kusema hapa hapako sawa hapa palipaswa kuwa hivi.
Kweli kabisa.
 
Je ni lini hiyo watakubali kunywa maji ya mto ? Tafakari kuhusu muda haujawahi kumsubiri mtu. Na je rasilimali za taifa zitaendelea kusubiri siku Watanzania waamke miaka mingapi ijayo je 50, 100 , 1000.

Kumbuka mkuu wafuja mali hawata wasubiri Watanzania waamke bali wataendelea na utaratibu wao huku sisi tukiendelea kusubiri huo muda wa kunywa maji mtoni hatari sana hii mkuu kwa usalama wa taifa.
Sijui umemielewa?Majitu majinga ambayo hayajitambui unataka uyafanyie nini?Yaache hivyohivyo.
 
Mara kadhaa nimeandika humu JF ni ngumu sana kuwapigania watu wasio jitambua Kama Watanzania,kuwa kuwa na kizazi Cha waoga na waimba mapambio hata mwalimu Nyerere alisha sema kinahitaji kizazi Cha vijana wanao hoji na kuwa waasi juu ya mifumo kandamizi sio vijana Kama hawa wa leo kusifia tu ili wapate teuzi.

Kama taifa inabidi tujitafakari Kuna sehemu hatupo sawa ukiangalia mienendo ya taifa letu kiza kinene kipo mbele kuliko mwanga
FB_IMG_1665472077577.jpg
 
WATANZANIA mpaka sasa tuna shindwa kukubaliana na ukweli kuwa tatizo kuu la taifa letu sio Chama Cha Mapinduzi [ CCM ] bali tatizo letu kuu linalo pelekea umasikini na matatizo mbalimbali kwetu ni sisi wenyewe WATANZANIA.

Mpaka leo hii mwaka 2022 toka uhuru wetu 1961 tumeshindwa kupambana na tatizo letu linalopekea umasikini wetu, ambalo tatizo lenyewe hasa ni “UOGA” hili ndilo tatizo sugu linapopelekea umasikini wetu.

Mpaka sasa tumeshindwa kabisa kufanya mageuzi makubwa ya taifa letu na tumebaki kuliacha taifa likiangamia huku kundi dogo la watu wakila minofu ya rasilimali za taifa letu huku kundi kubwa wakipiga miayo tu.

Mpaka sasa tumeshindwa kabisa na tunaendelea kushindwa kufanya mageuzi kama walio fanya Warusi chini ya Vladimir Lenin 1917, Wachina chini ya Mao Zedong 1949, Wafaransa chini ya Maximilien Robespierre 1789, Wamarekani chini ya George Washington 1765, Wairan chini ya Ruhollar Khomeini 1978.

Bado kwa uoga wetu tuna endelea kuamini kuwa mageuzi ya shida zetu yataletwa kwa sanduku la kura huku sanduku hilo likiwa mpaka sasa toka 1961-2022 limeshindwa kutuletea matokea chanya ya matarajio yetu, kiufupi sanduku la kura ni kiini macho kwa Watanzania.

Kama kweli tunataka kuona umasikini unakufa katika taifa letu basi hatuna budi kukubali pia kuzika hofu zetu ndani ya mioyo yetu na kukubali kuiotoa kafara miili yetu kwa ajili ya kuuzika umasikini katika taifa letu, bila kufanya hivyo tutakua hatuna tofauti na Democratic Republic Of Congo [ DRC ] ambao kwa takribani miaka zaidi ya 60 kwa sasa bado hawajajua kuwa wakutatua matatizo yao ni wao wenyewe na wala sio walinda amani wa umoja wa mataifa.

N.b :- Siku zote Watanzania wenzangu haki haiombwi bali haki inapiganiwa.

- Sanduku la kura haliweza kutuleta matokeo chanya ya kupambana na umasikini wetu, sanduku la kura ni kiini macho cha watawala kwa watawaliwa.

Tuchague moja kukubali kuendelea kuishi na uoga wetu huku tukiendelea kuumwagilia mbolea na maji umasikini wetu uli uzidi kumea zaidi katika taifa letu, au tukubali kufanya mageuzi makubwa kama walio fanya Marekani, Urusi, Ufaransa, China, Iran na kupelekea kukata huo mti wa umasikini wetu na kujenga nchi yetu itakayo kuwa na heshima hapa Afrika na dunia kiujumla.

MABADILIKO SIKU ZOTE HAYAJA WAHI KUWA MEPESI, NI HAYO TU KWA LEO NANYI NYOTE MUWE NA SIKU NJEMA.
Xiaoping!!
 
Niachangia na mm

Mali na burkinafaso na nchi zingine za kimagharib ya Africa wengi wao siyo waoga lkn bado Hali zao Ni mbaya sna kuliko sisi je uoga gani unausema mnk kwa Africa Kuna miamba amabyo hawataki ujinga ila mambo yao yamedoda
 
Back
Top Bottom