Dodoso: Tatizo la Tanzania sio CCM

Dodoso: Tatizo la Tanzania sio CCM

WATANZANIA mpaka sasa tuna shindwa kukubaliana na ukweli kuwa tatizo kuu la taifa letu sio Chama Cha Mapinduzi [ CCM ] bali tatizo letu kuu linalo pelekea umasikini na matatizo mbalimbali kwetu ni sisi wenyewe WATANZANIA.

Mpaka leo hii mwaka 2022 toka uhuru wetu 1961 tumeshindwa kupambana na tatizo letu linalopekea umasikini wetu, ambalo tatizo lenyewe hasa ni “UOGA” hili ndilo tatizo sugu linapopelekea umasikini wetu.

Mpaka sasa tumeshindwa kabisa kufanya mageuzi makubwa ya taifa letu na tumebaki kuliacha taifa likiangamia huku kundi dogo la watu wakila minofu ya rasilimali za taifa letu huku kundi kubwa wakipiga miayo tu.

Mpaka sasa tumeshindwa kabisa na tunaendelea kushindwa kufanya mageuzi kama walio fanya Warusi chini ya Vladimir Lenin 1917, Wachina chini ya Mao Zedong 1949, Wafaransa chini ya Maximilien Robespierre 1789, Wamarekani chini ya George Washington 1765, Wairan chini ya Ruhollar Khomeini 1978.

Bado kwa uoga wetu tuna endelea kuamini kuwa mageuzi ya shida zetu yataletwa kwa sanduku la kura huku sanduku hilo likiwa mpaka sasa toka 1961-2022 limeshindwa kutuletea matokea chanya ya matarajio yetu, kiufupi sanduku la kura ni kiini macho kwa Watanzania.

Kama kweli tunataka kuona umasikini unakufa katika taifa letu basi hatuna budi kukubali pia kuzika hofu zetu ndani ya mioyo yetu na kukubali kuiotoa kafara miili yetu kwa ajili ya kuuzika umasikini katika taifa letu, bila kufanya hivyo tutakua hatuna tofauti na Democratic Republic Of Congo [ DRC ] ambao kwa takribani miaka zaidi ya 60 kwa sasa bado hawajajua kuwa wakutatua matatizo yao ni wao wenyewe na wala sio walinda amani wa umoja wa mataifa.

N.b :- Siku zote Watanzania wenzangu haki haiombwi bali haki inapiganiwa.

- Sanduku la kura haliweza kutuleta matokeo chanya ya kupambana na umasikini wetu, sanduku la kura ni kiini macho cha watawala kwa watawaliwa.

Tuchague moja kukubali kuendelea kuishi na uoga wetu huku tukiendelea kuumwagilia mbolea na maji umasikini wetu uli uzidi kumea zaidi katika taifa letu, au tukubali kufanya mageuzi makubwa kama walio fanya Marekani, Urusi, Ufaransa, China, Iran na kupelekea kukata huo mti wa umasikini wetu na kujenga nchi yetu itakayo kuwa na heshima hapa Afrika na dunia kiujumla.

MABADILIKO SIKU ZOTE HAYAJA WAHI KUWA MEPESI, NI HAYO TU KWA LEO NANYI NYOTE MUWE NA SIKU NJEMA.
TATIZO la nchii hii ni viongozi kwanza wanang'ang'ania madaraka na uwezo wa kuongoza walionao ni mdogo mno, kuanzia ngazi ya shina mpaka juu. Watu wenye sifa na uwezo wanakataa kuongoza kutokana na hawa wanyang'anyi wananguvu kubwa na wako lazi kumdhulu yeyote. Sasa nchi hii inaongozwa na CCM ndio utaona kwanini urejee nilichosema awali.

Wananchi tuko wengi na tunahitaji uratibu thabiti kutoka viongozi, sasa imagine kundi la viongozi lilkaa na kuamua ili kuongeza mapato katika nchi hii ni kuweka tozo katika miamala, viongozi hawa wakajipigia makofi na kupitisha hawa
 
Back
Top Bottom