Dodoso: Tatizo la Tanzania sio CCM

DENG XIAOPING

JF-Expert Member
Mar 6, 2022
2,398
2,593
WATANZANIA mpaka sasa tuna shindwa kukubaliana na ukweli kuwa tatizo kuu la taifa letu sio Chama Cha Mapinduzi [ CCM ] bali tatizo letu kuu linalo pelekea umasikini na matatizo mbalimbali kwetu ni sisi wenyewe WATANZANIA.

Mpaka leo hii mwaka 2022 toka uhuru wetu 1961 tumeshindwa kupambana na tatizo letu linalopekea umasikini wetu, ambalo tatizo lenyewe hasa ni “UOGA” hili ndilo tatizo sugu linapopelekea umasikini wetu.

Mpaka sasa tumeshindwa kabisa kufanya mageuzi makubwa ya taifa letu na tumebaki kuliacha taifa likiangamia huku kundi dogo la watu wakila minofu ya rasilimali za taifa letu huku kundi kubwa wakipiga miayo tu.

Mpaka sasa tumeshindwa kabisa na tunaendelea kushindwa kufanya mageuzi kama walio fanya Warusi chini ya Vladimir Lenin 1917, Wachina chini ya Mao Zedong 1949, Wafaransa chini ya Maximilien Robespierre 1789, Wamarekani chini ya George Washington 1765, Wairan chini ya Ruhollar Khomeini 1978.

Bado kwa uoga wetu tuna endelea kuamini kuwa mageuzi ya shida zetu yataletwa kwa sanduku la kura huku sanduku hilo likiwa mpaka sasa toka 1961-2022 limeshindwa kutuletea matokea chanya ya matarajio yetu, kiufupi sanduku la kura ni kiini macho kwa Watanzania.

Kama kweli tunataka kuona umasikini unakufa katika taifa letu basi hatuna budi kukubali pia kuzika hofu zetu ndani ya mioyo yetu na kukubali kuiotoa kafara miili yetu kwa ajili ya kuuzika umasikini katika taifa letu, bila kufanya hivyo tutakua hatuna tofauti na Democratic Republic Of Congo [ DRC ] ambao kwa takribani miaka zaidi ya 60 kwa sasa bado hawajajua kuwa wakutatua matatizo yao ni wao wenyewe na wala sio walinda amani wa umoja wa mataifa.

N.b :- Siku zote Watanzania wenzangu haki haiombwi bali haki inapiganiwa.

- Sanduku la kura haliweza kutuleta matokeo chanya ya kupambana na umasikini wetu, sanduku la kura ni kiini macho cha watawala kwa watawaliwa.

Tuchague moja kukubali kuendelea kuishi na uoga wetu huku tukiendelea kuumwagilia mbolea na maji umasikini wetu uli uzidi kumea zaidi katika taifa letu, au tukubali kufanya mageuzi makubwa kama walio fanya Marekani, Urusi, Ufaransa, China, Iran na kupelekea kukata huo mti wa umasikini wetu na kujenga nchi yetu itakayo kuwa na heshima hapa Afrika na dunia kiujumla.

MABADILIKO SIKU ZOTE HAYAJA WAHI KUWA MEPESI, NI HAYO TU KWA LEO NANYI NYOTE MUWE NA SIKU NJEMA.
 
Kama kuitoa CCM madarakani imetupasa kutokuwa WAOGA, basi tatizo si woga, Bado CCM ni tatizo.

Bt chanzo Cha yote ni Katiba mbovu .

Tupambanie KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Ilipatikana hiyo, CCM imekufa automatically.

Angalizo: HOFU au UOGA ni DHAMBI.

Wa kuogopwa na kutetemekewa ni MUNGU pekee na Si WANADAMU,lakini kama tu umesimama ktk KWELI na HAKI.

Ameeeen.
 
Tundu Lissu alijaribu kuwaamsha Wadanganyika kwa maandamano. Alipoona uoga umezidi na hakuna aliyejitokeza, huyoo akapanda pipa kwenda kula maisha Ubelgiji na sidhani kama ana mpango wa kurudi. Inauma sana unapowapigania watu mpaka kuhatarisha maisha yako lakini unaowapigania wapo wapo tu hawajitambui.

Na kwa uoga huu CCM itatawala milele!
Hakika mkuu, sanduku la kura na katiba mpya kamwe haviwezi kubadilisha chochote kutokana na hali ya sasa na hakika njia aliyo pendekeza Tundu Antipas lissu ni miongoni mwa njia bora kabisa ya kuzika umasikini wetu endapo tukiitilia umakini na kuifuata itatupa kwa asilimia kubwa matokeo chanya ya shida zetu.
 
Kama kuitoa CCM madarakani imetupasa kutokuwa WAOGA, basi tatizo si woga, Bado CCM ni tatizo.

Bt chanzo Cha yote ni Katiba mbovu .

Tupambanie KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Ilipatikana hiyo, CCM imekufa automatically.

Angalizo: HOFU au UOGA ni DHAMBI.

Wa kuogopwa na kutetemekewa ni MUNGU pekee na Si WANADAMU,lakini kama tu umesimama ktk KWELI na HAKI.

Ameeeen.
Nakubaliana na wewe mkuu kuhusu kuitafuta katiba mpya lakini katiba mpya haipaswi kupatikana sasa kwa Watanzania walio waoga kwa kua itakua si chochote si lolote haitaleta matokeo chanya katika jamii ya watu waoga kwa kuwa pia nayo itaweza kukanyagwa na hao watu na waoga wasifanye chochote kile kui tetea.
 
"Kuitoa kafara miili yetu"ndio nini?
Nchi hii ina matatizo Mengi, ya kisiasa ni ccm, tuliambiwa enzi hizo, tunahitaji, watu, ardhi, Siasa safi, na uongozi Bora,

Vingine vipo kibao, Siasa safi na uongozi Bora,ndio shida kubwa.

Korea kusini, Philippine, Uturuki, China, Vietnam, hizi zote,viongozi walitoa Siasa safi na uongozi Bora, China hakuna demokrasia, lakini Kuna Siasa Bora!!

Bongo, hakuna Siasa safi Wala uongozi Bora, Kuna wezi tu pale Ikulu, wanatumia vyombo vya dola kubaki Madarakani, Hawa dawa yao,sio sanduku la kura, ni shaba tu za vichwa, na kutatuliwa malinda
 
Muda utafika, huu mchezo una mwisho hata kama sio kizazi chetu
Kwa hiyo tuendelee kuvumilia umasikini na matatizo yetu hata Kama yana tuumiza ? hiyo hari tutaivumilia mpaka lini ?

: Tusije tukawa kama wazee wetu waliovumilia mateso ya utumwa na ukoloni vizazi na vizazi kwa zaidi ya miaka takribani 500, tujitafakari kwa kweli kuhusu aina ya uvumilivu tunao taka kuwa nao sisi na vizazi vyetu.
 
"Kuitoa kafara miili yetu"ndio nini?
Nchi hii ina matatizo Mengi,ya kisiasa ni ccm,tuliambiwa enzi hizo,tunahitaji,watu,ardhi,Siasa safi,na uongozi Bora,
Vingine vipo kibao,Siasa safi na uongozi Bora,ndio shida kubwa.
Korea kusini,Philippine,Uturuki,China,Vietnam,hizi zote,viongozi walitoa Siasa safi na uongozi Bora,China hakuna demokrasia,lakini Kuna Siasa Bora!!
Bongo,hakuna Siasa safi Wala uongozi Bora,Kuna wezi tu pale Ikulu,wanatumia vyombo vya dola kubaki Madarakani,Hawa dawa yao,sio sanduku la kura,ni shaba tu za vichwa,na kutatuliwa malinda
Unaposema kuhusu China nadhani hasa unamaanisha China[ PRC] pitia historia yao kidogo mkuu, ujifunze ni kwa njia ipi waliya pata hayo yaliyo bora kwa sasa. kasome matatizo ya China kabla ya serikali ya watu wa China kusimikwa rasmi 1949. Je China ya sasa PRC ili kuwa hivi toka awali kabla ya uamuzi wa watu wa China na wakina Mao Zedong 1949 ?
 
Nakubaliana na wewe mkuu kuhusu kuitafuta katiba mpya lakini katiba mpya haipaswi kupatikana sasa kwa Watanzania walio waoga kwa kua itakua si chochote si lolote haitaleta matokeo chanya katika jamii ya watu waoga kwa kuwa pia nayo itaweza kukanyagwa na hao watu waoga wasifanye chochote kile.
Watangulizi waliwafungia watawaliwa ktk magereza ya HOFU.

MFUNGWA Ili alaumiwe Kwa HAKI lazima kwanza afunguliwe CHAINS au minyororo na pingu.

Mwenge Ule umetumika kuwatia USINGIZI watawaliwa wasijihangaishe na Watawala.

KAZI hiyo ya kuharibu madhabahu hiyo iliyowekwa pale ktk mlima mrefu imefanyika Kwa ufasaha,

Muda umefika, hao unaowaona WAOGA, watakavyoamka hutoamini.

Ameeeen.
 
Kama kuitoa CCM madarakani imetupasa kutokuwa WAOGA, basi tatizo si woga, Bado CCM ni tatizo.

Bt chanzo Cha yote ni Katiba mbovu .

Tupambanie KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Ilipatikana hiyo, CCM imekufa automatically.

Angalizo: HOFU au UOGA ni DHAMBI.

Wa kuogopwa na kutetemekewa ni MUNGU pekee na Si WANADAMU,lakini kama tu umesimama ktk KWELI na HAKI.

Ameeeen.
Yan ccm haohao katiba inawalinda ndio waibadilishe ili watolewe madarakani? Tena hakuna mchakato utakuja kuwa wa hovyo kama wa kuunda katiba mpya. Katiba itaandaliwa kimizengwe kwa kuendelea kuilinda ccm na wakati wenye akili wanaikataa, ishu ya demokrasia itakuja kuwa ipigiwe kura. Mtaenda kuiponda kweli kwa wananchi lakini c unajua sanduku la kura ni hilohilo la ccm.
 
Yan ccm haohao katiba inawalinda ndio waibadilishe ili watolewe madarakani? Tena hakuna mchakato utakuja kuwa wa hovyo kama wa kuunda katiba mpya. Katiba itaandaliwa kimizengwe kwa kuendelea kuilinda ccm na wakati wenye akili wanaikataa, ishu ya demokrasia itakuja kuwa ipigiwe kura. Mtaenda kuiponda kweli kwa wananchi lakini c unajua sanduku la kura ni hilohilo la ccm.
Hakika mkuu umenena, Katiba mpya na sanduku la kura hivi ni vyombo vya masilahi ya watawala kwa watawaliwa kuwa fanyia kiini macho watawaliwa ili waendelee kupumbazika kila uchwao wakiviamini.
 
Umegonga utosini..sanduku la kura ni kiini macho..bila nguvu ya umma kuamua na kujitoa mhanga hakuna jipya..sometimes naonaga wavaakobazi wenye itikadikali wako sawa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kama kuitoa CCM madarakani imetupasa kutokuwa WAOGA, basi tatizo si woga, Bado CCM ni tatizo.

Bt chanzo Cha yote ni Katiba mbovu .

Tupambanie KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Ilipatikana hiyo, CCM imekufa automatically.

Angalizo: HOFU au UOGA ni DHAMBI.

Wa kuogopwa na kutetemekewa ni MUNGU pekee na Si WANADAMU,lakini kama tu umesimama ktk KWELI na HAKI.

Ameeeen.
Kwa wakili yako unadhani ccm watakubali katiba itokanayo na rasimu ya warioba.

Pia katiba haijawahi kuwa suluhisho kama inapuuzwa na watawala..ona tu jinsi hii iliyopo wanavyoikanyaga waziwazi.


#MaendeleoHayanaChama
 
Tundu Lissu alijaribu kuwaamsha Wadanganyika kwa maandamano baada ya uchafuzi wa 2000. Alipoona uoga umezidi na hakuna aliyejitokeza, huyoo akapanda pipa kwenda kula maisha Ubelgiji na sidhani kama ana mpango wa kurudi. Inauma sana unapowapigania watu mpaka kuhatarisha maisha yako lakini unaowapigania wapo wapo tu hawajitambui.

Na kwa uoga huu CCM itatawala milele!
Mkuu mwaka gani
20221025_104220.jpg
 
Mleta mada acha kuzunguka zunguka

ukweli kuwa SERA YA UJAMAA NDIO TATIZO LILIPOANZIA

Ujamaa ulitufanya tuwe mabubu tuwe kizazi kisichohoji tuwaogope viongozi hata Kama wanakosea kwakigezo mkubwa hakosei

Nyerere alifanya mengi ila kwenye ujamaa yule mzee alituharibia nchi
 
Kwa wakili yako unadhani ccm watakubali katiba itokanayo na rasimu ya warioba.

Pia katiba haijawahi kuwa suluhisho kama inapuuzwa na watawala..ona tu jinsi hii iliyopo wanavyoikanyaga waziwazi.


#MaendeleoHayanaChama
Usiishi Kwa mazoea au kukariri.

Ungekuwa na " MACHO" ungeyatumia kuona.

Yatosha Kwa sasa.
 
Usiishi Kwa mazoea au kukariri.

Ungekuwa na " MACHO" ungeyatumia kuona.

Yatosha Kwa sasa.
Naona sana na nafuatiri siasa za nchi hii kwa ukaribu..

Kuhusu katiba mpya ni maigizo tu yanayoendelea.

Ccm haiwezi kubali katiba itakayo ibana kushindwa kutawala...never until nguvu ya umma itokee ama mapinduzi yatokee ndani ya ccm

Ccm sio chama cha siasa bali ni chama dola..inatawala kupitia katiba iliyoundwa kipindi cha chama kimoja.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom