Dodoso: Tatizo la Tanzania sio CCM

Dodoso: Tatizo la Tanzania sio CCM

Kama kuitoa CCM madarakani imetupasa kutokuwa WAOGA, basi tatizo si woga, Bado CCM ni tatizo.

Bt chanzo Cha yote ni Katiba mbovu .

Tupambanie KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Ilipatikana hiyo, CCM imekufa automatically.

Angalizo: HOFU au UOGA ni DHAMBI.

Wa kuogopwa na kutetemekewa ni MUNGU pekee na Si WANADAMU,lakini kama tu umesimama ktk KWELI na HAKI.

Ameeeen.
Vyama na katiba vyote vinatengenezwa na watu,kwa Katiba hii hii mbovu kuna mambo mengi yanafanyika yasiyoendana na Katiba ni action gani tulichukua?
Tatizo kubwa la Watanzania ni yoga unaoyokana na ujinga,halafu hii ni kwa wote waliosoma na ambao hawajasoma.
 
Tatizo la uoga katika hii Nchi alilitengeneza Nyerere ili aubudiwe,katika jamii ambayo ilikiluwa imejaa wajinga wengi Nyerere alitumia mwanya huo huo kujenga misingi mibovu ya watu kutohoji.

By the way kwa sasa hayupo na watu angalau asilimia Fulani wameelimika lakini tatizo bado ni kubwa sana.
 
Tundu Lissu alijaribu kuwaamsha Wadanganyika kwa maandamano baada ya uchafuzi wa 2000. Alipoona uoga umezidi na hakuna aliyejitokeza, huyoo akapanda pipa kwenda kula maisha Ubelgiji na sidhani kama ana mpango wa kurudi. Inauma sana unapowapigania watu mpaka kuhatarisha maisha yako lakini unaowapigania wapo wapo tu hawajitambui.

Na kwa uoga huu CCM itatawala milele!
Sema baada ya lissu kushindwa 'poto' ndio akatimka kujiunga na mashoga kina armstetdam huko ughaibuni. Usijidai kulikua na uchafuzi uchavuzi gani?
 
Mkuu acha hoja za shombo kama huna hoja ni bora kukaa kimya,kuishi ughaibuni sio hoja viongozi wetu wangapi wamesoma na kuishi huko ughaibuni?,wangapi wameugua na kupewa matibabu katika hizo Nchi za mashoga.unaweza usimpende kibinadamu lakini Ku acknowledge jitihada zake katika jambo Fulani sio vibaya.
 
Maneno haya yanafaa kuandikwa kwa wino wa dhahabu.
WATANZANIA mpaka sasa tuna shindwa kukubaliana na ukweli kuwa tatizo kuu la taifa letu sio Chama Cha Mapinduzi [ CCM ] bali tatizo letu kuu linalo pelekea umasikini na matatizo mbalimbali kwetu ni sisi wenyewe WATANZANIA.

Mpaka leo hii mwaka 2022 toka uhuru wetu 1961 tumeshindwa kupambana na tatizo letu linalopekea umasikini wetu, ambalo tatizo lenyewe hasa ni “UOGA” hili ndilo tatizo sugu linapopelekea umasikini wetu.

Mpaka sasa tumeshindwa kabisa kufanya mageuzi makubwa ya taifa letu na tumebaki kuliacha taifa likiangamia huku kundi dogo la watu wakila minofu ya rasilimali za taifa letu huku kundi kubwa wakipiga miayo tu.

Mpaka sasa tumeshindwa kabisa na tunaendelea kushindwa kufanya mageuzi kama walio fanya Warusi chini ya Vladimir Lenin 1917, Wachina chini ya Mao Zedong 1949, Wafaransa chini ya Maximilien Robespierre 1789, Wamarekani chini ya George Washington 1765, Wairan chini ya Ruhollar Khomeini 1978.

Bado kwa uoga wetu tuna endelea kuamini kuwa mageuzi ya shida zetu yataletwa kwa sanduku la kura huku sanduku hilo likiwa mpaka sasa toka 1961-2022 limeshindwa kutuletea matokea chanya ya matarajio yetu, kiufupi sanduku la kura ni kiini macho kwa Watanzania.

Kama kweli tunataka kuona umasikini unakufa katika taifa letu basi hatuna budi kukubali pia kuzika hofu zetu ndani ya mioyo yetu na kukubali kuiotoa kafara miili yetu kwa ajili ya kuuzika umasikini katika taifa letu, bila kufanya hivyo tutakua hatuna tofauti na Democratic Republic Of Congo [ DRC ] ambao kwa takribani miaka zaidi ya 60 kwa sasa bado hawajajua kuwa wakutatua matatizo yao ni wao wenyewe na wala sio walinda amani wa umoja wa mataifa.

N.b :- Siku zote matanzania wenzangu haki haiombwi bali haki inapiganiwa.

- Sanduku la kura haliweza kutuleta matokeo chanya ya kupambana na umasikini wetu, sanduku la kura ni kiini macho cha watawala kwa watawaliwa.

Tuchague moja kukubali kuendelea kuishi na uoga wetu huku tukiendelea kuumwagilia mbolea na maji umasikini wetu uliuzidi kumea zidi katika taifa letu, au tukubali kufanya mageuzi makubwa kama walio fanya Marekani, Urusi, Ufaransa, China, Iran na kupelekea kukata huo mti wa umasikini wetu na kujenga nchi yetu itakayo kuwa na heshima hapa Afrika na dunia kiujumla.

MABADILIKO SIKU ZOTE HAYAJA WAHI KUWA MEPESI, NI HAYO TU KWA LEO NANYI NYOTE MUWE NA SIKU NJEMA.
 
Ngumu sana japo inawezekana coz ccm ni wajanja na Wana uzoefu wa kushikia watu akili tangu kitambo...kwa kweli bado wenyewe tuna uvyama, ukanda ,ukabila na udini hatuwezi kuipindua ccm hata siku moja ....hakuna mtu yuko tayar chadema iingie madarakani kwani hii mikoa mingine wataishije? Tafuteni chama kingine kiwe na hali ya kuunganisha nchi nzima sio mnaswap chama cha watu fulani katika kabila lao eti kije kukomboa nchi.

Yatakuja tokea mauwaji ya kimbali bure.
 
Huo woga umeletwa na nani kama sio CCM?. HUWEZI KUITOA CCM KWENYE KILA MADUDU YANAYOENDELEA HAPA NCHINI.
Kwa hiyo tume kubali huo uoga uwe ndio mfumo mzima wa maisha yetu ya kila siku ? Na ni paka lini hii hari tutakubali kuishi nayo ?
 
WATANZANIA mpaka sasa tuna shindwa kukubaliana na ukweli kuwa tatizo kuu la taifa letu sio Chama Cha Mapinduzi [ CCM ] bali tatizo letu kuu linalo pelekea umasikini na matatizo mbalimbali kwetu ni sisi wenyewe WATANZANIA.

Mpaka leo hii mwaka 2022 toka uhuru wetu 1961 tumeshindwa kupambana na tatizo letu linalopekea umasikini wetu, ambalo tatizo lenyewe hasa ni “UOGA” hili ndilo tatizo sugu linapopelekea umasikini wetu.

Mpaka sasa tumeshindwa kabisa kufanya mageuzi makubwa ya taifa letu na tumebaki kuliacha taifa likiangamia huku kundi dogo la watu wakila minofu ya rasilimali za taifa letu huku kundi kubwa wakipiga miayo tu.

Mpaka sasa tumeshindwa kabisa na tunaendelea kushindwa kufanya mageuzi kama walio fanya Warusi chini ya Vladimir Lenin 1917, Wachina chini ya Mao Zedong 1949, Wafaransa chini ya Maximilien Robespierre 1789, Wamarekani chini ya George Washington 1765, Wairan chini ya Ruhollar Khomeini 1978.

Bado kwa uoga wetu tuna endelea kuamini kuwa mageuzi ya shida zetu yataletwa kwa sanduku la kura huku sanduku hilo likiwa mpaka sasa toka 1961-2022 limeshindwa kutuletea matokea chanya ya matarajio yetu, kiufupi sanduku la kura ni kiini macho kwa Watanzania.

Kama kweli tunataka kuona umasikini unakufa katika taifa letu basi hatuna budi kukubali pia kuzika hofu zetu ndani ya mioyo yetu na kukubali kuiotoa kafara miili yetu kwa ajili ya kuuzika umasikini katika taifa letu, bila kufanya hivyo tutakua hatuna tofauti na Democratic Republic Of Congo [ DRC ] ambao kwa takribani miaka zaidi ya 60 kwa sasa bado hawajajua kuwa wakutatua matatizo yao ni wao wenyewe na wala sio walinda amani wa umoja wa mataifa.

N.b :- Siku zote matanzania wenzangu haki haiombwi bali haki inapiganiwa.

- Sanduku la kura haliweza kutuleta matokeo chanya ya kupambana na umasikini wetu, sanduku la kura ni kiini macho cha watawala kwa watawaliwa.

Tuchague moja kukubali kuendelea kuishi na uoga wetu huku tukiendelea kuumwagilia mbolea na maji umasikini wetu uliuzidi kumea zidi katika taifa letu, au tukubali kufanya mageuzi makubwa kama walio fanya Marekani, Urusi, Ufaransa, China, Iran na kupelekea kukata huo mti wa umasikini wetu na kujenga nchi yetu itakayo kuwa na heshima hapa Afrika na dunia kiujumla.

MABADILIKO SIKU ZOTE HAYAJA WAHI KUWA MEPESI, NI HAYO TU KWA LEO NANYI NYOTE MUWE NA SIKU NJEMA.
Kwa hiyo kama ni dodoso basi huna utambuzi Wala muelekeo Nini kifanyika!
Yaani CCM kuwa na wabunge feki unaona sawa! Miradi inachakachuliwa! Pesa za Halmashauri zinapigwa Kwa kwenda Nyuma! Kuna pahali Pana tatizo!!
 
Ngumu sana japo inawezekana coz ccm ni wajanja na Wana uzoefu wa kushikia watu akili tangu kitambo...kwa kweli bado wenyewe tuna uvyama, ukanda ,ukabila na udini hatuwezi kuipindua ccm hata siku moja ....hakuna mtu yuko tayar chadema iingie madarakani kwani hii mikoa mingine wataishije? Tafuteni chama kingine kiwe na hali ya kuunganisha nchi nzima sio mnaswap chama cha watu fulani katika kabila lao eti kije kukomboa nchi.

Yatakuja tokea mauwaji ya kimbali bure.
Sawa mkuu asante kwa mchango wako. Vipi kuhusu donda sugu la uoga tulilo nalo ?
 
Kwa hiyo kama ni dodoso basi huna utambuzi Wala muelekeo Nini kifanyika!
Yaani CCM kuwa na wabunge feki unaona sawa! Miradi inachakachuliwa! Pesa za Halmashauri zinapigwa Kwa kwenda Nyuma! Kuna pahali Pana tatizo!!
Siwezi kuona sawa mabaya yanayo endelea hapa nchini . Ndio maana nikaandika hii thread inayo zungumzia tatizo kuu “Uoga” lita fakari kwa kina hilo neno natumai utauelewa ujumbe wangu haswa ni nini.
 
Sikubaliani na weye mkuu.Tatizo si UOGA.Tatizo ni MUDA.Ndiyo.Do not force a button!Waache Watanzania kwanza waipokee hali.Halafu waache waiishi hali.Na ndiyo walipofikia.Wanaiishi hali.Basi,uwaache hadi wapate kifu/waikinai hali hii wanayoiishi.Utafika tu muda na watapanga kuchagua moja.Kwamba,waendelee na hali hii waliyonayo au waikatae na kufanya maamuzi.Mto wanauona.Ni khiyari ya moyo kwenda kunywa maji au "ku-buy buy time"!Usiwalazimishe.Muda utawaelekeza njia ya uzima.
Je ni lini hiyo watakubali kunywa maji ya mto ? Tafakari kuhusu muda haujawahi kumsubiri mtu. Na je rasilimali za taifa zitaendelea kusubiri siku Watanzania waamke miaka mingapi ijayo je 50, 100 , 1000.

Kumbuka mkuu wafuja mali hawata wasubiri Watanzania waamke bali wataendelea na utaratibu wao huku sisi tukiendelea kusubiri huo muda wa kunywa maji mtoni hatari sana hii mkuu kwa usalama wa taifa.
 
WoGA siamini Mana WoGA unazao lake ,kunakitu hujakisema hicho kilikua muhimu Sana "elimu elimu elimu" ccm ilaaniwe kwa kuwanyima watanzania fursa hii ndo zao muhimu lilozalisha woga
Hakika mkuu Elimu , Elimu , Elimu inahitajika na sio Elimu tu bali Elimu bora ndilo hitaji la msingi kwa sasa kwa kila MTANZANIA.
 
Katiba mpya itafaa nini ikiwa iliyopo haiheshimiwi.

Maandamano na vurugu ndio njia sahihi ya kupata haki.
Lakini ndo ivo sasa sisi ni waoga kinoma, uoga umezaa ubinafsi wa kiwango kikubwa sana.
 
Back
Top Bottom