DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Zipo September seven nyingi za watanzania wenzetu.
1. Sept 7 ya Akwilina kupigwa risasi na watu wanaojulikana.
2. Sept 7 ya Wanafunzi wa UDOM kuondolewa chuoni.eti ni vilaza ,
3. Sept 7 ya watu kufariki kwa moto wakichota mafuta sababu ya ugumu wa maisha Morogoro
4. Sept 7 ya Membe kufukuzwa uanachama CCM.
5. Sept 7 ya watumishi kufukuzwa kazi kwa vyeti feki na kukosa michango yote waliyochangia.
6. Sept 7 ya wakulima wa korosho huko kusini kukosa malipo yao kwa wakati.
7. Sept 7ya waliombomolewa nyumba zao bila kufidiwa kwa kujenga kando mwa barabara.
8. Sept 7 ya watumishi wakopwaji wa loan board kukatwa 15% badala ya 8% kama mikataba inavvyosema.
9. Sept 7 ya watumishi kukosa kupandishwa madaraja, nyongeza ya kila mwaka ya mshahara na malipo mengine kama likizo.
10. Sept 7 ya vijana wanaoshindwa kuendelea na elimu ya juu kwa kukosa mikopo.
11. Sept 7 ya wafanyabiashara waliofungiwa biashara zao na TRA kwa kushindwa makadilio makubwa.
12. Sept 7 ya wahitimu vyuo wanaosota mitaani kwa kukosa ajira.
13. Sept 7 ya wagonjwa wanaokosa matibabu kwa kushindwa kulipia ghalama za matibabu.
14. Sept 7 ya watumishi ya serikali kukosa mishahara yao ya mwezi 7 na 8 kwa kugombea ubunge tena CCM ili wafikishe CV kwa mheshimiwa wafikiriwe ktk teuzi.
15. Sept 7 ya waliokatwa kugombea ubunge licha ya kushinda katika kura ya maoni CCM na CHADEMA.
16. Sept 7 ya wapinzani waliokatwa na NEC kugombea udiwani na ubunge.
17. Sept 7 ya wafanyabiashara kulazimishwa kuwakopa wabunge kama sakata la MO na Dr. Kigwa.
18. Sept 7 ya watu kubambikiziwa kesi za utakatishaji fedha.
19. Sept 7 ya wanafunzi kusomea katika mazingira yasiyo rafiki kujifunzia kama shule za kata. Huku wengine wakisoma shule maalumu na bora.
20. Sept 7 ya watanzania kujaa hofu, woga, kukosa uhuru na haki ya kukosoa.
 
Hakika lilikuwa tukio la kinyama na kikatili mkuuu. Lakini Mungu amedhihirisha Ukuu wake kupitia Lissu . Na bila wasi wasi Anaweza akamuinua sana juu zaidi.

Mungu aendelee kupambana na watesi wa lissu yeye mwenyewe. Akitaka kuwasamehe awasamehe yeye mwenyewe.

HAKIKA NILISHUHUDIA DODOMA TUKIO LA KINYAMA SANA.
 
Leo ni miaka mitatu rasmi na bado miezi miwili aapishwe kuwa Rais mpya, what a coincedence?
Ni kama vile neno coincidence umelitumia ndivyo sivyo.
Usije ukanifokea hebu ngoja Kwanza nikamuulize Ras Simba, maana na mie hata sina uhakika
 
Baada ya Shambulizi lile, Magufuli akachota pesa hazina na kutoa fungu kwa MaCCM Lumumba boku7 kujaa mitandaoni kufanya propaganda za kishamba na zilizokosa utu, kwa mauaji waliomfanyia Lissu.

Mungu kawaumbua, Lissu yu hai.
 
Dah! Nakumbuka nilibubujikwa na machozi mengi ofsn hadi wakanishangaa, lkn wengine niliwaliza pia. Sitasahau!

Mwenyezi Mungu Uendelee kumbariki, akafanikiwe MALENGO aliyompatia kwa mustakabariki mwema kwa Watanzania.

Tukio hili lilimuinua sana Tundu Lissu. Naamini 1/3 ya wapenzi sasa walimfahamu na kufuatilia baada ya tukio hili na yale yaliyofuatia kutendewa
 
Leo imetimia miaka mitatu 3 kamili toka Tundu Lissu ashambuliwe kwa risasi zaidi ya 38 tarehe 7/9/2017 na watu wasiojulikana Dodoma alipokuwa anahudhuria vipindi vya bunge....
Amina tunamshukuru Mungu kwa muujiza mkubwa na tunamuombea Lissu maisha marefu na ushindi mkubwa.
 
Back
Top Bottom