DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

hii hatar sasa.. walianza kwa kutishia hadharani na bunduki sasa wameanza kupiga kweliiii.... get well soon kamanda
 
chukua tokeo la bashite kuingia na watu wenye silaha clouds,,unganisha tokio la nape kutolewa silaha na muhusika hajulikani,,unganisha na kupigwa bomu kwa ofisi za mawakili pale upanga..baada ya hapo yachunguze majibu ya vyombo vyetu vya dola kuhusu matukio hayo..hapo kama unafikiri kwa kutumia kichwa basi utapata ni serikali ya aina gani inayotuongoza kwa sasa
Upo sawa mkuu...
na wote waliohusika katika tishia hawkushikwa
 
Kuna watu walienda Uingereza,India South RSA, Canada hawakurudi wakiwa hai.
First Aid kapewa Dodoma. Kama kumalizwa ingeshindikana?
Tuache utoto.
tutajuaje huenda hata kwenye hiyo first aid katiwa silent killer.Mungu aepushie mbali
 
na
Akipona aitwe mahakamani kujibu kesi zinazomkabili.
nahisi kama kuna movie fulani kanachezwa thats why nilitamani tuone wapi kawa injured, kila cku tunaendeshwa kwa matukio leo hili kesho lile mambo politics haya nikuwa achia wao anyway pona kwanza tundu then tuone hili nalo litaishia wapi
 
Subiri ujue amepigwa wapi hiyo risasi pia.. na acha kusingizia mamlaka wakati unajua na yeye ni msaliti na labda tapeli kwa anaowasaidia kuiba mali za nchi yetu.. pesa kala na ugumu wa serikali unaendelea kuwanyoosha wanaompa bahasha kuvuruga..
Naona unamuombea afe kabisa au sio
endeleea kuomba kwa bidii
 
Kwa hiyo hapa napinga nini sasa? Kwani sio mnafiki sasa? Jana unamuita mnafiki, leo unamuita hero what are you? Why jana hukumuita Hero au leo usiendelee kumtakia afya njema mropokaji?
Nchi ni yetu sote, siku moja mtawala atakuwa mpinzani, naombea tu asijekuwa kama wa sasa.
mbona nyie nape mlimuita hero!! upinzani sio uadui mpaka kwenye matatizo tusiombeane kheri kua kiakili aisee
 
Screenshot_2017-09-07-19-52-49.jpg
nguo za tundulisu hizo zikiwa zimelowa damu.
 
Kama wahusika kweli wako serious kukamata hao mashetani sidhani kama wataweza hata kutoka dodoma hapo...
 
Wah Wabunge. Hali ya Mhe. Lissu inaendelea kuimarika. Keshafanyiwa upasuaji wa awali.

Bunge na Serikali wako tayari kugharamia matibabu ndani ya nchi. Nimesisitiza kuwa hatuko tayari kumwacha nchi kwa sasa si kwa sababu ya uwezo wa madaktari wetu na hospitali, bali kwa sababu za kiusalama. Hawako tayari kugharamia. Tunalazimika kugharamia wenyewe.

Naendelea na mipango ya kumrusha leo kwenda Nairobi Aghakhan Hospital kupitia Dar Airport ambapo air ambulance inamsubiri.

Gharama hazijajulikana lakini ndege tu from Dom Dar Nairobi ni +_ US$10,000. Bado matibabu tutajua mbele.

Namwomba Mhe Kiwelu aanze emergecy fund mobilization. Angalao isipungue shs 500,000/- kwa Mbunge. Chama nacho kitachangia.

Nawashukuru kwa ushirikiano.

Freeman Mbowe
Mkt na KUB

Madaktari wanasema ataweza kusafirishwa baada ya saa limoja na nusu.
 
chukua tokeo la bashite kuingia na watu wenye silaha clouds,,unganisha tokio la nape kutolewa silaha na muhusika hajulikani,,unganisha na kupigwa bomu kwa ofisi za mawakili pale upanga..baada ya hapo yachunguze majibu ya vyombo vyetu vya dola kuhusu matukio hayo..hapo kama unafikiri kwa kutumia kichwa basi utapata ni serikali ya aina gani inayotuongoza kwa sasa,( Pia fuatilia maelezo ya serikali kuhusu maiti zinazookotwa kwenye viroba)
unganisha tukio la sanane na roma kutekwa na kati ya haya matukio ni pekee tukio la nape mhusika tulimuona na pia ni kutokana na mhusika roma nae amewataja wahusika
 
Back
Top Bottom