Dodoma: Rais Samia anazindua Mkakati wa Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi 2022

Tukio liko mubashara ITV, TBC na Channel ten

Rais Samia anazindua zoezi la uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi 2022 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.

=====

View attachment 1937255

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema bila kuwa na hesabu au takwimu sahihi, haiwezekani kugawa rasilimali na kutoa huduma kwa Haki na uwiano

Amesema hayo leo Jijini Dodoma katika uzinduzi wa Mkakati wa Uelishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022

Amesema, "Huwezi kushughulikia changamoto ya Ajira endapo hujui watu wasio na Ajira. Huwezi kupelekea huduma na kushughulikia matatizo ya watu wenye mahitaji maalum kama Wazee na wenye Ulemavu"

Rais ametoa wito kwa Watanzania wote kujiandaa kuhesabiwa zoezi la Sensa litakapoanza akisema, ili mchakato huo uweze kukidhi mahitaji ya kufanikisha malengo ni lazima watu wote washirikishwe

Kuhusu hoja za kwanini Tanzania iingie kwenye zoezi hilo na kutumia fedha zilizopangwa amesema "Nimekuwa nikiona hoja hizo zikipita na kuulizwa. Sababu ni kwamba kama tunaweza kufanya wenyewe na kupata idadi yetu kwanini tutumie idadi inayotolewa na Vyombo vingine vya Kimataifa?"

Pia amesema zoezi hilo likifanyika taarifa za majengo, nyumba na hesabu ya watu katika kila Kitongoji
mkuu hivi nkitaka connection niwe mmoja mwa watu wa kupiga dili la kuwahesabu watu nilipwe na fanyaje?
 
Sesa ni Jambo la Muhimu sana, Watanzania wote tupo Tayari kuhesabiwa kwa maendeleo yetu.
 
Ngoswe akazama penzini kwa mtoto mazoea baba mkwe mzee mitomingi akamua kuchoma nyara za serikali.

Umenkumbusha mbali sana mkuu miaka hiyo.

Wahenga tuu ndio wanaelewa🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom