Dkt. Slaa wewe ndio mpotoshaji mkubwa, Katiba ndio muongozo na jibu la kila kitu. Hii tuliyonayo sasa ina mapungufu makubwa

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Dunia nzima inafahamika kuwa katiba ndio supreme law of the state.

Leo hii sisi watanzania tuna katiba ambayo ilitungwa mwaka 1977. Na ukiangalia ilikuwa ikireflect kujibu matatitizo na kero zilizokuwepo wakati huo. Ndio maana kumekuwepo na mabadiliko ya katiba hapa nchini kwetu zaidi ya mara nne ili kukidhi mahitaji na matakwa ya taifa letu.

Hata Mwl Nyerere kwa kinywa chake aliwahi kusema kuwa hii katiba ya sasa inamapungufu na kama angetawala kwa kuifuata basi angekuwa dikteta.

Taifa letu linahitahi katiba ambayo itatoa majibu ya kila kero amabyo inalikabili kila siku. Mfano ufisadi ni kero ambayo mpaka sasa haijapata majibu. Lakini hii katiba ya sasa ipo kimya namna ya kuwawajibisha mawaziri au wateule wa rais wanaofanya ufisadi. Hii ni kwa sababu ni wateule wa rais. Lakini kama wangekuwa wajiiliwa wangeshulikiwa.

Leo hii tuna kilio kikubwa juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola. Malalamiko ya watanzania juu ya ndugu zao kufariki mikononi mwa vyombo vya dola ni mengi. Lakini hakuna namna ya kudai haki za hao ndugu zao mahakamani. Hii ni sababu katiba ya sasa hairuhusu.

Hivyo usichukulie juujuu tu kwa kuangalia shilingi upande mmoja. Hii katiba ya sasa ina mapungufu makubwa.
 
Dr.SLAA hana Kazi anatafuta TEUZI kwa NGUVU na Teuzi bila kujipendekeza ngumu sana kupata ndio maana huyu Mzee ameamua kuwapotosha Watanzania kwa Makusudi ila tunamwambia TUNATAKA KATIBA MPYA
20211207_144841.jpg
 
Wapinzani wakiwa upinzani wanakuwa wazuri sana, wanapohamia CCM wanakuwa watu wahovyo sana, sijui wanapohama upinzani wanahama bila akili, akili wanaziacha upinzani CCM wanakwenda bila akili.
 
Back
Top Bottom