Tunaposifia kutumiza miaka mitatu tusisahau na mapungufu yake!

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Wakuu twendeni pamoja

Na Sam Ruhuza

19/03/2021 aliapishwa Rais mpya kuwa Rais kufuatia kifo cha Rais aliyekuwapo, kwahiyo amepata nafasi hiyo kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Ninaandika baada ya kuona sifa nyingi mno za Mheshimiwa Rais kwa kutimiza miaka mitatu ya Urais.
Sifa za pongezi ni nyingi mno kuliko mapungufu ama ushauri, hilo hamjasaidia Mheshimiwa Rais katika kazi yake, mnatakiwa mkitoa sifa basi mtofautishe za kwake na za waliomtangulia kuliko sifa ambazo utafikiri hatujawahi kuwa na Rais nchini, hiyo ni makosa.

Rais aliyetangulia mbele ya haki kuna style yake ya Uongozi aliyotumia ambayo ukweli ilikuwa ni kero kubwa kwa wananchi ambapo hawakuwa na uhakika wa usalama binafsi hasa kwa wenye mawazo mbadala, kitu ambacho wanaosifia Leo kazi za Rais miaka mitatu, hawataki kuhusisha mapungufu ya mtangulizi wake na yeye, Ila wanayachukua yale mazuri ya mtangulizi na kumfanya Kama vile yamefanywa na Rais wa sasa!
Nimesikia sifa Mfano baadhi tu kwa uchache;

- SGR, aliyeanza kujenga ni Rais aliyepita
Hili japo ameendeleza, lakini imechukua muda mrefu sana kuliko tulioambiwa awali. Hapa atafanya vizuri kutoa uwazi wa gharama za Ujenzi na jinsi wakandarasi walivyopatikana!

- Bwawa la Mwalimu Nyerere (Stiglazigoji- Stiegler's Gorge dam)
Hili nalo limeanza kujengwa na mtangulizi wake. Hapa napo itakuwa nzuri tukipewa gharama zake na upatikanaji wa Wakandarasi!

- Madaraja hasa la Kigongo-Busisi, hili nalo ni la mtangulizi wake. Hapa pia tupewe uwazi wa gharama na upatikanaji wa mkandarasi.

Tujiulize;
- Mtangulizi wake alipokuwa Rais, Rais wetu wa Leo alikuwa wapi?
Alikuwa ndiye Makamu wa Rais. Yale mapungufu ya utawala ule yalifanywa na Rais wa chama gani?
Sasa Kama yeye alikuwa Makamu wake na hakujiuzulu na akagombea nae tena 2020, maana yake alikuwa anahusika na yote mazuri na yasio mazuri ya kipindi kile na hivyo mnatoa sifa kwenye Yale mazuri, mkumbuke kuna machungu pia kwa yale mapungufu, bebeni ili yafike mwisho ndio mtakuwa mmemsaidia!

- Kipindi cha mtangulizi wake waliibuka sijui tuwaite wahalifu, walikuwa wanaua, wanajeruhi watu, wanataka watu na hakuna taarifa zozote za hao wahalifu zaidi ya kuambiwa ni watu wasiojulikana! Ikashangaza baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuapishwa, matukio ya watu wasiojulikana yamepungua sana! Je hili lilikuwa na mkono wa nani? Kuna walioumia na Haya matukio na yalitokea akiwa Makamu wa Rais, je amekwisha kuomba radhi kwa huo udhaifu?!!? Au kiongozi hakosei?

- kuna sifa kubwa nimesikia ya kuruhusu mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama vya siasa!
Hii sijaielewa, aliyezuia ni mtangulizi wake yeye akiwa Makamu wake na Mikutano ya hadhara na maandamano ni Haki kisheria kulingana na sheria ya vyama vingi vya siasa 1992, hivyo ilizuiliwa kinyume na sheria, akiwa Makamu Rais hatukumsikia kulaani hilo, ameingia yeye, ameliona baada ya mwaka akaruhusu, tunapongeza kwa lipi, kwamba aliyezuia kinyume na sheria sasa ameruhusu?!

- Uchaguzi wa Mitaa na Vijiji 2019, Chaguzi mdogo, Uchaguzi Mkuu 2020, wote wanakiri zilikuwa chaguzi zilizonyima haki na kupelekea kupata Viongozi Mitaa/Vijiji, Madiwani, Wabunge, Rais kwa kura ambazo hazina ukweli, lakini wananchi wakatulia hasa pongezi nyingi kwa vyama vya upinzani kuwa wapole na kuepusha fujo!
Kwenye uchaguzi huo ndipo Makamu Rais nae alipatikana, je kuna tamko lolote la kuwataka ladhi walioathirika na chaguzi hizo?!

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu alipoingia madarakani alifanya jambo zuri la kutangaza 4Rs na hizo zimeleta utulivu na kwa hilo ni kubwa amelifanya na amerekibisha mapungufu ya mtangulizi wake, ni vizuri katika hizo 4Rs atumie hiyo fursa kuwaomba radhi kiungwana waathirika wa utawala wa mtangulizi wake, kwani nae alikuwa ni msaidizi wake na hivyo mapungufu yote yanamuhusu Kama ilivyo kwa mazuri.

Mheshimiwa Rais, katika kipindi chako cha miaka mitatu, kundi la Machawa limezidi. Machawa waliamza kipindi cha mtangulizi wako, lakini kipindi chako waneongezeka mno hadi imekuwa kero na kutishia uhai wa afya ya akili kwa Taifa letu iwapo Ugonjwa huu utaendelea!

Hao Machawa hatukuwasikia kabisa kukusifia sifia kipindi cha mtangulizi wako, wao walikuwa bize kumsifia yeye hadi kupendekeza atawale milele maana haijapata kutokea Rais Kama huyo. Leo wamegeuza sifa zote kwako na kumsahau mtangulizi wako na kudai haijapata kutokea Rais Kama wewe!!

Ninakuomba kukemea na kuwaacha machawa ili kuliponya Taifa maana sifa zao sio kwako binafsi, bali ni Kiti chako leo, kesho akija Rais mwingine, watazungumzia sana madhaifu yako na kudai Rais huyo ajae ni Rais bora haijapata kutokea.

Anachoangalia Chawa ni maslahi yake binafsi, akisifia, akalamba uteuzi ama akaendelea kubaki kwenye nafasi yake, basi gonjwa uchawa utaendelea kushamiri. Majuzi kwenye Hotuba yako umekana kwamba hauna Kundi, hilo halitoshi, kemea hadharani machawa maana uchawa sasa umeharibu hata fikra za Wabunge wengi na wamegeuka machawa na kusahau wajibu wao!

Mara nyingi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu amekuwa akiongea, ukimsikiliza vizuri anaonekana ni Kiongozi na mwenye hisia ya huruma na Haki, labda kwasababu ya history yake kwamba aliwahi Mwanaharakati, basi ni vyema yale unayoyaongea, wasaidizi wako hakikisha wanayatekeleza na wewe kuyasimamia ipasavyo.

Mwisho kwa Leo nisikuchoshe, nikupongeze kwa miaka mitatu, Ombi kubwa ni hakikisha Haki inapatikana kupitia Katiba mpya ya Wananchi na Tume HURU ya Uchaguzi kabla ya chaguzi zijazo, vinginevyo yatakuwa yaleyale. Kama ulivyo Mwanamke wa kwanza kuwa Rais Tanzania, basi ingependeza sana Kama utatuletea Katiba mpya kabla ya 2025.

Tanzania ni yetu sote!
 
Kama uchaguzi mkuu wa 2020 ulikuwa batili, na kwakuwa rais aliyepo kaupata urais kutokana na uchaguzi ule, basi hata urais wake ni batili.
 
Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.

Kwa wale ambao siyo mbuzi na wale ambao ni mbuzi lkn hawana kamba imekula kwao.
 
Rais Benjamin William Mkapa, pamoja na matatizo yake mengi, aliwahi kuonesha busara za kuwa mtu aliyedumu katika siasa na utumishi wa umma na wa serikali kwa muda mrefu tangu miaka ya sitini alipokuwa mhariri wa gazeti la Daily News.

Kulikuwa na wakati Rais Magufuli alikuwa anasifiwa sana, sana sana. Ilikuwa kila kitu Magufuli, Magufuli. Serikaki ya Magufuli, Serikali ya Magufuli.

Mkapa akasema kitu ambacho wengi hawakutegemea, hususan kwa sababu Magufuli ni protege wake. Mkapa ndiye aliyemteua Magufuli kuwa Waziri.

Rais Mstaafu Mkapa alisema, msiseme serikali ya Magufuli, hii ni serikaki ya CCM.

Mkapa alitukumbusha umuhimu wa fikra za kidhahania (abstract thinking) zinazosisitiza kanuni za uongozi wa uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility) na kuachana na tabia za uchawa wa kuangalia watu.

Alitukumbusha kwamba serikali inaongozwa kwa ilani ya chama na sera za serikali, sio na mtu.

Ukielewa hili, utaelewa kuwa uongozi ni kama mbio za kupokezana kijiti. Lengo ni timu ishinde kwa ushirikiano wa wanaokimbia. Na hakuna atakayeshinda kwa jitihada zake peke yake, ili Tanzania ishinde, Samia afanikiwe, atakimbia kwa kupokea kijiti kutoka kwa Magufuli, Magufuli naye alifanya hivyo hivyo kitoka kwa Kikwete, Kikwete kwa Mkapa, Mkapa kwa Mwinyi na Mwinyi kwa Nyerere.

Na kwa kweli, hata kwenye uongozi wa Rais mmoja, Rais anasaidiwa na watu wengi sana kufanya kazi yale. Hajui kila kitu.

Mara nyingi, sera huanza kuonekana zinazaa matunda miaka kadhaa baada ya kuanzishwa, hivyo kama unaangalia Rais ni nani wakati sera zimezaa matunda, kwa kiasi kikubwa utakosa kuona nani akiyeanzisha sera hizo. Tumeona hivyo kwa Barack Obama na Trump.

Tumeona hivyo sana Brazil baada ya Fernando Enrique Cardoso. Nilikuwa nasoma kitabu cha Mwinyi "Mzee Rukhsa: Safari ya Maisha Yangu". Marehemu Mzee Mwinyi kaandika wazi kuwa ingawa anapewa sifa nyingi sana katika kufungua nchi na kuanzisha economic liberalization, lakini sera hizo zilishaanza ama kuandaliwa ama kufanyiwa kazi tangu sehemu ya mwisho ya uongozi wa mwisho wa Mwalimu Nyerere.

Huu uchawa uliokithiri ndio alioukataa Mkapa. Tunaelewa kuwa Rais ndiye muhifadhi (custodian) wa mambo mengi Tanzania, kuanzia ardhi mpaka labda sifa za watumishi wa umma na serikali, kwamba anaposifiwa, mara nyingine anasifiwa kama kiongozi, anasifiwa kwa kuwakilisha wafanyakazi wote wa umma na serikali, lakini, tukizidisha sana sifa kwa mtu binafsi, tunaondoa hii maana. Inakuwa kama vile tunamsifia rais fulani genius mastermind anayejua kupanga mipango kuliko watumishi wote wa umma na serikali , na yeye ndiye anawaelekeza wote.

Hapana. Huu si ukweli. Huu ni uchawa.
 
Wakuu twendeni pamoja

Na Sam Ruhuza

19/03/2021 aliapishwa Rais mpya kuwa Rais kufuatia kifo cha Rais aliyekuwapo, kwahiyo amepata nafasi hiyo kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Ninaandika baada ya kuona sifa nyingi mno za Mheshimiwa Rais kwa kutimiza miaka mitatu ya Urais.
Sifa za pongezi ni nyingi mno kuliko mapungufu ama ushauri, hilo hamjasaidia Mheshimiwa Rais katika kazi yake, mnatakiwa mkitoa sifa basi mtofautishe za kwake na za waliomtangulia kuliko sifa ambazo utafikiri hatujawahi kuwa na Rais nchini, hiyo ni makosa.

Rais aliyetangulia mbele ya haki kuna style yake ya Uongozi aliyotumia ambayo ukweli ilikuwa ni kero kubwa kwa wananchi ambapo hawakuwa na uhakika wa usalama binafsi hasa kwa wenye mawazo mbadala, kitu ambacho wanaosifia Leo kazi za Rais miaka mitatu, hawataki kuhusisha mapungufu ya mtangulizi wake na yeye, Ila wanayachukua yale mazuri ya mtangulizi na kumfanya Kama vile yamefanywa na Rais wa sasa!
Nimesikia sifa Mfano baadhi tu kwa uchache;

- SGR, aliyeanza kujenga ni Rais aliyepita
Hili japo ameendeleza, lakini imechukua muda mrefu sana kuliko tulioambiwa awali. Hapa atafanya vizuri kutoa uwazi wa gharama za Ujenzi na jinsi wakandarasi walivyopatikana!

- Bwawa la Mwalimu Nyerere (Stiglazigoji- Stiegler's Gorge dam)
Hili nalo limeanza kujengwa na mtangulizi wake. Hapa napo itakuwa nzuri tukipewa gharama zake na upatikanaji wa Wakandarasi!

- Madaraja hasa la Kigongo-Busisi, hili nalo ni la mtangulizi wake. Hapa pia tupewe uwazi wa gharama na upatikanaji wa mkandarasi.

Tujiulize;
- Mtangulizi wake alipokuwa Rais, Rais wetu wa Leo alikuwa wapi?
Alikuwa ndiye Makamu wa Rais. Yale mapungufu ya utawala ule yalifanywa na Rais wa chama gani?
Sasa Kama yeye alikuwa Makamu wake na hakujiuzulu na akagombea nae tena 2020, maana yake alikuwa anahusika na yote mazuri na yasio mazuri ya kipindi kile na hivyo mnatoa sifa kwenye Yale mazuri, mkumbuke kuna machungu pia kwa yale mapungufu, bebeni ili yafike mwisho ndio mtakuwa mmemsaidia!

- Kipindi cha mtangulizi wake waliibuka sijui tuwaite wahalifu, walikuwa wanaua, wanajeruhi watu, wanataka watu na hakuna taarifa zozote za hao wahalifu zaidi ya kuambiwa ni watu wasiojulikana! Ikashangaza baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuapishwa, matukio ya watu wasiojulikana yamepungua sana! Je hili lilikuwa na mkono wa nani? Kuna walioumia na Haya matukio na yalitokea akiwa Makamu wa Rais, je amekwisha kuomba radhi kwa huo udhaifu?!!? Au kiongozi hakosei?

- kuna sifa kubwa nimesikia ya kuruhusu mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama vya siasa!
Hii sijaielewa, aliyezuia ni mtangulizi wake yeye akiwa Makamu wake na Mikutano ya hadhara na maandamano ni Haki kisheria kulingana na sheria ya vyama vingi vya siasa 1992, hivyo ilizuiliwa kinyume na sheria, akiwa Makamu Rais hatukumsikia kulaani hilo, ameingia yeye, ameliona baada ya mwaka akaruhusu, tunapongeza kwa lipi, kwamba aliyezuia kinyume na sheria sasa ameruhusu?!

- Uchaguzi wa Mitaa na Vijiji 2019, Chaguzi mdogo, Uchaguzi Mkuu 2020, wote wanakiri zilikuwa chaguzi zilizonyima haki na kupelekea kupata Viongozi Mitaa/Vijiji, Madiwani, Wabunge, Rais kwa kura ambazo hazina ukweli, lakini wananchi wakatulia hasa pongezi nyingi kwa vyama vya upinzani kuwa wapole na kuepusha fujo!
Kwenye uchaguzi huo ndipo Makamu Rais nae alipatikana, je kuna tamko lolote la kuwataka ladhi walioathirika na chaguzi hizo?!

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu alipoingia madarakani alifanya jambo zuri la kutangaza 4Rs na hizo zimeleta utulivu na kwa hilo ni kubwa amelifanya na amerekibisha mapungufu ya mtangulizi wake, ni vizuri katika hizo 4Rs atumie hiyo fursa kuwaomba radhi kiungwana waathirika wa utawala wa mtangulizi wake, kwani nae alikuwa ni msaidizi wake na hivyo mapungufu yote yanamuhusu Kama ilivyo kwa mazuri.

Mheshimiwa Rais, katika kipindi chako cha miaka mitatu, kundi la Machawa limezidi. Machawa waliamza kipindi cha mtangulizi wako, lakini kipindi chako waneongezeka mno hadi imekuwa kero na kutishia uhai wa afya ya akili kwa Taifa letu iwapo Ugonjwa huu utaendelea!

Hao Machawa hatukuwasikia kabisa kukusifia sifia kipindi cha mtangulizi wako, wao walikuwa bize kumsifia yeye hadi kupendekeza atawale milele maana haijapata kutokea Rais Kama huyo. Leo wamegeuza sifa zote kwako na kumsahau mtangulizi wako na kudai haijapata kutokea Rais Kama wewe!!

Ninakuomba kukemea na kuwaacha machawa ili kuliponya Taifa maana sifa zao sio kwako binafsi, bali ni Kiti chako leo, kesho akija Rais mwingine, watazungumzia sana madhaifu yako na kudai Rais huyo ajae ni Rais bora haijapata kutokea.

Anachoangalia Chawa ni maslahi yake binafsi, akisifia, akalamba uteuzi ama akaendelea kubaki kwenye nafasi yake, basi gonjwa uchawa utaendelea kushamiri. Majuzi kwenye Hotuba yako umekana kwamba hauna Kundi, hilo halitoshi, kemea hadharani machawa maana uchawa sasa umeharibu hata fikra za Wabunge wengi na wamegeuka machawa na kusahau wajibu wao!

Mara nyingi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu amekuwa akiongea, ukimsikiliza vizuri anaonekana ni Kiongozi na mwenye hisia ya huruma na Haki, labda kwasababu ya history yake kwamba aliwahi Mwanaharakati, basi ni vyema yale unayoyaongea, wasaidizi wako hakikisha wanayatekeleza na wewe kuyasimamia ipasavyo.

Mwisho kwa Leo nisikuchoshe, nikupongeze kwa miaka mitatu, Ombi kubwa ni hakikisha Haki inapatikana kupitia Katiba mpya ya Wananchi na Tume HURU ya Uchaguzi kabla ya chaguzi zijazo, vinginevyo yatakuwa yaleyale. Kama ulivyo Mwanamke wa kwanza kuwa Rais Tanzania, basi ingependeza sana Kama utatuletea Katiba mpya kabla ya 2025.

Tanzania ni yetu sote!
Ungeongeza kuwa katika miaka mitatu ufisadi na upigaji wa kodi za wananchi umeongezeka sana. Waziri anauza na kununua club za mpira wa miguu kama njugu huku pesa zilichotwa hazina na yeye anakodoa tu macho bila kuchukua hatua yeyote. Hii maana yake na yeye ni mwenzao
 
Back
Top Bottom