JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,327
- 5,510
Siku moja baada ya mwanasiasa Willbrod Peter Slaa kukosoa mchakato wa jamii kuichambua ripoti ya CAG kwa madai kuwa sheria hairuhusu kufanya hivyo mpaka Kamati ya Bunge iipitie, ameomba radhi kwa kueleza kuwa alikuwa anasimamia sheria ambayo haikufanyiwa kazi.
Dkt. Slaa alinukuliwa akisema “Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zitto Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu.
“Moja ya maelezo ya ile sheria inasema baada ya CAG kukabidhi ripoti yake kwa Rais kisha kuifikisha Bungeni siku saba baadaye, ripoti hiyo haitakiwi kuwa public discussion, kwa kuwa ni kama mhtasari tu wa ripoti.
“Inatakiwa Kamati ya Bunge ndiyo iifanyie kazi, mfano kuna sehemu unaweza kukuta risiti haikuonekana wakati wa ukaguzi lakini hiyo ikapitishwa na kuonekana ni wizi, tumepotosha maana ya ile taarifa ya CAG.
“Kwanza hata CAG mwenyewe amechangia kuleta hii taharuki kwa kuwa huwa ni ya awali tu na analijua hilo, inatakiwa irudi kwa akaunti ofisa wa Serikali ijadiliwe, pia CAG wakati anatoa taarifa zake hadharani hatakiwi kuingia ndani kutoa ufafanuzi zaidi kama anavyofanya.”
Zitto ajibu
Baada ya kauli hizo, Zitto Kabwe alijibu kusema: “Dk Slaa amekosea, anajua Ripoti ya CAG ikishawekwa mezani Bungeni inakuwa ni ‘public document’ na inapaswa kujadiliwa, suala la kujibu hoja alihusiani na public inachozungumza.
“Kuna hoja zinakaa hata miaka 10 bila kujibiwa.
“Kwa mujibu wa sheria za umma za sasa ambayo ilifanyiwa marekebisho wakati Slaa akiwa hayupo Bungeni, Ripoti ya CAG inapoletwa Bungeni inapaswa kuwasilishwa na majibu ya Serikali, hivyo hakuna tatizo public kuijadili.”
Dkt. Slaa aomba radhi
“Mimi nilikuwa nafanyia kazi sheria ya ukaguzi ya mwaka 2009, kwa bahati mbaya nilifanyia kazi taarifa ambayo haikuwa sahihi na siyo kwamba nilikuwa nina nia ya kupotosha, kama kuna marekebisho naomba radhi na sina sababu ya kubishana na Zitto.
“Kwa ufupi ni kuwa kwa bahati mbaya nilikuwa nafanyia kazi sheria ambayo haijafanyiwa marekebisho. Niliyokuwa naitumia ipo Google na inawezekana huko hawajaibadilisha iliyopo,” – Slaa.