Dkt. Slaa aomba radhi kwa hoja yake “Ripoti ya CAG inapotoshwa’, Zitto Kabwe atoa neno

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
981
2,658
Siku moja baada ya mwanasiasa Willbrod Peter Slaa kukosoa mchakato wa jamii kuichambua ripoti ya CAG kwa madai kuwa sheria hairuhusu kufanya hivyo mpaka Kamati ya Bunge iipitie, ameomba radhi kwa kueleza kuwa alikuwa anasimamia sheria ambayo haikufanyiwa kazi.

Dkt. Slaa alinukuliwa akisema “Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zitto Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu.

“Moja ya maelezo ya ile sheria inasema baada ya CAG kukabidhi ripoti yake kwa Rais kisha kuifikisha Bungeni siku saba baadaye, ripoti hiyo haitakiwi kuwa public discussion, kwa kuwa ni kama mhtasari tu wa ripoti.

“Inatakiwa Kamati ya Bunge ndiyo iifanyie kazi, mfano kuna sehemu unaweza kukuta risiti haikuonekana wakati wa ukaguzi lakini hiyo ikapitishwa na kuonekana ni wizi, tumepotosha maana ya ile taarifa ya CAG.

“Kwanza hata CAG mwenyewe amechangia kuleta hii taharuki kwa kuwa huwa ni ya awali tu na analijua hilo, inatakiwa irudi kwa akaunti ofisa wa Serikali ijadiliwe, pia CAG wakati anatoa taarifa zake hadharani hatakiwi kuingia ndani kutoa ufafanuzi zaidi kama anavyofanya.”

Zitto ajibu
Baada ya kauli hizo, Zitto Kabwe alijibu kusema: “Dk Slaa amekosea, anajua Ripoti ya CAG ikishawekwa mezani Bungeni inakuwa ni ‘public document’ na inapaswa kujadiliwa, suala la kujibu hoja alihusiani na public inachozungumza.

“Kuna hoja zinakaa hata miaka 10 bila kujibiwa.

“Kwa mujibu wa sheria za umma za sasa ambayo ilifanyiwa marekebisho wakati Slaa akiwa hayupo Bungeni, Ripoti ya CAG inapoletwa Bungeni inapaswa kuwasilishwa na majibu ya Serikali, hivyo hakuna tatizo public kuijadili.”

Dkt. Slaa aomba radhi
“Mimi nilikuwa nafanyia kazi sheria ya ukaguzi ya mwaka 2009, kwa bahati mbaya nilifanyia kazi taarifa ambayo haikuwa sahihi na siyo kwamba nilikuwa nina nia ya kupotosha, kama kuna marekebisho naomba radhi na sina sababu ya kubishana na Zitto.

“Kwa ufupi ni kuwa kwa bahati mbaya nilikuwa nafanyia kazi sheria ambayo haijafanyiwa marekebisho. Niliyokuwa naitumia ipo Google na inawezekana huko hawajaibadilisha iliyopo,” – Slaa.
 
Kitimoto

JF-Expert Member
Aug 25, 2012
2,528
1,651
Sisi tunaona Dk Slaa ndiyo wa hivyo! Hata mumtetee kiasi gani bado amekuwa debe tu, chawa na mchumia tumbo.

Sisi watu wa Manyara tunapenda kumsihi Dk Slaa kwamba uchawa kwa umri wake ni aibu kubwa sana. Wazee wa umri wake hushauri na huelekeza njia, siyo uchawa.
Mbaya zaidi kabila la Iraqw hainaga uchawa iwe kijana au mtu mzima, yeye anatoa wapi tabia hii tena uzeeni? Kwamba alifundishwa na Josephine Mushumbus?
Cc Dkt Slaa
Sijui Udokta wake ni wa nini!
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
12,221
46,628
Kwanza nimpongeze kwa kuwa mstaarabu amekubali kosa na kuomba radhi kuhusu uwasilishwaji wa ripoti ya CAG bungeni uliopo kisheria, sheria ilikuwa ammended yeye hakuwa na taarifa.

Lakini kwangu, naona hata yale masuala mengine aliyozungumzia ikiwemo Katiba Mpya kwamba sio hitaji la wananchi pia alipotosha umma. Katiba Mpya ni muhimu sana kwasababu hata yeye mwenyewe kwenye maelezo yake alikiri Katiba ya sasa ni mbovu.

Kama akipendezwa namshauri pia aombe radhi kwa hilo la Katiba Mpya.
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
65,589
73,028
Sisi tunaona Dk Slaa ndiyo wa hivyo! Hata mumtetee kiasi gani bado amekuwa debe tu, chawa na mchumia tumbo.

Sisi watu wa Manyara tunapenda kumsihi Dk Slaa kwamba uchawa kwa umri wake ni aibu kubwa sana. Wazee wa umri wake hushauri na huelekeza njia, siyo uchawa.
Mbaya zaidi kabila la Iraqw hainaga uchawa iwe kijana au mtu mzima, yeye anatoa wapi tabia hii tena uzeeni? Kwamba alifundishwa na Josephine Mushumbus?
Cc Dkt Slaa
Kwani bado wako pamoja na josemshumbz hehe

Ova
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
16,544
17,716
ameomba radhi kwa kueleza kuwa alikuwa anasimamia sheria ambayo haikufanyiwa kazi.

Kwa muktadha huo inabidi tuwe makini sana na kauli, mahojiano au hotuba atakazotoa Mzee Dr. Wilbrod Slaa.

Naisifia sana JF kwa kila mara wanaJF kuomba source, picha, 'clip', sheria inasemaje (na marekebisho yake), katiba inatamka nini, video, nukuu sahihi n.k wanaposoma taarifa yoyote ile itokayo kwa yeyote awaye bila kujali uzee wake, usomi wake, nafasi yake ktk jamii, uongozi wake,ukuhani wake n.k
 
darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
6,973
12,637
Kwenye kujenga hoja Zitto yupo vizuri...no wonder hata na ubabe wa Jiwe hakupata misukosuko kwa sababu alijenga hoja zake kitakwimu. Faraja pekee ya Jiwe ilikuwa pale opportunist Mwigulu alipoibuka na kuanza kumjibu Zitto.

.......Akazawadia uwaziri😂😂Slaa ameonyesha udhaifu sana.
 
balibabambonahi

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
11,959
9,489
Siku moja baada ya mwanasiasa Willbrod Peter Slaa kukosoa mchakato wa jamii kuichambua ripoti ya CAG kwa madai kuwa sheria hairuhusu kufanya hivyo mpaka Kamati ya Bunge iipitie, ameomba radhi kwa kueleza kuwa alikuwa anasimamia sheria ambayo haikufanyiwa kazi.

Dkt. Slaa alinukuliwa akisema “Kuna upotoshwaji kwenye taarifa ya CAG, nadhani Zitto Kabwe angelisaidia sana taifa hili kama angekuwa mkweli, mimi na Zitto tulishiriki kutengeneza sheria ya ukaguzi wa fedha 2009, hata maneno yaliyopo kwenye sheria hiyo yametoka kwetu.

“Moja ya maelezo ya ile sheria inasema baada ya CAG kukabidhi ripoti yake kwa Rais kisha kuifikisha Bungeni siku saba baadaye, ripoti hiyo haitakiwi kuwa public discussion, kwa kuwa ni kama mhtasari tu wa ripoti.

“Inatakiwa Kamati ya Bunge ndiyo iifanyie kazi, mfano kuna sehemu unaweza kukuta risiti haikuonekana wakati wa ukaguzi lakini hiyo ikapitishwa na kuonekana ni wizi, tumepotosha maana ya ile taarifa ya CAG.

“Kwanza hata CAG mwenyewe amechangia kuleta hii taharuki kwa kuwa huwa ni ya awali tu na analijua hilo, inatakiwa irudi kwa akaunti ofisa wa Serikali ijadiliwe, pia CAG wakati anatoa taarifa zake hadharani hatakiwi kuingia ndani kutoa ufafanuzi zaidi kama anavyofanya.”

Zitto ajibu
Baada ya kauli hizo, Zitto Kabwe alijibu kusema: “Dk Slaa amekosea, anajua Ripoti ya CAG ikishawekwa mezani Bungeni inakuwa ni ‘public document’ na inapaswa kujadiliwa, suala la kujibu hoja alihusiani na public inachozungumza.

“Kuna hoja zinakaa hata miaka 10 bila kujibiwa.

“Kwa mujibu wa sheria za umma za sasa ambayo ilifanyiwa marekebisho wakati Slaa akiwa hayupo Bungeni, Ripoti ya CAG inapoletwa Bungeni inapaswa kuwasilishwa na majibu ya Serikali, hivyo hakuna tatizo public kuijadili.”

Dkt. Slaa aomba radhi
“Mimi nilikuwa nafanyia kazi sheria ya ukaguzi ya mwaka 2009, kwa bahati mbaya nilifanyia kazi taarifa ambayo haikuwa sahihi na siyo kwamba nilikuwa nina nia ya kupotosha, kama kuna marekebisho naomba radhi na sina sababu ya kubishana na Zitto.

“Kwa ufupi ni kuwa kwa bahati mbaya nilikuwa nafanyia kazi sheria ambayo haijafanyiwa marekebisho. Niliyokuwa naitumia ipo Google na inawezekana huko hawajaibadilisha iliyopo,” – Slaa.
Wewe Mzee,chutama unaaibika unajiaibisha
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
16,544
17,716
Babu yetu Dr. Wilbrod Slaa Uongo haulipi

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

8 Reactions
Reply
Top Bottom